Haya Ndio Magari 10 Yenye Thamani Kubwa Zaidi Duniani (2016)

Kuna mwanamke mmoja aliwahi kuniambia kwamba wanawake wanapoangalia mwanaume mwenye “thamani” huangalia vitu kadhaa. Anasema huangalia saa uliyovaa,mkanda, kiatu na bila ubishi gari. Pia hunusa manukato.Hawana sana mpango na shati na suruali. Haziwapi picha kamili.

Kwa upande wa wanaume, ushindani wa kiumeni hufikia pia kwenye masuala ya magari. Magari ndio “toys” za wanaume watu wazima. Mara nyingi njiani nikiona gari limenipita kwa kasi na mbwembwe, tukifika kwenye mataa huwa naangalia abiria waliomo. Huwa kuna mwanamke pembeni. Basi hapo najua mwanaume anajifaragua. Ni kijana ambaye bado anajaribu kujitambua.

Jambo moja la ajabu sana ni kwamba japokuwa wanawake hutumia kigezo cha gari na mambo mengine katika kutafuta au kupima “thamani”, wanawake hao hao huwa hawajali (na wengi hawapendi) mbwembwe za barabarani.  Hawapendi kabisa mwanaume “show off”. Uliza. Kimsingi, mbwembwe zako,kujifaragua nk ni sababu za kutosha kwa mwanamke kumtosa mtu. Anaweza kukaa na wewe just for the sake of cash. Usiniulize what can be happening behind the scenes. Okay?

Unapomwekea sauti kubwa ili asikie “sound” ya subwoofer yako, unapoteza tu muda. She ain’t into all that. Take her shopping instead. Don’t tell her you are wealthy. Show her. Ustaarabu na mambo mengine ni muhimu. Tafsiri ya gentleman ina mengi.

Anyway, turudi kwenye topic. Haya hapa ni magari yenye thamani kubwa kwa mwaka jana (2016). Picha na habari ni kwa mujibu wa www.digitaltrends.com. Unaweza kusoma kwa undani zaidi kuhusu magari haya kwa kubonyeza hapa

$4.8 million – Koenigsegg CCXR Trevita

$4.5 million – Lamborghini Veneno

$3.4 million – W Motors Lykan Hypersport

$3.4 million – Limited Edition Bugatti Veyron by Mansory Vivere

$3.0 million – Ferrari Pininfarina Sergio

$2.6 million – Pagani Huayra BC

$2.5 million – Ferrari F60 America

$2.5 million – Bugatti Chiron

$2.0 million – Koenigsegg One:1

 

$2.0 million – Koenigsegg Regera

$8 million – Mercedes-Benz Maybach Exelero

$2.7 Million – LaFerrari FXX K

$2.2 million – Lamborghini Sesto Elemento

$1.9 million – Lamborghini Centenario LP 770-4

$1.4 million – Ferrari LaFerrari

$1.4 million – Aston Martin One-77

$1.2 million – Zenvo ST1

$1.15 million – McLaren P1

$1.1 million – Rolls-Royce Phantom Serenity

Comments Closed

Comments are closed.

Copyright © Bongo Celebrity