ViDeO: Maoni,Ushauri Wa Hashim Rungwe Kuhusu Vyeti Vya Makonda Na Vita Dhidi Ya Madawa Ya Kulevya

Hashim Rungwe Spunda, sio jina geni. Ni mwanasiasa, mwanasheria. Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, aligombea Urais kupitia Chama Cha Umma (CHAUMA). Yeye ndio Mwenyekiti.

Sifa yake moja ambayo humfuata kama kivuli ni pamoja na kuelezea mambo mbalimbali katika lugha ambayo inaeleweka kwa kila mtu na hususani anayeitwa mtu wa kawaida. Katika ubora wake, akiongea kama mgeni mwalikwa katika kipindi cha Kikaangoni Cha East Africa Television(EATV) ameongelea mambo kadha wa kadha ambayo hivi sasa yametawala katika vyombo vya habari, vijiweni, mitaani na bila shaka kwenye mitandao ya kijamii.

Kubwa zaidi ni kuhusu vita dhidi ya madawa ya kulevya na pia utata kuhusu majina na elimu ya  Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salaam. Kimsingi hivi sasa mkuu huyo anajulikana kwa majina mawili ikitegemea na unayemuuliza.  Msikilize

 

Comments Closed

Comments are closed.

Copyright © Bongo Celebrity