Tundu Lissu Achaguliwa Kuongoza Tanganyika Law Society (TLS)

Mwanasheria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, leo hii amechaguliwa kuwa Rais wa Chama Cha Wanasheria wa Tanganyika ambacho kwa Kiingereza kinajulikana kama Tanganyika Law Society (TLS).
Tundu Lissu amechaguliwa katika Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC, jijini Arusha, Kaskazini mwa Tanzania.

Matokeo ni kama ifuatavyo:

Urais: Kura zilizopigwa 1682
 1.     Tundu Lissu 1411  sawa na asilimia 88
 2.     Francis Stolla 64
 3.     Victoria Mandari 176
 4.     Godwin Mwapongo 64
Kwa upande wa nafasi ya Makamu wa Rais (TLS) mshindi ni Godwin Ngwilimi aliyekuwa Mwanasheria wa Tanesco na kutimuliwa kwa kupinga Escrow.
 
Council Members (Wajumbe wa Baraza )
 1.     Jeremiah Motebesya
 2.     Gida Lambaji
 3.     Hussein Mtembwa
 4.     Aisha Sinda
 5.     Steven Axweso
 6.     David Shilatu
 7.     Daniel Bushele
Comments Closed

Comments are closed.

Copyright © Bongo Celebrity