Mtizame Mwanamuziki Rihanna Akifundisha Hesabu Nchini Malawi

LOS ANGELES, CA – FEBRUARY 12: Recording artist Rihanna attends the 59th GRAMMY Awards at STAPLES Center on February 12, 2017 in Los Angeles, California. (Photo by Axelle/Bauer-Griffin/FilmMagic)

Mwanamuziki Rihanna anajulikana kwa mambo mengi ikiwemo urembo,kipaji chake cha muziki,fashion na pia kupitia mahusiano mbalimbali hususani ya kimapenzi  ambayo amewahi kuwa nayo na wasanii wenzake kama vile Chris Brown, Drake nk.

Lakini mbali na muziki, Rihanna ni mtu anayejali sana jamii. Mara nyingi amekuwa akisema tabia hiyo ameitoa kwa Bibi yake. Rihanna ambaye ni mwanzilishi wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Clara Lionel Foundation hivi karibuni alitembelea nchini Malawi kujionea mwenyewe changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi nchini humo kwa kushirikiana na shirika la Global Citizen na Global Partnership for Education kwa minajili ya kusaidia kuzitatua.

Akiwa nchini Malawi, kwa mujibu wa jarida la Time, Rihanna aliingia darasani na kutumia muda wake kuwafundisha hesabu, kuwasomea na baadae kucheza na wanafunzi.

Lengo la ziara ya Rihanna nchini Malawi na kwingineko ni kuwashawishi viongozi wa dunia kiasi cha $3.1 Billion kwenda katika shirika la Global Partnership for Education ambazo zitakwenda kusaidia kuboresha hali na upatikanaji wa elimu katika nchi 89. Kwa mujibu wa tovuti ya Global Citizen kiasi hicho cha fedha kitawasaidia zaidi ya wanafunzi na watoto milioni 800.

Mtazame Rihanna hapa chini

 You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

 

Comments Closed

Comments are closed.

Copyright © Bongo Celebrity