“See You Again” Ya Charlie Puth & Wiz Khalifa Yaitoa “Gangnam Style Kileleni Kwenye YouTube

Video ya wimbo See You Again wa Charlie Puth na Wiz Khalifa hivi sasa ndio wimbo ambao umetizamwa na watu wengi zaidi (au tuseme mara nyingi zaidi) katika mtandao wa YouTube.

Kwa kutazamwa na watu au mara Billion 2.896 inamaanisha video hiyo kwa sasa imeitoa kileleni video ya wimbo Gangnam Style ya mwanamuziki Psy kutoka Korea Kusini kwa kiwango kisichopungua milioni 2. Video ya tatu kutizamwa zaidi bado inakuwa wimbo wa Sorry kutoka kwa Justin Bieber.

Gangnam Style ilitolewa mwaka 2012 huku See You Again ikija mwaka 2015 kama dedication maalum kwa mwigizaji Paul Walker aliyejipatia umaarufu kwa kuigiza mfululizo wa filamu za Fast And Furious. Walker alifariki Novemba mwaka 2013 kwa ajali ya gari.

Kupitia mtandao wa Twitter, Charlie Puth amewashukuru mashabiki kwa kumwezesha kufikisha hii rekodi na kusema hakuwahi kuwaza kama video hiyo itakuja kupata mafanikio na namna hii.

Hii hapa video ya “See You Again”

Comments Closed

Comments are closed.

Copyright © Bongo Celebrity