“Naogopa”-Q Chilla (Official Release-NeW)

Tukisema tuongelee wanamuziki wenye vipaji vya kweli vya kuimba nchini Tanzania, hakuna shaka kwamba Q Chilla hatuwezi kumuweka kando. Zamani aliitwa Q-Chief na uwezo wake ulikubalika na pengine kusaidia sana kuisukuma mbele sanaa ya muziki wa kizazi kipya.

Lakini pamoja na kipaji, Q Chilla amepitia mengi. Ameanguka.Akasimama. Akaketi na kisha kuamka tena. Ujana umempeleka kwingi. Lakini jambo moja ambalo linabakia ni kipaji alichonacho. Usipomheshimu kwa mengine, utakuwa mchawi usipoheshimu kipaji alichonacho.

Huu hapa ni wimbo mpya kutoka kwake. Anasema anaogopa. Msikilize

Comments Closed

Comments are closed.

Copyright © Bongo Celebrity