Ronaldo, Messi, Neymar Miongoni Mwa Wachezaji 24 Wanaowania Tuzo Ya FIFA 2017

Kama ambavyo ilitarajiwa, Christiano Ronaldo, Lionel Messi na Neymar Jr, wametajwa miongoni mwa wachezaji 24 wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa FIFA kwa mwaka 2016/2017. 

Tofauti na miaka takribani 6 ambapo tuzo hizo za FIFA zilijulikana na Ballon D’or kutokana na ubia uliokuwepo kati ya FIFA na hilo Jarida maarufu la michezo la Ufaransa, tuzo za mwaka huu zinarejea kwa FIFA na hivyo kuendelea kujulikana kama FIFA Footballer Of The Year. Vipengele vingine vinavyowaniwa ni pamoja na Kocha Bora Wa Mwaka ambapo makocha Zinadine Zidane wa Real Madrid, José Mourinho wa Manchester United, Antonio Konte wa Chelsea na wengine 9 wanawania tuzo hiyo.

Katika orodha hiyo iliyotolewa mapema hivi leo, timu ya Real Madrid ambayo hapo jana iliwatandika mahasimu wao Barcelona na kubeba SuperCup De Espana, inaongoza kwa kuwa na wachezaji 7 walioteuliwa.

Tuzo za mwaka huu zitatolewa tarehe 23 October, 2017 jijini London nchini Uingereza.

Orodha kamili hii hapa.

Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund)
Leonardo Bonucci (AC Milan, Juventus in 2016-17)
Gianluigi Buffon (Juventus)
Dani Carvajal (Real Madrid)
Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
Paulo Dybala (Juventus)
Antoine Griezmann (Atletico Madrid)
Eden Hazard (Chelsea)
Zlatan Ibrahimovic (Free agent, Manchester United in 2016-17)
Andres Iniesta (Barcelona)
Harry Kane (Tottenham)
N’Golo Kante (Chelsea)
Toni Kroos (Real Madrid)
Robert Lewandowski (Bayern Munich)
Marcelo (Real Madrid)
Lionel Messi (Barcelona)
Luka Modric (Real Madrid)
Keylor Navas (Real Madrid)
Manuel Neuer (Bayern Munich)
Neymar (Paris Saint-Germain, Barcelona in 2016-17)
Sergio Ramos (Real Madrid)
Alexis Sanchez (Arsenal)
Luis Suarez (Barcelona)
Arturo Vidal (Bayern Munich)

Comments Closed

Comments are closed.

Copyright © Bongo Celebrity