Ujumbe Maridhawa Kutoka Kwa Lupita Nyong’o Kwenda Kwa Baba Yake

Katika Uchaguzi Mkuu wa nchini Kenya uliomalizika hivi karibuni, mambo mengi yalijiri. Kama kawaida ya siasa za Afrika, mshindi huwa hajashinda kihalali na mshindwa hupiga kauli mbiu ya “nimeibiwa”. Hiyo ni kuonyesha kwamba katika zama za demokrasia, sio rahisi hata siku moja kumpata mshindi ambaye hatolalamikiwa na upande mmoja huku akishangiliwa na upande mwingine.

Pamoja na kwamba katika siasa na chaguzi kuu nafasi ya Urais ndio hupewa kipaumbele zaidi, wapo wawakilishi ambao bila shaka tunapaswa kuwamulikia. Miongoni mwa hao ni pamoja na -Governors. Jimbo la Kisumu lilimchagua Prof.Anyang Nyong’o kuwa mkuu wao. Ingawa jina la Prof.Nyong’o ni la miaka mingi katika siasa, binti yake Lupita Nyong’o ambaye miaka kadhaa iliyopita alishinda tuzo maarufu ya uigizaji ya Oscar, umelipaisha zaidi jina la mshua.

Lupita na baba yake,Prof.Anyang Nyong’o

Alipoapishwa siku mbili zilizopita, binti yake huyo aliandika ujumbe maridhawa kupitia ukurasa wake wa Facebook kuwashukuru waliomchagua baba yake na pia kumpongeza. Huu hapa ujumbe mzima;

Comments Closed

Comments are closed.

Copyright © Bongo Celebrity