Twitter Inafanyia Majaribio Tarakimu 280 Badala Ya 140 Za Sasa!

Twitter 280 characters

Kama somo au mafunzo ya kufupisha story yalikupiga chenga, nina uhakika ugumu wa kutuma ujumbe unaoeleweka kwa kutumia tarakimu 140 tu, sio jambo la mzaha. Unaandika na kufuta. Wakati mwingine unakata tamaa kabisa na kujiachia.

Utaratibu wa kuandika kitu kwa kutumia tarakimu 140 tu au pungufu umekuwa ndio utaratibu wa mtandao maarufu wa kijamii wa Twitter.Nimewahi kuongea na watu ambao hawaupendi wala kuutumia mtandao wa Twitter kutokana na kikwazo hicho cha tarakimu 140.

Kama wewe ni miongoni mwa watu wanaopata tabu kuweka tarakimu 140 pamoja na kueleweka, kuna habari njema. Kupitia Twitter, mtandao huo umetangaza kwamba unafanyia majaribio uwezekano wa kuongoza idadi ya tarakimu kwa asilimia 100% kutoka 140 kwenda 280.

Hivi sasa mtandao huo umesema majaribio hayo yanafanyika kwa watu wachache waliowateua na kutokana na matokeo yake, ndipo watatangaza rasmi kama mimi na wewe tutaweza kuwa na uwanja mpaka zaidi wa kuhabarishana kupitia Twitter. Sisi tunapatikana kupitia @BongoCelebrity 

 

Comments Closed

Comments are closed.

Copyright © Bongo Celebrity