Hata Sielewi Lakini Naamini Unahitaji Kuiona Hii Video

Hata_Sielewi_MwanaFA_Maua_Sama_Tanzania

Huku nikiwa tayari nimeanza kuweka sawa orodha ya Nyimbo 20 Bora Na Zilizotamba Zaidi Kutoka TZ, MwanaFA akishirikiana na Maua Sama yaelekea hawana mpango wa kunirahisishia kazi. Hata Sielewi kwanini wanafanya hivi.

Nyimbo 20 (Top 20 Songs) Nilizozipenda Zaidi Kutoka Tanzania Mwaka 2016

Mapema hivi leo hashtag #HataSielewi ilitawala mitandao ya kijamii. Kwangu ilikuwa miongoni mwa habari ambazo Twitter waliona nahitaji kuzisoma. Hata Sielewi walijuaje. Lakini jambo moja dhahiri ni kwamba hawakunipotezea muda. Nilipenda.

Kitu kimoja ambacho hunifurahisha kwa wasanii kama MwanaFA huwa ni kukuza au kubadili lugha. Ana tabia ya kuingiza misemo mipya mitaani. Kama hujajua,sikiliza mitaani wiki ijayo.Niliwahi kuandika mahali kwamba MwanaFA ni kamusi inayotembea. Na hii ndio thamani mojawapo ya sanaa na msanii.

Nisiseme mengi. Wikiendi imewadia na Hata Sielewi itakuwaje? Here is the official video

Comments Closed

Comments are closed.

Copyright © Bongo Celebrity