Yaelekea Tekno Atafanya Collabo na Drake!

Miongoni mwa wasanii ambao wanaweza kusema mwaka 2017 ulikuwa mzuri kwao bila shaka Drake hakosi. Umekuwa mwaka mzuri kwake hususani kwa mauzo ya nyimbo zake na katika chati za muziki duniani.

Hivi sasa Drake ambaye anatarajiwa kuachia album mpya mwakani amekuwa akionyesha vionjo vya wasanii ambao atafanya nao collabo. Mengi yanasemwa kutokana na picha kadhaa ambazo amekuwa akizitoa kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa na wasanii. Mfano wa wasanii ni pamoja na Smokepurpp na hivi sasa Tekno ambaye ni msanii kutoka Nigeria.

Tekno ambaye jina lake la jukwaa ni Tekno Miles huku akijiita Alhaji mara kwa mara anafanya vizuri sana na wimbo wake Pana ambao umetokea kusikika kwa wingi barani Marekani ya Kaskazini. Huenda Drake alisikia nyimbo hiyo na kuamua kumshirikisha.

Hii hapa ni Instagram post ya Drake akiwa na Tekno ambaye jina lake la kuzaliwa ni Augustine Miles Kelechi. Alizaliwa katika jimbo la Bauchi nchini Nigeria.

Endapo Tekno atafanya collabo na Drake atakuwa anaendeleza wimbi la wasanii wa Afrika kufanya collabo na wasanii wa Marekani Kaskazini. Hivi karibuni msanii kutoka Tanzania, Diamond Platinumz aliachia collabo yake na Rapper Rick Ross. Wimbo unaitwa Waka Waka. Unaweza kuutizama hapa.

Tekkkkkkkkkkkk time

A post shared by champagnepapi (@champagnepapi) on

Comments Closed

Comments are closed.

Copyright © Bongo Celebrity