MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Anaitwa Irene Sporah Njau, ni mtangazaji wa Kipindi cha Sporah Show ambacho kinazidi kujipatia umaarufu na mashabiki.Lakini Sporah ni nani,ametokea wapi,ana malengo gani na ni kwanini anafanya anachokifanya? Ili kupata majibu ya maswali hayo na mengineyo bonyeza hapa kutembelea Spoti Starehe ili kucheki mahojiano kamili.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

KanumbaFrontKatika siku kama ya leo,miaka 26 iliyopita pale mkoani Shinyanga, alizaliwa kijana na kupewa jina la Steven. Hivi leo ni maarufu kama Steven Kanumba au kama mwenyewe anavyojiita wakati mwingine “The Great”. Kwa maana hiyo,leo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Steven Charles Kanumba.Happy Birthday!

Kwa mtu yeyote ambaye anafuatilia maendeleo ya tasnia ya filamu nchini Tanzania,bila shaka atakubaliana na mimi nikisema kwamba Kanumba ni miongoni mwa waigizaji wa filamu(Film Actors) ambao ni maarufu zaidi nchini Tanzania. Leo hii ni vigumu kuiongelea sanaa ya filamu nchini bila kumhusisha Kanumba kwa njia moja ama nyingine.

Kwa hivyo,haishangazi sana kuona kwamba,katika mwaka uliopita jina lake lilikuwa takribani la kudumu katika vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo vya mtandaoni,mitaani nk. Bila shaka unakumbuka jinsi habari ya Kiingereza Vs Kiswahili ilivyozua mjadala wa kitaifa. Kila mtu akasema lake.

Baada ya mambo kama yale,mijadala kama ile,watu hupenda kujua what next? Nilimtafuta Steven Kanumba ili kujua machache kuhusu mipango yake ya mwaka huu.

Unajua Kanumba angependa kupata chakula cha mchana (lunch) na actors gani maarufu hapa ulimwenguni? Una habari kwamba katika Curriculum Vitae(CV) yake ameongeza cheo cha “Blogger”? Unajua ana malengo gani mwaka huu? Una habari kwamba Kanumba hivi sasa amedhamiria kuibua vipaji vingine katika ulimwengu wa uigizaji filamu? Fuatana nami;

BC: Mpaka sasa unalionaje soko la filamu nchini Tanzania? Kumekuwa na mabadiliko gani ya kimsingi ukilinganisha toka ulipoanza mpaka hivi leo?

SK: Soko limetanuka kiasi kwamba tunatambulika kimataifa. Pia hivi sasa makampuni ya kusambaza kazi zetu yameongezea ikiwemo na pesa kwa kiasi fulani tofauti na hapo mwanzo.Safari bado ni ndefu lakini angalau inatia moyo.

BC: Mwaka 2009 ndio tumeumaliza.Jina lako liligonga vyombo vya habari kwa mambo kadha wa kadha.Unaweza kusema umejifunza mambo gani katika mwaka ulioisha? (more…)

ngugi1

Bila shaka unaitambua sura yake na bila shaka umewahi kumsoma au kusoma vitabu vyake. Anaitwa Ngugi wa Thiong’o. Ni miongoni mwa wanazuoni na waandishi ambao bara la Africa linajivunia kuwa nao.Je nikikupa nafasi ya kumuuliza swali Ngugi ungependa kumuuliza nini? Tuma swali lako kupitia sehemu ya maoni(comments) au kwa kutumia barua-pepe info at bongocelebrity dot com

HasheemT

Just a couple of weeks ago, he started his career as an NBA player. But before long, he broke his jaw in an incident involving him and his teammate, Zach Randolph. He actually suffered a ridgeline fracture in his mandible- a bone in his lower jaw.

Since the incident, his fans and well wishers have been praying for his quick recovery while his critics have also used the same opportunity to nail him down or try to elevate him. It just depends on how one looks at criticism.

I recently caught up with him, whereby, he took time to talk about his health and also to answer some of what his critics have been saying. Here is how my mini-interview with him went down…

BC: A lot of your fans and supporters have been worried about you since the jaw-breaking incident. Can you briefly tell me and of course…your fans how are you doing now and whether you are back in training and all that?

Hasheem Thabeet: Niko powa kabisa… I’m doing great. I have been back to work/practice since Monday and I am looking forward to play tonight when we play against L.A Clippers. I am a tough kid and don’t like to sit on a bench. I wouldn’t miss a game if it was my choice. But this is a professional level and coaches go with what they have been having or players that have been there before me. For now I am an additional and don’t mind playing that role.

BC: Some critics have been saying that you are not or were not ready for NBA and all that. I am sure you have heard such comments and criticism. What is your reaction?

Hasheem Thabeet: I know people have been talking and saying that I am not ready and or I should not have been drafted by Memphis and therefore suggesting I should have joined another team where there are more veterans so as to learn more and stuff. My answer to them is that; that is not or can’t work for everybody. If you may recall, Memphis Grizzlies drafted Pau Gasol. He was young and almost by himself. But eventually he ended where he is now…with a ring (Lakers).

I look at the situation differently. They drafted me for a lot of different reasons such as potential, progress, presence and production. That is what pushes to me to go out there and learn and strive to be better every day. There is a good reason they pay me $4 M per year.

So while I thank everybody for their advises, comments and criticism and try to understand those who keep doubting me or just hating for no well founded reasons, I wish to inform everyone that I am definitely making a progress and that is why I am able to survive the everyday’s routines of practices and the league itself.

BC: Thank you very much Hasheem. Wish you all the best.

Hasheem Thabeet: Thanks Jeff

befftabc1

Watanzania Ali Kiba, Pretty Poet( Jacqueline Kweka Kibacha) na kampuni ya Bongo UK ni miongoni mwa watu waliochaguliwa kuwania Tuzo za BEFFTA (Black Entertainment,Film,Fashion,Television and Arts Awards) zinazotarajiwa kufanyikia jijini London tarehe 17 October mwaka huu ndani ya London Hilton Metropole.

Ali Kiba amechaguliwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Best International Act huku Pretty Poet akichaguliwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Best Spoken Word Artist/Poets. Kampuni ya Bongo UK imechaguliwa kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Best Event Promoters.

Kwa orodha kamili ya waliochaguliwa kuwania tuzo hizo,tafadhali bonyeza hapa. Ili kuona kazi za Jacqueline Kweka Kibacha,bonyeza hapa na hapa na hapa.

Kama ilivyo kawaida ya tuzo siku hizi,kura zinapigwa na wananchi.Wakati ukiwadia kwa zoezi hilo,BC itakujulisha.Kwa sasa tunapenda tu kuwapongeza Ali Kiba,Pretty Poet na Bongo UK for the nomination.

chrisbc

Christabel Swai(Silipa) standing on the “Roof of Africa”

Kila mwaka maelfu ya watu hutoka kila pande za dunia na kuja nchini Tanzania na hususani mkoani Kilimanjaro wakiwa na nia ya kuupanda Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu kupita yote barani Afrika.

Pamoja na wageni wengi kuja nchini kwa lengo hilo,idadi ya watanzania ambao wameshawahi kuupanda mlima huo bado ni ndogo. Hapo ndipo suala zima la utalii wa ndani (internal tourism) linapokuja.

Lakini hivi karibuni yupo mtanzania ambaye ameonyesha mfano. Ni mtoto wa miaka 10! Anaitwa Christabel Swai. Mtoto huyo amefanikiwa kuupanda Mlima Kilimanjaro na kufika pale pale kileleni ambapo kina Kapteni Nyirenda(RIP) na wenzake waliuweka mwenge wa uhuru miaka takribani 48 sasa iliyopita.

Kwa maana hiyo,Christabel ambaye pia hujulikana kwa jina la Silipa,ameweka rekodi ya kuwa mtu mwenye umri mdogo zaidi nchini kuupanda mlima huo na kufika Uhuru Peak.

Mtoto huyo wa kike ni mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya Eden Garden ya mjini Moshi, alipewa cheti namba 60473 kinachoonyesha na kuthibitisha kwamba amefanikiwa kufika kilele cha mlima huo wenye urefu wa mita 5,895 kutoka usawa wa bahari.

chris-gilman

Silipa at Gilman’s Point. Wengi huishia hapa lakini ilipokuja kwa Silipa,alipumzika kama dakika 20 hivi kisha akamwambia baba yake “Dad,Lets go to Uhuru”

Christabel alifanikiwa kupanda mlima huo kupitia njia ya Rongai(miongoni mwa njia zinazosemekana kuwa ngumu zaidi) akiwa ameongozana na baba yake, Cathbert Swai ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Uwakala ya Utalii ya Ahsante Tours ya mjini Moshi.

BC inapenda kumpongeza sana Christabel a.k.a Silipa.Well done!

91

mandelabc

Jana ilikuwa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa Nelson Mandela.Huyu ni shujaa wa wengi.Nchini Marekani,mtu anakuwa hajafikia umaarufu wa kweli kama hajawahi kuonana na Nelson Mandela.Ndio maana unaona kila kukicha celebrities kutoka nchi hiyo wanamiminika kwenda Afrika Kusini japo wapate nafasi ya kupiga picha na Mzee Madiba.Kama nyumbani kwako huna picha ukutani ukiwa bega kwa bega na Mandela…bado!

Kwetu sisi waafrika,tunajua thamani ya mtu huyu.Ni mpigania haki za binadamu,mpinzani wa tawala dhalimu na pia mpenda amani.Lakini leo hii ni nani kama Mandela,Nyerere,Kwame Nkrumah,Lumumba na wengineo barani kwetu? Kwanini hatuna tena viongozi ambao kwa dhati wanajali maslahi ya wananchi na bara zima la Afrika? Wapi tulipotea?

Madiba,Hongera kwa kutimiza miaka 91.Kila la kheri.

Pichani ni Mzee Madiba akipuliza mshumaa kuashiria kutimiza miaka 91.Pembeni yake ni mke wake, Graca Machel-Mandela nyumbani kwao jijini Johanesburg hapo jana.

Photo/Yazbek-Nelson Mandela Foundation

Tafadhali naomba usinichoke kwa kupenda kutundika masuala/hotuba za Obama.Nafanya hivyo kwa kuamini kwamba kila siku binadamu tunajifunza au tunatakiwa tujifunze mambo mapya.Hotuba za Obama zawezekana kuwa hazikufunzi mambo mapya ila kwa mapana na marefu naaamini zinatukumbusha mambo mbalimbali.Pia namfuatilia Obama kwa sababu angalau yeye ndio mwanasiasa ambaye namuona hapendi “kuongopa waziwazi”.Obama hawezi kukuambia kesho atakujengea daraja wakati moyoni mwake anajua kabisa hela za daraja alishakula. Hawezi pia kutoa ahadi za maisha bora kwa wote bila kukumbusha kwamba kazi ndio msingi wa maendeleo.

Obama anaweza kuwa anaongea na kundi fulani tu la watu lakini akawa anatoa ujumbe mkali kwa jamii mbalimbali.Cha msingi labda ni kusikiliza kwa makini na kufanya tathmini makini. Hivi majuzi Obama alialikwa na kutoa hotuba wakati wa kusherekea miaka 100 ya chombo muhimu cha Wamarekani Weusi kinachoitwa NAACP(National Association for the Advancement of Colored People)

Katika hotuba yake,Obama aliongelea mengi.Muhimu zaidi ambalo naamini hata sisi watanzania tunaweza kujihusisha nalo ni suala la elimu kwa watoto wetu,jamii zetu. Ulimwengu wa leo,wa ushindani wa namna hii,unahitaji elimu makini.Je tunafanyaje katika hilo? Viongozi wetu wanatupeleka wapi? Hebu tujiulize, tangu marais wetu waliofuatia baada ya J.K.Nyerere wametusaidia kujenga maktaba ngapi? Hivi unajua jiji la Dar-es-salaam lina maktaba ngapi?

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

obama-ghanabc

Kama ulikuwa hutambui jinsi Rais wa Marekani,Barack Obama,alivyo maarufu na kipenzi cha waafrika walio wengi,basi ulichotakiwa kufanya ni kuelekeza macho na masikio jijini Accra nchini Ghana huko magharibi mwa bara la Afrika hivi leo.

Taarifa mbalimbali nilizonazo kupitia vyombo mbalimbali vya habari na pia washirika wa BC waliokuwapo jijini Accra hivi leo wanasema Ghana nzima ni kama vile ilisimama. Kila kona ilikuwa imepambwa kwa mabango,nguo nk vikimkaribisha kwa shangwe na vifijo Rais huyo wa Marekani ambaye alikuwa pia ameambatana na mkewe Michelle pamoja na mabinti zao wawili,Sasha na Malia.

Lakini tukiachana na shangwe,fujo na vigeregere vilivyojiri huko Ghana,muhimu sana ni kile alichokisema Obama wakati akihutubia Bunge la nchi hiyo. Kimsingi Obama alitumia muda huo kuongea na bara zima la Afrika.Wengi wameiita hotuba ya Obama kuwa ilikuwa ni ‘lecture” kwa viongozi wetu na vile vile wananchi.

Ukombozi wa Bara la Afrika uko mikononi mwa waafrika wenyewe. Hatuna tena sababu za kuendelea kulaumu historia ya biashara ya utumwa na ukoloni kwa mabaya yanayojiri barani mwetu hivi leo.Tuachane na vita za ukabila,udini,utaifa nk.Bado nasikia maneno hayo kutoka kwa Obama hata hivi ninavyoandika.

Ili kutunza kumbukumbu hii muhimu,hapo chini unaweza kusikiliza hotuba nzima ya Obama. Pia kama kwa sababu moja au nyingine,lugha aliyotumia Obama huielewi unaweza kubonyeza hapa ili kusoma kwa Kiswahili tafsiri ya hotuba hiyo.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Baada ya kumaliza kumsikiliza Obama,hoja zilizonijia kichwani kwangu ni kwamba

  • Je,viongozi wetu au sisi waafrika kwa ujumla tutazinduka kidogo baada ya kusikia hoja nzito za ‘Ukombozi wa Bara la Afrika ni Jukumu Letu Sisi Wenyewe” kutoka kwa Obama?
  • Je viongozi wetu wamesikiliza kwa makini alichokisema Obama? Wapo tayari kuianza upya safari ya kulikomboa bara letu au ndio hadithi ya sikio la kufa?

Photo/Chuck Kennedy/White House

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page