Siku chache zilizopita nilipokea taarifa kutoka kwa Msanii Nonini kutoka nchini Kenya kwamba ameachia wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Colour kwa Face kutoka katika album yake ya tatu aliyoipa jina The Godfather of Genge(ipo sokoni hivi sasa) akimshirikisha mwanadada Christine Apondi.

Kwa bahati mbaya sikupata muda wa chapchap wa kuusikiliza wimbo huu mpaka hivi leo.Kwa kawaida huwa siweki wimbo mpya hapa mpaka niwe nimeshausikiliza na kuupitisha(kuna watoto wanaingia hapa,lazima tuzingatie maadili fulani)

Baada ya kuusikiliza ilinibidi kusitisha vyote nilivyokuwa nafanya,kwenda ndani,kutoka nje na kuketi tena.Katika wimbo huu Nonini ambaye ni mwanaharakati wa kutetea watu wenye ulemavu wa ngozi(albino)anatuma ujumbe mpana sana kupitia wimbo huu.Kama mtakumbuka,Taifa letu la Tanzania liliingiwa na kashfa ya kimataifa pale ulimwengu ulipogundua kwamba kuna binadamu fulani wenye roho za ajabu wanawageuza watu wenye ulemavu wa ngozi “deal”.Nonini anaongelea hilo pamoja na mambo mengine ya kubaguana.Anaasa kupendana.Mpende kaka yako,mpende jirani na mpende kila mtu.Kwanini kubaguana?

Wimbo umetengenezwa na Musyoka kutoka Decimal Records.Usikilize…

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Unaweza kutizama picha za Nonini akiwa katika harakati zake za kupinga ukatili wowote dhidi ya albinos kwa kubonyeza link hii http://www.noninimusic.com/v2/national-albinism-day-may-4th/

East Africa’s most-beloved singer presents a joyous new studio album bearing the message: Life is sweet, but short. Let’s have some fun – Come dance with me! The mighty Orchestra Virunga is joined here by guest artists including Suzanna Owiyo, Awillo Mike, Ballou Canta, sax maestro Jimmy Mvondo, guitar luminaries Syran Mbenza, Huit Kilos and Zaiko Langa Langa’s Beniko Popolipo, and introducing the extraordinary John Bashengezi.

Employing a delightful spectrum of rhythms and messages, Samba ventures into Latin and reggae beats and socially conscious topics such as tribalism and environmental awareness. Ecstatic dance-inducing songs “Maisha Ni Matamu” and “Nipigie Simu”; the luscious rumbas of “Zanzibar” and “Tupande Miti”; “Jirani,” a caution to nosy neighbors delivered with a lilting Caribbean swing; and the gentle acoustic tour de force of “Tupendane” offer an utterly entrancing musical excursion conducted by the unparalleled international music ambassador Samba Mapangala.

The album is released worldwide by Virunga Records. Retail CD sales through CDBaby.com, Amazon, Amoeba Records in Los Angeles, PanAfricanAllstars.com and your friendly local record shop. Digital downloads available from CDBaby, Amazon.com, iTunes and all major music sites. Wholesale CD distribution worldwide via Super D One-Stop, and AI Records Ltd.

read more

This one is from Kigali-Rwanda from StepUp Records by Bac-T.Its a mix of Swahili, English and Kinyarwanda.The track is from an upcoming album from Bac-T titled January to December.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Hii ni collaboration ya Kenya na Tanzania.Wimbo unaitwa Nimetoka Mbali.Ni kutoka kwa msanii Jaguar kutoka nchini Kenya akiwa amemshirikisha wa kwetu wenyewe,AY.Ni mojawapo ya track mpya mpya zinazotamba kwenye vituo vya radio,televisheni bila kusahau katika kumbi mbalimbali za raha.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

jose_juma_naturebc

Mojawapo ya mambo ambayo yanaweza kukufurahisha kama unapenda muziki kutoka Afrika Mashariki ni pale wasanii kutoka nchi zinazounda Afrika Mashariki wanapoamua kushirikiana katika kazi zao. Mifano ipo mingi kuonyesha jinsi gani mipaka iliyowekwa na mtawala wa enzi hizo inaweza kuvukwa japo kwa kutumia muziki.

Nimewahi kuandika siku za nyuma kwamba wakati viongozi wetu wanasuasua katika kukamilisha muundo wa jumuiya ya Afrika Mashariki(ukiniuliza mimi nitakwambia ni kwa sababu kila mmoja anaweka mbele maslahi binafsi badala ya faida nyingi za muungano makini) wasanii wao wameshavuka kizingiti hicho.Wanashirikiana.

Miongoni mwa mifano ya ushirikiano huo ni huu wa Juma Nature akimshirikisha Jose Chameleon(Uganda) katika wimbo unaokwenda kwa jina Mikiki Mikiki. Kama ujuavyo hawa wote ni ‘majina makubwa” katika muziki wa ukanda wetu. Wanaposhirikiana tunategemea kitoke kitu makini.Nakuomba uwe muamuzi.Sikiliza Mikiki Mikiki hapo chini.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Picha na Muziki kwa niaba ya GetMziki.

chokinyotabc

Yupo mwanamuziki mmoja wa zamani kidogo aliwahi kuimba kwamba “wivu katika mapenzi ni lazima….japo kidooogo”. Alimaanisha kwamba wivu ni sehemu ya mapenzi ingawa pia aliashiria kwamba ukizidi unaweza kuwa kero na wakati mwingine kuleta balaa kabisa. Si ushasikia mtu kamchinja mwenzake kisa wivu?

Swali la kujiuliza ni je nini husababisha wivu? Ni kutojiamini,kupenda kumiliki kitu mwenyewe au ni kweli kwamba mapenzi ndio husababisha wivu?Na kama jibu ni ndio je hayo huwa mapenzi ya dhati au ndio tulivyo tu sisi wanadamu?

Huo ni upande mmoja.Upande wa pili ni kuhusu “mpenzi wa zamani”. Hivi watu wakishaachana bado huwa wanaachana kweli au huwa wanapeana nafasi? Na inakuwaje unapoona mpenzi wako wa sasa anaendeleza sana mawasiliano na mpenzi wake wa zamani? Ni sababu tosha ya kuwa na wivu?

Ali Choki akishirikiana na msanii Nyota Ndogo anayetokea nchini Kenya maeneo ya Mombasa(Naamini unamkumbuka kutoka katika kibao chake Watu na Viatu) wanaimba kuhusu mambo ya wapenzi wa zamani na “wivu”. Mmoja anakuwa haelewi,wivu unamtatiza.Mwenzake anamwambia tulia,usiwe na papara wala wasi,hakuna kitu. Mwenzake anamsihi kwamba asimfiche na ndio maana wimbo unaitwa Usinifiche. Mimi najiuliza;akiambiwa ukweli ataweza kuhimili? Can he handle the truth? Usikilize wimbo Usinifiche kwa kubonyeza player hapo chini.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

blu3-new-1

Wanaitwa Blue 3.Wanatokea nchini Uganda.Ni miongoni mwa makundi ya muziki yanayofanya vizuri katika anga za burudani na muziki katika ukanda wa Afrika Mashariki.Mara nyingi wamekuwa wakitoa burudani safi katika matamasha mbalimbali yanayofanyikia Afrika Mashariki ikiwemo hivi karibuni walipoalikwa kwenye utoaji wa tuzo za Kili.Nawatafuta kujua kwanini wanajiita Blue 3. Why Blue?

frankbcNiliwahi kusikia mahali fulani watu wa nchi jirani na Tanzania wakisema kwamba Tanzania huwa inachelewa kidogo kuanza mambo lakini pindi wanapoanza huwa wanakuja juu kwa kasi ya ajabu! Bila kuingilia mazungumzo yao,jamaa wakawa wanataja mifano kama vile jinsi ambavyo Tanzania imepiga hatua kwenye shughuli za kisanii kama vile muziki na hivi sasa filamu.

Kuna ukweli ndani yake; tunaweza kuanza mwisho lakini tukawa vinara. Yote inategemea jinsi ambavyo tunaamua kujiweka na kusonga mbele. Mojawapo ni kukubali kwamba kuna kukosea na pia kujirekebisha. Hivi sasa sanaa ya filamu inazidi kukua nchini Tanzania. Inatia moyo sana kuona watu wa mataifa mengine wanaangalia filamu ambazo zinaitwa “za kibongo”. 

Pamoja na hayo kazi kubwa bado ipo mbeleni.Kama alivyowahi kusema Steven Kanumba tulipohojiana naye,kuna haja ya serikali kutoa support ya kutosha ili kuzidi kuinua sanaa hiyo. Marekani ipo hapo ilipo kwa sababu ilitangaza sanaa na sera zake za mambo ya nje kupitia kwenye filamu. Ikulu ya Marekani ina kitengo cha kushughulikia masuala ya filamu.Kama filamu itaonekana haijakaa “vizuri” kwa mujibu wa taratibu zao,basi haitoki.Mradi unakufa.

Lingine ni hili ambalo muigizaji Mohamed Mwikongi(pichani) almaarufu kama Frank katika uigizaji ameliongelea majuzi alipofanya mahojiano na jamaa wa Global Publishers. Frank anasema lazima wasanii na washika dau wote katika nyanja za filamu wakubali kukosolewa. Wazungu wanaita hii constructive criticism. Unapokubali kukosolewa unajipa nafasi ya ushindi kwani maana yake ni kwamba kesho utafanya kizuri zaidi.Lakini pia ipo haja ya wakosoaji kutokuwa “wabezaji”. Unapokosoa basi useme pia sababu zako na utoe ushauri wa kujenga kwamba nini kifanyike.Kwa mwendo huo filamu za kibongo zitazidi kupata jina na sio ajabu kabisa siku moja nasi tukaona Slumdog Millionare za kikwetu.

 

Kwa njia tofauti,katika nyakati tofauti,Raisi wa Kenya,Mwai Kibaki na mkewe Lucy Muthoni Kibaki wameongelewa sana katika vyombo mbalimbali vya habari ulimwenguni.Sote tunajua kwamba hivi karibuni jina la Mwai Kibaki lilitawala katika vyombo vya habari baada ya “muujiza’ wa uchaguzi wa Kenya.Lakini unajua kwanini Lucy Muthoni Kibaki ni mmojawapo miongoni mwa “First Ladies” wa Afrika wenye umaarufu wa kipekee pekee hivi?Unaweza kupata dalili kwa kubonyeza hapa.

BC inakutakia siku njema ya wajinga duniani.Kuwa makini leo,its April’s Fools Day.

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page