Home Balozi

Category: Balozi

Post

BALOZI KALLAGHE AKARIBISHWA RASMI NA BRITAIN-TANZANIA SOCIETY

Balozi Peter Kallaghe bado ni mgeni nchini Uingereza. Kwa maana hiyo ndio kwanza yupo katika ziara mbalimbali za kuwatembelea watanzania,washika dau mbalimbali nchini humo.Pia bado yupo katika kipindi cha kukaribishwa rasmi na wanajumuiya mbalimbali. Hapo majuzi,ilikuwa ni zamu ya Britain-Tanzania Society kumkaribisha.Britain-Tanzania Society au kifupi BTS ni jumuiya yenye lengo la kudumisha ubadilishanaji wa maarifa,maelewano...

Post

BC EXCLUSIVE: AN INTERVIEW WITH AMBASSADOR PETER KALLAGHE

Miezi michache iliyopita, Rais Jakaya Kikwete, alifanya mabadiliko na teuzi kadhaa za mabalozi wetu katika nchi mbalimbali. Miongoni mwa mabadiliko hayo ni pamoja na yale ya kumhamisha Balozi Peter A.Kallaghe kutoka nchini Canada kwenda kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Uingereza. Wakati akijiandaa kuondoka nchini Canada kuelekea katika kituo chake kipya cha kazi nchini Uingereza,BC...

Post

MALAMBUGI ATEULIWA KUWA BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI BRAZIL

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete amemteua Balozi Francis Malambugi(pichani) kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Brazil . Uteuzi wa Balozi Malambugi umetokana na na kuteuliwa hivi karibuni kwa aliyekuwa Balozi wa nchi hiyo Balozi Daktari Joram Mkama Biswaro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na kwenye Umoja wa Afrika. Balozi...

Post

SIKU BALOZI CISCO MTIRO ALIPOWAKILISHA HATI ZAKE

Unapotaja jina la Balozi Cisco Mtiro bila shaka watu tisa kati ya kumi wanamtambua vyema. Hivi karibuni(kama inavyoonekana pichani) aliwakilisha hati zake za utambulisho wa kibalozi kwa Rais Gloria Aroyo wa Phillipines huko katika ikulu ya Phillipines jijini Manila. Balozi Cisco Mtiro ndio mwakilishi(balozi) wetu katika nchi za Malaysia, Phillipines, Cambodia,Singapore na Laos. Picha na...

Post

KOFFI YUPO DAR,ATEMBELEA RADIO YA WATU

Mwanamuziki maarufu kutoka DRC,Koffi Charles Olomide yupo nchini Tanzania kwa ziara ya siku mbili akiwa kama Balozi  maalumu chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto, UNICEF.Katika ziara hiyo Koffi atatembelea sehemu mbalimbali ukiwemo mji wa kihistoria wa Bagamoyo hapo kesho. Leo hii,kama inavyoonekana pichani,alitembelea kituo cha radio cha Clouds FM(Radio ya...

Post

KELLY ROWLAND NDANI YA BONGO

Bila shaka utakuwa bado unalikumbuka kundi maarufu la muziki lililokuwa linajulikana kama Destiny’s Child kutoka nchini Marekani. Miongoni mwa mabinti waliokuwa wanaunda kundi hilo ni Kelly Rowland(pichani).Wenzake walikuwa ni Beyonce Knowles(mke wa Jay Z hivi sasa) na Michelle Williams. Kundi hilo lilivunjika rasmi mwaka 2005 ingawa mara moja moja bado huwa inatokea wakafanya maonyesho pamoja....

Post

BALOZI MWANAIDI SINARE MAAJAR

Pichani ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar.Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza kwa kushirikiana na Jumuiya ya Watanzania nchini humo,hivi karibuni uliandaa mkutano/au kongamano lililoitwa Tanzania Diaspora jambo ambalo limechukuliwa na wengi kama mfano wa kuigwa na balozi zingine za Tanzania duniani. Tovuti ya Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza unaweza kuitembelea kwa...

Post

BALOZI PETER KALLAGHE

Tunaendelea na mfululizo wetu wa mabalozi wa Tanzania nchi za nje.Pichani ni Balozi Peter Kallaghe, balozi wa Tanzania nchini Canada. Kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada, Peter Kallaghe alikuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Habari -Ikulu Tanzania. Ukitaka kutembelea tovuti ya Ubalozi wa Tanzania nchini Canada bonyeza hapa. Share on: WhatsApp

  • 1
  • 2