
Takribani mwezi mmoja ujao,Tanganyika(Tanzania Bara) kutakuwa na shangwe na vifijo kusheherekea miaka 50 ya kujitawala wenyewe(unapojitawala unaweza kujisimamisha au kujiangusha). Kauli mbiu ambayo inaongoza maandalizi ya kuelekea kwenye kilele cha sherehe hizo za kujitawala ni Tumethubutu,Tumeweza na Tunasonga Mbele.
Kwa sababu ambazo bado nazitafutia mantiki, kauli mbiu hiyo ndiyo iliyonijia mara nilipomaliza kusikiliza wimbo mpya kutoka kwa MwanaFA(jina halisi Hamisi Mwinjuma) unaokwenda kwa jina Yalaiti. Ni lazima kwanza uthubutu kisha uweze, ujiwezeshe au uwezeshwe ndipo utakapokuwa na moyo wa kusonga mbele.
Katika wimbo huu MwanaFA amemshirikisha mwanadada Linah ambaye sio tu anaitendea haki vilivyo chorus ya wimbo huo bali anatukumbusha ipasavyo kuhusu mwimbaji maarufu wa taarab aliyewahi kutokea.Namzungumzia Sitti Binti Saad kutoka Visiwani Zanzibar.Linah amenifanya nijiulize mara mbili mbili kwamba kwanini binti huyu asiimbe pia muziki wa mwambao? I believe she can!
Baadaye nilimtafuta MwanaFA nikitaka kujua kwanini akaamua ku-sample muziki huu wa Sitti Binti Saad? FA akanijibu
Because I wanted to keep the good music alive na huo ni miongoni mwa nyimbo nzuri kabisa nilizokuwa nazisikia wakati nakua.
I couldn’t agree more MwanaFA.It Is a good music and I am glad you are keeping it alive! Kama nilivyosema hapo mwanzo,umethubutu,umeweza na lazima usonge mbele.Natumaini more stuff like this are on the way.
Wimbo huu umekuwa produced na Marco Chali pale MJ Records.Sikiliza Yalaiti
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Kama utakumbuka wiki kadhaa zilizopita tulikuletea picha kadhaa toka katika location ya making of “Nitarejea” Video by Diamond. The official video is out and here it is for your enjoyment;

Bila ubishi Inspekta Haruni ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Flava ambao wanastahili na wana haki kabisa ya kujiweka katika lile kundi la “wakongwe katika fani”.Pia Inspekta anadumu katika lile kundi la “wataalamu wa vina(mashairi) na tunzi ambazo baada ya kutoka hewani hugeuka zikawa misemo ya mitaani.
Kama hukubaliani name,basi jaribu kuusikiliza kwanza wimbo mpya kutoka kwa Inspekta unaokwenda kwa jina la Haina Ngwasu kwa kubonyeza player hapo chini.
Na kama jadi mpya ya wasanii wa bongo flava mashairi ya wimbo huu yanaelekea kuwa “ujumbe” kwenda kwa mtu fulani au watu fulani?Mawazo yangu.Sikiliza na wewe utuambie.Pata burudani.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Photo/Ahmad Michuzi

Everybody deserves a second chance!Bila shaka ushawahi kusikia msemo huo.Ni kweli kabisa na ni haki.Hali hiyo ndiyo iliyothibitika hivi karibuni kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed ‘TID’ (kulia katika picha)pale alipopanda jukwaani kuungana na wana Twanga Pepeta wakati wa onyesho maalumu la usiku wa Zain ndani ya ukumbi wa Mango Garden jijini Dar-es-salaam.Ilionekana wazi kwamba watu walikuwa wamemmiss TID na pia kwamba wapo tayari kumpokea na kumpa tena nafasi kama mwanajamii.
Noti uionayo kwenye paji la uso la TID alituzwa na rapa wa Twanga Pepeta Saulo John “Ferguson”.
Photo/Michuzi.

Bila shaka unalikumbuka kundi maarufu la Hard Blasterz Crew(HBC).Hilo ni mojawapo ya makundi ambayo tunaweza kabisa kusema yalichangia kwa kiasi kikubwa kuuweka muziki wa kizazi kipya hapo ulipo.Sasa kuna habari njema ambazo zimeripotiwa na Full Shangwe kwamba huenda mwaka 2009 ukashuhudia kurudi kwa kundi hilo baada ya miaka kadhaa kutokuwepo hewani ingawa mwenzao Prof.Jay aliendelea na game kwa muda wote huu.
Kundi lile lilikuwa linaundwa na Joseph Haule aka Prof.Jay,Willy Shundi aka Big Willy na Terry aka Fanani lilikuwa na makazi yake maeneo ya Upanga jijini Dar-es-salaam.Tunawatakia kila la heri HardBlasterz.BC itaendelea kufuatilia maendeleo ya kuundwa upya kwa kundi hilo.
Pichani juu kutoka kushoto ni Big Willy,katikati ni Profesa Jay na kulia ni DJ Choka ambaye ni mmojawapo miongoni mwa producers wanaotarajiwa kuwatoa upya HBC.Kwa undani wa habari unaweza kubonyeza hapa.

Steve B,miongoni mwa DJs mahiri nchini Tanzania hivi sasa.Tukikukuuliza nani unamchukulia kuwa DJ bora nchini Tanzania,hivi sasa au hapo zamani utamtaja nani?Wa kituo gani cha redio au club gani?Kwanini?

MSANII wa muziki wa kizazi nchini Khalid Mohammed ‘maarufu kama TID’ aliyekuwa akitumikia kifungo cha mwaka mmoja katika gereza la Segerea, jana aliachiwa huru kupitia msamaha kwa wafungwa uliotolewa na Rais Kikwete katika maadhimisho ya miaka 47 ya Uhuru.Kwa habari zaidi bonyeza hapa.
Mara kwa mara tumekuwa tukipata e-mails kutoka kwa watu wanaouliza au kutaka kujua kama kuna radio za kibongo ambazo zinapatikana mtandaoni(online).Kwa bahati nzuri jibu tulilonalo ni kwamba kwa upande wa radio za burudani radio pekee ya kibongo inayopatikana mtandaoni 24/7 ni Bongo Radio.
Kwa hiyo kama unataka kuburudika na Bongo Flava,Zilipendwa,Muziki wa dansi na muziki wa kiafrika kwa ujumla huku ukiendelea na kazi zako,basi Bongo Radio ndio jibu lako.Bonyeza hapa kuitembelea Bongo Radio.
Kimsingi Tanzania tupo nyuma kidogo katika uwanja huu wa radio ambazo zinapatikana pia mtandaoni.Tatizo sijui liko wapi kwa kweli.Sio mbaya kama radio zingine za kibongo kama vile Clouds FM,Radio One,Times FM nk nazo zikaangalia uwezekano wa kuwepo mtandaoni pia kwa maana ya kusikika mtandaoni.
**Kama kuna mtu anazifahamu radio zingine za kibongo zilizopo mtandaoni tafadhali tujulishe.

Mtakumbuka kwamba Top in Dar(TID) au kwa jina halisi Khalid Mohamed,miezi michache iliyopita alihukumiwa kwenda jela mwaka mmoja kwa kosa la kushambulia na kujeruhi.
Habari zinapasha kwamba TID amekata rufaa kutokana na hukumu hiyo.Pichani ni jana alipokuwa akiwasili mahakama kuu jijini Dar-es-salaam kueleza nia ya kukata rufaa hiyo.
Picha kwa hisani ya Bongo Pix.


sending...