Home Bongo Fleva

Category: Bongo Fleva

Post
Hata Sielewi Lakini Naamini Unahitaji Kuiona Hii Video

Hata Sielewi Lakini Naamini Unahitaji Kuiona Hii Video

Huku nikiwa tayari nimeanza kuweka sawa orodha ya Nyimbo 20 Bora Na Zilizotamba Zaidi Kutoka TZ, MwanaFA akishirikiana na Maua Sama yaelekea hawana mpango wa kunirahisishia kazi. Hata Sielewi kwanini wanafanya hivi. Nyimbo 20 (Top 20 Songs) Nilizozipenda Zaidi Kutoka Tanzania Mwaka 2016 Mapema hivi leo hashtag #HataSielewi ilitawala mitandao ya kijamii. Kwangu ilikuwa miongoni...

Post
Listen N’Download: “Usmart”- Dii Mavoice (BrAnD New)

Listen N’Download: “Usmart”- Dii Mavoice (BrAnD New)

Umaridadi huficha umasikini. Neno ni “huficha”. Hauondoi umasikini au ufukara. Lakini kwa sababu kila mtu ana siri yake moyoni, na wewe unabaki na ya kwako. Unaruhusiwa. Dii Mavoice anaelekea kuunga mkono hoja hii. Anasema kuwa smart. Hakuna atakayejua yaliyoko moyoni au kichwani kwako. Dii Mavoice anaelekea kuwa na maudhui fulani ambayo unaweza kuyafananisha na yale...

Post
“Naogopa”-Q Chilla (Official Release-NeW)

“Naogopa”-Q Chilla (Official Release-NeW)

Tukisema tuongelee wanamuziki wenye vipaji vya kweli vya kuimba nchini Tanzania, hakuna shaka kwamba Q Chilla hatuwezi kumuweka kando. Zamani aliitwa Q-Chief na uwezo wake ulikubalika na pengine kusaidia sana kuisukuma mbele sanaa ya muziki wa kizazi kipya. Lakini pamoja na kipaji, Q Chilla amepitia mengi. Ameanguka.Akasimama. Akaketi na kisha kuamka tena. Ujana umempeleka kwingi....

Post
“Wale Wale”-Shetta (Latest)

“Wale Wale”-Shetta (Latest)

When I first met Shetta a couple of years ago, he was an underground artist.It was on location shooting a video for one of Professor Jay’s songs. At the time, I was managing Jizze. Shetta is one of Professor Jay’s protegĂ©s. He grew up watching him and wanted to walk in the same line.He was...

Post
Tizama: “Atabadilika”-Lameck Ditto (Video Rasmi)

Tizama: “Atabadilika”-Lameck Ditto (Video Rasmi)

Kama umewahi kupenda, unajua maana ya “kubadilika”. Alivyoanza sivyo alivyo. Alichosema ukikikumbuka unashikwa na butwaa. Akili inapwaya kama vazi lisilo lako. Lakini bila shaka unajua pia kwamba kwenye mapenzi kuna kukingiana kifua. Unatetea. Unamtetea japo unajua sio kweli. Unafanya hivyo ukiamini atabadilika. Unaamini atakuja kuketi na kubadili mwelekeo. Lakini utamtetea mpaka lini? Mara ngapi? Nahisi...

Post
“Sina Kinyongo”-Salum Simba “Twaha” (BrAnD New)

“Sina Kinyongo”-Salum Simba “Twaha” (BrAnD New)

Kuna mwanamuziki aliwahi kuimba penzi la kweli halikosi wivu. Na mwingine akasema penzi ni kama kikohozi.Huwezi kukificha. Katika wivu na mapenzi, panaweza kujitokeza kinyongo. Kwenye vinyongo kuna visasi. Waliokuwa wakipendana kama chanda na pete, hawaelewani tena. Ni paka na chui. Wanafanana lakini hawapikiki chungu kimoja. Naam. Salum Simba almaarufu kama Twaha, ndio kwanza anaianza safari...

Post
“Wapo”-Ney Wa Mitego | Na Maoni Yangu

“Wapo”-Ney Wa Mitego | Na Maoni Yangu

Siku hizi kila kukicha kuna tukio au matukio ambayo huvuta hisia. Ni kweli. Viongozi wamebakia kuwa washindania habari za kurasa za mbele. Mbaya zaidi wanatabirika. Hata mtu asiye mnajimu anaweza kuwatabiri. Kuna matamko mengi kuliko ya Agano la Kale. Wiki iliyopita, msanii Ney Wa Mitego aliachia wimbo “Wapo”. Utabiri haukuwa mgumu. Ney atakamatwa. Amekashfu. Kakashfu...