MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Lisemwalo lipo,kama halipo laja.Msemo wa kwetu huo.Baada ya kuvuma kwa tetesi nyingi kwamba mwanamuziki maarufu,mzaliwa wa Haiti,Wcylef Jean,anatarajia kugombea Urais wa Haiti,hatimaye habari hizo leo zimethibitishwa baada ya mwanamuziki huyo kurudisha rasmi fomu za kuomba kupitishwa kugombea nafasi hiyo nyeti.

Huffington Post wanayo habari kamili.

Mcheki hapo chini katika wimbo wake maarufu “If I was A President”.Bila shaka wimbo huu sasa utapigwa na kuimbwa zaidi na zaidi baada ya mjuzi huyo kutangaza nia.

Wyclef anaongoza shirika lisilo la kiserikali linaloitwa Yele Haiti.Bonyeza hapa kuona mengine zaidi kuhusu shirika hilo,kazi zake nk.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Photo Credit.Ajani.ca

Washiriki wa shindano la mwaka huu la Big Brother Africa ndio wameanza kutajwa muda mfupi uliopita na Mwisho Mwampamba ambaye alishiriki shindano hilo mwaka 2003(Big Brother 1) na kuibuka mshindi wa pili ndiye mwakilishi wa Tanzania! Mwisho ndiye housemate wa kwanza kuingia ndani ya jumba la Big Brother.

Kwa ujumla washiriki wote wa mwaka huu,waliwahi kushiriki shindano hilo siku za nyuma na ndio maana limeitwa BBA All-star.Wengine waliorudi ni Paloma kutoka Zambia(Big Brother Africa 4),Jen kutoka Msumbiji(Mozambique) aliyeshiriki Big Brother Africa 4, Munya kutoka Zimbabwe(Big Brother Africa 4),Yacob kutoka Ethiopia(Big Brother Africa 4),Sheila kutoka Kenya(Big Brother Africa 3),Sammy kutoka Ghana(Big Brother Africa 1),Kaone kutoka Botswana(Big Brother Africa 4),Meryl kutoka Namibia(Big Brother Africa 2),Uti kutoka Nigeria(Big Brother Africa 3),Lerato kutoka South Africa(Big Brother Africa 2),Hannington kutoka Uganda(Big Brother Africa 4),Tatiana kutoka Angola(Big Brother Africa 2) na Code kutoka Malawi(Big Brother Africa 2)

Mhadhiri mshiriki wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa Jwani Timothy Mwaikusa, mpwawe na jirani yake wameuawa na majambazi usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake maeneo ya Salasala jijini Dar-es-salaam.

Sambamba na mauaji ya Profesa Mwaikusa, majambazi hayo pia yaliua mtoto aliyekuwamo ndani ya nyumba ya Profesa huyo, Gwamaka Daudi na jirani John Mtui.

Polisi wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa jirani huyo ambaye alikuwa na bastola aliuawa alipokuwa akienda kutoa msaada kwa Profesa huyo.

Jumuia ya wafanyakazi na wanafunzi wa UDSM walikumbwa na simanzi kuu leo baada ya kupokea taarifa hizo ingawa wanafunzi walikuwa wakiendelea na mitihani ya kumaliza mwaka.

Mkuu wa Kitivo cha Sheria(Faculty of Law) Chuoni hapo Profesa Palamagamba Kabudi, alisema kifo cha Profesa Mwaikusa siyo tuu pigo kwa chuo hicho bali tasnia nzima ya sheria na taifa kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Profesa Kabudi, mpaka wakati kifo kinamkuta Profesa Mwaikusa alikuwa, Profesa Mshiriki katika idara ya Sheria za Umma (Public Law).

Alisema Profesa Mwaikusa alizaliwa Julai 21 mwaka 1952, na kuwa aliajiriwa kama mhadhiri msaidizi na chuo hicho mwaka 1986. Alisomea sekondari ya Mirambo, Tabora.

Career:

* Professor of Law, Faculty of Law, University of Dar es Salaam 1999
* Mkono & Co Advocates since 1998
* Advocate, High Court of Tanzania since 1988
* Managing Editor of the Tanzania Law Reports.

Qualifications:

* Ph.D., School of Oriental & African Studies, University of London, UK, 1995
* LL.M, University of Birmingham, UK, 1985
* LL.B (Hons), University of Dar es Salaam, Tanzania, 1981.


Chama cha Mapinduzi(CCM) leo kimemchagua rasmi Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mgombea wake katika Uchaguzi Mkuu mwezi Octoba mwaka huu.

Baada ya mashauriano na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Rais Kikwete amemteua Dr.Mohammed Gharib Bilal, kuwa mgombea mwenza.Kwa maana hiyo tiketi ya CCM itabebwa na Jakaya Mrisho Kikwete na Dr.Mohammed Gharib Bilal.

Dr.Gharib Bilal alizaliwa tarehe 6 Februari,1945 huko Unguja. Dr.Bilal ni mwanasayansi aliyepata stashahada ya kwanza katika sayansi ya nuklia kutoka Chuo Kikuu cha Howard nchini Marekani mwaka 1967. Alipata Masters Degree katika masuala hayo hayo ya sayansi ya nuklia kutoka Chuo Kikuu Cha California mwaka 1969 kabla ya kupata PhD katika fizikia kutoka chuo hicho hicho cha California mwaka 1976. Kuanzia mwaka 1976 mpaka mwaka 1990 alikuwa Lecturer(mkufunzi) katika Chuo Kikuu Cha Dar-es-salaam-Idara ya Fizikia

Kati ya mwaka 1990 na 1995 alikuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Sayansi,Tekinolojia na Elimu ya Juu katika serikali ya Muungano.Mwaka 1982 alikuwa Mkuu wa Kitivo Cha Sayansi,Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam.

Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, aliteuliwa na Rais Salmin Amour kuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar. Mwaka 2000 aligombea Urais wa Zanzibar bila mafanikio. Mwaka huu alikuwemo miongoni mwa waliojitokeza kuomba ridhaa ya CCM kusimama kama mgombea Urais Zanzibar lakini bahati hiyo ikamuangukia Dr.Ali Mohammed Shein.Badala yake na kwa maana hii,atasimama na Kikwete kama mgombea mwenza na hivyo,endapo watashinda,atakuwa Makamu wa Rais wa serikali ya Muungano.

Photo/Francis Godwin

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Marekani,Al Gore,ametangaza kutengana na mke wake, Mary Elizabeth “Tipper” Gore, baada ya miaka 40 ya ndoa!

Kwa mujibu wa barua pepe waliyowatumia marafiki zao na baadaye kuthibitishwa na msemaji mkuu wa Al-Gore,Kalee Kreider, wanandoa hao ambao wiki kama mbili zilizopita walisheherekea miaka 40 ya ndoa yao,kwa pamoja wamesema wamefikia uamuzi wa kuifikisha mwisho ndoa yao baada ya mlolongo mrefu wa majadiliano baina yao.Hawakutoa maelezo zaidi na wameomba watu wote kuheshimu maamuzi na faragha yao.

Al Gore, mshindi wa Tuzo ya Nobel,ambaye watu wengi wanaamini alipokwa ushindi wa kiti cha urais na George W.Bush mwaka 2000, alikutana na mkewe tangu wakiwa shule ya sekondari. Walioana tarehe 19,Mei mwaka 1970 huko Washington,DC. Wana watoto wanne wakubwa.

Ama kweli aliyesema kwamba ndoa sio mchezo wa kuigiza bila shaka alikuwa na mantiki.

Habari ambazo tumezipata hivi punde zinaeleza kwamba mwigizaji na mchekeshaji maarufu nchini Marekani, Gary Coleman, amefariki dunia katika kituo cha Afya kiitwacho  Utah Valley Regional Medical Center huko Provo,Utah nchini Marekani.

Gary Coleman ambaye alijizolea umaarufu tangu alipoanza kuigiza akiwa bado mtoto, amefariki kutokana na ugonjwa wa ini.Alijipatia umaarufu zaidi katika sitcom iliyokwenda kwa jina Different Strokes.Humo aliigiza kama Arnold Jackson, mtoto mtundu(mweusi) ambaye amekuwa adopted na familia ya wazungu matajiri wa Manhattan,New York.

Muigizaji huyo  alizaliwa huko Zion,Illinois tarehe 8 February 1968. Amefariki akiwa na umri wa miaka 42. Ameacha mke,Shannon Price,aliyefunga naye ndoa miaka miwili iliyopita. Rest in Peace Gary.What Are You Talking About Willis?

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Msanii maarufu wa vipindi vya redio,maarufu kama Mzee Pwagu(jina lake halisi ni Rajab Kibwana Hatia),amefariki dunia hivi leo katika Hospitali ya Amana jijini Dar-es-salaam alipokuwa amelazwa kwa muda,akisumbuliwa na ugonjwa wa kwikwi(hiccups) pamoja na matatizo mengine yatokanayo na uzee.

Kama utakumbuka, kabla ya ujio wa televisheni au luninga nchini Tanzania kila mtu alikuwa akitegemea Radio Tanzania Dar-es-salaam(RTD) katika kupata habari,burudani na elimu kupitia sanaa ya kuigiza kupitia kitu kilichojulikana kama “michezo ya redio”. Hapo ndipo vipindi kama vya Pwagu na Pwaguzi vilipotamba.

Kipindi cha Pwagu na Pwaguzi kilikuwa kinarushwa hewani hewani kila Jumamosi kuanzia saa 11:45 hadi 12;00 jioni na Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) tangu mwaka 1966 mpaka miaka ya 1980.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kikundi cha Sanaa cha Kaole ambapo marehemu alikuwa mwanachama(kama mshauri) mpaka alipofariki, mazishi yanaweza yakafanyika kesho. Shughuli zote za msiba zinafanyikia nyumbani kwake maeneo ya Kigogo Mbuyuni jijini Dar-es-salaam.

Mzee Pwagu alizaliwa mwaka 1923 mjini Tabora. Ameacha mke na watoto wawili. Mmoja kati ya watoto wake ndiye mama mzazi wa msanii chipukizi Abdul Ahmad Salum maarufu kwa jina la Mr Benny wa kundi la Sanaa la Kaole.

Mwenzake,Pwaguzi, ambaye jina lake kamili ni Ali Said Keto,naye alishafariki dunia miaka kadhaa iliyopita.

MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI,AMINA.

Picha na sehemu za habari/Habari Leo Ukitaka kujikumbusha kidogo mchezo wa Pwagu na Pwaguzi,Bonyeza hapa.

Rais wa Nigeria, Umaru Yar’Adua(pichani) amefariki dunia. Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari likiwemo Shirika La Habari la Uingereza(BBC), Rais Yar’Adua amefariki dunia leo hii huko katika mji wa Abuja ambao ndio mjii wa Nigeria. Alikuwa na umri wa miaka 58.

Rais Yar’Adua amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu hali iliyopelekea aliyekuwa makamu wake, Goodluck Jonathan kukabidhiwa madaraka na Bunge la nchi hiyo  ili kunusuru mgogoro mkubwa wa kisiasa uliokuwa unanukia katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi yenye watu wengi kupita zote barani Afrika. Nigeria ina jumla ya watu wanaokadiriwa kufikia milioni 150.

Rais huyo ambaye aliingia madarakani mwaka 2007 ndiye Rais pekee wa nchi hiyo ambaye aliweka wazi mali alizonazo pindi alipoingia madarakani ikiwa ni ishara ya uadilifu na upingaji wa ufisadi.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.Amin.

123Kawawa

Mzee Rashid Mfaume Kawawa,amefariki! Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari zikiwemo blogs,Mzee Kawawa amefikwa na mauti katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili ambako alikuwa amelazwa.

Rashid Mfaume Kawawa alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza nchini Tanzania na baadaye kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi.Alizaliwa mwaka 1926 katika kijiji cha Matepwende Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Tanzania. Alianza elimu ya Msingi huko Liwale -Lindi mnamo 19411942 na kuendelea na masomo ya sekondari katika shule ya Dar es Salaam Secondary School.

Ni hivi karibuni tu Mzee Kawawa alizindua kitabu kinachoelezea maisha yake.

Kawawa12

Majuzi Rais Kikwete na mkewe Salma Kikwete,walikwenda Muhimbili kumuona Mzee Kawawa.Laiti wangelijua kwamba hawatomuona tena Mzee Kawawa akiwa hai!

Kwa mujibu wa ratiba ya mazishi ambayo imetolewa,Mzee Rashid Mfaume Kawawa anatarajia kuzikwa Jumamosi nyumbani kwake Madale nje kidogo ya jiji la Dar-es-salaam.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Mwili wa marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa ukitolewa katika hospitali ya rufaa ya Muhimbili kwenda kuhifadhiwa katika hospitali ya jeshi ya Lugalo.Anayesikika akilia kwa uchungu ni mkewe Asina Kawawa.

KawawaEnzi

Rashid Mfaume Kawawa enzi za ujana wake.

KawawaMuungano

Utumishi wa Mzee Rashid Mfaume Kawawa kwa taifa letu ni wa siku nyingi.Pichani kulia anaonekana akishuhudia Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akichanganya michanga ya ardhi ya Tanganyika na Zanzibar kuashiria Muungano.Hiyo ilikuwa ni mwaka 1964

KIMDJ mkongwe na maarufu nchini Tanzania,DJ Young Kim, amefariki dunia. Kwa mujibu wa blog ya Issa Michuzi, DJ Kim amefariki dunia akiwa katika hospitali moja ya binafsi inayojishughulisha zaidi na tiba za magonjwa ya moyo iliyopo Manzese jijini Dar-es-salaam.

DJ Young Kim ni miongoni mwa DJs waliochangia sana maendeleo ya disco na mashindano ya kucheza muziki(disco) ambapo ndipo yalipoibuka majina maarufu katika muziki kama vile Black Moses(RIP),Ommy Sidney,Othman DigaDiga na wengine wengi.

Pia kwa wale ambao wanafuatilia chimbuko la muziki ambao leo hii tunauita wa kizazi kipya,mchango wa DJ Kim kupitia mashindano ya Yo Rap Bonanza ,ulikuwa ni chachu muhimu katika mwanzo au mwendelezo wa muziki wa hip hop nchini Tanzania.Pumzika kwa amani DJ Young Kim.

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page