MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Sijui kama nitakuwa nimekosea nikisema kwamba pengine AY na MwanaFA mpaka hivi sasa wanaweza kuwa wanashikilia rekodi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao wameshirikiana zaidi katika kazi zao.Kumbuka hawa wametoka mbali tangu enzi zao wakiwa East Coast Team iliyokuwa ikiongozwa na King Crazy GK ambaye sina uhakika yuko wapi siku hizi na anafanya shughuli gani.

Kuthibitisha kuzidi kukomaa kwa ushirikiano wao,AY na MwanaFA wakimshirikisha Hard Mad,wameachia single inayokwenda kwa jina Dakika Moja. Hii ni production kutoka B’Hitz Production iliyo chini ya Hermy B.

Sikiliza hapo chini;Ujumbe ni kwamba anaomba dakika moja tu aseme yaliyopo moyoni.Mmh,inawezekana kweli ndani ya dakika moja kikaeleweka?Sijui.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Zahir Zorro

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

A couple of months ago, a friend asked me if I could come up with at least 100 songs that I consider to be most inspirational and motivational. This friend knows that I love music than a sleep. In fact, I have never imagined how the world could be without music. I have always said that there are three things that I run into whenever I feel like the skies are yellow and not blue; God, Family and Music!

However, I don’t love just any music even though I listen or could say I have listened to all genres of music available out there. I love music with lyrics that bears a message. It being good or evil, it gotta have a “message”. Of course, at the end of the day, I tend to stick with the ones that motivate and inspires.

I have therefore compiled a list of 120 songs that I consider to be both inspirational and motivational. I have already shared this list with a friend who asked and thought it’s not a bad idea if I share the same with you. I know some of you are also music fanatics.

These are the songs that keep me going even when things seem to get almost too tough to handle. Whenever I need to hear a voice different from the one from Heaven that tomorrow could be better, I tune in and listen to some of them.

Now before you start examining my list, please allow me to say this; I appreciate the fact that everyone will have their favorites and if none of the above is inspirational songs or motivational song, in your point of view, please accept my deepest regrets! This list is in random order. The numbers don’t have much meaning. Feel free to add some of your favorites through the comments section. I am planning to review this list in a couple of months. I will be happy to add some of your recommendations. Enjoy;

  1. One Love/People Get Ready- Bob Marley & The Wailers
  2. Three Little Birds- Bob Marley & The Wailers
  3. Smile- 2Pac Shakur Ft. Scarface
  4. A Beautiful Day- India Arie
  5. Don’t Worry ‘Bout A Thing-Stevie Wonder
  6. What’s Going On-Marvin Gaye
  7. Keep Ya Head Up-2Pac Shakur
  8. Beautiful Day-U2
  9. Beat It-Michael Jackson
  10. Beautiful Life-Ace of Base
  11. Sky Is The Limit- Notorious BIG Ft 112
  12. I Gotta A Feeling- Black Eyed Peas
  13. It’s My Life- Bon Jovi
  14. Soar- Christina Aguilera
  15. Keep Holding On-Avril Lavigne
  16. I Believe- Fantasia Barinno
  17. Sign Of Victory- R.Kelly
  18. You Gotta Be- Des’ree
  19. Redemption Song- Bob Marley
  20. Wind Beneath My Wings- Bette Midler
  21. Live Like You Were Dying-Tim McGraw
  22. Chariots Of Fire- Vangelis
  23. Win- Brian McKnight
  24. One Moment In Time-Whitney Houston
  25. When I Get Where I am Going-Brad Paisley Ft. Dolly Parton
  26. Unwritten- Natasha Bedingfield
  27. Walk On- U2
  28. True Colors- Cyndi Lauper
  29. Thugz Mansion- 2Pac Shakur
  30. Greatest Love Of All-Whitney Houston
  31. My Heart Will Go On- Celine Dion
  32. What A Feeling- Irene Cara
  33. Circle Of Life- Elton John
  34. That Is What Friends Are For- Dionne Warwick Ft Gladys Knight, Elton John and Stevie Wonder (more…)

Je,kuna siri ya watu wawili?Yawezekana.Haiwezekani.Ukishamwambia mtu mmoja sio siri tena!Kweli?

Ushawahi kuambiwa na mtu “hii ni siri,usimwambie mtu” au kwa kizungu “this is between you and me,don’t tell anyone”.Basi ni kwanini hakuna siri ya watu wawili?Ina maana katika watu wawili mmoja hawezi kukaa na kitu moyoni,asimwambie mtu?Ndivyo binadamu tulivyo?

Ninapoandika hapa,najaribu kuwaza kuhusu mambo mbalimbali ambayo niliwahi kuyafanya nikitegemea kwamba yangekuwa siri lakini yakageuka kuwa sio siri baada ya kuthubutu kumwambia mtu mmoja mwingine! Kwanini mtu yule au watu wale hawakuchukulia maanani maneno kama “hii naomba iwe siri baina yangu na wewe pekee,asijue mtu tafadhali”.Hivi ni kweli haiwezekani kutunza siri?

Maudhui hayo ndio yaliyopo kwenye Zilipendwa ya Ijumaa hii.Wimbo unaitwa Siri Yako kutoka kwao Bima Lee Orchestra. Burudika.Ijumaa Njema.Weekend Njema.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Unakumbuka Kisa Cha Mesenja Kuleta Balaa kutoka kwao hawa hawa Bima Lee?

Miaka kama miwili hivi iliyopita,wasanii wachache sana walikuwa wameshtukia kitu kinachoitwa ‘blogs”.Leo hii mambo ni tofauti.Badala ya kujiuliza msanii gani ana blog,tunajiuliza nani hana!Maendeleo.

Lakini wapo ambao walikuwa na blog tangu enzi hizo au kwa maneno mafupi,walizishtukia tangu hapo mwanzo.Miongoni mwa wasanii hao ni Ilunga Khalifa au maarufu kama CPwaa(pichani).Siku hizi anaitwa King of BongoCrunk.Hii hata kwangu ni mpya.Nimepitwa kidogo kuhusu “bongocrunk”.Ntamtafuta Cpwaa anijulishe zaidi. Enzi hizo CPwaa ambaye tunaweza kusema alikuwa msanii wa kwanza wa muziki wa kizazi kipya kuwa na blog,alikuwa akiblog kwa kutumia camera ya kwenye simu yake ya mkononi tu.Ilikuwa ni kitu kipya na nakumbuka tuliandika kuhusu wasanii na tekinolojia.

Sasa Cpwaa bado anaendeleza kusambaza ujumbe na kazi zake kwa kutumia tekinolojia za kisasa.Hivi karibuni ameifanyia marekebisho na matengenezo tovuti yake rasmi.Mtembelee.

Mambo vipi,shikamoo,marahaba,habari gani msomaji?Natumaini hujambo.Sisi hapa BC wote wazima kabisa.

Ijumaa ndiyo hiyo imewadia tena.Siku zinakwenda kama kimbunga cha nyikani.Lakini Ijumaa humaanisha burudani kupitia hapa BC.Ni wakti wa Zilipendwa.

Huu ni wakati wa kuenzi enzi ambazo,kama tungeendelea nazo,bila shaka leo hii nasi tungekuwa tuna midundo,sauti nk ambazo zikipigwa tu,kila mtu angejua huo ni mziki kutoka Tanzania. Si unajua leo hii ukisikia mdundo fulani tu unajua huo ni kutoka Afrika Kusini?Au ukisikia mdundo fulani unajua huo ni kutoka Ghana au Nigeria au Somalia?

Kuna watu ambao ni wagumu sana kuomba msamaha hata pale wanapokuwa wamekosea.Neno Samahani kwao ni kama jela.Akilitoa anahisi amepungukiwa akili hivi.Kuna ubaya gani kuomba msamaha unapokosea?Binadamu hatujakamilika.Tunakosea.Ni jukumu letu kuomba msamaha tunapokosea.

Maudhui hayo ndiyo yaliyopo katika wimbo wetu wa leo.Unaitwa Fikiri kutoka kwao DDC Mlimani Park Orchestra maarufu Sikinde.Pata Burudani.Weekend Njema.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page