MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Mwanamitindo maarufu ulimwenguni,Naomi Campbell,yaelekea akaingia matatani tena kwani hivi sasa polisi wa jijini New York nchini Marekani,wanamsaka!

Naomi,ambaye mwaka jana alitua nchini Tanzania na kushiriki katika onyesho la hisani kwa ajili ya akina mama, safari hii anatafutwa akikabiliwa na shutuma za kumchapa vibao dereva wake huko New York.

Mwanamitindo huyo ambaye inasemekana ni mpenda ugomvi sio mgeni na vyombo vya usalama.Siku za nyuma amekwisha kutwa na hatia ya kumpiga mfanyakazi wake wa ndani jijini New York, kumpa kibano msaidizi wake jijini Toronto na pia kumwangushia kisago polisi ndani ya ndege katika uwanja wa ndege wa Heathrow jijini London.Katika makosa yote hayo hapo juu,Naomi alikiri makosa yake na alihukumiwa kufanya kazi za kijamii(community services) kwa masaa zaidi ya 200.Kazi kweli kweli.Hivi kwanini kuna baadhi ya watu huwa wanadhani wanayo haki ya kuwaadhibisha watu wengine kiholela tu?Ni matunzo,jamii au?

NB:Hivi unajua Naomi Campbell alipokuwa mdogo alishiriki katika video ya Mfalme wa Reggae,Bob Marley katika wimbo One Love? Mtizame katika video hiyo hapo chini.Alikuwa na umri wa miaka 7 tu na hiyo ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kuwa katika spotlight.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Baada ya kimya cha takribani miezi mitatu tangu alipokumbwa na kashfa mfululizo juu ya mahusiano yake na “vimwana” nje ya ndoa yake,mcheza golf maarufu ulimwenguni,Tiger Woods, anatarajiwa kuonekana hadharani na kuzungumza na waandishi wa habari juu ya sakata lake.

Kwa mujibu wa wakala wake,Mark Steinberg, mchezaji huyo ataongea na kundi dogo tu la waandishi wa habari siku ya Ijumaa kutokea katika clubhouse ya TPC Sawgrass huko Ponte Vedra Beach jimboni Florida,yalipo makao makuu ya PGA Tour.

Tiger anatarajiwa kuongelea juu ya yaliyojiri,mipango yake ya sasa na baadaye na pia anatarajiwa kuomba msamaha(kwa kinywa chake mwenyewe) juu ya tabia zake. Tayari kuna hisia kwamba Tiger Woods ameamua kujitokeza na kuongea na waandishi wa habari siku hiyo,saa hizo, sio tu kwa sababu anataka kurudi uwanjani,bali pia kwa sababu anataka kuwakomoa waliokuwa wadhamini wake(Accenture) kwani katika muda huo kutakuwa na shindano lililodhaminiwa na Accenture liitwalo Accenture Match Play Championship kutokea Arizona.

Kwa kuongea na waandishi wa habari katika muda huo,matarajio ni kwamba macho na masikio(attention) vitaelekezwa kwake Tiger.Accenture walikuwa wadhamini wa kwanza kutangaza kumtema Tiger Woods mara tu sakata lake lilipoibuka.

Je hiyo ndio kusema Tiger Woods ameamua kurudi tena uwanjani baada ya hapo awali kutangaza kupitia mtandao wake kwamba anapumzika kucheza golf?

Kama nilivyokuahidi wiki kama mbili zilizopita,huu hapa ni wimbo,re-make ya We Are The World ambayo imefanywa na artists wanaotamba hivi sasa ikiwa ni miaka 25 baada ya We Are The World ya kwanza.

Kwa mtazamo wangu,pamoja na kwamba najumuika na walimwengu wote katika kuunga mkono juhudi kama hizi za wanadamu kusaidiana na pia ukweli kwamba wimbo huu haukutengenezwa kwa minajili ya kushindana bali kusaidia wenzetu wa Haiti,nadhani bado We Are The World original ilikuwa ni bomba zaidi! Naona kama vile zamani kulikuwa na waimbaji kuliko sasa.Kwa mtazamo wangu,auto-tune inapunguza vipaji.Wasanii wengi wa sasa wanajenga tabia ya kuwa tegemezi na vifaa vya studio kiasi kwamba linapokuja suala la kuimba bila vifaa hivyo,panakuwa na utata kidogo.Wewe unasemaje?

Itazame We Are The World original kwa kubonyeza hapa na kisha We Are The World-remake hapo chini

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Miongoni mwa matukio ya ki-muziki ambayo yataendelea kukumbukwa kwa muda mrefu ni pamoja na tukio la jumla ya wanamuziki 45 kukusanyika katika studio za Jim Henson za jijini Los Angeles mwaka 1985 na kutengeneza wimbo ulioitwa We Are The World ambao ulikuwa mahsusi kwa kuchangia fedha kwa ajili ya Afrika na hususani nchi ya Ethiopia ambayo ilikuwa imekumbwa na ukame wa kutisha kuanzia mwaka 1984-1985.Ulikuwa ni umoja na upendo wa aina yake waliouonyesha wanamuziki wale sio tu kwa bara la Afrika bali kwa taasisi nzima ya ubinadamu. Wanamuziki Lionel Richie na Michael Jackson(RIP) ndio walioandika wimbo ule ambao ulifanikiwa kuchangisha jumla ya dola milioni 30 zilizokwenda kusaidia waathirika wa ukame ule.

Katika kujaribu kurudia kile walichofanya superstars wa ulimwengu wa muziki takribani miaka 25 iliyopita, hapo juzi jumla ya wasanii 100 (wengi wao kutoka Marekani) ambao wanatamba hivi sasa katika muziki ulimwenguni,walikusanyika katika studio moja chini ya Producer yule yule aliyefyatua We Are The World ya mwaka 1985,Quincy Jones ili kuutengeneza upya wimbo wa We Are The World(remake of We Are The World). Lakini safari hii sio kwa ajili ya kuchangia Afrika bali ndugu zetu wa Haiti ambao kama unavyojua wiki chache zilizopita nchi yao ilipata tetemeko la ardhi ambalo linahofiwa kwamba lilichukua maisha ya jumla ya watu 200,000.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Original We Are The World.

Baadhi ya wanamuziki wenye majina makubwa ambao wamo katika We Are The World mpya ni pamoja na Wyclef Jean, Kanye West,Celine Dion,Jennifer Hudson,Miley Cyrus,Barbra Streisand,Tony Bennett,Jamie Foxx,Natalie Cole, Akon, Carlos Santana,Josh Groban,Justin Bieber(kijana wa miaka 15 raia wa Canada,alikuwa hajazaliwa huyu mwaka 1985), Snoop Dogg,Drake,LL Cool J na hata Rapper Lil Wayne ambaye anasema alidhani wanamtania alipoambiwa kwamba anahitajika “kuimba”.

Wengine ni kama vile Usher,Jonas Brothers,Pink, Gladys Knight,Wil.i.am,Brandy,Keri Hilson,Busta Rhymes,T-Pain,Robin Thicke,Trey Songz,Adam Levine,Tyrese na wengine kibao.Nitaendelea kuongeza majina ya washiriki wengine katika orodha hii kwa kumbukumbu ya vizazi vijavyo.

Janet Jackson(dada wa Michael Jackson) ambaye hakuwepo studio anatarajiwa kuimba sehemu ya marehemu kaka yake kabla ya kutolewa rasmi kwa video ya remake hii ya We Are The World ambayo inatarajiwa kuonyeshwa rasmi tarehe 12 mwezi huu katika kituo cha televisheni cha NBC cha nchini Marekani kwenda sambamba na ufunguzi wa michezo ya Olympics ya majira ya baridi(Winter Olympics) inayofanyikia huko Vancouver nchini Canada kwa mwaka huu. Video ya wimbo huu mpya imeongozwa na Director wa movie ya Crash(kama hujaiona fanya bidii uione),Paul Haggis.

Je unadhani kuna uwezekano wa wimbo huu uliotengenezwa upya,kuushinda ule wa zamani au kupata mafanikio zaidi ya original? Kuna watu wanasema ni vyema kwamba Lionel Richie na Quincy Jones wapo kusimamia na kuhakikisha kwamba the “1985 spirit ” inabakia pale pale lakini bila kuwepo kwa Michael Jackson ni pengo kubwa sana.Wewe unasemaje?

Photo/Kevin Mazur/wireimage.com. Kwa picha zaidi bonyeza hapa.

Tuzo maarufu za muziki za Grammy zimemalizika muda mfupi uliopita jijini Los Angeles.Kama kawaida ya tuzo maarufu kama hizo,huwa kuna kuvunjwa kwa rekodi au kuwekwa rekodi mpya,vituko mbalimbali, mavazi ya kukumbukwa na pia performances za kukumbukwa.

Kwa mwaka huu,rekodi mpya imewekwa na Beyonce Knowles.Binti huyo ambaye ni mke wa rapper maarufu ulimwenguni,Jay-Z ameibuka na jumla ya tuzo sita na hivyo kuweka rekodi ya kuwa mwanamuziki wa kike wa kwanza kushinda idadi hiyo ya tuzo katika usiku mmoja wa tuzo za Grammy!

Kwa upande wa performances ambazo nitazikumbuka kwa muda ni pamoja na performance aliyofanya Pink huku akijibinubinua hewani kwa kutumia kipande cha nguo! Kuna haja ya kuchunguza zaidi ili kujua kiasi gani cha ile performance ni kweli na kiasi gani ni uzushi.It was hot though.

Nyingine niliyoipenda ni performance ya Lil Wayne(yuko mbioni kwenda jela kwa miezi nane na huenda hii ilikuwa ni performance yake ya mwisho), Drake na Eminem. Nilifurahi kumuona Eminem akiwa bado yupo fit na huku uwezo wake wa kumiliki jukwaa ukiwa pale pale.Hapo katikati alipotea kutokana na matumizi ya kutisha ya madawa ya kulevya.

Mavazi: Mimi sio mtaalam sana wa mambo ya mavazi.Lakini hata hivyo hiyo haikunizuia kuona kwamba Lady Gaga alitia fora kwa kivazi alichovaa baada ya ku-perform na kuungana na wenzake katika audience.Sijui bado jina la kitu alichovaa;ni gauni au?

Kwa ujumla tuzo kubwa kubwa zilienda kama ifuatavyo;

  • Record of the Year – Kings of Leon – “Use Somebody”
  • Album of the Year – Taylor Swift – ‘Fearless’
  • Song of the Year – Beyonce – “Single Ladies (Put a Ring On It)”
  • Best New Artist – Zac Brown Band
  • Best Female Pop Vocal – Beyonce – “Halo”
  • Best Male Pop Vocal – Jason Mraz – “Make It Mine”
  • Best Duo or Group With Vocals – Black Eyed Peas – “I Gotta Feeling”
  • Best Pop Vocal Album – Black Eyed Peas – ‘The E.N.D

Kwa orodha kamili ya washindi,bonyeza hapa.

Kama wewe ni mpenzi wa muziki aina ya soul,bila shaka kabisa utakuwa unamtambua vyema mwanamuziki Teddy Pendergrass.

Habari za kusikitisha ni kwamba Teddy Pendergrass amefariki dunia hivi leo huko Philadelphia nchini Marekani.Kwa mujibu wa mtoto wake Teddy Pendergrass II, baba yake alifanyiwa colon cancer surgery miezi minane iliyopita na hakupona vizuri tangu hapo.Amefariki akiwa na umri wa miaka 59 katika hospitali ya Philadelphia’s Bryn Mawr.

Teddy ambaye nyimbo zake zilizojaa mahaba na bashashi zilitamba sana katika miaka ya 1970s na 1980s, alizaliwa March 26,1950 huko Philadelphia. Nyimbo kama vile “Turn Off The Lights”,”Close The Door” ni miongoni mwa nyimbo ambazo zilitokea kupendwa sana na mpaka hivi leo bado zinapendwa.

Teddy alitangaza rasmi kustaafu kutoka katika shughuli za muziki mwaka 2006 lakini akarudi tena jukwaani mwaka mmoja baadaye kwa ajili ya concert ya kuchangisha fedha kwa Taasisi yake ya Teddy Pendergrass Alliance inayosaidia watu walio na matatizo ya uti wa mgongo.

Kama utakumbuka Teddy Pendergrass mwenyewe alipata ajali mbaya ya gari mwaka 1982 ambapo aliumia vibaya uti wake wa mgongo kitu kilichosababisha alazwe hospitali kwa muda wa miezi sita.Baada ya hapo alirejea tena studio na kutoa albamu ya “Love Language”.

Pumzika kwa amani Teddy.Sikiliza wimbo wake “Close The Door” hapo chini.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Judge maarufu wa television show ijulikanayo kama American Idol,Simon Cowell(pichani) ametangaza kwamba msimu huu ni mwa mwisho kwake.Msimu huu unaoanza wiki hii(kesho),ni wa tisa kwa show hiyo ambayo inasemekana kuwa ndio yenye watazamaji wengi kupita show zingine zote nchini Marekani.

Cowell amesema kwamba anaachana na American Idol ili kupata muda zaidi wa kuwa Judge katika show ijulikanayo kama “The X Factor” ambayo ameianzisha na ambayo ni maarufu nchini Uingereza nchi ambayo anatokea Simon Cowell.The X Factor kwa upande wa Marekani itaanza mwaka huu wakati wa majira ya fall.

Mwenyewe amesema kwamba aliombwa sana kubakia katika show na akaahidiwa pesa nyingi zaidi lakini yeye binafsi alishachoshwa na American Idol na hivyo alitaka challenge mpya. Simon alikuwa analipwa takribani $ 36 milioni

Katika mwaka huu American Idol itakuwa na sura tofauti kwani jaji wa miaka iliyopita Paula Abdul aliondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na mtangazaji wa televisheni,Ellen DeGeneres.

Analysts mbalimbali wa masuala ya televishenvi nchini Marekani wanaamini kwamba show hiyo itapoteza watazamaji kutokana na kuondoka kwa Simon Cowell, jaji ambaye inasemekana alikuwa ni kivutio cha aina yake katika show hiyo.

American Idol mpaka hivi sasa imeweza kutoa wanamuziki wanaotamba kama vile Kelly Clarkson, Carrie Underwood and Chris Daughtry,Ruben Studdard na Fantasia Barino. Je utaendelea kuangalia American Idol hata baada ya kuondoka kwa Simon Cowell??


Pombe sio maji.Si umeshawahi kusikia hivyo au umewahi wewe mwenyewe kukanywa na watu wanaojua? Mwanamuziki Mariah Carey yeye aliona inawezekana ikawa maji.Inategemea tu unaiweza kiasi gani.Kumbe hakuwa anaiweza.Kilichotokea,tizama video hapo chini.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Nilipokuwa kijana zaidi,miongoni mwa wanamuziki niliopenda kuwasikiliza alikuwa ni Sade.Niliupenda zaidi wimbo wa Smooth Operator Enzi hizo sikujua kama Sade pia ni jina la bendi anayoiongoza ambayo inabeba jina lake.

Huyu ni mzaliwa wa kule Ibadan,Oyo State nchini Nigeria aliyekulia nchini Uingereza.Wazazi walikutana nchini Uingereza kisha baadaye wakaenda kujaribu kuishi nchini Nigeria.Mambo hayakuwa mambo na hivyo akiwa bado kinda kabisa akarejea Uingereza na mama yake.Jina lake halisi ni Helen Folasade Adu na alizaliwa tarehe 16 Januari mwaka 1959.

Baada ya miaka kadhaa yenye mafanikio makubwa katika muziki,Sade walipotea.Sasa mwaka huu,mwezi wa Februari,wanarudi.Albamu inaitwa Soldier of Love.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

BBE

Mapenzi kati ya wanamuziki mashuhuri,wanandoa, Beyonce Knowles na Jay-Z yanazidi kukolea. Katika kuthibitisha hilo,wapenzi hao wameamua kubadilisha au tuseme kubadilishana mpaka majina sasa!

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Star la nchini Uingereza,hivi punde Jay-Z ambaye jina lake halisi ni Shawn Carter atakuwa anajulikana kama Shawn Knowles-Carter huku Beyonce atakuwa akijulikana kama Beyonce Knowles-Carter.

Wakati Beyonce na Jay-Z wanaendelea kukoleza penzi,mambo hayaendi vizuri kwa wazazi wa Beyonce,Tina na Mathew Knowles kwani hivi karibuni mama yake Beyonce ameomba talaka kutoka kwa mume wake huyo kwa miaka 29 iliyopita.Kisa na mkasa? Baba yake Beyonce inasemekana “amechapa nje” na kwamba anatarajiwa kuwa baba kwa mtoto wa nje ambaye bado hajazaliwa. Mwanamke anayemshtaki baba yake Beyonce anaitwa Alexandra Wright.


Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page