Recent Articles

BIG BROTHER AFRICA 2013-THE CHASE: TIZAMA HII VIDEO KWA MAKINI...

[youtube:https://www.youtube.com/watch?v=fxxH4hukUSo] Umesikia fununu na hisia.Nani ataiwakilisha Tanzania? Nakuhakikishia ni fununu na hisia tu. Jiandae Kushangaa!!

Read More

“UMENIPOTEZA”- INNOCENT MKUMBA (BrAnD NeW)

UMENIPOTEZA- INNOCENT MKUMBA (BrAnD NeW)

Ujumbe uliowekwa kwenye e-mail iliyoniletea wimbo huu imenisihi kwamba nitoe support kwa wimbo bora wa mwaka. Ukweli ni kwamba unapopokea ujumbe kama huo, unajiuliza maswali ...

Read More

“BYE BYE”-CANNIBAL (BrAnD NeW)

BYE BYE-CANNIBAL (BrAnD NeW)

Hii ni brand new toka kwa Cannibal baada ya kuachia Legend iliyotambulika zaidi kwa video yake ya kipekee,Cannibal ameamua kufanya wimbo huu as a special ...

Read More

MKALI WA VODACOM

MKALI WA VODACOM

Je, unajiamini kuwa na kitu kinachokufanya uwe mkali mtarajiwa? Vodacom inatafuta mtangazaji mpya wa kipindi cha TV kitakachoanza hivi karibuni. Soma namna ya kushiriki na ...

Read More

SIKUKUU YA WAAFRIKA DUNIANI KUADHIMISHWA SOMA CAFE DAR ES SALAAM

SIKUKUU YA WAAFRIKA DUNIANI KUADHIMISHWA SOMA CAFE DAR ES SALAAM

Fikra za Umoja wa Waafika zilianza kuzungumziwa na kuchipuka kupitia Marcus Garvey- mwanarahakati wa Kijamaika aliyewasisimua viogozi wa mwanzo wa bara, miaka ya 1920 na ...

Read More

SHUHUDIA FAINALI YA KOMBE LA UEFA JUMAMOSI HII KUPITIA DStv

SHUHUDIA FAINALI YA KOMBE LA UEFA JUMAMOSI HII KUPITIA DStv

  Jumamosi imekaribia. Mashabiki wa soka duniani wanalo la kuzungumzia, kujadili na kisha siku ya siku kujumuika kwa pamoja kushuhudia mechi kali na ya aina yake. ...

Read More

“KAMA ZAMANI”-MwanaFA Feat. THE KILIMANJARO BAND, MANDOJO & DOMOKAYA (BrAnD NeW)

KAMA ZAMANI-MwanaFA Feat. THE KILIMANJARO BAND, MANDOJO & DOMOKAYA (BrAnD NeW)

Huu wimbo ulitoka rasmi wiki iliyopita. Kwa makusudi sikuuweka hewani. Nilikuwa na bado nina maana yangu. Ukiendelea kusoma bila shaka utanielewa. Kila kizazi kina tabia au ...

Read More

WASANII KUTOKA NIGERIA, KENYA NA AFRIKA KUSINI KUPAMBA UZINDUZI WA BIG BROTHER AFRICA-THE CHASE

WASANII KUTOKA NIGERIA, KENYA NA AFRIKA KUSINI KUPAMBA UZINDUZI WA BIG BROTHER AFRICA-THE CHASE

Wasanii mbalimbali kutoka Nigeria, Kenya na Afrika Kusini wanatarajiwa kupamba shughuli ya kuanza kwa msimu mpya wa show kabambe ya Big Brother Africa siku ya ...

Read More

“SHANNI NA JENNY”-ABBY SKILLS Feat.CHEGE

SHANNI NA JENNY-ABBY SKILLS Feat.CHEGE

Ni muda kidogo hatujasikia kitu kutoka kwa Abby Skills ambaye kwa watu wanaokumbuka enzi zile Bongo Fleva inaanza kushika kasi, mtamkumbuka vizuri. Huu hapa ni ...

Read More

BREAKING NEWS: PROFESSOR JAY AJIUNGA NA CHADEMA/ AKABIDHIWA KADI YA UANACHAMA DODOMA

BREAKING NEWS: PROFESSOR JAY AJIUNGA NA CHADEMA/ AKABIDHIWA KADI YA UANACHAMA DODOMA

Pichani Professor Jay akiwa na Kiboya,mdau mkubwa wa muziki nchini ambaye pia ni mwanachama wa CHADEMA. Picha kwa hisani ya Twitter ya Professor. Habari ambazo zinatambaa ...

Read More

BILLBOARD MUSIC AWARDS: JUSTIN BIEBER AZOMEWA/ MIGUEL APIGA MWELEKA

Yawezekana hukupata nafasi ya kuangalia baadhi ya mambo yaliyojiri jana wakati wa Billboard Music Awards ambazo zilitangazwa kutokea Las Vegas,Nevada-mji wa kila aina ya dhambi ...

Read More

KINACHOMPONZA PRODYUZA TUDD THOMAS NI UCHAWI AU KUSAHAU?

KINACHOMPONZA PRODYUZA TUDD THOMAS NI UCHAWI AU KUSAHAU?

Prodyuza Tudd Thomas. MASHABIKI wa mtayarishaji wa muziki (Producer), mwenye uwezo wa kipekee, aliyetayarisha wimbo wa Leka dutigite wa Kigoma All Stars na zingine nyingi, Tudd ...

Read More

“NASHINDWA KULALA”- BONFACE MATEZA

NASHINDWA KULALA- BONFACE MATEZA

Huu hapa ni wimbo mpya kutoka kwa msanii Bonface Mateza. MSANII   :  BONFACE MATEZA WIMBO   :  NASHINDWA KULALA STUDIO  :   JAIM RECORD PRODUCER  :  GEORGE   JAMES

Read More

YANGA YAICHAPA SIMBA 2-0/ MASHABIKI BARANI AFRIKA WAFURAHIA MECHI KUPITIA SuperSport EAST 9

YANGA YAICHAPA SIMBA 2-0/ MASHABIKI BARANI AFRIKA WAFURAHIA MECHI KUPITIA SuperSport EAST 9

Yanga wakifurahia mojawapo ya magoli kutoka katika mechi hiyo. Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry Blog Timu ya soka ya Yanga, jioni hii imewadhihirishia mashabiki wao ...

Read More



Jijini Dar siku hizi yupo mchekeshaji mmoja ambaye anazidi kujipatia mashabiki.Anaitwa Evans Bukuku na stand-up comedy yake hufanyikia pale Sweet Eazy(Oysterbay Hotel). Wiki hii BC ilipata nafasi ya kuhudhuria stand-up comedy hiyo.

Ingawa kuna mambo mengi ambayo yanahitaji marekebisho,(kama vile watu kulipa kiingilio na kushindwa hata kuingia mahali husika kwa sababu ya watu kufurika na sauti kuwa na mwangwi nk),naamini ni mwanzo mzuri na huenda siku moja tukawa na stand-up comedy kama zile za Kings of Comedy na Queens of Comedy kutoka US..au Def Jam kabisa.

Here are some images all taken by Ahmad Michuzi JR

Comedian Evans Bukuku

The audience: I am sure you can spot Muhidin Issa Michuzi,Jokate Mwegelo and Hasheem Thabeet, some of many celebrities in attendance.The event was hosted by Taji Liundi.

The audience…he sure can make people show their teeth!

Be Sociable, Share!

jjb

Naitwa…

jjb2c

Photo/Kennedytz

Be Sociable, Share!

kaundabc

Bila shaka huyu bwana pichani hahitaji utambulisho.Au? Lakini swali ni je unadhani hapo alikuwa anajaribu kumuigiza nani?

Be Sociable, Share!

Kama kuna kitu ambacho kilitokea katika upande wa burudani nchini Tanzania hivi karibuni na kuteka hisia za watanzania wengi,bila shaka kitu hicho ni kundi lililokuwa linajulikana kama Ze Comedy.Tunasema lililokuwa linajulikana kama “Ze Comedy” kwa sababu mpaka sasa kuna utata au kesi kuhusiana na haki miliki ya jina hilo!Kesi iko kwa pilato.

Ilifikia kipindi ukimtafuta mtu siku ya Alhamisi jioni(wakati kipindi cha Ze Comedy kipo hewani) usipompata yawezekana kabisa yupo mbele ya luninga yake akiwacheki Ze Comedy huku simu yake akiwa ameiweka katika mtetemko(vibration) katika kumaanisha kwamba “hataki usumbufu”.

Wakati kundi hilo likizidi kujipatia umaarufu mara ghafla zikaja habari kwamba Ze Comedy wanakwenda “mapumzikoni”.Pamoja na kwamba tangazo hilo liliwasikitisha watu,ilieleweka kwamba mapumziko ni jambo muhimu kwa kila binadamu kwa hiyo watu wakaelewa!

Tatizo lilikuja pale mgogoro ulipofumka baina ya Ze Comedy na uongozi wa kituo cha EATV ambacho ndio kilikuwa kinarusha kipindi cha Ze Comedy kila siku ya Alhamisi saa moja jioni.Mapatano ya mezani yakashindikana.Kesi ikaenda mahakamani(bado ipo).Siasa nazo zikaingilia kati.Vigogo wa nchi wakaingilia lakini wapi.

Leo hii watu wengi wanajiuliza,je Ze Comedy watarudi? Na wakirudi watarudi kwa namna gani,kwa kutumia jina gani?Unadhani watakamata tena?Unadhani kilichotokea mpaka hivi sasa kinatoa mafunzo gani kwa vikundi vingine na washika dau wote wa fani ya burudani nchini Tanzania?

Kuna habari ambazo bado hazijaweza kuthibitishwa zinazosema kwamba vijana hao mahiri kwa kuvunja watu mbavu huku wakielimisha jamii wana mpango wa kufanya ziara kabambe nje ya Tanzania.Tunasubiri.

Be Sociable, Share!

Kwa wale ambao mnafuatilia habari au kuangalia vipindi mbalimbali vya vichekesho kutoka nchini Marekani, habari ambazo si za kufurahisha ni kwamba mchekeshaji (comedian) na muigizaji filamu maarufu Bernie Mac(pichani) amefariki dunia.Bernie Mac ambaye alijizolea umaarufu kutokana na kipindi chake cha televisheni cha The Bernie Mac Show amefariki leo asubuhi katika hospitali ya Northwestern Memorial Hospital ya jijini Chicago nchini Marekani alipokuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa pneumonia.Wengine mtamkumbuka Bernie Mac kwa uigizaji wake wa hivi karibuni katika filamu kama vile Ocean Thirteen na Transformers.Bernie Mac alikuwa na umri wa miaka 50.Kwa undani zaidi wa habari hii unaweza kubonyeza hapa.

Be Sociable, Share!

Ushawahi kusikia mtu akikuambia kwamba Wamarekani huenda ndio wanaongoza kwa “ujinga/umbumbumbu” duniani kote? Inasemekana wamarekani wengi hawajui hata kwamba duniani kuna nchi zingine,mila zingine nk.Pia inasemekana kwamba baadhi yao mahali wanapopajua ni hapo hapo walipozaliwa na kukulia.Kuna wengine wanaamini kwamba ili aweze kusafiri kutoka New York kwenda Illinois basi ni lazima awe na passport.Je unaamini kwamba wamarekani ni wajinga? TV moja ya kutoka Australia iliamua kuwahoji baadhi ya wamarekani kuhusu mambo mbalimbali.Tizama video hiyo hapo chini.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Be Sociable, Share!

Pichani si wengine bali kundi maarufu la Ze Comedy walipokuwa wakiingia kwenye ukumbi wa MAELEZO ambapo walitangaza “kupumzika” kutoka katika mkataba wao na kituo cha televisheni cha EATV.

Photo Credit:Athumani Hamisi

Be Sociable, Share!

Kwa wengi anajulikana kama Mpoki ingawa hilo sio jina lake halisi.Jina halisi anaitwa Mjuni Silvery.Ni kutoka kundi maarufu la kuvunja mbavu huku likielimisha jamii la Ze Comedy.Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na maoni tofauti tofauti kuhusu Ze Comedy.Wengine wanasema bado linaendelea kama lilivyoanza huku wengine wakisema kwa namna fulani limeanza kuiacha barabara.Wewe unasemaje?

Be Sociable, Share!

 

Msomaji wetu mmoja ametuandikia na kutuuliza swali ambalo limetuwia gumu kidogo kulijibu.Anasema, hivi karibuni alipokuwa nchini Tanzania(anaishi ughaibuni) alikuwa akisikia sana msemo wa mitaani unaoitwa “kubonyeza kizenji”.Anasema alipojaribu kuuliza wenyeji wake akaambiwa kwamba msemo huo umeanzia au kuanzishwa na Joti,muigizaji maarufu kutoka kundi la Ze Comedy.Miongoni mwa wenyeji wake na jamaa aliowauliza hakuna aliyempatia jibu la kuridhisha au kujitosheleza.Ndio maana akawa hana jinsi bali kutuandikia akitumaini kupata jibu kutoka kwetu.

Kwa bahati mbaya hata sisi hapa BC swali hilo limetupiga chenga.Na kama kawaida,hali hiyo ikitokea huwa hatuna budi kuomba msaada kwako msomaji/mtembeleaji wetu.Kama unafahamu,hebu msaidie huyu msomaji; Kubonyeza kizenji maana yake nini? Chanzo chake nini?

Pichani ni Joti akifanya hiyo mikogo ya “kubonyeza kizenji”

Be Sociable, Share!

 

Wachekeshaji(Comedians) ni wasanii ambao wana umuhimu wa aina yake katika jamii.Hawa ndio hufanya wakati mwingi watu tusahau uchungu wa maisha kwa jinsi ambavyo wanatuvunja mbavu tukiwasikiliza radioni,kuwaona kwenye luninga au hata kubambana nao mitaani. Si unakumbuka tangu enzi zileee za kina Mahoka…za kina Pwagu na Pwaguzi?

Kwa bahati mbaya sana,nchini Tanzania bado hakuna mifumo mizuri kwa ajili ya wasanii kama hawa kufaidi vizuri jasho lao.Wengi wao wanakuwa na hali za kimaisha ambazo hazilingani na vipaji walivyonavyo.Isitoshe wasanii hawa,kwa kupitia michezo au vichekesho vyao,hutoa mafunzo mazuri sana ya kijamii.Tatizo huwa linakuwa wapi katika kutengeneza mifumo imara ambayo itahakikisha wasanii wanafaidika?Swali hili linaelekea kuzidi kuwa gumu badala ya jepesi siku baada ya siku.Hatupendi kulirudiarudia lakini tunathamini sana mchango wako msomaji katika kubadilisha mambo kadha wa kadha ambayo kwa hakika yanawezekana kabisa.

Pichani ni baadhi ya wachekeshaji maarufu ambao wameshawahi kutokea nchini Tanzania.Kushoto ni Mzee Small na kulia ni Kingwendu.

Be Sociable, Share!

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page