Habari mbalimbali ambazo zinazidi kusambaa mtandaoni na pia katika vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo vile vya kimataifa kama vile CNN, The Guardian UK,Reuters,AFP,Al Jazeera nk zinasema kwamba aliyekuwa Rais wa Libya,Moammar Ghadhafi, amefariki dunia baada ya kushambuliwa na kuumizwa vibaya katika mapambano makali yaliyotokea katika mji aliozaliwa wa Sirte kati ya waasi(National Transitional Council-NTC) na majeshi yake.

Kwa mujibu wa msemaji wa NTC,Abdel Majid Mlegta,Ghadhafi ambaye aliitawala Libya kwa miaka takribani 42, amefariki kutokana na kuumizwa vibaya kichwani wakati wa mashambulizi hayo na wakati akijaribu kukimbia.

Hizi hapa ni baadhi ya picha ambazo zinazidi kusambaa mtandaoni zinazoonyesha sura ya Moammar Ghadhafi baada ya mashambulizi.Tunaomba radhi kwa picha hizi!

Ghadhafi?

Bado tunaendelea kufuatilia kwa makini habari hizi ambazo zinaendelea kuthibitishwa na pande mbalimbali.Mkutano baina ya waandishi wa habari na kiongozi wa sasa wa Libya,unatarajiwa hivi punde.Stay tuned

UPDATE: Mwili wa Kanali Moammar Ghadhafi umewasili katika mji wa Misratah.Mtoto wa Ghadhafi ajulikanaye kama Mutasim ameuawa pia katika mashambulizi hayo.Alikuwa na baba yake.

UPDATE: Waziri Mkuu wa Libya,Jibril amethibitisha muda mfupi uliopita kwamba Moammar Ghadhafi amefariki au kuuawa na majeshi ya NTC.

Hapa chini tunayo screen shot kutoka Al Jazeera inayoonyesha mwili wa Ghadhafi.Picha hii imepatikana kutoka katika video ya kwenye simu.Bonyeza More kuitazama.Warning: Picha hizi sio nzuri kwa kila mtu.

read more

Ukanda wa Afrika Mashariki unaendelea kuwa ukanda uliojaa simanzi kwani wakati Tanzania tukiendelea kuomboleza msiba mzito wa watu waliofariki katika ajali ya kupinduka kwa meli ya MV Spice Islander huko Zanzibar,jirani zetu Kenya nao wapo katika msiba mzito kufuatia watu wengi kupoteza maisha kufuatia mlipuko wa bomba la mafuta katika eneo la viwanda la Lunga Lunga jijini Nairobi.

BBC WANAYO RIPOTI KAMILI

Nchi yetu Tanzania leo ipo katika msiba mkubwa kufuatia kuzama kwa meli ya LCT MV Spice Islanders visiwani Zanzibar ilipokuwa safarini kutoka Unguja kwenda Pemba alfajiri ya kuamkia leo.Watu wengi wamepoteza maisha yao na wengi wamejeruhiwa.Shughuli za uokoaji zinaendelea kwa ushirikiano mkubwa wa vyombo vyote vya usalama nchini kama vile Jeshi la Wananchi Tanzania na Jeshi la Polisi.Majeruhi wanaendelea kuokolewa na pia miili ya waliopoteza maisha inaendelea kuibuliwa toka majini.

BC inaungana na kila mtanzania,ndugu,jamaa na marafiki zetu popote pale walipo kuwapa pole wote waliopoteza ndugu,jamaa au marafiki na pia kuwatakia uponaji wa haraka wale wote waliojeruhiwa.Mwenyezi Mungu azilaze pema peponi roho za wote waliopoteza maisha.Amina

Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ali Kiba pamoja na madansa wake alfajiri ya jana(Jumapili) wamenusurika vifo kufuatia kupata ajali ya gari katika eneo la Mikumi mkoani Morogoro walipokuwa safarini kutokea Mbeya kuelekea jijini Dar-es-salaam.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika gazeti la Nipashe ambazo BC imeweza kuzithibitisha kutoka kwa Ali Kiba mwenyewe,jumla ya watu saba wamejeruhiwa katika ajali hiyo huku watatu kati yao wamelazwa katika hospitali ya mkoa Morogoro.Ali Kiba ambaye aliumia mguuni na mkononi  tayari ameruhusiwa kutoka hospitali na amesharejea nyumbani kwake Dar ambapo ameieleza BC kwamba anaendelea vyema. Ali Kiba alikuwa awe miongoni mwa wasanii waliotumbuiza katika tamasha la Serengeti Fiesta lililofanyikia CCM Kirumba Mwanza hapo jana.

Chanzo kamili cha ajali hiyo hakijawekwa wazi na polisi tayari wanachunguza.BC inawatakia wote waliojeruhiwa katika ajali hiyo kupona haraka ili waweze kurejea katika kazi zao.


Kiongozi wa kundi la Al-Queda, Osama Bin Laden, ameuawa huko nchini Pakistani.Hiyo ni kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari na taarifa rasmi kutoka kwa Rais wa Marekani, Barack Obama, aliyoitangaza muda mfupi uliopita.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Osama ameuliwa na kikosi kidogo maalumu cha Marekani kikishirikiana na “mshirika” wa Marekani jumapili hii(jana) huko Abbottabad nchini Pakistan na kwamba mwili wake upo mikononi mwa majeshi ya Marekani hivi sasa.

Kwa miongo kadhaa sasa,Marekani imekuwa ikimsaka kwa udi na uvumba mzaliwa huyo wa Saudi Arabia ambaye ndiye anaaminika kuwa mhimili wa mpango mzima uliopelekea mashambulizi ya World Trade Center nchini Marekani katika jiji la New York ,September 11, ambayo yalibadili kwa kiwango kikubwa siasa za dunia ikiwemo habari za kigaidi.

Kiongozi wa Bendi ya Msondo Ngoma”Baba ya Muziki”, Muhidin Maalim Gurumo, amelazwa tena katika Hospitali ya Muhimbili.Hiyo ni kwa mujibu wa Blog ya Bongo Weekend ya Khadija Kalili.

Hii ni mara ya pili katika kipindi kisichozidi miezi sita kwani kama mtakumbuka Maalim Gurumo alilazwa hospitalini hapo mwezi Novemba mwaka jana akisumbuliwa na mapafu kujaa maji. Baadaye alitoka hospitalini hapo na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii lakini bila yeye mwenyewe kupanda jukwaani.

Hivi karibuni alihudhuria mpambano wa bendi yake ya Msondo Ngoma na Sikinde pale Diamond Jubilee.

BC inamtakia Muhidini Maalim Gurumo kila la kheri,apone haraka.

Habari ambazo zimethibitishwa ndani ya Clouds FM kupitia Mkuu wa Polisi mkoani Morogoro,zinapasha kwamba wanamuziki wa kikundi cha Five Stars Modern Taarab wamepata ajali mbaya ya gari karibu na Mikumi mkoani  na Morogoro na watu 12 wamepoteza maisha yao huku wengi wao wakihofiwa kuwa ni wanamuziki wa kundi hilo lililoanzishwa chini ya miaka mitatu iliyopita.

Wanamuziki hao walikuwa wakisafiri kwa gari aina ya Coaster wakitokea mikoa ya Mbeya,Iringa na Ruvuma kwa ajili ya shughuli zao za muziki.Inasemekana ajali ilitokea baada ya Coaster hiyo kulivaa lori bovu la mizigo lililokuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabarawakiwemo waimbaji, mafundi mitambo na mkurugenzi wa bendi.

Kwa mujibu wa mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Morogoro Be. Ibrahim Mwamakula, marehemu hao ni Issa Kijoti, Nasoro Madenge, Mapande, Fembe Juma, Omary Hashim, Tizo ,Omari Tall,Ngeleza Hasan,Hamisa Omari,Maimuna , Haji Msaniwa na mcheza show wa kundi la Kitu Tigo Ilala

Katika ajali hiyo, alikuwemo pia mwimbaji mkongwe Mwanahawa Ally ambaye alinusurika baada ya kuumia vibaya, aliungana nao kama mwimbaji mwalikwa akitokea Melody ModernTaarab.
Mungu awalaze mahali pema peponi marehemu wote na awasaidie waliojeruhiwa waweze kupona haraka na kuwapa nguvu ndugu,jamaa na marafiki wote katika wakati huu mgumu.Amina
Zifuatazo ni picha mbalimbali kuhusiana na ajali hiyo kutoka vyanzo mbalimbali vikiwemo Global Publishers,Issa Michuzi,Dj Choka,nk.ONYO: BAADHI YA PICHA NI ZA KUTISHA.TAFADHALI USIFUNGUE KUANGALIA KAMA HUNA UWEZO WA KUSTAHIMILI
read more

Habari ambazo zimetufikia muda si mrefu uliopita zinapasha kwamba mtanzania wa kwanza kucheza katika ligi ya NBA,Hasheem Thabeet aliyekuwa akichezea timu ya Memphis Grizzlies, ameuzwa kwenda timu ya Houston Rockets ya jijini Houston,Texas katika mabadilishano maalumu baina ya timu hizo mbili.

Katika mabadilishano hayo,mchezaji Shane Battier aliyekuwa akichezea timu anayokwenda Hasheem(Houston Rockets) anajiunga na Memphis Grizzlies.

read more

Baada ya tukio la jana la milipuko ya mabomu huko Gongo la Mboto,suala ambalo limebakia kuumiza vichwa vya watu wengi ni suala la uwajibikaji. Nini kimesababisha tukio hili la kusikitisha ambalo wengi tunashindwa kuliita “ajali” kutokana na ukweli kwamba miaka miwili tu iliyopita(April 2009),tukio linalofanana na hili lilitokea kule Mbagala na maisha ya watu wengi kupotea? Nani awajibike?

Katika kutafuta majibu kwa swali hilo na mengineyo,Shirika la Sauti ya Amerika(Voice of America) kupitia idhaa yake ya Kiswahili na kupitia mtangazaji wake Sunday Shomari,lilimuuliza Waziri wa Ulinzi wa Tanzania,Dr.Hussein Mwinyi swali hilo na mengineyo. Sikiliza mahojiano hayo hapa;

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Kwa habari zingine kuhusu tukio hili,tembelea tovuti ya VOA Swahili kwa kubonyeza hapa.



Ni siku nyingine ya majonzi makubwa nchini Tanzania kufuatia milipuko iliyotikisa jiji la Dar-es-salaam jana jioni.Milipuko hiyo ilitokea  katika ghala la kuhifadhi silaha za kijeshi huko Gongo la Mboto.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Uingereza(BBC) kupitia idhaa yake ya Kiswahili,watu 20 wameuawa na mamia ya watu kujeruhiwa. Taarifa hiyo imemnukuu mnadhimu mkuu wa majeshi,Lt.Gen Shimbo

Mashirika mbalimbali ya habari ulimwenguni likiwemo la CNN,yameripoti kuhusu tukio hili.Hii ni mara ya pili kwa milipuko kama hiyo kutoka jijini Dar es Saalam katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.Mwaka 2009 zaidi ya watu 20 waliuawa na wengine 300 kujeruhiwa kufuatia milipuko iliyotokea katika ghala lingine la kijeshi katika maeneo ya Mbagala jijini Dar-es-salaam.

Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu wote mahali pema peponi na awaponye majeruhi wote.

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page