
Muziki ni lugha ya ulimwengu(universal language). Bila shaka umeshawahi kusikia msemo huo. Mimi binafsi nakubaliana kabisa na msemo huo. Kuna nyakati nimewahi hata kujiuliza,hivi dunia ingekuwaje kama kusingekuwa na muziki? Tunapokutana na kusheherekea tukio fulani,vigelegele na mayowe vingetosha?
Wakati kazi ya kubwa ya kutuletea burudani ya muziki inaanzia kwa msanii mwenyewe,pembeni yake, kwa miaka nenda rudi, amekuwepo mtu muhimu katika kukamilisha safari hiyo. Mtu huyo ni DJ au Deejay au Disco Jokey kwa wale wenzangu na mie tuliokula chumvi kidogo!
Mwanamuziki/Msanii anapomaliza kazi yake kwa kushirikiana na producer wake, hukimbilia kwa DJ kwani anatambua kabisa kwamba huyo ndiye kiungo kikuu kati yake na mashabiki au wapenzi wa muziki kwa ujumla.
Miongoni mwa DJs ambao sio tu wameifanya kazi yao kwa ustadi mkubwa bali pia waliowahi kujizolea sifa na mashabiki wa kutosha ni DJ John Dillinga Matlou au maarufu kama DJ JD. John ana historia ndefu katika muziki. Mwenyewe anasema,aliianza safari yake tangu akiwa mtoto kabisa. Mpaka hivi leo bado anaendelea kuwapa watu burudani. Hivi sasa anaendesha kampuni ya JD Entertainment ambayo inashughulika na masuala yote ya burudani,promotions na kadhalika.
Nilipofanya naye mahojiano ambayo utayasoma hivi punde,niligundua mambo kadhaa muhimu;DJ JD ni mbunifu wa aina yake. Aina za vipindi alivyovianzisha na kuviendesha(hususani redioni) ndivyo pengine vilivyochangia mafanikio ya baadhi ya vituo vya redio vya FM tunayoyaona hivi sasa.Pia niligundua kwamba huyu ni miongoni mwa wale DJs ambao wanaifanya kazi yao sio kwa ajili ya kutafuta pesa peke yake bali kwa sababu anaupenda muziki na yote yale yatokanayo na muziki mzuri wenye kuleta burudani na starehe.
Fuatana nami katika mahojiano haya ambapo,pamoja na mambo mengine,DJ JD anaelezea hisia zake kuhusu ulimwengu wa muziki na burudani hivi sasa. Pia anajibu swali ambalo wapenzi wengi wa muziki wamekuwa wakitaka kumsikia akijibu; Je yeye na DJ Bonny Luv ni mahasimu au ni watu wawili wanaoipenda kazi yao na pia kushirikiana kwa karibu? Je unajua kwamba baba mzazi wa DJ JD sio mtanzania bali raia wa…? Endelea kusoma
BC: Karibu sana ndani ya BC. Tunafurahi kupata fursa hii ya kufanya nawe mahojiano haya.Mambo vipi?
JD: Mambo sio mabaya kusema ukweli.Namshukuru Mungu.
BC: Kwa sababu hii ni mara yetu ya kwanza kufanya nawe mahojiano na kwa sababu tunatambua kiu ya wengi(hususani mashabiki wako) labda ungeanza kwa kutueleza kwa kifupi historia ya maisha yako.Ulizaliwa wapi,ukakulia wapi na mambo kama hayo. 

Unamjua Dina Marios kama mtangazaji maarufu wa Clouds FM kupitia kipindi chake cha Leo Tena. Ambacho unaweza kuwa hukijui kuhusu Dina ni kwamba yeye pia ni blogger. Dina ana-blog kupitia www.dinamarios.blogspot.com. Ninachopenda kuhusu blog ya Dina ni topics mbalimbali ambazo anazirusha kila mara.Mtembelee ujionee mwenyewe kwa kubonyeza hapa.

Steve B,miongoni mwa DJs mahiri nchini Tanzania hivi sasa.Tukikukuuliza nani unamchukulia kuwa DJ bora nchini Tanzania,hivi sasa au hapo zamani utamtaja nani?Wa kituo gani cha redio au club gani?Kwanini?
Huwezi kuzungumzia historia ya disco nchini Tanzania na kuacha kumtaja DJ Bonny Luv (pichani). Ukifanya hivyo,wanaoielewa historia, ladha na utamu wa disco, enzi hizo lilipokuwa disco haswa, watakuona una lako jambo.
Huyu ni miongoni mwa DJs wachache ambao, miaka nenda miaka rudi,wamekuwa wakijizolea sifa za kipekee katika kuhakikisha kwamba mashabiki wa muziki sio tu kwamba hawabanduki stejini pindi akiingia mitamboni bali pia wanapata “raha kamili”. Hali hiyo ndio imesababisha watu wengine wathubutu hata kusema kwamba ikiwa hujawahi kuhudhuria disco au shughuli nyingine yeyote yenye burudani za miziki huku udhibiti wa kule inakotokea burudani ukiwa chini ya DJ Bonny Luv, basi huenda ukawa hujapata bado hiyo “raha kamili”. Hata hivyo habari njema ni kwamba hujachelewa kwani Bonny Luv alikuwepo, bado yupo na ataendelea kuwepo.
Sasa kwa wale ambao mnakumbuka enzi zile mlipokuwa hamkosi viwanja au enzi zile mlipokuwa hambanduki stejini kutokana na kunogewa na miziki, basi mwaka huu mnayo nafasi ya pekee kukumbuka enzi hizo sio kupitia kwenye njozi bali uhalisia.Kivipi?
Katika tukio la nadra, tarehe 5 mwezi wa saba(5th July 2008) ndani ya jiji la Columbus katika jimbo la Ohio(Columbus,Ohio) nchini Marekani, DJ Bonny Luv kwa kushirikiana na wakali wengine kama DJ Mix Master Luke kutoka Washington DC na TNT Jackson wanatarajia kutoa burudani ya aina yake. Waandaji wameliita tukio hilo(au ukipenda liite Party) Old School Party of The Century. Ukikosa,usije kumlaumu mtu na kusema hukuambiwa.Habari ndio hiyo.
Hivi karibuni tulipata nafasi ya kufanya mahojiano na DJ Bonny Luv kuhusiana na mambo mbalimbali kuhusu muziki na burudani na pia kuhusu ujio wake kwenye party hii ya aina yake ya Columbus,Ohio. Kwa mengi zaidi fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; 

Blog ya Father Kidevu inaripoti kwamba mtangazaji na MC maarufu,Robert G.Mongi a.k.a Bobby na mkewe Helena Mkonyi wamebarikiwa kupata mtoto wa kiume leo asubuhi katika hospitali ya Agha Khan jijini Dar-es-salaam.Mtoto amepewa jina la Ephan Patrick.BC inawapa hongera na kuwatakia kila la kheri katika kumlea mtoto na kuendeleza ndoa.Pichani ni Bobby akiwa amembeba mwanae Ephan Patrick.

Mtangazaji wa East Africa Radio na EA TV (Channel 5),Baby Kabaye au jina maarufu “Sister Dread”. Sister Dread pia ni msimamizi/muongozaji maarufu wa shughuli (MC).
Picha na Mroki(Father Kidevu)

Wiki chache zilizopita tulipoweka picha ya mtangazaji Dina Marios wa Clouds FM, mvua ya maoni ilianza kumwagika. Wasomaji wengi wakaonyesha kutamani sana kusoma mahojiano kamili na Dina Marios.BC hatukuwa na jinsi bali kumsaka Dina ili kukidhi haja ya wasomaji na watembeleaji wetu ambao kimsingi ndio “wafalme na malikia” wa BC.
Kipindi maarufu anachoendesha Dina hivi leo kinaitwa Leo Tena kupitia Clouds FM kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa mida ya saa tatu asubuhi mpaka saba mchana. Umaarufu wa kipindi cha Leo Tena haujaanza leo.Ulianzishwa na marehemu Amina Chifupa.Haishangazi basi hivi leo kusikia watu wakimtaja Dina Marios kama “mrithi wa Amina Chifupa au anayekalia kiti alichowahi kukalia Amina Chifupa”.Lakini cha maana zaidi ni kwamba Dina anajitahidi kuendesha kipindi cha Leo Tena kwa kufuata yale yote mazuri aliyoyaanzisha AC na kuongeza mengi mengine.Ubunifu,kipaji na kiu ya kufanya vizuri zaidi kila siku ndivyo vinavyomsaidia.
Hivi karibuni,katika kuitikia hiyo “popular demand” ya wasomaji na watembeleaji wetu,tulifanya mahojiano ya Dina Marios.Tulipofanya hivyo tuliongelea mengi yakiwemo masuala kama anajisikiaje kuwa mrithi wa Amina Chifupa hivi leo hususani baada ya kufariki(Dina alimrithi Amina pale Clouds FM kabla hajafariki).Unajua Amina Chifupa alimuomba Dina ampigie wimbo gani ambao Dina anauona kama ndio ulikuwa wa kumuaga? Je ni kweli sauti yake inafanana na ya marehemu AC kama ambavyo wengi husema?Yeye mwenyewe anasemaje?Kwa hayo na mengine mengi fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; 

Tumewahi kusema siku za nyuma kwamba tofauti moja kubwa baina ya watangazaji wa radioni na wale wa kwenye luninga ni kwamba hawa wa kundi la pili huwa tunapata nafasi ya kuziona sura zao mara kwa mara.Wakati mwingine hata kila siku ikiwezekana kutegemea na kile anachokifanya mtangazaji huyo wa televisheni.
Hali hiyo ndiyo inayosababisha muendelezo fulani wa uhusiano (mtangazaji na msikilizaji) pindi ikitokea ukakutana nao mitaani au katika shughuli fulani au japo kuwaona katika picha kama unavyoweza leo kuwaona kundi hili la Djs wa Clouds FM ambao kwa pamoja wanajulikana kama Nyuki DJz.
Kutoka kushoto waliochuchumaa/kaa ni Steve B,Dj Too Shot,Dj Fetty,Mully B,na waliosimama toka kulia ni Pitter Moo,DJ Venture pamoja na Dj Nelly.
Picha kwa hisani ya MichuziJR.

Anaitwa Salama Jabir.Ni miongoni mwa watangazaji mahiri nchini Tanzania.Ingawa anajulikana zaidi kutokana na kipindi chake cha Planet Bongo kinachorushwa na Channel 5 au EATV,Salama pia ni mmoja wa majaji katika mchakato wa kuibua vipaji au nyota wapya ujulikanao kama Bongo Star Search.
Kipindi chake cha Planet Bongo kinarushwa kila siku ya jumatano kuanzia saa tatu mpaka tatu unusu usiku na kurudiwa siku ya Alhamisi mchana kuanzia saa sita mpaka sita na nusu.Pia ni mtangazaji wa East Africa Radio na ni mpenzi mzuri wa michezo.
Picha kwa hisani ya Mrocky.

Gea Habib(pichani) mmojawapo kati ya watangazaji mahiri wa Clouds FM. Anaendesha kipindi kiitwacho Kwa Raha Zetu ambacho husikika kila jumapili kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 3 usiku.


sending...