MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

KanumbaFrontKatika siku kama ya leo,miaka 26 iliyopita pale mkoani Shinyanga, alizaliwa kijana na kupewa jina la Steven. Hivi leo ni maarufu kama Steven Kanumba au kama mwenyewe anavyojiita wakati mwingine “The Great”. Kwa maana hiyo,leo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Steven Charles Kanumba.Happy Birthday!

Kwa mtu yeyote ambaye anafuatilia maendeleo ya tasnia ya filamu nchini Tanzania,bila shaka atakubaliana na mimi nikisema kwamba Kanumba ni miongoni mwa waigizaji wa filamu(Film Actors) ambao ni maarufu zaidi nchini Tanzania. Leo hii ni vigumu kuiongelea sanaa ya filamu nchini bila kumhusisha Kanumba kwa njia moja ama nyingine.

Kwa hivyo,haishangazi sana kuona kwamba,katika mwaka uliopita jina lake lilikuwa takribani la kudumu katika vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo vya mtandaoni,mitaani nk. Bila shaka unakumbuka jinsi habari ya Kiingereza Vs Kiswahili ilivyozua mjadala wa kitaifa. Kila mtu akasema lake.

Baada ya mambo kama yale,mijadala kama ile,watu hupenda kujua what next? Nilimtafuta Steven Kanumba ili kujua machache kuhusu mipango yake ya mwaka huu.

Unajua Kanumba angependa kupata chakula cha mchana (lunch) na actors gani maarufu hapa ulimwenguni? Una habari kwamba katika Curriculum Vitae(CV) yake ameongeza cheo cha “Blogger”? Unajua ana malengo gani mwaka huu? Una habari kwamba Kanumba hivi sasa amedhamiria kuibua vipaji vingine katika ulimwengu wa uigizaji filamu? Fuatana nami;

BC: Mpaka sasa unalionaje soko la filamu nchini Tanzania? Kumekuwa na mabadiliko gani ya kimsingi ukilinganisha toka ulipoanza mpaka hivi leo?

SK: Soko limetanuka kiasi kwamba tunatambulika kimataifa. Pia hivi sasa makampuni ya kusambaza kazi zetu yameongezea ikiwemo na pesa kwa kiasi fulani tofauti na hapo mwanzo.Safari bado ni ndefu lakini angalau inatia moyo.

BC: Mwaka 2009 ndio tumeumaliza.Jina lako liligonga vyombo vya habari kwa mambo kadha wa kadha.Unaweza kusema umejifunza mambo gani katika mwaka ulioisha? (more…)

Imekuwa gumzo ulimwenguni kote.Ni filamu kutoka kwa Muongoza Sinema(Film Director),James Cameron. Huyu ndiye pia aliyetengeneza filamu maarufu ya Titanic.

Mpaka hivi sasa imeshaingiza zaidi ya $ 1 billion katika mapato ya sehemu mbalimbali za ulimwenguni.Rais Barack Obama na familia yake,waliitizama walipokuwa vacation huko Hawaii hivi karibuni. Ilibidi secret services watoe kila mtu kwenye jumba la sinema ili Obama na familia yake wapate kuiona bila bugudha au tishio lolote.Mambo ya wakubwa hayo!

Umeshaiona Avatar? Mimi sijaiona bado.Nipe ushauri.Nikaitazame pia au nisubiri tu kuiazima kwenye DVD? Tizama trailer yake hapo chini.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

baby-powder

Kila kukicha,watanzania mbalimbali waliotapakaa ulimwenguni kote wanazidi kuwa wabunifu na watu wanaothubutu kufanya mambo fulani fulani ambayo sio tu yanazidi kuiweka Tanzania mahali inapostahili katika ramani ya dunia ,bali pia kuongeza ujuzi,kuingiza vipato halali na zaidi to make us proud!

Hayo yanatokea katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya filamu!Bila shaka ulifuatilia filamu za Kibira za Bongoland.Ukipenda unaweza kusema ule ulikuwa ni mwanzo tu.Wengine wamefuata nyayo hizo na wanakuja na filamu inayokwenda kwa jina la BABY POWDER. Ni watanzania wanaoishi jijini Atlanta,GA.

Filamu hii inatarajiwa kuonekana kwa mara ya kwanza kabisa ndani ya jiji la Atlanta lililopo jimboni Georgia nchini Marekani tarehe 14 November,2009.Baada ya hapo itaonyeshwa jijini Houston huko Texas tarehe 26 November,2009 na kisha jijini Washington,DC tarehe 5 December 2009. Baada ya hapo itakuwa zamu ya watu wa Minnesota kuiona tarehe 19 December 2009 kabla ya tour ya Europe na Africa haijaanza tarehe 25 December 2009. Tarehe na miji itakapoonyeshwa filamu hiyo zitatangazwa baadaye.

BABY POWDER ni filamu inayogusa maisha ya kweli . PHILIP NKASA (Lambert “LBT” Tibaigana) ni kijana wa kitanzania ambaye anakwenda Marekani kwa matumaini ya kupata elimu ili kuweza kuboresha maisha yake na ya familia yake nyumbani. Philip ananzaa maisha yake ndani ya Marekani katika mji mdogo wa Wichita,KS na baada ya kumaliza shule na kushindwa kupata kazi ,Philip anakata shauri kwenda kujaribu bahati yake katika jiji la Atlanta, GA.

Mambo hayawi kama Philip alivyotegemea.Upatikanaji wa kazi jijini Atlanta unakua wa shida.Ili kuendesha maisha Philip anachukua kazi ya malipo kidogo pamoja na kuwa tayari ni msomi mwenye shahada ya kwanza(degree)Hali ya maisha ya wazee wake inaendela kuwa mbaya kutokana na mapato yake kuwa kidogo na hivyo kushindwa kuwasaidia.

Tizama Trailer hapa;

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Baada ya kugundua mfanyakazi mwenzake Mamdo (Albert Levasseur) anafanya biashara haramu, Philip anaona hiyo ndio nafasi ya kutatua matatizo yake.Baada ya kuonja asali anachonga mzinga. Anaingia katika biashara  haramu kwa nguvu zote. (more…)

vinara-voting3-copybc

TUZO ZA
VINARA WA FILAMU 2009 KUWASHIRIKISHA WANANCHI

Mchakato wa kutafuta vinara wa filamu Tanzania kwa mwaka huu utawahusisha wananchi kupitia upigaji kura.

Wapenzi wa tasnia ya filamu nchini watapendekeza filamu ambazo wanaona zinastahili kuingia tuzo za vinara wa filamu. Mbali an wananchi pia kuna taasisi mbali mbali kama vile kampuni ya uhasibu inayotambulika kimataifa litasimamia zoezi la mapendekezo ya filamu. Filamu zenye kura nyingi ndizo zitakazoingia katika tuzo hizi. Pia filamu zitakubaliwa kutokana na mapendekezo ya waandaaji na majaji.

Kuteua filamu ni kwa njia ya ujumbe mfupi ambapo mpenzi atatakiwa kuandika neon vinara kasha jina la filamu anayoipenda na kutuma kwenda 15551 kwa gharama ya Tshs 300.

Vipengele vitakavyowaniwa mwaka huu katika tuzo za vinara ni Mwigizaji bora wa kiume na wa kike wa mwaka, Mwigizaji chipukizi wa kiume na wa kike, Filamu bora ya mwaka, Muongozaji bora wa Mwaka, Mwandishi bora wa filamu, Adui bora, Msanii bora msaidizi wa kiume na wa kike, Mhariri bora wa mwaka, Mtunza Sauti bora, Mtunza Mwanga bora, Mpiga picha bora wa mwaka, Mtayarishaji bora wa filamu, Mtunzi bora wa filamu, Mapambo na maleba bora, msanii maarufu wa kiume na kike na Tuzo ya heshima.

Vipengele vilivyoongezwa ni mtunza taa bora, mtayarishaji bora wa filamu (producer) na wasanii maarufu wa kike na wakiume (People’s choice Award).

Mwaka huu kampuni mbali mbali zimejitokeza kudhamini mashindano haya lakini yatatajwa baada ya upigaji kura

Filamu zinazostahili kupendekezwa ni zile zilizotengenezwa kuanzia januari 2009. Filamu zitakazo ingia moja kwa moja ni zile ambazo bado hazijaingia sokoni lakini yatawasilishwa na watengeza filamu wenyewe.

Zoezi la kupendekeza filamu litafanyika hadi septemba 30 kabla ya kupatikana wahusika kwenye kila kipengele kabla ya wananchi kupiga kura kuwapata washindi.

Khadija Khalili

Mratibu


frankbcNiliwahi kusikia mahali fulani watu wa nchi jirani na Tanzania wakisema kwamba Tanzania huwa inachelewa kidogo kuanza mambo lakini pindi wanapoanza huwa wanakuja juu kwa kasi ya ajabu! Bila kuingilia mazungumzo yao,jamaa wakawa wanataja mifano kama vile jinsi ambavyo Tanzania imepiga hatua kwenye shughuli za kisanii kama vile muziki na hivi sasa filamu.

Kuna ukweli ndani yake; tunaweza kuanza mwisho lakini tukawa vinara. Yote inategemea jinsi ambavyo tunaamua kujiweka na kusonga mbele. Mojawapo ni kukubali kwamba kuna kukosea na pia kujirekebisha. Hivi sasa sanaa ya filamu inazidi kukua nchini Tanzania. Inatia moyo sana kuona watu wa mataifa mengine wanaangalia filamu ambazo zinaitwa “za kibongo”. 

Pamoja na hayo kazi kubwa bado ipo mbeleni.Kama alivyowahi kusema Steven Kanumba tulipohojiana naye,kuna haja ya serikali kutoa support ya kutosha ili kuzidi kuinua sanaa hiyo. Marekani ipo hapo ilipo kwa sababu ilitangaza sanaa na sera zake za mambo ya nje kupitia kwenye filamu. Ikulu ya Marekani ina kitengo cha kushughulikia masuala ya filamu.Kama filamu itaonekana haijakaa “vizuri” kwa mujibu wa taratibu zao,basi haitoki.Mradi unakufa.

Lingine ni hili ambalo muigizaji Mohamed Mwikongi(pichani) almaarufu kama Frank katika uigizaji ameliongelea majuzi alipofanya mahojiano na jamaa wa Global Publishers. Frank anasema lazima wasanii na washika dau wote katika nyanja za filamu wakubali kukosolewa. Wazungu wanaita hii constructive criticism. Unapokubali kukosolewa unajipa nafasi ya ushindi kwani maana yake ni kwamba kesho utafanya kizuri zaidi.Lakini pia ipo haja ya wakosoaji kutokuwa “wabezaji”. Unapokosoa basi useme pia sababu zako na utoe ushauri wa kujenga kwamba nini kifanyike.Kwa mwendo huo filamu za kibongo zitazidi kupata jina na sio ajabu kabisa siku moja nasi tukaona Slumdog Millionare za kikwetu.

dokiiNatumai hujamsahau. Jina lake halisi ni Ummy Wenceslaus.Kwa mashabiki wa sanaa ya uigizaji ukimtaja kwa jina la Dokii watakuelewa kirahisi zaidi. Enzi za kikundi cha uigizaji cha Mambo Hayo, Dokii alijizolea umaarufu kwa jinsi alivyoweza kuigiza katika lafudhi ya kiswahili cha nchi jirani ya Kenya.Ilifikia mahali wengine wakaamini kabisa kwamba Dokii ni Mkenya!

Baada ya hapo,kimya kilitanda.Dokii akabadili uelekeo wa maisha baada ya “kujisalimisha kwa Bwana”.Akahamia kwenye muziki wa injili ambapo hakuna uhakika sana kuhusiana na kutamba au kutokutamba kwake.

Sasa Dokii ameamua kurejea tena kwenye uigizaji na filamu.Anakuja na filamu itakayokwenda kwa jina “Bad Friend”.Anasema katika filamu hiyo,lafudhi si ya kikenya tena bali safari hii ni kijaluo.

Yote hayo na mengine tele hususani suala zima la kuokoka na kuigiza amemueleza Eugenia Kimolo wa Tanzania Daima.Bonyeza hapa usome zaidi.

Photo/Darhotwire.

Siku hizi inaelekea Tanzania inakuwa ndio chaguo la superstars wengi kutoka Marekani linapokuja suala la kupumzika au kutoa misaada mbalimbali ya kijamii ingawa wengi bado wanapenda kuingia na kutoka kimya kimya pengine kwa kuogopa “paparazzi wa kibongo”

Kuthibitisha hayo hivi leo waigizaji mashuhuri kutoka nchini Marekani,Will Smith na mkewe Jada Pinkett(si unawaona pichani?), leo hii wameonekana jijini Dar-es-salaam wakiwa wanatoka ndani ya The Kilimanjaro Hotel Kempinski tayari kuelekea visiwani Zanzibar.Kabla ya hapo Willy na Jada walikuwa wametoka Bagamayo mkoani Pwani ambapo walitoa msaada wa vyandarua katika Hospitali ya Wilaya Bagamoyo.

Shukrani Jiachie kwa picha hii.

Jina lake kamili ni Robert Gathecha Mongi.Wengi hivi leo tunamtambua kama Bobby.Bila shaka kabisa,Bobby ni miongoni mwa wasimamizi mahiri wa shughuli(MC),watangazaji wa radio na televisheni ambao Tanzania ya leo inaweza kujivunia.Awe anasimamia shughuli,radioni au kwenye televisheni ukimsikiliza utagundua jambo moja;anaipenda kazi yake na anaifanya kwa umakini na utulivu wa hali ya juu.Pengine utulivu huo ndio uliomfanya awe ni mtangazaji wa kutegemewa katika vituo mbalimbali vya radio nchini Tanzania na pia msimamizi wa shughuli zenye hadhi za kimataifa.

Pamoja na mafanikio na “soko” ambalo tayari alikuwa ameshajitengenezea,hivi karibuni alifanya uamuzi mgumu wa kuamua kurudi shuleni ili kunoa zaidi kipaji alichonacho.Hivi sasa anasoma katika Chuo Kikuu cha Cape Town nchini Afrika Kusini.Mbali na kuamua kurudi shule,Bobby ndio kwanza alikuwa “amepata jiko” kabla ya kuwa baba mapema baadaye.Mchanganyiko huo wa mambo ndio unaotufanya tuuite uamuzi wake wa kurudi shule kuwa mgumu!How is he handling all these?

Hivi karibuni tulipata nafasi ya kuzungumza naye machache kuhusiana na maisha yake,shule,ndoto zake na mengineyo mengi.Je anasemaje kuhusu Afrika Kusini anaposomea hivi sasa?Anasomea nini?Nini ushauri wake kwa vijana wanaoota kila siku kwenda “bondeni”?Anazungumziaje maendeleo ya muziki na filamu ya Tanzania akilinganisha na Afrika Kusini? Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; (more…)

Jina lake halisi ni Yvonne Cherry.Ila ukitaka watu watambue haraka kwamba unamuongelea nani basi huna budi kumuita “Monalisa” kwani ndio jina ambalo wengi wamelizoea kutokana na fani yake ya uigizaji filamu kitu ambacho binti huyu amebobea.Monalisa aliwahi kuwa mke wa prodyuza maarufu wa filamu aitwaye George Otieno almaarufu kama Tyson kabla mambo hayajakwenda ndivyo visivyo.

Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar au kwa lugha ya wenzetu Zanzibar International Film Festival limemalizika hivi karibuni huko Zanzibar.Tamasha lilifana na pia lilipambwa na wasanii mbalimbali mahiri wa kitanzania.Ngoja picha ziongee. Picha zote na Peter Bennett.

Prof.Jay alikuwepo kuwapa raha kamili mashabiki wake.

Bingwa wa mashairi au mistari, MwanaFA alikuwa gado jukwaani kujibu swali MwanaFA unaoa lini?

AY hakuachwa nyuma.Hapa kwa kushirikiana na MwanaFA(unayemuona kwa mbali) walikuwa wanasema Habari Ndio Hiyo

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page