Recent Articles
“NASIMAMA”-LADY JAYDEE [OFFICIAL VIDEO]

NASIMAMA-LADY JAYDEE [OFFICIAL VIDEO]

If life was like a straight line, it would probably be very boring. I believe, as human beings, we are made to see and cope ...

Read More

RAY C SET TO MAKE A COMEBACK IN MUSIC

RAY C SET TO MAKE A COMEBACK IN MUSIC

The story of her life is now one of the most inspiring. She was once upon a time one of the most sought,loved and paid ...

Read More

REST IN PEACE MAALIM GURUMO

REST IN PEACE MAALIM GURUMO

After an on and off lengthy illness, Tanzanian veteran musician,Maalim ,Gurumo passed away yesterday in Dar es Salaam. Maalim Gurumo died at the Muhimbili National ...

Read More

MZUNGU KICHAA ALMOST “TELL-IT-ALL” ON THE SPORAH SHOW

MZUNGU KICHAA ALMOST TELL-IT-ALL ON THE SPORAH SHOW

I predict this interview will create some buzz...in good and probably not  so good vibes[it all depend on the mindset]. Mzungu Kichaa talks about Tanzanian ...

Read More

LUPITA ON MARIE CLAIRE [MAY ISSUE OF "FRESH FACES"]

LUPITA ON MARIE CLAIRE [MAY ISSUE OF FRESH FACES]

“I wasn’t a follower of fashion. It was a world unknown. Then I met my stylist, Micaela Erlanger, and we came to interpret my style: ...

Read More

RAHA ZA JAY Z, MKEWE BEYONCE NA MTOTO WAO KUTOKA DOMINICAN REPUBLIC

RAHA ZA JAY Z, MKEWE BEYONCE NA MTOTO WAO KUTOKA DOMINICAN REPUBLIC

Hakuna ubishi kwamba Jay Z na mkewe Beyonce ni couple inayotamba zaidi kiasi kwamba kila wanalolifanya au kusema hupamba kurasa za mbele za vyombo vya ...

Read More

THE OTHER SIDE OF ANNE KANSIIME

THE OTHER SIDE OF ANNE KANSIIME

Anne Kansiime is without a doubt the top female comedian in East Africa as I write this post. If you haven't heard of her I'd ...

Read More

“MY GAL”-PREZZO [OFFICIAL VIDEO]

MY GAL-PREZZO [OFFICIAL VIDEO]

If you dare touch the cables containing words like love,celebrities from East Africa, social networks etc...somewhere in between the name Prezzo will pop up. He ...

Read More

“LISA LOVE”-MILLIAN Feat.CHID

LISA LOVE-MILLIAN Feat.CHID

I am not sure whether Millian has a recollection of what I am about to write here. I have known him since late 90s. We ...

Read More

PANEL DISCUSSION AT HOWARD UNIVERSITY: THE FUTURE OF EDUCATION IN TANZANIA

PANEL DISCUSSION: THE FUTURE OF EDUCATION IN TANZANIA

Read More

“FAITH”-MAD ICE [OFFICIAL VIDEO]

FAITH-MAD ICE [OFFICIAL VIDEO]

Few weeks ago, we introduced Mad Ice's latest single titled Faith. It was and still is one of the best songs I have heard for ...

Read More

2 SINGLES FROM WAKAZI

2 SINGLES FROM WAKAZI

The Tanzanian Emcee Drops 2 new singles as part of his new ritual of dropping 2 songs at a time. Sexy Lady, produced by Lucci, ...

Read More

“UKIPENDWA RINGA”-Z-ANTO

UKIPENDWA RINGA-Z-ANTO

Z-Anto anasema Ukipendwa Ringa. Eti ni kweli? Utajuaje unapendwa?Mmmh well...Z-Anto anasema ruksa "kujishebedua" mtoto wa kike ukipendwa.Msikilize  

Read More

WEMA SEPETU AND GLOBAL PUBLISHERZ

WEMA SEPETU AND GLOBAL PUBLISHERZ

This may surprise you or it may not. It all depends on who you are and what kind of life you live. Wema Sepetu knows ...

Read More

“VUMILIA”-JOHN RODGERS,SHILAH AND DAVIZO[NeW TrAcK]

VUMILIA-JOHN RODGERS,SHILAH AND DAVIZO[NeW TrAcK]

Tangu tukiwa watoto tumekukuwa tukisisitiziwa suala la uvumilivu. Wenzetu wa magharibini wanasema Patience.Naam,vumilia kila aina ya majaribu utakayokutana nayo hapa duniani. Ni mengi.Jua linapochomoza yapo.Jua ...

Read MoreJuu hapo ni cover ya filamu mpya ya Marehemu Steven Charles Kanumba. Inasambazwa na Steps Entertainment.One of the films I’d like to watch.

Be Sociable, Share!

Maisha yana majaribu.Kila siku ina changamoto yake.Labda hivyo ndivyo tunavyoweza kusema kwa kusoma,kusikia na kuona yale ambayo Ray Kigosi amepitia kwa mwaka huu tu wa 2012.Bila shaka ni mengi.Na mengi zaidi.Wiki iliyopita,Jumatatu ile,ndiye aliyeketi na Salama Jabir katika Mkasi na kusema yaliyo moyoni mwake.

Haya hapa mahojiano kamili ambayo kama yalivyo mengine,yote huanzia pale Amaya Beauty Salon & Spa,katikakati ya jiji la Dar-es-salaam(ndani ya kampaundi ya Air Tanzania Corporation-ATC) katika makutano ya mitaa ya Garden na Ohio.Hebu usijivunge,wapigie(0753 26 29 24, 078426 29 24 and 0716 60 44 95),watembelee na wewe upendeze kama wenzako wajanja wa mjini.WORD!

 You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Be Sociable, Share!

Over the weekend, there was one event that attracted quite an attention in Tanzania especially across the  social media platforms.It was a launch of a movie titled Super Star which tells a life story(so far) of a former Miss Tanzania and actress,Wema Sepetu.The launch happened at Hyatt Hotel in Dar-es-salaam.

The above is a photo from the event.For more photos and news on this event,press here.

Be Sociable, Share!

Siku chache zijazo,msanii Steve Nyerere,ambaye yaelekea ameamua kujikita katika filamu zenye uhalisia fulani hususani zenye mrengo wa kisiasa,anatarajiwa kuzindua filamu yake mpya inayokwenda kwa jina Respect Nyerere ikiwa ni filamu kuhusu baadhi ya matukio au mambo yatokanayo na maisha ya Baba wa Taifa,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Steve Nyerere ambaye hivi karibuni alitoa filamu ya Mr.President ambayo ni filamu yenye matukio sambamba na maisha ya Rais wa sasa,Jakaya Mrisho Kikwete,amesema filamu ya Respect Nyerere itazinduliwa rasmi tarehe 14 Februari 2012 katika Hotel ya Serena jijini Dar-es-salaam.

Be Sociable, Share!

Jina lake unayemuona hapo juu ni Zuwena Mohamed.Ila kwa wengi anajulikana kama Shilole.Sina hakika kama Shilole jina lake la tokea utotoni au ni jina la kisanii.Ni muigizaji wa filamu nchini Tanzania na yes anaimba pia.

BC inajiandaa kuambaa na Shilole katika mahojiano maalum.Je,unalo swali au maswali ambayo ungependa Shilole ayajibu?Kama jibu lako ni NDIO basi usisite kuyatuma maswali yako kwenda bongocelebrity at gmail dot com(anuani pepe imewekwa hivyo ili kupunguza hackers).

ANGALIZO: Maswali yalenge katika kujenga na sio kubomoa

Picha kwa hisani ya Global Publishers.

Be Sociable, Share!

Miezi kadhaa nyuma niliwahi kuuliza swali kuhusu nani aliye zaidi katika ya Steven Kanumba na Ray Kigosi.Mashabiki na wafuatiliaji wa Bongo Movies mkatoa ushirikiano mkubwa na kueleza bayana yule ambaye mnadhani ni zaidi ya mwenzake.Mpaka leo hii bado comments kuhusu hoja ile bado zinaendelea.Hiyo,kwa upande mwingine,inaonyesha ni kwa jinsi gani watu zaidi wanafuatilia sanaa ya filamu nchini Tanzania.Ni jambo zuri.

Leo naomba tuhamie kidogo upande wa waigizaji wa kike kwani ni wazi kabisa na wao wanafanya vizuri sana katika kuendeleza fani hii ambayo kwa miongo kadhaa ilipewa kisogo.Mchango wao ni dhahiri.Hapa naomba niwaweke “kikaangoni” Monalisa (Yvonne Cherryl) na Blandina Chagula maarufu kama Johari. Bila shaka umeshawahi kuwaona katika uigizaji wa aina mbalimbali.Endapo ungekuwa na filamu yako na ukawa unatafuta mwigizaji wa kike(lead actress) ungemchagua nani katika ya Monalisa au Johari.Kwa ufupi unadhani nani zaidi kati yao?Kwanini?

Johari

Be Sociable, Share!

Muigizaji maarufu wa filamu za kibongo(Bongo Movies), Steve Kanumba, ana muonekano mpya.Sio muonekano mpya wa kubadili labda style ya nywele au rangi ya ngozi yake bali size ya mwili wake.Anasema baada ya kushauriwa na mashabiki wake kwamba ameanza kuelekea kwenye “michelin marathon”,akaamua kuitikia wito wa mashabiki wake waliomtaka apungue ili arudie zama zake. Sasa ameshapungua kama picha zinavyoonekana. Anauliza mashabiki wake kama aendelee kupungua au aishie hapo hapo.

Unaweza kumpa ushauri hapa au kwa kutembelea blog yake kwa kubonyeza hapa.Hizi hapa baadhi ya picha jinsi alivyo hivi sasa.

Be Sociable, Share!

Kwa takribani miezi minne sasa,watanzania na watu wote wanaoongea au kutumia lugha ya Kiswahili wamekuwa wakiburudika na kuelimika kupitia channel mpya kabisa ndani ya DSTV inayokwenda kwa jina Africa Magic Swahili inayopatikana katika namba 127. Hivyo hutokosea ukiamua kuiita Channel 127 ya DSTV.Kama bado hujapata fursa ya kutazama Channel 127,nakushauri ufanye hivyo leo hii.

Nini kilipelekea kuanzishwa kwa Channel hiyo ambayo kila kukicha inazidi kujipatia umaarufu? Inawasaidiaje wasanii wa tasnia ya filamu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati katika kutimiza malengo yao na kupanua soko lao?Je,utaratibu wa kuingiza filamu yako katika Channel hiyo kama wewe ni muundaaji,muongozaji au msanii wa filamu ukoje?

Ili kupata majibu kwa maswali hayo na mengineyo,nilimtafuta Meneja Masoko wa DSTV-Tanzania,Furaha Samalu(pichani).Hapo chini ni maswali niliyomuuliza na majibu kutoka kwake;Fuatana nasi…

BC: Furaha,karibu sana ndani ya BC,pole na kazi.Mambo yanakwendaje?

FS : Mambo ni safi kabisa…Ahsante sana

BC :    Yapo mambo mengi sana ambayo tunaweza kuzungumzia kuhusiana na kazi yako au kazi zenu lakini kwa leo tumekutafuta ili kuzungumzia Channel 127 katika DSTV.Channel hii imeanza rasmi lini na kwanini mkaamua kuanzisha channel hii? Mchakato huo ulikwendaje?

FS : Kwanza kabisa nishukuru sana BC kwa kunipa nafasi ya kuzumza na watanzania na kuwafahamisha zaidi juu ya chaneli yetu maarufu kabisa iitwayo AFRICA MAGIC SWAHILI inayopatikana katika vifurushi vyote vya DStv kwenye chaneli number 127.Africa Magic Swahili ilianza kurushwa kwenye DStv platform tarehe 1st of July 2011 na inaonekana masaa 24 katika nchi zifuatazo Tanzania, Kenya, Uganda, Ethiopia, Rwanda, Burundi, Congo and the DRC.

DStv iliamua kuanzisha chaneli hii mahususi kabisa kwa nchi za Afica Mashariki kama sehemu pekee ya kuonyesha kazi na utamaduni wa nchi hizi…kwa kuzingatia uwezo na utajiri mkubwa katika fani ya sinema na burudani mabalimbali uliopo katika nchi hizi.


BC : Nimepitapita mitaani na kukuta watu wengi wakitizama Channel 127.Sasa huu wangu unaweza kuwa mtazamo ambao sio sahihi kwa njia moja au nyingine.Kwenu ninyi wenyewe,mpaka hivi sasa mwitikio umekuwaje?

FS : Napenda kuwashukuru sana watanzania na hasa wasanii wa fani mbali mbali kama sinema, muziki na tamthilia kwa muitikio wao mzuri sana ambao unaifanya chaneli yetu hii ya Africa Magic Swahili iendelee kukuwa siku hadi siku.

Mpaka sasa watanzania ndio tunaoongoza kwa kutuma kazi zetu kwenye chaneli hii, nchi zingine za Africa mashariki zikifuata.

read more

Be Sociable, Share!

Msanii wa filamu za kitanzania maarufu kama Bongo Movies,Jacqueline Wolper Massawe,ana muonekano mpya kama picha zinavyoonyesha.Nini maoni yako?Amechemsha au ametoka swadakta?

Photos Courtesy of Ray The Greatest Blog

Be Sociable, Share!

Ingawa historia ya filamu za kitanzania au Kiswahili ina historia ndefu(tangu enzi za kina Yombayomba,Chale Mwembamba na Mnene,Maangamizi nk),hakuna ubishi kwamba unapoongelea masuala ya sanaa hiyo hivi sasa,ni vigumu kuwaweka kapuni vijana wawili;Steven Kanumba na Ray Kigosi(kama wanavyoonekana hapo juu pichani).Kwa sababu mbalimbali,zikiwemo wingi wa filamu walizocheza na kuongoza(hili bado halinipi amani ya kweli),ndizo zinazowaweka mbele ya wenzao.

Mbaya au zuri ni kwamba Kanumba na Kigosi ni marafiki.Wenyewe wanapenda kutumia neno “swahiba” wanapotajana iwe ni hadharani au katika blog zao(Ya Kanumba hii hapa na ya Kigosi hii hapa).Pamoja na urafiki walionao,ninavyojua mimi Ray na Kanumba ni washindani. Wamewahi wenyewe kuongelea suala na “kufunikana” kama filamu.Kwamba mimi ni zaidi ya wewe na mambo kama hayo.

Hilo ndilo linalonifanya leo nikuletee wewe msomaji (natumaini u-mpenzi wa filamu za kitanzania[bongo films/movies]) nafasi ya kuwa jaji.Kwa mtizamo wako na kwa jinsi ambavyo umekuwa ukifuatilia filamu au uigizaji wa Steven Kanumba na Ray Kigosi nani unadhani ni zaidi ya mwenzake? Na je unaweza kusema ni kwanini unadhani huyo unayesema ni zaidi ni zaidi ya mwenzake?Una ushauri gani kwake au kwao?

Be Sociable, Share!

← Read the Previous PageRead the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page