Here is the official video for Turn Up The Music by Chris Brown. This is his lead single from his fifth album titled Fortune.
Mashabiki wengi walitegemea kwamba picha za kwanza za mtoto wa Jay Z na Beyonce zitakapotoka zitakuwa baada ya wazazi hao kuingia mkataba labda na jarida moja kubwa kama ambavyo wazazi wengine maarufu wamekuwa wakifanya pindi wanapobarikiwa kupata mtoto.Katika hali ambayo imewashangaza mashabiki wengi,Jay Z na Beyonce wameziachia picha zinazowaonyesha wao na mtoto bila kuzitengenezea fedha juu yake.Hizi hapa.Mtoto Blue Ivy Carter huyo hapo
Anaitwa Macaulay Culkin,Ana miaka 32 hivi sasa.Aliwahi kutamba sana akiwa mtoto hususani katika movie maarufu sana ya Home Alone.Hivyo ndivyo anavyoonekana hivi sasa.Picha hizo za Entertainment Tonight zimeenea mtandaoni na wengi wameonyesha,kupitia maoni,kumuonea huruma kwa jinsi anavyoonekana kudhoofika.Watu wake wanasema hana tatizo lolote kiafya.Ni bukheri wa afya.Sasa nini nini basi?Maisha tu labda.
Alivyokuwa mdogo wakati wa filamu ya Home Alone
Wiki kadhaa tu baada ya kujifungua,mwimbaji Beyonce,hivi karibuni alijitokeza in public na anaonekana yuko gado na tayari ameshakata ile baby’s weight kwa kiasi chake.Hii ilikuwa hivi karibuni wakati alipohudhuria katika club ya 40/40 (ya mumewe Jay Z) jijini New York.
Wanawake wengi huwa wanapata tabu au wamekuwa wakilalamika sana kuhusu kuondoa baby weight baada ya kujifungua.Pamoja na hayo celebrities wengi hususani pande za US wameonekana kutokuwa na tatizo hilo sana kwani wiki kadhaa tu baada ya kujifungua huwa wanaonekana mtaani wakiwa tayari washa-loose weight kama anavyoonekana Mamake Ivy Blue hapo juu.Wanafanyaje?Na Je,kama wewe ni mwanamke au mtaalamu wa masuala ya afya ya kinamama na unasoma hapa,ungemshauri nini mwanamke ambaye anataka kutoa baby’s weight baada ya kujifungua?Na je,ina usalama kiafya?
Katika hatua ya kushangaza mwanzilishi wa show ya X-Factor, Simon Cowell ameamua kufanya mabadiliko makubwa katika show yake yake ya kuibua vipaji ya X-Factor inayorushwa na kituo cha televisheni cha Fox cha nchini Marekani. Simon,raia wa Uingereza mwenye sifa ya maneno makali lakini yenye ukweli ndani yake, alianza “vurugu” za kuipanga upya timu ya X-Factor kwa kumuondoa aliyekuwa host wa kipindi hicho raia mwenzake wa Uingereza, Steve Jones kabla ya kuwaweka pembeni Majaji wa show hiyo Paula Abdul(jaji mwenzake wa zamani katika American Idol) na Nicole Scherzinger na hivyo kumaanisha rasmi kwamba katika msimu wa pili wa show hiyo majaji watakaorudi tena ni LA Reid na yeye Simon pekee huku ikisubiriwa kwa hamu kuona kina nani wataziba pengo hilo.
Kwa mujibu wa mtandao wa The Hollywood Reporter, hivi karibuni Simon aliitisha kikao cha siri na timu ya wabunifu wa show hiyo huko nchini Uingereza ambako ndiko chimbuko la show hiyo. Nia ya kikao hicho inasemekana ilikuwa ni kufanya tathmini juu ya kilichotokea katika msimu wa kwanza wa show hiyo kwa upande wa Marekani kwani tofauti na ilivyokuwa imetarajiwa show hiyo haikupata watazamaji wengi au wa kutosha. Show hiyo ilianza kurushwa nchini Marekani tarehe 21 Septemba mwaka 2011.
Taarifa za awali kwamba Steve Jones asingerejea katika msimu wa pili wa show hiyo zilikuja jana Jumatatu pale kupitia mtandao wa Twitter, Steve mwenyewe alipoandika katika ukurasa wake akisema “sitorudi tena kama host katika msimu unaofuata,ni aibu lakini siwezi kulalamika kwani nilikuwa na wakati mzuri.Nawatakia kila la kheri wote katika show”
Yasemekana pia kwamba Simon hakumpigia simu Steve kumpa habari hizo na badala yake akamuachia jukumu hilo Producer wa show.
Muda mfupi baada ya hapo zikaja habari kwamba Nicole Scherzinger ambaye anajulikana zaidi kama member wa zamani wa kundi la Pussycat Dolls na ambaye mwezi Mei mwaka jana aliibuka mshindi katika shindano la Dancing With The Stars alikuwa pia anatemwa au anaachia ngazi kama jaji wa show hiyo. Taarifa mbalimbali zinapasha kwamba Nicole aliomba mwenyewe(na amepata baraka za Simon) kuachana na show hiyo ili aelekeze nguvu zake katika muziki wake huku akijiandaa na tour ya Ulaya mwaka huu.
Wakati Fox imethibitisha kuondoka kwa Jones na Scherizinger, neno rasmi juu ya Abdul bado halijatolewa huku show hiyo ikitarajiwa kurudi tena hewani tarehe 6 Februari .Inasemekana Simon ametaka majaji wenye majina makubwa na hivyo kuja.Christina Aguilera, Cee Hakika Green, Adam Levine, na Blake Shelton.
A good friend of mine,once told me that single people should pay more tax.I curiously asked him why! He told something I can never forget.He said,”Jeff, single people are more happy.Therefore,they deserve to pay more tax”. We laughed and joked a lot about it and the daylight went off.
Now looking at the new video by Ruben Studdard titled June 28th(I’m Single) and seeing how Ruben seems happy and smiling all through,I remembered what that friend of mine told me.We know that Ruben is single(apparently his wife is said to have asked for divorce when Ruben finances started stumbling.What a Jerk). Whether he is so happy because he is single now is a kind of question that only him can answer.I am not single so I just can’t tell,not now.Watch it below.
Recently Rihanna made headlines-again.As in most cases,it wasn’t for a great cause but another teenage in action.She was photographed smoking a joint/a puff,a blunt,a getta and you name it. If you have ever tasted a joint or tried it when you were younger,you probably can relate very well with Rihanna.She is experiencing.Trying.Is it supposed to be a big deal? You tell me
Sio mara nyingi kuona filamu kutoka Hollywood hususani ya Action ambayo kwa asilimia kubwa sana imesheheni waigizaji weusi(black actors). Marekani bado kuna mambo ya kibaguzi sana.Masuala ya rangi ya ngozi ya mtu(race) yangali yakitawala sana maisha ya wamarekani ingawa kwa kiasi kikubwa wamepiga hatua.Ni mzimu unaoendelea kuitafuna Marekani.
Nikizingatia ninayoyajua kuhusu siasa za ubaguzi wa rangi nchini Marekani na jinsi ambavyo vijana mtaani(weusi) wanajitumbukiza katika masuala yasiyofaa kwa kukosa tu role models na hata vitu vya kawaida vinavyoweza kuwafanya watembee kifua mbele na kujisikia watu wenye mchango mkubwa katika ujenzi wa taifa la Marekani,napata hamu sana ya kuiona filamu ya Red Tails ambayo imetoka hivi majuzi. Mtengeneza filamu maarufu,George Lucas,ndio ameongoza filamu hii.Mbali ya kutaka kuona jinsi gani filamu ya Action ya weusi watupu inavyoweza kuwa,kuna actors wawili ambao nawazimia sana ambao wanaongoza(lead actors) katika filamu hii.Hao ni Terrence Howard na Cuba-Gooding Jr.
Nasubiri kwa hamu kuiona filamu hii.Kama umeshaiona usinisimulie hapa.Niambie tu niende au nisiende.
Baada ya kupata mafanikio makubwa katika anga za muziki barani Afrika na duniani kote,Mwanamuziki maarufu kutoka nchini Senegal, Youssou N’Dour, ameamua kugeukia upande wa siasa na sasa ametangaza kwamba atagombea kiti cha Urais wa nchi hiyo katika uchaguzi mkuu wa Urais wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao wa February.
Youssou N’Dour,mwimbaji mashuhuri,mtunzi na muandaaji muziki,na sasa mfanyabiashara maarufu nchini Senegal,anatarajiwa kutoa upinzani mkali kwa Rais wa sasa wa nchi hiyo Abdoulaye Wade ambaye ametawala nchi hiyo tangu mwaka 2000. Sababu mojawapo anayoitaja N’Dour ambayo imechangia uamuzi wake wa kuingia kwenye kinyanganyiro cha Urais ni pamoja na kuombwa na watu wengi sana afanye hivyo.
Akitangaza nia yake kupitia kituo cha televisheni anachokimiliki,Television Futurs Medias, amesema “Nimezunguka dunia nzima na nimeona watu mbalimbali duniani kote na hivyo nadhani ninao uwezo wa kuiongoza nchi yangu ya Senegal.Mimi ndio chaguo mbadala”
Youssou N’Dour ambaye anatajwa na Jarida maarufu la Rolling Stone kama mwanamuziki maarufu zaidi barani Afrika miongoni mwa wanamuziki walio hai, amekuwa mpinzani mkali wa Rais wa sasa wa Senegal,Wade mwenye umri wa miaka 85 na amewahi kunukuliwa akisema Rais huyo sio tu kwamba ni mzee sana bali hivi sasa anasikia kupitia Mono na sio Stereo kama ilivyo kwake yeye.
Je,Youssou N’Dour atafanikiwa kushinda kiti hicho cha Urais kufuatia umarufu mkubwa alionao duniani kote kutokana na sanaa ya muziki?Tusubiri tuone.


sending...






