
Muimbaji wa nyimbo za Injili(Gospel) Upendo Nkone (pichani) anatarajiwa kufunga ndoa tarehe 17 October 2010 na Mchungaji John Mbeyela ambaye pia ni mjane mwenye watoto watatu.Ndoa hiyo itafungwa katika kanisa la Naioth kwa Mchungaji Mwasota.
Kwa mujibu wa mtandao wa Strictly Gospel,ndoa hiyo inakuja baada ya miaka 9 ya kuwa mjane. Upendo Nkone tayari anazo albamu tatu kibindoni zikiwa ni Mungu Baba,Hapa Nilipo na Zipo Faida.
We wish them all the best.
Photo Courtesy of Waimbaji wa Muziki wa Injili Tanzania Photostream
Nimewahi kusema siku za nyuma kwamba mojawapo ya mambo ambayo nayapenda hapa BC ni kupata nafasi ya kumtambulisha msanii katika jamii ya watembeleaji,wachangiaji na washirika wa BC.
Leo ninayo furaha kumtambulisha Patrick Newman,mtanzania, msanii wa muziki wa Gospel ambaye makazi yake ni pale Seattle,Washington nchini Marekani.
Kimsingi Patrick sio mgeni katika anga za muziki.Kwa muda sasa amekuwa akifanya kazi zake nchini Marekani.Amewahi pia kufanya maonyesho kadhaa nchini Tanzania na hivi sasa anajiandaa kufyatua album yake.
Huu hapa ni wimbo wake unaoitwa Siku ya Kifo.Bila kujali dini yako wala kabila,ni wimbo wenye ujumbe mzuri sana.Je ukifa hivi leo marafiki zako watasemaje? Watasema mazuri yepi na mabaya yepi?Usikilize.Well done Patrick.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Zaidi unaweza kutembelea blog ya Patrick kwa kubonyeza hapa.
Je imewahi kutokea ukahisi kukata tamaa ya kuishi kutokana na sababu mbalimbali za kimaisha? Yawezekana kabisa kwani huo ndio ukweli wa maisha.Kuna nyakati za furaha na kuna nyakati za kilio.Ndio maisha.
Ingawa maisha ndivyo yalivyo,siku zote tunashauriwa kutokukata tamaa.Tunaambiwa maisha ni mapambano na hivyo tuendelee kupambana daima. Mtu mmoja ameshawahi kuniambia kwamba katika dhambi kubwa ambazo binadamu anaweza kufanya hapa duniani,hakuna iliyozidi “kukata tamaa”.
Ujumbe kama huo hapo juu ndio uliomo katika wimbo mpya kutoka kwa Flora Mbasha. Ni wimbo wa ki-injili lakini ambao hauhitaji dini yeyote ili kupata ujumbe halisi uliomo.Wimbo unaitwa Usife Moyo. Karibu.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

A musical labor of love and faith that’s been a long time coming is completed and you’re invited to the celebration.
A California based artist and Minister, Dennis Massawe who is a native of Tanzania, has put his inspirational message of faith into songs and you’re invited to celebrate the release of his CD No More Limbo. His message transcends all faiths and his uplifting rhythms that combine gospel, reggae and soul will move you to get into the spirit of love.
His journey has not been easy but he believes all things are possible when you follow the path you were called to walk on. From childhood to teenage, Dennis grew up in the slums of Nairobi Kenya. He later moved to his native country Tanzania with his father where he started his family at the age of twenty five.
Massawe and his family were lead from Dar-es-salaam Tanzania to Southern California and when you hear his music you too will be inspired, motivated and encouraged to go from your journey of challenges and desperation to one filled with hope and purpose.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
** To listen to No More Limbo press the player above.To purchase the album click here.
For more information on Dennis Massawe, click here.
Muimbaji nyota wa nyimbo za Injili Tanzania mwenye album za JIPE MOYO, UNIFICHE, FURAHA YAKO,Flora Mbasha pichani (akiwa na mumewe Emmanuel Mbasha) ambapo kwa sasa anasikika na wimbo wake wa WANAWAKE ulioimbwa katika mahadhi ya mchiriku,ndiye msanii pekee wa muziki wa Injili atakayetumbuiza kwenye tamasha la uzinduzi wa album ya MSETO WA WAHAPAHAPA litakalofanyika Juni 7 2009 viwanja vya Coco Beach, mbali na yeye kushiriki tamasha hilo, waimbaji wengine watakaokuwepo kwenye tamasha hilo ni pamoja na Mzee Yusuph (Muimbaji wa Taarabu kutoka kundi la Jahaz Modern Taarab) Banana Zoro (kutokana B-Band), Enika (Muziki wa kizazi kipya) Calora Kinasha na Wahapahapa Band watatumbuiza kwa siku hiyo.
Pia WAHAPAHAPA ni tamthilia ya mchezo unaosikika kila jumatatu kwenye Radio Free Africa (RFA) na Radio One, lengo lao likiwa ni kuangalia athari za VVU/UKIMWI kwa vijana.

Akiwa tayari na albamu zisizopungua tano kibindoni, Jennifer Mgendi(pichani) ni miongoni mwa wanamuziki wa muziki wa injili au kwa kiingereza Gospel nchini Tanzania ambao wamejijengea sifa na umaarufu mkubwa kutokana na kazi yake hiyo ya uimbaji na kumtukuza mola.
Lakini tofauti moja kubwa ya Jennifer na wanamuziki wengine wa muziki wa injili ni kwamba yeye pia ni mtunzi mzuri wa hadithi za filamu.Baadhi ya filamu alizowahi kutunga ni kama vile Pigo la Faraja, Joto la Roho na Teke la Mama.
Alianza rasmi kujishughulisha na kazi ya muziki wa injili mwaka 1995.Albam yake ya kwanza iliitwa ‘Nini?’. Baada ya hapo alitoka tena na albamu zake zilizokwenda kwa majina ‘Ukarimu wake’, ‘Yesu Nakupenda’,'Nikiona Fahari’ na ya hivi karibuni zaidi inayoitwa Mchimba Mashimo.
Hivi karibuni tulipata nafasi ya kufanya naye mahojiano ambayo utayasoma hivi punde. Katika mahojiano haya,Jennifer anakupa kwa undani kuhusu historia yake kimuziki na kibinafsi. Ni kweli kwamba muziki wa injili wa leo ni wa “kidunia” zaidi ya “kiroho”? Anasemaje kuhusiana na hoja hiyo? Je Jennifer anaongeleaje tofauti za muziki wa injili na ule wa Bongo Fleva?Unakubaliana naye?
Nini mipango yake kwa mwaka huu wa 2009 na ana ushauri gani kwa vijana?Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;
BC: Karibu Jennifer ndani ya BC.Sijui nikuambie mambo vipi au bwana asifiwe?
JM:Asante sana ndugu yangu. Yote mema tu kwani mambo ni safi na Bwana anaendelea kusifiwa…
BC:Kwa kifupi tu unaweza kutueleza historia ya maisha yako?
JM:Nilizaliwa miaka karibu 37 iliyopita hapa hapa jijini Dar es Salaam katika familia ya watoto watatu nikiwa nimetanguliwa na kaka wawili. Nimepata elimu yangu katika mikoa ya Dar es salaam na Tanga. Nilianza uimbaji rasmi mwaka 1995 na hapo katikati nilifanya kazi kadhaa za kuajiriwa kama Ualimu na Ukutubi lakini tangu mwaka 2007 niliacha kazi za kuajiriwa na mpaka hivi leo ninafanya shughuli zangu binafsi. (more…)

Bila shaka unamkumbuka mwanamuziki au mwimbaji Renee Lamira(pichani).Aliwahi kutamba vilivyo na albamu yake iliyoitwa Ngoma ya Kwetu.Lakini je unafahamu kwamba Renee siku hizi ameachana na nyimbo zinazoitwa za “kidunia” na badala yake anafanya nyimbo za injili?

Pichani ni Flora Mbasha,mmojawapo miongoni mwa wanamuziki au waimbaji maarufu wa muziki wa injili(gospel) nchini Tanzania. Hapo alikuwa akiimba kwa hisia kali wimbo wake wa “Adui Yako”.
Flora ni miongoni mwa wana-gospel ambao nyimbo zao zinapatikana katika mkusanyiko wa nyimbo za injili ujulikanao kama Halleluya Collection(toleo la nne) kutoka kampuni ya Msama Promotions.Wasanii wengine walio na nyimbo ndani ya Halleluya Collection ni kama vile Rose Mhando, Modest Mogani,Catherine Mchepa,Hosana Group na Amos Muungwana.Collection hiyo inapatikana mitaani.Get your copy!

The Mission Band.Kutoka kushoto kwenda kulia ni Methuselah Kadigi (keyboard player and back-up singer),Fred J.Mwaituka(bass guitar player),Happy K.Holm(vocal lead),Hellen J.Mwaituka(back-up singer) na Isack L.Mayala(lead guitar player,back-up singer)
Bendera ya Tanzania ulimwenguni inapeperushwa na watu wengi,kwa njia mbalimbali. Njia mojawapo ambayo imekuwa ikitumika na ambayo pengine ndio rahisi na ya haraka zaidi ni kupitia muziki.Toka kona moja ya dunia mpaka nyingine muziki unakubalika kuwa ni “universal language”.
The Mission Band (pichani),kundi maarufu la watanzania linalopiga muziki wa injili(gospel) kutokea Alabaster,Alabama nchini Marekani wanalitambua hilo kwani ni mojawapo ya makundi ambayo yanaipeperusha bendera ya Tanzania vilivyo kwa kutumia muziki.Kwa wale ambao wako Marekani na wameshabahatika kuwashuhudia The Mission Band wakifanya vitu vyao,nadhani watakubaliana nasi kwamba bendi hii inaipeperusha bendera ya Tanzania vilivyo na ni watoa burudani ya aina yake.
Iwe wanapiga kwenye matamasha,harusi au makongamano kila mahali wamekuwa wakijizolea mashabiki kwa kutoa burudani ya gospel wakichanganya vionjo vya kiafrika na vya ki-magharibi katika nyimbo zao.
Hivi sasa wapo studio wakiandaa CD yao ya kwanza itakayokwenda kwa jina la The Mission.Ukitaka kujua mengi zaidi kuhusu The Mission Band,ratiba ya maonyesho yao,picha mbalimbali za maonyesho yao na pia kusikiliza sample kidogo ya kazi zao,tembelea tovuti yao ya themissionband.org.Pale pia unaweza kuona jinsi unavyoweza kuwaalika katika shughuli yako.BC inawatakia kila la kheri katika kazi zao.

Tunapoongelea muziki wa kizazi kipya siku hizi hatuongelei bongo flava pekee bali pia muziki wa injili (gospel).Aina hii ya muziki inazidi kupanda chati na kujipatia wapenzi lukuki.Cha kufurahisha zaidi ni kwamba vijana ndio haswa wanaupa nafasi muziki wa injili.Miongoni mwa vijana hao ni hao pichani Mary Fue na Matha Fue(tumeshindwa kutambua yupi ni yupi). Vijana hawa ni mapacha ambao wanasema wamedhamiria kuipeleka gospel kutoka Tanzania kimataifa.BC inawatakia kila la kheri.


