This is the Nyerere legacy I hold close to my heart when I see today’s Tanzania: Nyerere – A Leader Who Dared! (Nyerere – Kiongozi aliye thubutu).

Whatever may be your view of his legacy, Nyerere was the author of his story; and to the benefit of many across Africa and the world at large, he dared to do it his way. Nyerere challenges leaders of today to dare to be the authors of their story and to dream and act in support of a vision greater than the moment, even when faced with the greatest odds and most compelling adversity…

Pengine bila kiongozi kama Nyerere kusingekuwa na Mandela wala Afrika Kusini ilio huru na ndiyo maana Tanzania ilikuwa ni nchi ya kwanza aliyo itembelea Mandela baada ya kutoka jela. Lazima tukubali na kujivunia kuwa na kiongozi shupavu na mwenye muono wa namna hii. Hususani mwaka huu wa Kombe la Dunia, dunia ilipo shuhudia manufaa halisia ya ukombozi wa Taifa kubwa kama Afrika Kusini na kuweza kulileta Kombe hilo ndani ya bara letu. Tulistahili tumpe sifa Mwalimu kwani ndie kiongozi pekee aliye thubutu kusimamia mapambano dhidi ya Mabeberu bila kikomo. Si Mmarekani, si Mchina, si Mholanzi bali ni Taifa changa la Tanzania lililo kuwa mstari wa mbele likiongozwa na Mwalimu J K Nyerere – Kiongozi aliye thubutu.

Pengine bila kiongzi kama Nyerere tusingekuwa na taifa lenye mshikamano na lenye kuchukia utengano kama ilivyo sasa Tanzania. Siwezi fikiri ni wangapi walio na ujasiri wa kupangua mifumo ya utawala wa kikabila na wa kikoloni ili waweza kusimamia mwono wao wa Taifa moja linalo takiwa. Nyerere alidhubutu kufanya hivi. Hakutumia muda wake mwingi kulalamika na kushangaa mapungufu. Bali alithubutu kupangua na kupanga upya mambo jinsi alivyo ona yeye inafaa bila kujali maneno na minong’ono ya wanafiki wachache na wasio jali maslai ya wengi au kuwa na muono wa mbali. Hii ndio ilikua tabia yake mzee wetu Mwalimu J K Nyerere – kiongozi aliye thubutu.

Kama Baba wa Taifa alithubutu kufanya makubwa kama haya mbele ya upinzani mzito na vitisho ndani na nje ya nchi, je wewe Mwana wa Taifa unathubutu katika lipi?

Written By C.V Magavilla

www.magavilla.com

Julius Nyerere

Sote tunaweza kuwa maarufu, tunaweza kuwa chochote tunachotaka . Pamoja na hayo, jambo moja ambalo ni dhahiri itakuwa ni vigumu sana kulifikia ni kuwa maarufu na kuheshimika duniani kote kama ilivyokuwa kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye hivi leo tunakumbuka miaka kumi na moja (11) tangu afariki dunia mnamo tarehe kama ya leo mwaka 1999 kule nchini Uingereza katika hospitali ya Mtakatifu Thomas kwa ugonjwa wa saratani ya damu (leukemia).

Serikali ilipotangaza rasmi kwamba Nyerere hatunaye tena, uchungu na simanzi uliikumba nchi nzima na dunia kwa ujumla hususani kwa wale waliokuwa wanamjua Nyerere na kujua alichokuwa akikisimamia na alichokiamini. Bara la Afrika likawa limempoteza kipenzi chake, mtoto wa Afrika ambaye thamani ya mchango wake katika ukombozi wa bara la Afrika haina kipimo. Mpaka anafariki dunia alikuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha amani barani Afrika.Mfano mzuri ni mgogoro wa Burundi aliokuwa akijaribu kuusuluhisha. Mwenyewe aliwahi kutamka kwamba yeye ni mwafrika kwanza na kisha mjamaa.

Mpaka leo hii jina la Nyerere linabakia kuwa kitambulisho chetu kikubwa .Wakati mwingine zaidi hata ya jina la nchi yetu yaani Tanzania.Wapo watu wanaolijua jina la Nyerere na wala wasijue jina la Tanzania au hata Tanganyika. Haishangazi, alikuwa ni mwana wa Afrika kamili. Kadiri siku zinavyopita, taratibu baadhi yetu, hususani vijana wanaoitwa wa kizazi kipya, wanazidi kulisahau jina la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Viongozi wetu wengi wa sasa( ingawa wakati wa msiba wake waliahidi kumuenzi kwa hali na mali) wanaelekea kusahau kabisa ahadi zao! Wengi wanabakia kumuenzi kwa maneno na sio vitendo. read more

Leo imetimia miaka 26 tangu Tanzania ilipoondokewa na aliyekuwa Waziri Mkuu, Hayati Edward Moringe Sokoine,aliyefariki kwa ajali ya gari nje kidogo ya mji wa Morogoro akiwa safarini kutokea mkoani Dodoma yalipo makao makuu ya chama na serikali kuhudhuria kikao cha Bunge.

Sokoine,alionekana kuwa tegemeo la watu,ndoto ya kweli ya wanyonge.Bahati mbaya ni kwamba ajali ile ndio ilihitimisha safari yake hapa duniani na kuwaacha wengi wakiamini kwamba endapo angeishi zaidi,huenda Tanzania tunayoiona leo,ingekuwa tofauti.

Je ni kitu gani kinafanya imani kwamba angeendelea kuishi angeibadili sura ya Tanzania?Ni kauli zake,vitendo vyake au imani tu ya mwananchi wa kawaida? Na je unadhani angekuwa hai hivi leo angepambana vipi na “ufisadi”? Mungu aendelee kuilaza pema peponi roho yake.

Posti hii nilitakiwa kuipandisha jana lakini sikufanikiwa maana jana nilifunga kiroho na kifikra ili kumkumbuka Malcom X, mpigania haki za watu weusi kule Marikani. Malcom X alizaliwa na kupewa jina la Malcom Little kisha akaamua kubadili “Little” na kuweka “X” kwa kile alichodai kuwa jina la awali lilikuwa ni la kikoloni na lenye nia ya kuiba utu wake. “X” inasimama kama “Aliyepotea/Asiye na Jina” ikimaanisha Mwafrika aliyepoteza utambulisho wake baada ya kutekwa na kupelekwa utumwani kule Marikani.

Nimeona niweke posti hii ili tuelewe kwamba isingekuwa Malcom X na wengine waliotangulia kama Martin Luther King Jr., Mama Rosa Parks, au mapambano ya kuwakomboa watumwa ya Reli ya Ardhini” (Undeground Railroad) yaliyoongozwa na mwanamke mweusi Harieth Turbman, pengine Marekani ya leo isingekuwa na Rais Mweusi tunayemfahamu na kumshabikia, Barack Obama.

Malcom X alizaliwa katika familia yenye maisha duni na akiwa na umri wa miaka 13, baba yake ambaye alikuwa mpigania haki za watu weusi pia aliuawa na wazungu wabaguzi waliojulikana kama Ku Klux Klan (KKK), na mama yake alikuwa amefungiwa katika hospitali ya wagonjwa wa akili. Hivyo Malcom akaanza maisha ya kujitegemea akitumia wizi wa mifukoni kama njia ya kujipatia kipato.

Mwaka 1946 Malcom alifungwa jela kutokana na wizi. Akiwa Jela, Malcom ambaye hakuwahi kusoma vitabu akajikuta akiwa msomaji mkubwa wa vitabu ambavyo vilimwongezea maarifa aliyokuja kuyatumia baadae katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa watu weupe kwa watu weusi. read more

haroubbc

marijanbLeo imetimia miaka 14 tangu Marijani Rajabu au “Jabali la Muziki” aiage dunia.Marijani alikuwa nyota njema ya muziki kwa miaka mingi.Aliweza kushiriki katika uimbaji na utunzi wa nyimbo nyingi ambazo zilipendwa,zinapendwa na zitaendelea kupendwa au kusikilizwa kwa miaka mingine nenda rudi.

Tunzo zake nyingi ziliweza kutamba kutokana na ukweli kwamba ziliichoma au kuigusa jamii moja kwa moja.Alitunga na kuimba kwa nyakati zilizokuwepo enzi za uhai wake na kwa wakati ujao ambao ndio huu tulio nao mimi na wewe.

Tunapomkumbuka Marijani Rajabu hivi leo tumechagua nyimbo mbili za kuendana na kumbukumbu hii.Wa kwanza unaitwa Ndoa za Mateso.Hizi bado zipo.Hivi leo kuna watu wanateseka ndani ya ndoa.Inakuwaje na kwanini?Ni vigumu sana kuelewa na pengine ndio yale wengine wanapenda kuyaita “ya dunia” huku wakimuachia anayeitwa muumba awaongoze.Hayati Marijani Rajabu aliyaona hayo,kuyatungia nyimbo na kuyaimba majukwaani.Leo tunamkumbuka.

Ukisikiliza sana nyimbo za siku hizi utagundua jambo moja.Ni chache sana zinazogusia hali halisi ya siasa au uchumi achilia mbali sehemu zingine za jamii zaidi ya mapenzi. Leo hii karibuni kila wimbo unaotoka ni kuhusu mapenzi,kutamaniana,kuumizana kimapenzi nk.Sehemu zingine za jamii(ambazo naamini ni muhimu pia) zimesahauliwa. Jabali la Muziki yeye hakuwa hivyo.Aligusia karibuni kila kona.Pengine ndio maana,pamoja na kutoweka kwake miaka 14 iliyopita,anabakia kuwa “Jabali”.Wimbo wa pili ni uthibitisho wa ninachokiongelea hapo juu.Unaitwa  Dunia Uwanja wa Fujo.Hili sidhani kama linahitaji mjadala mwingi kwani ni wazi kwamba dunia ni uwanja wa fujo.Sikiliza kwa makini nyimbo zake kisha tusaidiane kujiuliza swali zuri; Nani mrithi wake miongoni mwa wanamuziki wa leo?

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Endelea kupumzika kwa amani Marijani.We still remember you!

Special Thanks: www.changamotoyetu.blogspot.com

maina

Mwisho wa wiki umewadia.Ni muda wa kupumzisha tena akili ingawa kimsingi sio kupumzika haswa bali ni kubadili muelekeo wa majukumu.Badala ya kuniga tai na kuelekea “mjini” kazini au kutafuta kazi,huu unakuwa ni muda mzuri wa vikao mbalimbali kama vile vya kifamilia,harusi ya rafiki,ubatizo,ubarikio nk.

Imekuwa wiki ngumu kiasi.Hapa BC tumekuwa “bize” kidogo tukijaribu kufanya mabadiliko kidogo kwenye mtandao.Bado tupo matengenezoni.Tunatumaini kwamba tutakapofikia tamati ya matengenezo basi tutakuwa na kitu bora zaidi na ambapo tutakuwa na uhuru zaidi.Tunashukuru kwa uvumilivu wako msomaji.

Kama ambavyo mmeshasikia,wiki hii fani ya muziki nchini Tanzania ilipata pigo la kuondokewa na mwimbaji mahiri wa Msondo,Joseph Maina(pichani). Maina alifikwa na mauti ndani ya daladala akiwa njiani kuelekea studio kufanya kile alichokuwa akikipenda maishani mwake(kuimba).

Kifo cha Maina ni pigo sio tu kwa wana Msondo Ngoma bali wapenzi wote wa muziki nchini Tanzania,ndugu,jamaa na marafiki.Tunatoa pole za dhati kwa wahusika wote.Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Katika kumkumbuka Joseph Maina,bonyeza hapa umtizame Joseph Maina anavyolalamika katika wimbo Kalunde.Pumzika salama Maina.

Kila nchi ulimwenguni ina mashujaa wake.Lakini tafsiri ya shujaa katika nchi nyingi ulimwenguni ikiwemo yetu ya Tanzania,huwa ni wale waliopigana vita iwe ya msituni,nchi kavu,majini nk.Hivi juzi nchini Tanzania ilikuwa ni siku ya kumbukumbu ya mashujaa.

Kama inavyoonekana pichani,katika siku kama hiyo,huwa ni wakati wa wanasiasa kuweka pembeni tofauti zao za kisera,kiitikadi na kimtazamo na kuikumbuka siku hiyo muhimu.

Pamoja na hayo,yawezekana kabisa kwamba wewe binafsi ukawa na shujaa wako binafsi.Kwa mfano,kwangu mimi shujaa ni mama yangu,aliyenizaa na kunilea mpaka kufikia hapa nilipo.Je kwako wewe nani ni shujaa wako ukiachilia mbali “mashujaa” tuliowakumbuka juzi?

Pichani ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi,CUF, Prof. Ibrahimu Lipumba (kulia) akifurahia jambo na mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, walipokutana katika maadhimisho ya siku ya mashujaa iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam juzi.

Leo ni mwaka mmoja tangu Mheshimiwa Amina Chifupa afariki dunia.BC inapenda kuungana na wote katika kumkumbuka.Muhimu ni kuhakikisha kwamba tunaendeleza yale mazuri yote aliyoyafanya,kuyaamini na kuyasimamia enzi za uhai wake.R.I.P Amina Chifupa.

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page