
Kila nchi ulimwenguni ina mashujaa wake.Lakini tafsiri ya shujaa katika nchi nyingi ulimwenguni ikiwemo yetu ya Tanzania,huwa ni wale waliopigana vita iwe ya msituni,nchi kavu,majini nk.Hivi juzi nchini Tanzania ilikuwa ni siku ya kumbukumbu ya mashujaa.
Kama inavyoonekana pichani,katika siku kama hiyo,huwa ni wakati wa wanasiasa kuweka pembeni tofauti zao za kisera,kiitikadi na kimtazamo na kuikumbuka siku hiyo muhimu.
Pamoja na hayo,yawezekana kabisa kwamba wewe binafsi ukawa na shujaa wako binafsi.Kwa mfano,kwangu mimi shujaa ni mama yangu,aliyenizaa na kunilea mpaka kufikia hapa nilipo.Je kwako wewe nani ni shujaa wako ukiachilia mbali “mashujaa” tuliowakumbuka juzi?
Pichani ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi,CUF, Prof. Ibrahimu Lipumba (kulia) akifurahia jambo na mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, walipokutana katika maadhimisho ya siku ya mashujaa iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam juzi.

Pichani ni Afande Alfred Tibaigana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar-es-salaam. Ungepata nafasi ya kuhojiana naye ungependa kumuuliza maswali gani? Picha kwa msaada wa Haki Ngowi.

RAIS Jakaya Kikwete amempandisha cheo Luteni Jenerali Davis Adolf Mwamunyange ,kuwa Jenerali na kumteua kuwa Mkuu wa Majeshi.
Jenerali Mwamunyange anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali George Waitara, ambaye amestaafu rasmi jana.
Kabla ya uteuzi huo, Mwamunyange alikuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Kwa habari zaidi bonyeza hapa.
Pichani Raisi Kikwete alipokuwa akimpa cheo cha Luteni Jeneral D.A Mwamunyange kabla ya kumpandisha tena na sasa kuwa Jenerali jana.


sending...