
Yapo mambo mengi hapa duniani ambayo hatuwezi kuwa na uhakika nayo.Lakini yapo machache ambayo tunaweza kuwa na uhakika nayo.Mojawapo ni kwamba kijana Hasheem Thabeet anafanya vizuri katika mpira wa kikapu vyuoni nchini Marekani.Anaendelea kuwa “balozi” mzuri wa Tanzania kupitia michezo.
Majuzi nilipata nafasi ya kuongea naye machache. La msingi nililotaka kujua ni mipango yake kuhusu kujiunga na ligi ya NBA hapo mwakani. Hasheem anasema ni mapema bado kuliongelea swala hilo kwani hivi sasa anajaribu kuelekeza nguvu na akili yake katika michezo ya vyuo inayoendelea huku timu yake,maarufu kama The Huskies (kama wanavyoonekana pichani) wanaendelea kufanya vizuri.Hivi sasa wanatajwa kuwa miongoni mwa timu bora kabisa za mpira wa kikapu za vyuoni nchini Marekani.
Kesho(Jumamosi) saa nane mchana kwa saa za mashariki (2:00pm Eastern Time),The Huskies wanapambana na vijana wa Notre Dame katika mchezo wa marudiano.Katika mchezo wa kwanza The Huskies walishinda kwa vikapu 69-61. Mchezo wa kesho utaonyeshwa katika vituo vya CBS na vingine vingi vya michezo.Kila la kheri.
Update: Mchezo umekwisha na The Huskies wameshinda 72-65. Good job Hasheem na wenzako.
Kwa wale ambao mnafuatilia habari au kuangalia vipindi mbalimbali vya vichekesho kutoka nchini Marekani, habari ambazo si za kufurahisha ni kwamba mchekeshaji (comedian) na muigizaji filamu maarufu Bernie Mac(pichani) amefariki dunia.Bernie Mac ambaye alijizolea umaarufu kutokana na kipindi chake cha televisheni cha The Bernie Mac Show amefariki leo asubuhi katika hospitali ya Northwestern Memorial Hospital ya jijini Chicago nchini Marekani alipokuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa pneumonia.Wengine mtamkumbuka Bernie Mac kwa uigizaji wake wa hivi karibuni katika filamu kama vile Ocean Thirteen na Transformers.Bernie Mac alikuwa na umri wa miaka 50.Kwa undani zaidi wa habari hii unaweza kubonyeza hapa.
Kwa sababu tulikuletea matangazo kuhusu BBQ iliyofanyika jijini Chicago mwishoni mwa wiki iliyopita,tunadhani ni busara kukuletea pia picha kidogo ili kama hukupata nafasi ya kuhudhuria,basi japo uone jinsi mambo yalivyokuwa.Here we go;

Bingwa wa DanceHall kutoka Chicago,Bantuman,akiwapa burudani waliohudhuria.

Panapofuka moshi mara nyingi huwa pana chakula.

Ilipofika jioni mambo yalikuwa kama unavyoona pichani.

Pichani ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa Tanzania,Mheshimiwa Dr.David Homeli Mwakyusa(kushoto) akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Dr Asha-Rose Migiro wakiwa katika ofisi za Umoja wa Mataifa jijini New York hivi karibuni.
Siku hizi watanzania wanaotembelea ofisi za Umoja wa Mataifa wanasema wanajisikia faraja zaidi na kuhisi wako nyumbani kutokana na kuwepo kwa Dr.Migiro ambaye amekuwa akiwapokea vizuri sana.Safi sana Mama Migiro.
UN Photo/Paulo Filgueiras

Sifa moja ya miji mingi mikubwa duniani huwa ni pamoja na kuwa na majengo,ma-sanamu au kitu kingine chochote kikubwa ambacho hutumiwa kama kitambulisho au alama rasmi ya jiji husika.Kwa jiji la London lililopo nchini Uingereza, Tower Bridge(pichani) ni mojawapo ya “landmark” muhimu za jiji hilo.
Unaweza kusoma kuhusu historia ya Tower Bridge kwa kubonyeza hapa.Lakini wengi nadhani tungependa zaidi kusikia kutoka kwa wenzetu wanaoishi London au nchini Uingereza kuhusu umuhimu wa Tower Bridge kwa jiji la London.Tunakaribisha pia picha kama hizi kutoka katika majiji mengine duniani ambako tuna hakika watanzania wametapakaa huko.Hii yote ni katika kusaidiana katika kufunguana macho.Na je kwa jiji letu la Dar-es-salaam,tunaweza kusema “Askari Monument” ndio kitambulisho chetu rasmi?


sending...
