MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

kitangoma-adbc

ijumaa-front-pgbc

Kwa undani wa vichwa hivyo vya habari, bonyeza hapa au jipatie nakala yako mitaani.

kj

Kila siku ya Jumanne(kama leo hivi) watanzania siku hizi hupata nafasi ya kujiongezea maarifa mbalimbali,kuburudika,kujielimisha na kujifahamisha kupitia gazeti la Kwanza Jamii kama linavyoonekana katika picha ya hapo juu.Hiyo ni taswira halisi ya gazeti la wiki hii ambalo limeshatinga mitaani.

Humo ndani utakuta makala mbalimbali kutoka kwa waandishi mbalimbali nikiwemo mimi,Jeff Msangi. Wengine ni  kama vile Maggid Mjengwa, Freddy Macha, BAP (Born Again Pagan), Subi Sabato,Prof.Joseph Mbele, Dr.Bukaza Chachage, Joseph Mihangwa, Padri Privatus Karugendo, Eliamani Laltaika bila kusahau kona ya Aunt Subira na wengine wengi.

Lakini kama uko mbali na Tanzania au kwa sababu moja au nyingine huwezi kupata kopi halisi ya Kwanza Jamii, habari nzuri ni kwamba unaweza kuperuzi habari mbalimbali kupitia mtandaoni. Bonyeza hapa.

mjengwa-jamiibc

Maggid Mjengwa sio jina geni.Bila shaka kabisa umewahi kumsikia,kumsoma na pengine hata kutembelea blog yake ambayo kimsingi ni kimbilio la yeyote yule anayependa kupata picha halisi ya maisha ya mtanzania wa kawaida hususani yule anayeishi kijijini kama ilivyo kwa babu na bibi yangu.Wasomaji,watembeleaji na wachangiaji wa blog yake wanapenda kumuita “Mwenyekiti”.

Yeye ni miongoni mwa waandishi wa makala zenye kuchoma kama sio kugusa hisia za wengi.Ukitaka kujua historia yake ya uandishi unaweza kuipata kwa kusoma mahojiano tuliyowahi kufanya naye siku za nyuma kwa kubonyeza hapa.

Maggid ni mpenzi wa michezo hususani wa soka.Ni mnazi wa Simba.Ni upenzi huo wa soka na michezo kwa ujumla ambao ulimfanya aanzishe gazeti lililoitwa “Gozi Spoti” ambalo lilidumu mitaani mpaka hivi karibuni alipoamua kulisitisha.

Jambo jema ni kwamba, kuondoka kwa “Gozi Spoti” kulifanyika kwa makusudi ili kulipisha gazeti jipya litakalojulikana kama Kwanza Jamii ambalo litaingia mitaani siku si nyingi chini ya usimamizi wa Ikolo Investment Ltd kampuni iliyo chini ya mwenyewe “Mwenyekiti”.Kwa hiyo tunaweza kabisa kuongeza cheo kimoja kwa “Mwenyekiti” na kumuita Mjasiriamali.

Kwanza Jamii ni jarida la uchambuzi wa masuala yanayohusu na kuigusa jamii.Haya ni pamoja na siasa,uchumi,elimu,michezo na utamaduni.Pia yatakuwemo masuala ya mazingira,jinsia na ukimwi . Ni jarida litakalokuwa linatoka kila siku ya Jumanne.

Tumepata nafasi ya kufanya mahojiano mafupi na ‘Mwenyekiti” kuhusiana na ujio wa jarida hili na pia kumdadisi kuhusu anachokiona kila atembeleapo vijiji na vijiji vya Tanzania.Anaona nini?Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; (more…)

uyowa2bc

Irene Uwoya

wemabc

Wema Sepetu

Kwa muda sasa jamaa wa Global Publishers,kupitia gazeti lao la Ijumaa,wamekuwa wakiendesha shindano lililojulikana kama Ijumaa Sexiest Girl.Kilichokuwa kinafanyika ni kwamba kila wiki mrembo mmoja alikuwa anatolewa baada ya kupata kura za chini kushinda wengine.Wapiga kura walikuwa ni wananchi,wasomaji wa gazeti la Ijumaa.Kulikuwa na namba ya simu +255 784 275 714 ambapo wananchi walikuwa wanatuma ujumbe mfupi wa maneno(SMS) wakimpendekeza msichana ambaye kwa mujibu wao anastahili kushinda.Jumla ya warembo 12 walishirikishwa katika shindano hili.Unaweza kusoma zaidi kuhusu shindano hilo kwa kutembelea tovuti ya Global Publishers na kisha katika Search andika Ijumaa Sexiest Girl.

Sasa baada ya mchakamchaka mzima,warembo wawili, Irene Uwoya na Wema Sepetu(pichani) ndio wamebakia na mshindi anatarajiwa kutangazwa Ijumaa ijayo. Inawezekana hukupata nafasi ya kupiga kura wakati shindano lilipokuwa linaendelea.Pamoja na hayo,hapa una nafasi ya kutoa maoni yako.Nani unadhani ataibuka mshindi?Kwanini?

mengi

Miongoni mwa habari za watu maarufu ambazo bila shaka zimegubika vichwa vya wengi wiki hii ni ile ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP,Reginald Mengi kukanusha taarifa za gazeti moja kwamba amefunga ndoa mpya na mwanamke mmoja wa jijini Dar-es-salaam(Lilian Kimaro) na kulaumu uandishi wa habari unaokwenda kinyume na misingi ya taaluma hiyo.Kwa habari zaidi unaweza kubonyeza hapa.

Pia unaweza kubonyeza hapa ili kuona baadhi ya maswali ambayo waandishi wa habari walimbana nayo Mengi lakini akakwepa kwa kigezo kwamba wakatafute wenyewe ukweli!

Photo/Venance Nestory

Pichani ni Jenerali Ulimwengu.Huyu ni miongoni mwa waandishi wa habari nchini Tanzania walio na uwezo wa aina yake katika kujenga na kubomoa hoja iwe ni katika maandishi au maongezi.Makala zake siku hizi zinapatikana katika gazeti la Raia Mwema.

Photo/Bob Sankofa

Ukiweza kumalizia kichwa cha habari hapo juu utakuwa umepata mwangaza wa mtizamo wangu kuhusu vuta nikuvute inayoendelea kati ya Mchungaji Christopher Mtikila na Mbunge wa Igunga,Rostam Aziz.Kwa msaada zaidi wa kinachoendelea(kama bado hujafuatilia kinachoendelea) bonyeza hapa.Mwananchi amuamini nani?

Mjadala kuhusu mchango wa magazeti ya “Udaku” katika kujenga au kubomoa jamii una historia ndefu sana. Ni mjadala ambao ulikuwepo,upo na utaendelea kuwepo labda mpaka hapo itakapotokea kwamba maisha na watu watapotea katika sura ya ulimwengu.

Binadamu anabakia kuwa kiumbe mdadisi anayependa kupata habari,kujua kinachoendelea na pia hata kujua alichokifanya jirani yake jana usiku kama sio alichokifanya au anachokifanya mkuu wa nchi awapo mapumzikoni.

Nchini Tanzania, baada ya mapinduzi ya habari na mawasiliano,yaani baada ya kuvuka kile kipindi ambacho kulikuwa na magazeti matatu na kituo kimoja cha redio, paliibuka magazeti ambayo baadaye tumekuja kuyaita “magazeti ya udaku”. Hapo ndipo nasi tulipoingia rasmi kwenye mjadala wa; Je magazeti haya yana mchango gani katika jamii? Yanajenga au yanabomoa?

Hivi karibuni tulipata fursa adimu ya kufanya mahojiano na Abdallah Mrisho Salawi (pichani) Meneja Mkuu wa kampuni inayoongoza kwa uchapishaji wa magazeti ya “udaku” nchini Tanzania ya Global Publishers.Pamoja na mambo kadha wa kadha kumhusu yeye binafsi, Abdallah Mrisho anajaribu kueleza kuhusu kazi zao kama wanahabari na mchango wao au ubomoaji wao wa jamii.Hiyo itatokana na unavyoona wewe hasa baada ya kusoma alichotuambia Abdallah Mrisho.Pia anatoa ushauri muhimu kwa jamii hususani vijana kuhusiana na majanga kama umasikini,ukosefu wa ajira,ukimwi nk.Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; (more…)

↑ Go Back to Top of Page