MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Sheikh Yahya

MTABIRI maarufu wa Afrika Mashariki, Shehe Yahya Hussein ametabiri kuwa Rais Jakaya Kikwete atashinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao na atakayempinga ndani ya chama chake atakufa ghafla.

Sambamba na hilo, atakayeonekana kumshinda nje ya chama chake pia atapoteza maisha vivyo hivyo.

Akitoa utabiri wake jana Dar es Salaam, juu ya uchaguzi mkuu mwakani, Shehe Yahya alisema ushindi wa Rais Kikwete unatokana kurithishwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1995 ilipodaiwa kuwa Rais Kikwete alishinda kwenye kura za maoni lakini akamsihi amwachie Benjamin Mkapa.Kwa undani wa habari hii bonyeza hapa.

Je huu unaweza kuuita “utabiri” au ni…Unakubaliana naye ?Kwanini ?

Pichani juu ni Sheikh Yahya akiwa nyumbani kwake mapema mwaka huu.Ubavuni mwake ni mkewe Bi.Fetty

weddingbcWeekend ndio imewadia tena. Kama ulidhani wiki hii ingekuwa kavu kavu nchini Tanzania bila mikikimikiki basi ulikosea.Ilikuwa ni wiki ya “mipasho”. Ilikuwa ni rusha kombora nirushe kombora au kama vile alivyowahi kuimba Prof.Jay ukimwaga ugali mimi namwaga mboga!

Bahati nzuri ni kwamba nadhani watu wazima wamejiona ovyo na kuamua kufuata njia zinazostahili. Mchezo sasa umegeuka kuwa wa kudaiana “vijisenti”. Bila shaka umesikia mmoja kadai fidia ya Tshs Bilioni 10 huku mwingine akidai fidia ya Tsh 1 tu. Kama ingewezekana huenda angedai ile ya mkoloni kabisa iliyokuwa na tundu katikati. Sijui tugange yajayo au bado tuendelee na nguvu ya hoja,uchambuzi nk.

Tuyaache hayo.Leo ni burudani ya kale.Wenyewe mnaziita Zilipendwa. Natamani tungeziita Tunazozipenda kwani ukweli ni kwamba bado nyimbo hizi zina mafundisho kemkem na ni kama zilitungwa jana. Leo tunaye Gwiji Marijan Rajab(RIP). Wimbo unaitwa Ndoa ya Mateso. Binti karudi kwao.Anasema ndoa imemshinda.Mume anamtesa.Pesa zote anamalizia kwenye makuku ya kukaanga akiwa na “vimwana’ wake huko nje wakati familia inakufa kwa njaa.Binti hana msaada wowote,hana ndugu wala jamaa hapo alipo.Kwa masikitiko anauliza kwani kuolewa ni utumwa? Binti anaomba talaka yake.Mjumbe ndie anaombwa kuwa shahidi. Kwa uchungu na aibu anasimulia yaliyokuwa yanamsibu.Anataka kurudi nyumbani kwao kwani anasema hakuzaliwa juu ya miti bali ana kwao.Ana baba na mama. Mateso.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Pata burudani,pata ujumbe na furahia weekend yako. Maisha mafupi haya.

Jina lake kamili ni Robert Gathecha Mongi.Wengi hivi leo tunamtambua kama Bobby.Bila shaka kabisa,Bobby ni miongoni mwa wasimamizi mahiri wa shughuli(MC),watangazaji wa radio na televisheni ambao Tanzania ya leo inaweza kujivunia.Awe anasimamia shughuli,radioni au kwenye televisheni ukimsikiliza utagundua jambo moja;anaipenda kazi yake na anaifanya kwa umakini na utulivu wa hali ya juu.Pengine utulivu huo ndio uliomfanya awe ni mtangazaji wa kutegemewa katika vituo mbalimbali vya radio nchini Tanzania na pia msimamizi wa shughuli zenye hadhi za kimataifa.

Pamoja na mafanikio na “soko” ambalo tayari alikuwa ameshajitengenezea,hivi karibuni alifanya uamuzi mgumu wa kuamua kurudi shuleni ili kunoa zaidi kipaji alichonacho.Hivi sasa anasoma katika Chuo Kikuu cha Cape Town nchini Afrika Kusini.Mbali na kuamua kurudi shule,Bobby ndio kwanza alikuwa “amepata jiko” kabla ya kuwa baba mapema baadaye.Mchanganyiko huo wa mambo ndio unaotufanya tuuite uamuzi wake wa kurudi shule kuwa mgumu!How is he handling all these?

Hivi karibuni tulipata nafasi ya kuzungumza naye machache kuhusiana na maisha yake,shule,ndoto zake na mengineyo mengi.Je anasemaje kuhusu Afrika Kusini anaposomea hivi sasa?Anasomea nini?Nini ushauri wake kwa vijana wanaoota kila siku kwenda “bondeni”?Anazungumziaje maendeleo ya muziki na filamu ya Tanzania akilinganisha na Afrika Kusini? Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; (more…)

Bila shaka hujafanya bado dhambi ya kumsahau Mr.Paul.Huyu ni miongoni mwa wanamuziki ambao wapo katika lile kundi linaloweza kuitwa la “waanzilishi” wa aina za miziki ambazo hivi leo tunaziita miziki ya kizazi kipya.

Mr.Paul ambaye jina lake kamili ni Paul Mbena hivi sasa anaishi nchini Australia.Anafanya nini huko?Bado anajishughulisha na masuala ya muziki?Hivi karibuni alifanya mahojiano na blog ya Spoti na Starehe ambayo ndio kwanza imehamia katika makazi yake mapya ili kukupa wewe msomaji ladha zaidi na mambo lukuki zaidi.Bonyeza hapa ili kuwatembelea Spoti na Starehe na pia kusoma mahojiano yao na Mr.Paul.

Pichani juu ni Mr.Paul(kushoto) akiwa na mkewe Natascha Klocker huko nchini Australia.

Imekuwa ni wiki yenye mambo mchanganyiko.Wiki ilianza kwa mrembo mpya wa Miss Universe kupatikana.Kwa bahati mbaya hakuwa yule ambaye wengi wetu tungependa kuona anashinda.Taji likaenda nchini Venezuela.Hamna tabu,tutajaribu tena mwakani.

Kisha baada ya hapo likaja suala ambalo sisi hapa BC tumeona ni suala ambalo linahitaji kutokupuuziwa wala kupumzishwa kwa sababu zozote zile.Ni suala la mauaji ya albinos. Shukrani kwenu nyote mlioguswa pia na habari hizo na pia kuwa tayari kuungana nasi katika kuzidi kukemea na kujaribu kutokomeza kabisa imani hizo potofu na pia mauaji ya albinos kwa ujumla.Cha muhimu ni kuzidi kuelimishana na kuwapeleka katika mkono wa sheria wote wanaobainika kuhusika na ukatili huo.Kwa pamoja tunaweza.

Baada ya hapo likaja suala la Mtikila na mwenzake Rostam.Leo hii kila mmoja wetu anajua amuamini nani na amuache nani au la basi wote wanaingia kwenye lile kundi la politricians na wala sio politicians.Ili mradi tu imekuwa ni wiki nyingine yenye mauzamauza ya siasa.

Kama kawaida yetu,Ijumaa ni siku ya burudani na kupumzisha vichwa kidogo.Leo tumeona tuhame kidogo nchini kwetu na kuelekea Zaire(siku hizi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo).Pale tunamkuta Mbilia Bel ambaye ni miongoni mwa wanamuziki waliowahi kutamba sana barani Afrika.Kibao kinaitwa Nadina.Tunatumaini kitakukumbusha “enzi zako” au kama wewe sio wa “hapo zamani” basi pia kitakuburudisha.Tunakutakia Weekend Njema.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Wiki hii Tanzania ilitembelewa na Kelly Rowland,mmoja kati ya wanamuziki waanzilishi wa kundi maarufu la muziki lililojulikana kama Destiny’s Child.Kelly alikuwa nchini Tanzania kama Balozi Maalumu wa Taasisi ya MTV Staying-Alive.Ukitaka kujua mengi kuhusiana na taasisi hiyo,bonyeza hapa.

Alipokuwa nchini Tanzania,Kelly Rowland ambaye aliongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Georgia Arnold, alitembelea sehemu mbalimbali za jiji,alikutana na watu na vikundi mbalimbali kama ambavyo unaweza kuona katika picha hapo chini.

Kelly Rowland (kushoto) akiwa na binti aitwaye Eliza(katikati) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa MTV Staying-Alive Foundation,Georgia Arnold(kulia) wakati wa ziara ya Kelly nchini Tanzania .Eliza anaongoza Kikundi kijulikanacho kama Elizabeth Youth Group kinachojishughulisha na miradi mbalimbali ya vijana katika kutoa elimu kuhusu ukimwi na matumizi ya madawa ya kulevya.Eliza mwenyewe ambaye ni muathirika,aliwahi kufanya kazi ya kujiuza kabla hajaamua kubadili maisha yake na kuamua kusaidia wengine.Iangalie documentary kuhusu Uwanja wa Fisi(Hyena Square) na Eliza kwa kubonyeza hapa

Kwa picha zaidi na maelezo zaidi,bonyeza (more) hapo chini; (more…)

Leo ni siku ya kina baba.Kwa kutumia ile lugha ya malikia,tunaweza kusema Today is Father’s Day! Ni siku maalumu ya kumkumbuka baba yako,awe hai au awe alishaaga dunia. Ni siku ya kukumbushana upendo,amani na kutakiana mafanikio mema baina yako na mzazi wako.Kama kumetokea kutokuelewana kati yenu,basi siku hii inaweza tumika kama fursa nzuri ya kurekebisha mambo.

Bila shaka tunakubaliana kwamba kama ilivyo kwa mama,bila baba hakuna mtoto.Kwa maana hiyo mchango wa baba na mama katika malezi ni jambo muhimu.Kinachohitajika ni kila mmoja kutimiza wajibu wake.

Kuisindikiza siku hii,sikiliza kwa makini Wosia huu mzito kutoka kwa Baba kwa kubonyeza player hapo chini.Kisha zingatia yasemwayo katika wimbo huo.Happy Father’s Day.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Pichani ni wasanii wa Kikundi cha Splendid wakiigiza kama Mama mjamzito akiwa na watoto wake wakiwa wamekaa kwa masikitiko.Hii ilikuwa ni wakati wa shughuli za uzinduzi wa Kampeni ya Kukataa Kunyanyaswa Kwa Wanawake zilizofanyika jijini Dar-es-salaam jana.

Kama inavyoonekana pichani mama mjamzito amezungukwa na majukumu ya watoto wake bila kuwapo kwa mzazi mwenzake(mwanaume). Sasa ingawa waliopo pichani wanaigiza tu,hali halisi ndio hiyo katika jamii zetu.Single motherhood linazidi kuwa suala la kawaida katika jamii zetu.Nani wa kulaumiwa katika hili?Ni wanawake au wanaume? Jamii je?

Hii ndio picha yetu ya wiki na ni kwa hisani ya Athumani Hamisi.

Piga picha hii,mwanamke kaolewa,mume wake anampenda na anajitahidi kumtimizia haja zake zote.Anatokea jamaa anamrubuni.Anamwambia jamaa hakufai,jamaa si lolote si chochote.Njoo kwangu nikupe raha za dunia.Kumbuka kurubuni huku huenda na hongo kadha wa kadha.Bia na nyama choma,viwalo kutoka “mamtoni”,usafiri nk.

Mwanamke anaingia mtegoni na kumuacha mume wake kisha anafuatana na “mshikaji”.Baada ya muda mfupi tu jamaa anasema hamtaki tena.Jamaa keshapata alichokitaka kisha analala mbele,anasema Next!!Mwanamke anaanza kujuta,balaa gani hili?

Mambo haya si yanatokea jamani?Nani wa kulaumiwa kwenye situation kama hizi?Mwanamke au mwanamume?Huo ndio ujumbe muhimu kutoka kwa International Orchestra Safari Sound(IOSS) katika wimbo wao Homa Imenizidia.Bonyeza player hapo chini upate burudani.Ijumaa Njema.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Na kwa wale wazee wa kuruka majoka kutoka majuu,pata burudani kutoka kwa Mfalme wa Pop,MJ,katika Wanna Be Startin’ Something.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Tangu tuweke hewani sehemu ya kwanza ya mahojiano yetu na Freddy Macha wiki chache zilizopita,siku imekuwa haipiti bila kupokea barua pepe,simu au ujumbe mfupi kupitia simu za viganjani nk.kutoka kwa baadhi yenu wasomaji na wachangiaji wa BC mkitaka kupata uhondo wa sehemu ya pili.Hatuwezi kuwalaumu,tunaelewa ni jinsi gani Freddy Macha,iwe ni kupitia uandishi,ushairi na pia muziki,anagusa hisia za wengi.

Kama tulivyoahidi,hii hapa sehemu ya pili ya mahojiano yetu na Freddy Macha akizungumzia zaidi kazi zake za muziki,mambo mbalimbali ya kijamii na mengineyo kedekede.Kama ilivyo katika uandishi na ushairi,kwa upande wa muziki Freddy Macha pia kajaa tele.Anayo mengi ya kusimulia na kuweka wazi kuliko unavyoweza dhania.

Unataka kujua Freddy ametokea wapi mpaka kujikita kwenye sanaa ya muziki? Je una habari kwamba huyu bwana ni mtaalamu na mcheza karate wa kutupwa? Anasemaje kuhusu muziki wa kizazi kipya?Ana ushauri gani?Nini chanzo cha Kitoto Band?Je…

Mwisho wa mahojiano haya,utaweza kusikiliza baadhi ya nyimbo za Freddy akiwa na kundi lake lijulikanalo kama Kitoto Band.Hiyo ni zawadi maalumu kutoka kwa Freddy Macha na BC kwako msomaji,mchangiaji na hususani mpenzi wa muziki.Kwa hakika,kama wengi wenu mnavyopenda kusema,haya ni “mahojiano-shule”.Fuatana nasi; (more…)

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page