Piga picha hii,mwanamke kaolewa,mume wake anampenda na anajitahidi kumtimizia haja zake zote.Anatokea jamaa anamrubuni.Anamwambia jamaa hakufai,jamaa si lolote si chochote.Njoo kwangu nikupe raha za dunia.Kumbuka kurubuni huku huenda na hongo kadha wa kadha.Bia na nyama choma,viwalo kutoka “mamtoni”,usafiri nk.
Mwanamke anaingia mtegoni na kumuacha mume wake kisha anafuatana na “mshikaji”.Baada ya muda mfupi tu jamaa anasema hamtaki tena.Jamaa keshapata alichokitaka kisha analala mbele,anasema Next!!Mwanamke anaanza kujuta,balaa gani hili?
Mambo haya si yanatokea jamani?Nani wa kulaumiwa kwenye situation kama hizi?Mwanamke au mwanamume?Huo ndio ujumbe muhimu kutoka kwa International Orchestra Safari Sound(IOSS) katika wimbo wao Homa Imenizidia.Bonyeza player hapo chini upate burudani.Ijumaa Njema.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Na kwa wale wazee wa kuruka majoka kutoka majuu,pata burudani kutoka kwa Mfalme wa Pop,MJ,katika Wanna Be Startin’ Something.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Yamebaki takribani majuma mawili tu tuseme bye bye mwaka 2007. Majira haya ni nyakati za wafanyabiashara kuvuna na wengine “kuchunwa”. Kama hutambui kinachoongelewa ni dhahiri kwamba hutambui! Kwa wengine huu ndio wakati wa kuonyeshana mapenzi. Mapenzi ya zawadi lakini. Huna haja ya kuyalalia mlango wazi mapenzi ya namna hii. Shauri yako.
Lakini mbali na hayo yote,huu ndio wakati wa kuuaga mwaka.Wakati wa kumalizia malizia kutafakari yaliyojiri mwaka huu na kuanza kupanga yajayo.Si uliwahi kusikia habari za yaliyopita si ndwele…?Huu ndio wakati wake. Isitoshe, kwa sababu mbalimbali za kibinaadamu, mwisho wa mwaka pia huwa na ugomvi ugomvi hivi. Bwana kanuna kwa sababu zake na bibi pia kajikalia kona yake. Mojawapo ya sababu kubwa ni “hakuninunulia zawadi” lakini nasikia fulani yeye alimnunulia! Mwisho wa mwaka huwa una mambo. Pia ni kutokana na ukweli kwamba mwisho wa mwaka huwa pia umejaa “shughuli”.Sasa kama tujuavyo,shughuli ni watu na penye watu, ingawa hapaharibiki neno,huwa kuna mambo.
Cha muhimu ni kwamba mwisho wa siku,mwisho wa ugomvi, mmoja lazima ajishushe na kuomba msamaha.Bila shaka,ukiomba msamaha kwa dhati,utasamehewa. Ndio maana Mlimani Park Ochestra (Wana Sikinde) katika wimbo wao Fikirini Nisamehe,wanasisitiza kuhusu kuomba msamaha. Pata burudani hapo chini.Ijumaa Njema.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Bila kusita tunaweza kuanza kwa kusema Lady Jaydee(pichani) ni miongoni mwa wanamuziki wa Tanzania ambao hawahitaji utambulisho mrefu sana miongoni mwa wapenzi wa muziki wa kizazi kipya popote walipo nchini Tanzania na duniani kote. Leo hii ukipenda waweza kumuita Jide au Lady Jaydee. Aliwahi pia kuwa na majina mengine lukuki.Unayakumbuka?

Pamoja na hayo jina lake rasmi ni Judith Daines Wambura Mbibo.Ukipenda unaweza kumuita Mrs.Gardner G.Habash jina ambalo ana haki zote za kulitumia kwani ameolewa na Gardner,mtangazaji maarufu wa Clouds FM. Judith Wambura alizaliwa mkoani Shinyanga tarehe 15 Juni,1979 kwa Martha na Lameck Isambua Mbibo ambao ndio wazazi wake.Inasemekana alianza kuimba akiwa na umri wa miaka saba.Alianzia kuimba kanisani kama ilivyo kwa wasanii wengi.Baada ya kumaliza shule,Lady Jaydee aliwahi kufanya kazi Clouds FM kabla ya kuamua kujikita kwenye uanamuziki moja kwa moja mwaka 2000.
Baada ya kudumu kwa muda mrefu kama solo artist,mwaka huu Lady Jaydee amefanikiwa kufanya mambo mawili muhimu.Kwanza alianzisha rasmi bendi yake iitwayo Machozi Band na pili kutoa albamu yake ya nne aliyoipa jina Shukrani. Kabla ya hapo alishatoa albamu tatu ambazo ni Machozi(2000),Binti(2003) na Moto(2005).
Leo hii ukitaka kumuona Lady Jaydee kifanya vitu vyake akiwa na bendi yake,Machozi Band, unachotakiwa ni kujongea kila Ijumaa usiku ndani ya ZHONG HUA GARDEN, Regent Estat- Ally Hassan Mwinyi Road jijini Dar-es-salaam. Hutojutia uamuzi wako.
Hivi karibuni tulifanya mahojiano na Lady Jaydee ambapo tuliongelea mambo kadha wa kadha yakiwemo yake binafsi kama mwanandoa,binti maarufu,kazi zake za kimuziki,matarajio yake ya baadaye na mengine mengi.
Ingawa albamu yake ya Shukrani imetoka miezi kadhaa iliyopita,hatukuona haja ya kutoongelea machache juu ya albamu hiyo ambayo kama zilivyo albamu zake zilizopita,hii nayo inasambazwa na GMC Wasanii Promotors ya jijini Dar-es-salaam.Hii ndio albamu yenye wimbo uliotamba sana mwaka huu wa Siku Hazigandi. Bado inapatikana mitaani na madukani kwa wale ambao wangependa kuinunua.Yafuatayo ni mahojiano kamili; 

Yapo mambo ya kitaifa ambayo sote hatuna budi kushirikiana katika kupambana nayo.Mojawapo ni ugonjwa wa ukimwi.Raisi wetu,Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Salma Kikwete miezi michache iliyopita,kama wanavyoonekana pichani,walituongoza kwa mfano wa kivitendo katika vita hiyo.BC leo inapenda kukumbusha kuhusu kampeni hiyo yenye kauli mbiu Tanzania bila Ukimwi inawezakana.Bila kunyosheana vidole,kutengana,kutupiana lawama wala kumnyanyapaa mwingine kila mmoja wetu ana wajibu katika vita hii.


sending...