
Ukiweza kumalizia kichwa cha habari hapo juu utakuwa umepata mwangaza wa mtizamo wangu kuhusu vuta nikuvute inayoendelea kati ya Mchungaji Christopher Mtikila na Mbunge wa Igunga,Rostam Aziz.Kwa msaada zaidi wa kinachoendelea(kama bado hujafuatilia kinachoendelea) bonyeza hapa.Mwananchi amuamini nani?

Kwa wengine bado anaendelea kuwa mchora katuni aliye maarufu zaidi nchini Tanzania.Kwa wengine ni mtangazaji maarufu wa redioni ambaye kila asubuhi huwapa wasikilizaji habari mbalimbali na pia burudani. Lakini kwa wengine,yeye ni mbunifu wa mitindo(fashion designer) ambaye anakuja juu kwa kasi ya aina yake.Huyu si mwingine bali Ali Masoud,(pichani) maarufu kama Masoud Kipanya au ukipenda KP.
Leo hii yawezekana kabisa kusema kwamba Masoud ni kijana mjasiriamali ambaye anajaribu kutizama mbali kushinda maelezo. Ni kijana anayependa kujishughulisha kwa bidii na maarifa bila kuchoka wala kukata tamaa.Mwaka jana alitimiza mojawapo ya ndoto zake za muda mrefu kwa kuzindua lebo/nembo ya KP iliyokwenda sambamba na KP Wear.Hivi leo sio ajabu kukutana na watu mitaani waliovalia nguo zenye nembo na ubunifu kutoka kwa KP!
Kwa mara ya pili,hivi karibuni BC ilifanikiwa kupata fursa ya kufanya naye mahojiano kuhusiana na sio uchoraji katuni wala utangazaji bali ubunifu wa mitindo. Nini kilimsukuma kuingia kwenye fani ya ubunifu wa mitindo?Unataka kuijua falsafa inayomuongoza katika fani hii?Je anahofia kitu gani zaidi linapokuja suala zima la ubunifu wa mitindo?Nini mipango yake ya sasa na baadaye kidogo?Kwa hayo na mengineyo mengi zikiwemo picha za baadhi tu ya viwalo vilivyosheheni ubunifu wake,fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; 
Kila mwaka,tarehe 14 February(Siku ya Wapendanao),yeye hukumbuka au kusheherekea siku yake ya kuzaliwa. Alipozaliwa wazazi wake walimuita Fina.Leo hii wengi tunamfahamu kama Fina Mango(pichani),mtangazaji maarufu wa kituo cha radio cha Clouds FM.
Yeye ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto watano(5) kwa upande wa mama yake, Fortunata M.Mango na watoto saba(7) kwa upande wa Marehemu baba yake,,Joseph Mango.Anaye dada mmoja na kaka watatu(3) wa kuzaliwa tumbo moja na dada mmoja na kaka mmoja wa kambo.
Alianza pilikapilika za masuala ya elimu mkoani Arusha katika shule ya Mtakatifu Constantine(St.Constantine) na baadaye kujiunga na shule ya sekondari Jitegemee jijini Dar-es-salaam kwa ajili ya masomo ya O-Level.Kisha akajiunga na shule ya Shaaban Robert ya jijini Dar-es-salaam kwa masomo ya A-Level na kuhitimu mwaka 1999. Baada ya hapo akajiunga na Clouds FM ingawa kimasomo hakuishia hapo kwani baadaye alijiunga na FTC(Financial Training Centre) ambapo amesomea masuala ya biashara.Bado ana mpango wa kuendelea zaidi kimasomo.
Leo hii yeye ni Brand Manager wa kipindi cha Power Breakfast ambacho anakiendesha kwa kushirikiana na Masoud Kipanya (KP).Kipindi kinarushwa kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 12 alfajiri mpaka saa 3 asubuhi.
Fina Mango pia ni mjasiriamali, yeye ndio mmiliki wa kampuni ijulikanayo kama One Plus Communication ambayo inashughulika na masuala ya Usimamizi wa Shughuli na Matukio ya Mashirika mbalimbali na Uhusiano wa Jamii (Corporate Events Management & Public Relations (PR). Ofisi za One Plus Communication zipo maeneo ya Victoria ilipo Victoria Gas Station pembezoni mwa barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Hivi karibuni tulipata fursa ya kufanya naye mahojiano ambapo tuliongelea mambo mengi kuhusiana na kazi yake ya utangazaji,maisha yake binafsi na mipango yake ya baadaye.Kumbukumbu na uwazi alionao Fina ni jambo ambalo limetuvutia sana. Unataka kujua Fina anasemaje kuhusu maendeleo ya kisayansi na kitekinolojia ulimwenguni? Asingekuwa mtangazaji angependa kuwa nani?Je umeshawahi kuona picha za utotoni za Fina? Fuatana nasi katika mahojiano haya ya pekee. 
Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la Tanzania Daima, aliyewahi kuwa mume wa kuwa mume wa Mbunge wa Viti Maalumu, marehemu Amina Chifupa (UVCCM), Mohammed ‘Meddy’ Mpakanjia, ambaye habari zilizokwisha thibitishwa ni kwamba amelazwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, Dar es Salaam, hali yake ni mbaya na sasa analishwa kwa kutumia mirija.
Habari zaidi za habari hii yenye kusikitisha unaweza kuipata kwa kubonyeza hapa.BongoCelebrity inaendelea kujitahidi kupata habari zaidi juu ya hali halisi ya Mpakanjia. Pindi zitakapopatikana tutawafahamisha.


sending...