Tanzania Football Federation (TFF) iko katika mchakato wa kutengeneza mpango wa maendeleo wa muda mrefu. Ni nia ya TFF kufanyia kazi maoni ya wadau ili kuhakikisha yanaingia katika mpango huo.

Hivyo wadau wanakaribishwa kutuma maoni yao kupitia email- tfftz@yahoo.com au sanduku la barua 1574 Dar es Salaam. Maoni yawe yametumwa kufikia mwishoni mwa Novemba mwaka huu.

Pia TFF kupitia Kurugenzi ya Ufundi itakutana na makundi mbalimbali kusikiliza maoni yao. Novemba 2 mwaka huu imepanga kukutana na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na pia waandishi wa habari.

Pichani ni Leodgar Tenga,Rais wa TFF.


Nahodha wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa ameumia nyonga (groin) kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika jana (Oktoba 3 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa daktari wa Taifa Stars, Dk. Mwanandi Mwankemwa, maumivu hayo yatamweka Nsajigwa ambaye pia ni Nahodha wa Yanga nje ya uwanja kwa kati ya wiki mbili hadi nne.

Kutokana na ushauri wa daktari, Kocha Jan Poulsen amemuondoa kwenye kikosi hicho ambacho kitasafiri Oktoba 6 mwaka huu kwenda Casablanca, Morocco kwa ajili ya mechi dhidi ya Morocco itakayochezwa Oktoba 9. Badala yake Kocha Poulsen amemuita kwenye timu yake Nassoro Masoud Said ‘Cholo’ wa Simba kuziba nafasi ya beki huyo wa pembeni.

WACHEZAJI KUTOKA NJE

Wachezaji wanaocheza nje ya nchi walioitwa na Kocha Poulsen wameanza kuwasili. Idrissa Rajab anayechezea Sofapaka ya Kenya na Mbwana Samata wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wamewasili jana jioni na tayari wameripoti kambini Taifa Stars.

Henry Joseph wa Kongsvinger IL ya Norway), Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada) na Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden) wanatarajiwa kuwasili leo (Oktoba 3 mwaka huu) usiku kwa ndege ya KLM. Washambuliaji Abdi Kassim na Dan Mrwanda wanaochezea timu ya DT Long An ya Vietnam ndiyo watakaokuwa wa mwisho kujiunga na kambi ya Stars ambapo watawasili nchini kesho (Oktoba Freetown,Seirra Leone,

Boniface Wambura

Ofisa Habari

TFF.

Mchezaji Netiboli Mwanaidi Hassan anayechezea timu ya JKT Mbweni,ameibuka mshindi wa tuzo ya jumla ya mwanamichezo bora nchini Tanzania kwa mwaka 2010 kupitia tuzo za Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania au TASWA(Tanzania Sports Writers Association) zilizotolewa usiku huu katika Hotel ya Movenpick jijini Dar-es-salaam chini ya udhamini wa kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited(SBL).

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Mwanaidi Hassan kushinda tuzo hiyo.Alishinda tena tuzo hiyo kwa mwaka 2009.Kwa ushindi huo,Mwanaidi alijinyakulia zawadi ya gari Toyota GX 100.

Pichani ni mgeni rasmi katika hafla hiyo,Makamu wa Rais wa Tanzania,Dr.Gharib Bilal,akimkabidhi Mwanaidi tuzo ya Mchezaji Bora Tanzania.Anayeshuhudia pembeni ni Waziri wa Vijana,Habari,Utamaduni na Michezo Dr.Emmanuel Nchimbi.

Photo:Ahmad Michuzi

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Benjamin William Mkapa,usiku huu amepewa Tuzo ya Heshima wakati wa tuzo za michezo zinazotolewa na Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Nchini(TASWA) usiku huu katika viwanja vya Movenpick Hotel jijini Dar-es-salaam.Rais Mstaafu huyo amepewa Tuzo hiyo ya Heshima kutokana na mchango wake katika michezo nchini Tanzania hususani kwa mchango wake katika ujenzi wa uwanja mpya wa taifa ambao kwa namna ya kipekee umeiletea heshima mpya nchi ya Tanzania katika medani ya michezo ulimwenguni.

Akipokea tuzo hiyo,Mkapa alikiri kwamba katika kipindi chake cha kwanza cha urais,hakuwahi kuhudhuria hata tukio moja la michezo.Alikuwa na sababu.Priority zingine zilimkabili.Masuala ya uchumi.

Rais Mkapa alitumia fursa hiyo kukanusha habari “nyepesi nyepesi” kwamba uwanja ule ulijengwa kwa msaada wa Uchina kwa asilimia mia moja.Badala yake,Mkapa amesema,ukweli ni kwamba uwanja mpya wa taifa,ulijengwa kwa mgawanyo sawa wa gharama katika ya China na Tanzania.Kwa maana hiyo,China ilitoa asilimia 50 na Tanzania ikatoa aslimia 50.

Photo Courtesy:Othman Michuzi

Ninapoandika habari hii Tuzo za michezo za Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania au kwa kiingereza Tanzanians Sports Writers Association(TASWA) zingali zikitolewa katika ukumbi wa wazi ulioandaliwa maalum kwa ajili ya shughuli hii katika viwanja vya Movenpick Hotel jijini Dar-es-salaam. Tuzo hizi ambazo kadiri miaka inavyozidi kwenda zinazidi kujipatia maarufu, zimedhaminiwa na kampuni ya Serengeti Breweries Limited ambao bila shaka wanastahili kila aina ya pongezi kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakijitolea katika kudhamini mambo mbalimbali yahusuyo michezo na burudani zingine. Wakati bado tunasubiri kupata matokeo kamili ya washindi,hii hapa ni orodha ya waliokuwa wanawania tuzo hizo;

  1. Riadha
    Wanaume:
    1. Samson Ramadhan
    2. Marco Joseph
    3.John Bazil
    Wanawake:
    1. Zakia Mrisho
    2. Mary Naali
    3. Magdalena Mushi

  2. Wavu

    Wanaume:
    1. Kevin Peter (Magereza Wanaume)
    2. –Mbwana Ally Mzinga Morogoro
    3. Ibrahim Cristopher( Nyuki Zanzibar).
    Wanawake:1. Hellen Richard Mwegoha (Magereza Wanawake).
    2. Yasinta Remmy (Jeshi Stars)
    3. Zainabu Thabit (Jeshi Stars)

    3 Netiboli
    1. Lilian Sylidion-Filbert Bayi
    2. Mwanaid Hassan-JKT Mbweni
    3. Sekela Dominick-JKT Mbweni
    4. Karate
    Wanaume:

    1. Sempai Steven Bella
    2. Semapai Ayub seleman
    Wanawake: Kuna jina moja haliwezi kutangazwa.

    5.Kikapu
    Wanaume:
    George Otto Tarimo- Savio-Dsm
    Lusajo Samwel Mwakipunda- Oilers-Dsm
    Gilbert Batungi read more

Hasheem Thabeet (born Hashim Thabit Manka) on February 16,1987 in Dar-es-salaam-Tanzania

Played for Connecticut Huskies in 2006/2007,2008/2009 seasons. The Huskies won NCAA Championship last night by beating Butler 53-41 in the final game.

In the 2009 NBA Draft,Hasheem Thabeet, was drafted 2nd pick overall by Memphis Grizzlies.

On February 25,2010,the Memphis Grizzlies sent Hasheem to the NBA Development League(D-League).He was assigned to the Dakota Wizards.He stayed there for just over two weeks and was recalled to Memphis Grizzlies.He made history by becoming the first 2nd pick to be sent to the D-League.BC interviewed Hasheem on how he felt about being assigned to D-League.You can read that interview here.

On February 24,2011 ,Hasheem was traded to the Houston Rockets along with a first pick in exchange for Shane Battier.

On March 21,2011,Hasheem Thabeet was once again assigned to the D-League.This time to Rio Grande Valley Vipers in Hidalgo,Texas where he is currently playing.

Here is the video of one of his games at Rio Grande Valley Vipers. Hasheem is in jersey # 42.

read more

Houston Rockets center Hasheem Thabeet was assigned to the Rio Grande Valley Vipers, the Rockets’ NBA Development League affiliate, it was announced today. The assignment marks the 48th time in the 2010-11 season an NBA player has been assigned to an NBA D-League affiliate, and it is the second assignment for Thabeet, a second-year pro out of Connecticut.

Thabeet, the No. 2 overall selection in the 2009 NBA Draft, is the 34th NBA player to be assigned to the NBA D-League this season, which is an all-time high. The Memphis Grizzlies, who drafted Thabeet, assigned him to the Dakota Wizards last season, where he averaged 13.8 points, 11.2 rebounds and 3.8 blocks in six games.

Thabeet (7-3, 263) has appeared in 115 career NBA games, averaging 2.3 points and 2.8 rebounds in 10.9 minutes. As a rookie with Memphis last season, Thabeet led the NBA in blocks per 48 minutes with 4.84 (min. 60 games). He also averaged 11.4 points, 8.6 rebounds and 2.8 blocks in five games with Memphis’ 2010 NBA Summer League team. Thabeet has appeared in two games with Houston since joining the Rockets via trade on Feb. 24.

The first Tanzanian-born NBA player, Thabeet played three collegiate seasons at Connecticut, averaging 10.3 points, 8.5 rebounds and 4.17 blocks in 100 games. Thabeet led the Big East in blocks all three seasons, and his 4.17 average ranks 11th in NCAA history. Thabeet was an AP All-America Second Team selection and the Big East Co-Player of the Year in 2008-09. He was also named the Big East Defensive Player of the Year and National Defensive Player of the Year by the National Association of Basketball Coaches in both his sophomore and junior seasons.

Thabeet joins the Vipers for the team’s home game tonight against the Idaho Stampede. Rockets fans can keep track of Thabeet and the Vipers by logging onto NBA.com/dleague to watch every game live, online, for free.

read more

Habari ambazo zimetufikia muda si mrefu uliopita zinapasha kwamba mtanzania wa kwanza kucheza katika ligi ya NBA,Hasheem Thabeet aliyekuwa akichezea timu ya Memphis Grizzlies, ameuzwa kwenda timu ya Houston Rockets ya jijini Houston,Texas katika mabadilishano maalumu baina ya timu hizo mbili.

Katika mabadilishano hayo,mchezaji Shane Battier aliyekuwa akichezea timu anayokwenda Hasheem(Houston Rockets) anajiunga na Memphis Grizzlies.

read more

Zipo siku ambazo hapa BC huwa tunapenda kujikumbusha mambo mbalimbali yaliyojiri hapo zamani.Hapo ndipo huwa tunapata muda wa kujikumbusha miziki ya kale. Hapo ndipo tunapopenda kuwakumbuka mashujaa wetu ambao kupitia utumishi wao kwetu na kwa dunia kwa ujumla,leo hii tupo tulipo. Huwa ni wakati adimu kwetu tunapowakumbuka mashujaa wetu,walio hai na waliotangulia kwa Mola kwani ni watu kama hao ambao kwa kufanya kile walichokifanya,kwa kujitolea vile walivyojitolea,leo hii wanatufanya sote “tujisikie” na u-utanzania wetu.Kichwa mbele,mabega juu.

Katika mlolongo wa uchambuzi wetu huo,leo jina ambalo limetujia ni lile la John Stephen Akhwari. Kama ulizaliwa miaka ya hivi karibuni inawezekana kabisa ukawa hujawahi kulisikia jina la Akhwari. Siwezi kukulaumu.Bado hatuna mfumo mzuri wa kuwakumbuka na kuwaenzi mashujaa wetu ipasavyo.Tunahitaji kuunda mfumo huo.

John Stephen Akhwari ni mtu anayekumbukwa sana katika ulimwengu wa michezo hususani ile ya Olympic. Huyu bwana,alishiriki katika mchezo wa riadha akiiwakilisha Tanzania katika michezo ya Olympic iliyofanyikia nchini Mexico mwaka 1968.

Wakati akichuana,Akhwari alianguka na kuumia vibaya gotini. Madaktari wakamwendea na kumfunga bandeji huku wakidhani kwamba jamaa ndio amefikia mwisho wa mashindano na atajitoa. Mambo yalikuwa tofauti.Akhwari akasimama na kuendelea kukimbia. Bila shaka wauguzi wale na hata mashabiki waliomuona waliona jamaa wazimu ushampanda. Hakujali fikra za watu wengine.Alijua anachokifanya.

John Stephen Akhwari

Huku watu wakiwa washaanza kuondoka wakijua mambo yeshakwisha maana zaidi ya saa moja lilishapita tangu mshindi wa kwanza avuke kamba na giza likiwa lishaanza kuingia,Akhwari akatokea. Wa mwisho! Jumla ya washindani walikuwa 74 lakini waliofanikiwa kumaliza walikuwa 57 huku John Stephen Akhwari akichukua namba hiyo ya 57.

Walioshuhudia wakati mtanzania huyu jasiri akimalizia mbio, walishikwa na  mshangao.Kwanini huyu bwana hakujitoa ingali ameumia namna hiyo na anajua fika kwamba nambari moja,mbili au tatu si zake? Waandishi wa habari wakamzunguka kutaka kujua. Huku akihema na kutokwa na jasho, Akhwari akawaambia waandishi…

Nchi yangu haikunituma kutoka umbali wa zaidi ya maili 500o kuja hapa kuanza tu mbio bali kumaliza.

Ingawa alishindwa,John Stephen Akhwari, akawa ametoa mfano mkubwa sio tu kwa wanamichezo bali watu wote.Unapoingia katika mashindano,yawe ni michezoni au katika maisha,huna budi kushindana mpaka mwisho. No quitting!

John Stephen Akhwari akionyesha jinsi ya kukimbia katika mojawapo ya matangazo ya kuhamasisha Olympic ya China mwaka 2008

Wakati wa mashindano ya Olympic mwaka 2008 yaliyofanyikia huko nchini China,jina lake lilivuma kwa mara nyingine.China ilimtumia katika mambo mbalimbali ya uhamasishaji wa Olympic. Pengine ndio maana walizoa medali nyingi namna ile.Who knows?

Heshima kwako John Stephen Akhwari. You taught us never to quit,but to make sure we finish.Thank You.

FINISH THE RACE-PERSONAL STORY OF COURAGE

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Photo Credits: Crienglish

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page