Miss Venezuela Ivian Sarcos was crowned Miss World 2011 at an extravagant ceremony here at the Earls Court Sunday evening.

The 21-year-old won the diamond-shaped throne defeating over 100 beauties from various parts of the world at the 61st Miss World contest.

Miss Philippines Gwendoline Ruais was the first runner-up and Miss Puerto Rico Amanda Perez became the second runner-up.

The gala event kicked off with a dynamic performance by British street dance troup Diversity and ended with Miss World 2010 Alexandria Mills crowning Sarcos.

The jury included former Miss World winners — Cindy Breakspeare (1976), Nigeria Agbani Darego (2001), Zhang Zilin (2007) and Kaiane Aldorino (2009).

Our representative, Miss Tanzania 2011-Salha Israel did her best but once again, the game is still tough. We just can’t ask ourselves same questions again,right? She tried…a consolation from our board.

Pichani ni Vodacom Miss Tanzania 2011, Salha Israel,akipunga mkono wa kwaheri kwa baadhi ya ndugu,jamaa,marafiki na watanzania waliojitokeza kumuaga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere(JNIA) jijini Dar-es-salaam hapo jana.

Salha ameondoka kwenda kushiriki katika mashindano ya dunia (Miss World) yatakayofanyikia jijini London nchini Uingereza mwezi ujao tarehe 6 Novemba katika ukumbi wa Earls Court Two ambapo mshindi wa Miss World 2010,Mmarekani Alexandria Mills atakabidhi taji lake kwa mshindi mpya.

Swali kubwa ambalo najiuliza na ningependa nawe msomaji ujiulize ni kwamba je,mwaka huu Tanzania ina matumaini ya kufanya vizuri zaidi kuliko miaka ya nyuma?Tumefanya maandalizi ya kutosha ili kwenda kushindana na sio kushiriki katika mashindano haya?Na endapo tutaishia kuwa wasindikizaji,mwakani tujiandae namna gani?Tuwapate vipi wanaokwenda kutuwakilisha?

Bila shaka majibu ya baadhi ya maswali hayo magumu yapo mikononi mwa Kamati ya Miss Tanzania.Kwetu sisi hapa BC,tunamtakia Salha kila la kheri.

Hatimaye zoezi lililochukua miezi kadhaa la kumtafuta mrembo mpya wa Tanzania kwa mwaka huu wa 2011(Miss Tanzania 2011),lilifikia kilele chake jana usiku katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar-es-salaam na mwanadada Salha Israel kuibuka mshindi na hivyo kuvikwa rasmi taji la Miss Tanzania 2011 kutoka kwa Genevive Emmanuel Mpangala(Miss Tanzania 2010) aliyekuwa akilishikilia taji hilo mpaka hapo jana.

Katika kilele cha shindano hilo lililodhaminiwa kwa kiasi kikubwa na kampuni ya Vodacom na kupambwa na burudani ya mziki kutoka kwa wasanii mbalimbali wanaotamba Afrika Mashariki na Kati kama vile Diamond,Bob Junior,Kidumu na wengineo,mshindi wa pili alikuwa Tracy Sospeter na mshindi wa tatu akawa Alexia William.

Tunampongeza Salha kwa taji jipya.Lakini pongezi hizo ni vyema zikaenda na maswali magumu.Je,Salha anatoa matumaini kwa Tanzania kufanya Vizuri katika steji ya dunia(Miss World)?Je,Tanzania itaishia kuwa wasindikizaji tu katika fainali za dunia zinazotarajiwa kufanyika tarehe 6 November huko jijini London nchini Uingereza?Kuna lolote jipya ambalo Kamati Ya Miss Tanzania imejifunza kutokana na “uzoefu” wa miaka ya nyuma?

Upo ushauri ambao uliwahi kutolewa kwa kamati ya Miss Tanzania kupitia hapa BC.Je,umezingatiwa?Ni suala la kusubiri na kuona.

Miss Tanzania 2011,Salha Israel(katikati) akiwa na Tracy Sospeter(kulia-Mshindi wa Pili) na Alexia William(kushoto-Mshindi wa Tatu) mara baada ya kutangazwa mshindi.




Mmoja kati ya warembo unaowaona hapo juu,tarehe 10 September mwaka huu ndani ya Mlimani City,atatwaa title mpya na atakuwa Miss Tanzania 2011.Jumla ya warembo 30 wameshaingia kambini tayari kwa mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa tena na Vodacom Tanzania.Je,nani atatwaa taji hilo?Je,mwaka huu Tanzania itang’ara katika stage ya kimataifa yaani Miss World?

Kwa upande wa Tanzania,hadithi ya kuwa wasindikizaji,inaelekea  kuendelea.Mrembo wetu,Genevieve, ameshindwa kufua dafu katika fainali za mwaka huu za mrembo wa dunia, Miss World,zilizofanyikia Sanya nchini China.

Katika mashindano hayo ambayo yalikuwa yanafanyika kwa mara ya 60 tangu yaanzishwe, mshindi ameibuka kuwa mrembo kutoka nchini Marekani, Alexandria Mills.Mshindi wa Pili, ni mrembo kutoka Afrika,nchini Botswana, Emma Wareus huku mshindi wa tatu akiwa ni Adriana Vasini kutoka nchini Venezuela.

Alexandria Mills ni binti mwenye umri wa miaka 18 tu kutoka jijini Louisville ndani ya Jimbo la Kentucky. Ana urefu wa mita 1.75(5’9) na tayari kabla ya kushinda taji hilo,ni model aliyemo kwenye orodha ya models wa Elite Models Agency.

Sina hakika kama mambo haya mawili,kwa kuzingatia umuhimu wake,yanafanana. Lakini kwa sababu ni “matukio”, basi kwa namna moja au nyingine, naamini tunaweza kuyaweka kwa pamoja. La kwanza lina umuhimu wa aina yake. Ni Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania kwa mwaka 2010.

Jumapili hii,Tarehe 31 October 2010, mamilioni ya watanzania watapanga foleni ndefu ndefu ili kutimiza miongoni mwa wajibu wa msingi wa raia;Kuchagua viongozi. La,sio viongozi tu bali viongozi bora na sio bora viongozi.

Kama “Polls” ni jambo la kuaminika, uwezekano wa Tanzania kujitengenezea historia ya aina yake ni mkubwa. Kuna mwamko ambao haukuwepo miaka mitano iliyopita. Kuna hali ya wananchi kutaka mabadiliko fulani. Business as usual inaelekea kuwa kauli ambayo inaanza kutoingia vichwani mwa watu. Kinachoombwa ni kutawala kwa amani,haki na kuzingatia msemo wa Asiyekubali Kushindwa Si Mshindani. Ikitokea wapiga kura wakakataa kumpa mtu fulani ridhaa ya kuwaongoza,jazba ziwekwe kando.We pray for peace!

La pili ni mashindano ya kumsaka mrembo wa dunia,Miss World 2010.Kulinganisha na hilo la hapo juu,naweza kabisa kuthubutu kusema kwamba hili halina maana sana. Lakini lina maana yake na nafasi yake.

Bendera ya Tanzania itakuwa inapepea huko Sanya nchini China wakati Miss Tanzania 2010,Genevieve Mpangala, atakapokuwa anawania taji la Dunia la Urembo/Ulimbwende. Ukitaka kusoma kidogo kumhusu Genevieve kwamba anapenda nini, ana mafanikio gani maishani mwake mpaka hivi sasa,bonyeza hapa. Tunamtakia kila la kheri.

Miss Tanzania 2010, Genevieve Mpangala

Naam,wikiendi ya aina yake hiyo inakuja.Kama unavyo vigezo vyote vya kupiga kura,tafadhali NENDA KAPIGE KURA,GO VOTE!!!

Mshindi wa taji la ulimbwende nchini Tanzania kwa mwaka 2010(Miss Tanzania 2010),Genevieve Emmanuel, asubuhi ya leo hii(kwa saa za Tanzania) amekabidhiwa rasmi bendera ya Tanzania tayari kabisa kwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya ulimbwende ya dunia(Miss World 2010) yanayotarajiwa kufanyika huko Sanya nchini China tarehe 30 Oktoba 2010.Anatarajiwa kuondoka nchini kesho.

Shughuli ya kumkabidhi bendera mrembo huyo ilifanyikia katika viwanja vya Tanzania Investment Centre(TIC) jijini Dar-es-salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa kituo hicho cha uwekezaji,Bw.Emmanuel Ole Naiko, Miss Tanzania 2009,Miriam Gerald, Mratibu wa Miss Tanzania,Hasheem Lundenga,wawakilishi wa wadhamini wa shindano la Miss Tanzania kutoka kampuni ya mawasiliano,Vodacom na wengineo.

Miss Tanzania 2010,Genevieve Emmanuel(kushoto) na Miss Tanzania 2009,Miriam Gerald.

Mashindano ya mwaka huu yanaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo.Awali mashindano ya mwaka huu yalikuwa yafanyikie nchini Vietnam lakini nchi hiyo ilijiondoa katika uandaaji huo na hivyo China kupewa nafasi ya kuyaandaa.

Picha:MichuziJR

Miss Tanzania 2010-Genevieve Emmanuel

Miongoni mwa mahojiano ambayo yamewahi kutia fora hapa BC ni pamoja na yale niliyowahi kuyafanya na Miss Tanzania 2007,Richa Adhia(pichani). Kama hukuwahi kuyasoma,unaweza kufanya hivyo sasa.

Sasa jana kuna msomaji mmoja kaniuliza;yuko wapi hivi sasa Richa? Kwa faida yake na ya wengine ambao wanaweza kuwa na swali hilo mioyoni mwao,jibu ni kwamba sina uhakika sana.Juhudi zangu za kutaka kufanya naye mahojiano mengine kuhusu anachotarajia kufanya baada ya kuvua taji la Miss Tanzania,ziligonga ukuta.

Ila kwa mujibu wa tovuti ya Miss Tanzania, Richa hivi sasa yupo jijini Dar-es-salaam akiwa amefungua clinic yake ya masuala ya urembo inayoitwa Beauty Clinic maeneo ya Mikocheni.Bado ana ndoto za kufungua chuo au shule ya masuala ya urembo.

KESI ya kushambulia na kuharibu mali iliyokuwa inamkabili Miss Tanzania, Miriam Gerard, pamoja na rafiki yake imefutwa na wawili hao pamoja na mtu wanae shitakiana nae sasa watamalizana nje ya mahakama.

Kwa mujibu wa blog ya Father Kidevu, Uamuzi huo umefikiwa leo katika Mahakama ya Kinondoni ambako kesi hiyo ilifikishwa mwezi Februari.

Bila shaka habari hizi ni njema kwa Kamati ya Miss Tanzania inayoongozwa na Uncle Hashim Lundenga ambayo kimsingi ndio msimamizi mkuu wa shughuli za kijamii zinazofanywa na mrembo huyo mpaka hapo atakapoachia taji lake.Life goes on.

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page