Rais Jakaya Mrisho Kikwete,jana mchana aliwaongoza viongozi mbalimbali wa serikali na maelfu ya wananchi katika mazishi ya aliyekuwa mnajimu maarufu Afrika Mashariki na Kati,Sheikh Yahya Hussein aliyefariki juzi kutokana na maradhi ya moyo.
Mbali na Rais Kikwete,viongozi wengine wa vyama mbalimbali vya siasa nchini wakiwemo Freeman Mbowe(Mwenyekiti-CHADEMA),John Cheyo(Mwenyekiti-UDP),Prof.Ibrahim Lipumba(Mwenyekiti-CUF) pia walihudhuria mazishi hayo yaliyofanyikia katika makaburi ya Tambaza jijini Dar-es-salaam. Kabla ya hapo dua ya kumuombea ilifanyika katika msikiti wa Manyema.Amefariki akiwa na umri wa miaka 79.Hizi hapa ni baadhi ya picha

Rais Kikwete akitia mchanga katika kaburi la Sheikh Yahya Hussein hapo jana.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililobeba mwili wa Sheikh Yahya Hussein tayari kwa mazishi.

Baadhi ya wanafunzi wa Sheikh Yahya Hussein wakishiriki katika shughuli nzima ya mazishi yake nyumbani kwake Magomeni Mikumi.

Makamu wa Rais,Dr.Gharib Bilal alikuwa ni miongoni mwa viongozi mbalimbali wa serikali walioshiriki shughuli ya mazishi ya Sheikh Yahya.Pichani ni Dr.Gharib akimfariji mjane wa marehemu,Kate Yahya Hussein,nyumbani kwao Magomeni Mikumi jijini Dar-es-salaam.

SEASONED and veteran journalist, Adam Lusekelo (54) passed away while being rushed to Muhimbili National Hospital (MNH) on Thursday night, his wife Scolastica Lusekelo, said.
Ms Lusekelo said the deceased’s health deteriorated on Thursday night when relatives rushed him to MNH.
“He didn’t even reach the hospital, he breathed his last on the way at around 11pm,” Ms Lusekelo said. The ‘Sunday News’ columnist has been battling diabetes for a long time and was surviving on medication.
“Oh, no! We have lost a ‘Sunday News’ readers’ favourite,” lamented the newspaper’s Editor, Ichikaeli Maro upon receiving news of Mr Lusekelo’s death.
His column, a unique blend of writing serious issues of national importance with a soft touch, won many hearts and souls.
“My husband will miss him badly, he was his favourite columnist,” said Joyce Sabuni, Tanzania Standard Newspapers employee in the circulation section.
TSN Acting Managing Editor, Mkumbwa Ally also mourned the death of one of journalism’s most gifted writers. Burial arrangements are being made at his home at Ubungo Maziwa, but the body is likely to be transported to his home region of Rungwe in Mbeya, his wife said.
The late Lusekelo is survived by a wife and three children, two daughters and a son. He worked with TSN briefly in the 1980s before joining BBC as a correspondent based in Dar es Salaam.
News Source: Daily News
Photo Courtesy of Da Chemi @ Swahili Time
Adam was also a Blogger.Click Here to Check his Blog.His last post was 14th December,2010
THIS IS NOT APRIL FOOL’s PRANK.BC has confirmed.
Kama mnavyojua wenzetu wa Gongo la Mboto na maeneo mengine ya jiji la Dar-es-salaam walipatwa na janga la mabomu yaliyolipuka kutoka katika ghala nambari 5 la Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ)
Ni tukio la kusikitisha ambalo bado linatatiza wengi.Katika kuonyesha mshikamano na wote walioathirika,CEO wa Tongwe Records “Jay Murder” alijiwa na wazo la kuwaunganisha wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya ili kutengeneza wimbo ambao sio tu ni kama rambirambi kwa wote waliopoteza maisha au kuondokewa na ndugu,jamaa na marafiki bali pia kuelezea mambo kadhaa waliyonayo kama wasanii(kioo cha jamii).
Matokeo ya mkusanyiko huo wa wasanii ni wimbo uliopewa jina Toa Ndugu.Usikilize hapa.The Song was Produced By J-Ryder From Tongwe Records. To Know More About This Song, Contact Fid Q (Main Speaker of The Song)
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Mpangilio wa wasanii walioshiriki katika wimbo huu ni kama ifuatavyo;
Verse 1
Banana Zorro, G – Nako, Adam Mchomvu, Barnaba, Dj Fetty.
Chorus (Nurueli)
Verse 2
Cyrill, R.O.M.A, Domokaya, Jos Mtambo, Lord Eyez, Chege.
Chorus (Nurueli)
Verse 3
C Pwa, Ncha Kali, Bwana Misosi, Papaya, Darasa.
Chorus (Nurueli)
Verse 4
Anna, Soprano, Amini, Ditto.
Chorus (Nurueli)
Outro (Fid Q)
God Bless Tanzania, Bless Gongo La Mboto, and Bless Tongwe Records.

Kwa niaba ya Tanzanian Canadian Association (TCA), chama cha jumuiya ya Watanzania tunaoishi Toronto , Ontario , Canada na vitongoji vyake, tunapenda kuchukua fursa hii kwanza kabisa, kutoa rambirambi zetu kwa familia za wananchi waliopoteza wapendwa wao katika ajali ya mabomu yaliyolipuka katika kambi ya jeshi eneo la Gongo La Mboto, Dar-es- Salaam , Tanzania .
Tunawaombea wote waliopoteza maisha yao Mwenyezi Mungu awapumzishe kwa amani; tunawatakia majeruhi waugue pole, wapone haraka ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku. Vilevile, tunawatakia wote waliopotezana na ndugu zao hususan watoto waliopotezana na wazazi wao waweze kupatikana na kukutana tena.
Tumesikitishwa na taarifa za maafa hayo na kuhuzunishwa kuona kwamba ni mara ya pili tukio kama hili linatokea nchini kwetu. Wengi watakumbuka siku si nyingi janga kama hili lilitokea kule Mbagala. Tunapenda kuuomba uongozi wa jeshi uangalie upya namna silaha kali zinavyohifadhiwa; katika utaratibu wa kuhifadhi mabomu, tunapendekeza yafanyike marejeo na marekebisho yatakayozingatia usalama wa raia.
Katika kuhitimisha, tunalisisitizia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), lichukue hatua madhubuti na za haraka katika kuhakikisha majanga yanayoweza kuepukika kama haya hayatokei tena.
Mungu Ibariki Tanzania .
Uongozi – Tanzanian Canadian Association (TCA)

Familia ya marehemu mwalimu Julius Banzi wa Mafiga Morogoro, inasikitika kuwatangazia msiba wa Mwalimu Innocentia Banzi kilichotokea alfajiri ya tarehe 12/01/2011 Dar-es-salaam-Tanzania.
Marehemu ni mama wa:
Dennis Londo wa Helsinki-Finland; Esther Londo na Walonzi Tatala wa Tampere-Finland;
Michael Gomela wa Reading-United Kingdom; Daniel Mtebe wa Stockholm-Sweden.
Habari za msiba huu ziwafikie wakuu wa shule zote za sekondari Tanzania, walimu na wanafunzi wa Kilakala sekondari, Morogoro sekondari na Masanze sekondari. Pia ziwafikie wanachama wote wa chama cha msalaba mwekundu Tanzania; wanachama wote wa chama cha maskauti Tanzania na wanamichezo wote wa Mkoa wa Morogoro.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika Morogoro mara tu watoto wa marehemu watakapowasili.
Wale wote ambao mpo Finland msiba upo:
Lautamiehentie
2B 39 Vantaa (kwa maelezo zaidi piga simu 050 4863508, 040 5892123, 040 3750820)
Tanzania upo nyumbani kwa marehemu Mafiga-Morogoro, na Dar-es-salaam upo Mbezi Luis-njia panda ya kwenda Makabe (ulizia kwa Kunambi) Kwa maelezo zaidi piga simu namba: +255 732201098, +255 717365676, +255 713233843
One of the Tanzanian and African music legend,Dr.Remmy Ongala,is gone.He was laid to rest this afternoon in Sinza-Dar-es-salaam. Here are some of the photos from the farewell ceremony that took place at the Biafra Grounds in Dar-es-salaam.Rest in Peace Dr.Remmy Ongala.

10th February 1947-12th December 2010

Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza kumuaga Dr.Remmy

Mjane wa Marehemu,watoto na wajukuu

Mtoto wa marehemu mwanasoka Kali Ongala akitoa heshima za mwisho kwa baba yake.

Baadhi ya viongozi wakitoa heshima zao.Wanaoonekana hapo ni John Mnyika,Mbunge wa Ubungo na Iddi Azan-Mbunge wa Kinondoni.

Waziri wa Utamaduni,Vijana na Michezo,Dr.Emmanuel Nchimbi akitoa heshima zake.

Mzee Makassy,mjomba wa marehemu ambaye ndiye alimshawishi Dr.Remmy kuja Tanzania akitokea DRC. 

Mwanamuziki mkongwe nchini Tanzania, Dr.Remmy Ongala,amefariki dunia.Kwa wiki kadhaa,Dr.Remmy alikuwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari.Mipango ya mazishi inafanyikia nyumbani kwa marehemu Sinza(Sinza kwa Remmy) jijini Dar-es-salaam.Pumzika kwa amani Dr.Remmy Ongala
BC iliwahi kuandika kwa kirefu historia ya Dr.Remmy Ongala.Bonyeza hapa kuisoma historia ya mkongwe huyu wa muziki ambaye mchango wake katika muziki na katika kuitangaza Tanzania kimataifa ni mkubwa na ambao hautokaa usahaulike.
Miongoni mwa nyimbo zake ambazo zilitamba na bila shaka katika siku ya leo utapigwa zaidi ni pamoja na ule wa Kifo. Unaweza kuusikiliza kwa kubonyeza player hapa chini;
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Hizi hapa ni baadhi ya picha kutoka vyanzo mbalimbali zinazoonyesha maisha ya Dr.Remmy Ongala.

Dr.Remmy Ongala-a youth

Remmy loved life and life loved him.


We regret to announce the death of Mr. HUMPHREY NOEL MKONDYA, a Veteran Lawyer, husband to Edith Chisenga Mkondya, father to Eric, Kenneth, Lawrence and Dr. Ellen which occurred on Friday the 12th of November, 2010 at the Apollo Hospital in Chennai, India.
The funeral service will take place on Wednesday 17th November, 2010 at 1400hr, at his residence, House No. 23, Wakulima Road, Hannanasif Estate Kinondoni, Dares Salaam.
The body of the late Mr. Mkondya will be laid to rest on the very day at 1500hrs at Kinondoni cemetery
The Lord gave and the lord hath taken away;
Blessed be the name of Lord. Job 1: 2 1b
May his Soul Rest in Eternal Peace. Amen.
Taarifa zimetufikia kwamba, mwanamuziki na mshairi(poet) maarufu, Mrisho Mpoto, amepata msiba wa kuondokewa na mama yake mzazi.Mwanaisha Mrisho ambaye amefariki leo katika hospitali kuu ya wilaya ya Temeke(Temeke Hospital) alipokuwa amelazwa tangia juzi akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari(Diabetes)
Mipango ya mazishi zinafanyika.Marehemu anatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda nyumbani kwao Ikwiriri-Rufiji kwa mazishi.
BC inaungana na wote katika kumpa pole Mrisho,ndugu,jamaa na marafiki wote.

Naomba uniwie radhi msomaji wa BC kwa kimya kidogo kilichojitokeza hapa BC.Wiki hii ilikuwa ya majonzi.Nilipatwa na msiba wa kuondokewa na Babu Mkwe wangu Mzee Anselm Lyander(1928-2010).
Kutokana na msiba huo,mambo yakawa mengi na nguvu ya kuandika ikapotea ghafla. Shukrani kwa wote mlionitumia ujumbe kutaka kujua kulikoni.Kwa bahati mbaya sijapata muda wa kuwajibu nyote.Sababu ya msingi ni msiba huo.Maadam Babu amekwisha pumzishwa katika nyumba yake ya milele,hatuna budi kuendelea na maisha.
Tunapoendelea na maisha,tafadhali sikiliza nasi,kibao cha Jabali la Muziki,Hayati Marijani Rajabu na Dar International kiitwacho Rufaa ya Kifo
Kama ingelikuwa binadamu anakata rufaa ya kifo,Oh oh, kinapotokea,mbele ya Mungu na mimi ningekata rufaa, nirudishiwe wangu eeh, niliyempenda hapa duniani lakini nimeshindwa sijui nifanyeje….
Pumzika kwa amani Babu.Bwana alitoa na Bwana ametwaa.Jina lake lihimidiwe.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.


sending...
