Mwishoni mwa wiki iliyopita alifanya uzinduzi rasmi wa nyimbo hii.Huyu sio mwingine bali ni Barnaba,msanii ambaye yupo ameketi na ametulia kabisa katika orodha ya waimbaji ambao naamini kabisa kwamba wanaweza kuimba katika steji yoyote duniani na kuamsha hisia za mashabiki.He can sing!

Wimbo aliozindua pale Club Billicanas unaitwa Gube Gube.Sijajua bado kwa hakika nini maana ya neno hili.Ntamtafuta Barnaba nizungumze naye kuhusu undani wa wimbo huu katika siku za usoni.Lakini kwa haraka haraka nilipochungulia Kamusi ya Kiswahili niliyonayo inasema Gube au aghalabu Magube ni Hila au Ujanja Ujanja…Unaweza kusema Fanya Magube ukamaanisha fanya ujanja ujanja.Anyway,usikilize wimbo huu hapa chini. Hii ni production ya Tudd Thomas na Mosse Kinanda.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Wakati huo huo tunayo furaha kumtambulisha Ally Nipeshe,huyu ni msanii mpya ambaye bila kwere anaonekana kuwa na kipaji kizuri cha kuimba.Hapa anakuja na wimbo wake unaokwenda kwa jina Ntalila.Hii pia ni production ya Tudd Thomas na Mosse Kinanda.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Mwezi wa kwanza wa mwaka 2012 ndio huo tumeshaanza kuuwashia indicator.Upo ukingoni.Wakati tukihesabu siku,kwenye tasnia ya Bongo Fleva,tayari wasanii kadhaa wameshaanza kuachia ngoma zao ambazo itakapofika Desemba mwaka huu,zitakamilisha orodha ya nyimbo zilizotoka mwaka huu.

Leo hapa tunao wimbo kutoka kwa Godzilla,msanii ambaye ana style inafanana kwa karibu na 50….(malizia mwenyewe kama unaafikiana nami).Hapa anakuja na wimbo Milele akiwa amemshirikisha Ally Kiba.Milele ni production nyingine kutoka pale MJ Records chini ya Marco Chali(wenyewe siku hizi wanapenda kumuita Dr.Chali). Usikilize hapo chini

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

 

Wimbo huu nimeupokea siku kadhaa zilizopita.Muda wa kuusikiliza kwa makini nao ukawa haba.Mambo ya mwanzo wa mwaka,kurudi kazini,watoto kurudi shuleni(gharama zake sasa!).Duh,elimu imekuwa bidhaa ya ghali sana.Sijui nichague elimu mtaani?

Lakini kingine kilichonifanya “niskute” kidogo(niskute neno la zamani hili kiasi,enzi hizo) ni mabadiliko yaliyopo katika wimbo na msanii huyu.Ni kweli kwamba huyu ni Ferouz,yule yule alipitia enzi za kundi maarufu la Daz Nundaz.Ni kipaji au kujaribu soko.Ni kuingia au kutoka.Ni risk.Good or bad.Inategemea na maoni yako wewe msikilizaji.

Msikilize Ferouz katika wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina Majoto ukiwa katika style ya mchiriku,maarufu kutoka jijini Dar na pembezoni aka Pwani.Nini maoni yako?Kaelekea kuliko au kachemsha?

Ā 

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

- Song – Majoto
- Artist – Ferouz
- Producer – Pancho Latino
- Studio – B Hit’z

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Single mpya kutoka kwa The Heavy Weight MC,Professor Jay akimshirikisha Marco Chali(Dr.) inayokwenda kwa jina KamiliGado inaendelea kufanya vizuri sana katika anga mbalimbali za muziki iwe ni mtandaoni,radioni,clubs,mtaani nk.Sasa kwa kuwa Professor Jay ameitoa single hii kama zawadi yake kwako wewe shabiki wake na shabiki wa muziki kwa ujumla,unakumbushwa kuisikiliza na kui-download kupitia www.kamiligado.com.Usichelewe kufanya hivyo.

Na kwa wale wenzangu na mie wanaotumia simu za viganjani: Kwa wateja wa Airtel,unaweza kuiweka KamiliGado kama Callertune yako kwa kutuma “DEF 9521 kwenda Namba 15578.Kwa wateja wa TIGO,tuma “A1″ kwenda Namba 15050.

Black Rhino au Black Chata,bila shaka bado walikumbuka na kulitambua jina hilo.Nimeanza kwa kusema kwamba bila shaka walikumbuka kwa sababu kwa muda kiasi Black Rhino au jina halisi Nicholaus Haule alikuwa kimya kidogo katika masuala ya muziki.Mwenyewe anasema maisha ilibidi ayaelekezee kwingine kidogo.Akaenda chuoni na kupata wakti wa kuvaa lile joho(la shule ya wakubwa na sio chekechea) na kisha baada ya hapo akaanza “mzigo” kama watu wengine. Kukaa kwake kimya kukatafsiriwa na watu wengine kwamba ndio amekacha muziki au muziki umemkacha.Hapana! He is back and doing what he knows best;good music. Na mara hii,pamoja na elimu aliyonayo,bila shaka hata soko la muziki atakuwa analiangalia tofauti. Juu ya yote,Black Rhino anathibitisha kwamba ukitoka kwenye familia ya muziki,basi muziki kamwe haukuachi na wewe huna jinsi bali kwenda nao sambasamba.Majina mengine kutoka katika familia yake ni kama vile The Heavy Weight MC,Professor Jay,Kolihombi,Simple X na Mr.Teacher.

Wimbo unaitwa Taking Ova.Umetengenezwa pale Dhahabu Records chini ya Producer anayekuja juu sana anayekwenda kwa jina Mbezi.Sikiliza Taking Ova hapa chini;

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

 

Sina uhakika unaisomea wapi habari hii lakini nahisi unaisomea ukiwa katika mitkasi yako ya kila siku iwe ni kazini au katika sehemu zinginezo za kutafutia riziki.Kwa ufupi unafanya kitu! Lakini je,umeshawahi kuketi chini na kujiuliza kwa undani kabisa kwamba kwanini unafanya unachokifanya? Nini kinakusukuma kufanya hivyo?Unapohisi kukata tamaa na kitu unachokifanya,kwanini unaendelea?

Maudhui kama hayo hapo juu ndio yaliyomo katika wimbo mpya wa Mike Tee(Mnyalu) ambao amemshirikisha Fareed Kubanda au ukipenda Fid Q. Wimbo unazungumzia zaidi sanaa ya muziki.Ni wangapi wanafanya muziki kwa sababu wanapenda au wengi wanafanya kwa “Sababu Ya Njaa”?Msikilize kwa makini Mike Tee hapa.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Photo Courtesy:Get Mziki

Album ya msanii Diamond sasa ipo madukani.Jitahidi upate kopi yako halisi(original).It is one of the best albums I have heard in a long time.Believe you me!

Nani Kama Mama? Jibu jepesi ni kwamba hakuna!Ukitaka kugombana na mtu basi jaribu kuingilia kati ya uhusiano wake na mama yake.Na hii sio kumaanisha kwamba watu hawana uhusiano au mahusiano na baba zao,bali ndio hali halisi.Mothers are the best!

Pengine ni msimamo kama huo ndio uliompelekea msanii(mpya mpya huyu) kutoka nchini Kenya anayekwenda kwa jina Syd kutoka nchini Kenya kutunga wimbo Guardian Angel ambao, kwa mujibu wa maelezo yake, ni maalumu kwa wakina mama wote na hususani wakina mama wanaolea watoto wao peke yao yaani bila msaada wa baba watoto(Single Mothers).

Katika wimbo huu ambao umesimamiwa vilivyo na Ogopa DJs, Syd(pichani juu) amemshirikisha msanii maarufu wa nchini humo,Wyre. Sikiliza audio ya wimbo huo hapa chini na tizama video yake.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Bendi maarufu ya muziki wa dansiĀ  ya Twanga Pepeta, inatarajiwa kuzindua album yake inayokwenda kwa jina Dunia Daraja mnamo tarehe 6 Novemba(next weekend) pale katika viwanja vya Leaders-Kinondoni jijini Dar-es-salaam.Pichani ni baadhi ya watunzi wa nyimbo zilizomo katika album hiyo.Unaweza kuwatambua kwa majina baadhi ya unaowaona hapo? Na labda kwa kuongezea tu,ni kibao gani cha Twanga Pepeta ambacho unakikumbuka au kukipenda zaidi?Binafsi nakizimia sana Kisa Cha Mpemba.

Kampuni ya African Stars Entertainment imeandaa tamasha kubwa la burudani kwa ajili ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara na Uzinduzi rasmi wa Albamu ya 11 ya Bendi yake ya African Stars “Twanga Pepeta”.

Tamasha hilo linataraji kuwahusisha wasanii wa fani mbalimbali za Muziki wa hapa nchini na kutoka nje ya nchi. Fani zitakazohusishwa ni pamoja na Taarab, Muziki wa Kizazi kipya na Muziki wa Dansi na msanii mmoja kutoka Nchini Kenya ambaye bado uongozi wa ASET unaendelea kufanya naye mazungumzo.


Tamasha hilo la uzinduzi linataraji kufanyika katika viwanja vya Leaders Club vilivyopo maeneo ya Kinondoni Jijini Dar es salaam siku ya Jumapili ya tarehe 06-11-2011 kuanzia saa sita za mchana.

Albamu itakayozinduliwa bado haijapatiwa jina ila nyimbo zilizopo kwenye albamu hiyo ni pamoja na “Mapenzi hayana Kiapo” utunzi wake Saleh Kupaza, “Penzi la Shemeji” utunzi wake Mwinjuma Muumini au Kocha wa Dunia, “Umenivika umasikini” utunzi wake Luizer Mbutu, “Dunia Daraja” utunzi wake Charlz Baba, “Mtoto wa Mwisho” utunzi wake Dogo Rama na nyimbo ya mwisho ni “Kauli” iliyotungwa na Rogart Hegga.

Nyimbo zote zimesharekodiwa katika CD kwenye studio ya Metro chini ya Mtengenezaji Allen Mapigo na nyimbo tatu zinatamba redioni na kwenye stesheni za redio mbalimbali hapa Nchini na nje ya nchi.

Maandalizi ya Tamasha yanaendelea vizuri na katika kufanikisha Tamasha hili, ASET imeandaa ligi ndogo itakayoshirikisha timu 12 ikiwemo Timu ya Twanga Pepeta FC iliyoundwa na wanamuziki na wadau wa karibu wa Bendi.

Uzinduzi wa mwaka huu tumeamua kuuweka tofauti kama zinduzi zilizopita ili kuenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara. Bendi inataraji kuingia kambini wiki moja kabla ya tarehe ya uzinduzi ili kujitayarisha vizuri kwa ajili ya shoo kali.

HASSAN REHANI.

MENEJA ASET.

The Ladies of Twanga Pepeta

Ni mwendo wa kutwanga na kupepeta.


Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page