MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Mtagwa

BONDIA Mtanzania anayeishi nchini Marekani Rogers Mtagwa anatarajia kupanda ulingoni Januari 23 mwakani kupambana na Yuriorkis Gamboa, pambano la raundi 12 litakalofanyika jijini New York.

Pambano hilo la ubingwa linalotambuliwa na HBO litakuwa la uzito wa Feather, ambako mabondia hao wanaendelea kujifua kwa ajili ya shughuli hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Marekani zinaleza kuwa Mtagwa ana rekodi ya kushiriki mapambano 26 na kushinda 13 kwa pointi, kupoteza mawili na kushinda kwa KO 18.

Mpinzani wake Gamboa amecheza mapambano 16 na kushinda kwa KO 14, mawili kwa pointi na hajapoteza hata pambano moja.

Aidha, mbali ya pambano hilo pia kutakuwa na pambano la uzito kama huo ambalo litamshirikisha Juan Manuel Lopez atakayezichapa na Steven Luevano.

Pambano jingine linalotarajiwa kufanyika siku hiyo jijini Pasay nchini Philippines, Donnie Nietes atazipiga na Ivan Meneses.

Source:Tanzania Daima

EvanderHolyfield

BINGWA wa zamani wa masumbwi katika uzito wa juu duniani, Evander Holyfield wa Marekani amepanga kwenda Uganda kuzichapa na Francois ‘White Buffalo’ Botha wa Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa waratibu wa pambano hilo la kimataifa, wababe hao watazichapa Januari 16, wakiwania mkanda wa dunia wa WBF.

Pambano hilo ambalo litavuta hisia za wengi, litapiganwa siku hiyo katika Uwanja wa Taifa wa Mandela, mjini Kampala, Uganda. Kwa habari zaidi,bonyeza hapa.

Pichani ni Ephraim Kibonde mmojawapo miongoni mwa watangazaji mahiri wa Clouds Fm.Mbali  na utangazaji, Ephraim  pia ni mshereheshaji kwenye shunghuli mbalimbali zikiwemo,harusi,tafrija mbalimbali na hata mambo ya kijamii.Pia kama mnavyojua,Kibonde ndio mtangazaji mahiri nchini wa mapambano ya ndondi(ngumi).

Hapo pichani alikuwa akiwajibika kama MC katika send off moja hivi karibuni jijini Dar-es-salaam.

 

Pichani ni bondia Francis Cheka(kushoto) na Mbwana Matumla(aliyeipa mgongo kamera) walipokuwa wakipambana mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar-es-salaam.

Bondia Francis Cheka alimshinda Matumla kwa knock-out katika raundi ya kumi na hivyo kufanikiwa kutwaa ubingwa wa UBO(Universal Boxing Association) kanda ya Afrika.Kwa ushindi huo Cheka hivi sasa anahesabika kuwa “mbabe” wa familia ya kina Matumla kwani aliwahi pia kumtwanga bondia maarufu kutoka familia hiyo,Rashid Matumla.

Photo credits:Global Publishers

↑ Go Back to Top of Page