Bila shaka jina la Ali Kiba hivi sasa lipo miongoni mwa top performing artists kutoka Tanzania. Mbali ya kutoa show kali kali,Kiba amekuwa akitoa vibao ambavyo vinatokea kupendwa na kukubalika sana.Unaweza kuiita ngekewa au bahati lakini ndivyo ilivyo.Inasemekana ndiye msanii ambaye ameshafanya tour za nje ya Tanzania kuliko msanii mwingine yeyote.Anaitwa Ali Kiba,yule tule wa Dushelele,Mac Muga,Cinderella,Nakshi Nakshi,Mapenzi yana-run dunia na zinginezo nyingi.
Sasa alipokuwa katika tour yake ya Europe mwaka jana alipita katika studio za See Records zilizopo nchini Italy katika jiji la Napoli ambapo alikutana na Producer anayekwenda kwa jina la Alasko(raia wa Benin anayeishi nchini Italy). Wakaketi studio na kutengeneza kitu ambacho utakisikia punde.Wimbo unaitwa Mi Nimo…kuna maneno yanasema “Mi Nimo Najikongoja taratibu ndani ya hili shimo”…
Studio ya See Records,ambayo inatarajiwa kufungua tawi lake jijini Dar-es-salaam kuanzia mwezi Machi mwaka huu, imeshawahi kufanya kazi na wasanii wengine wengi kama vile Diamond,Hussein Machozi na pia imeshatengeneza videos za wasanii kama vile Asley Ft Mh.Temba,Tip Top Connection,Miaka 50 Mkubwa na wanae,Ramso Ft Godzilla nk.
Usikilize wimbo Mi Nimo kwa kubonyeza player hapo chini
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Toka pande za Mwanza(Tetemesha Recordz) kuna toleo jipya.Ni kazi mpya toka kwa msanii anayechipukia kutoka nchini Uganda anayekwenda kwa jina la Dan Flevor. Dan Flevor amekuja nchini akiwa na ndoto ya kuendeleza kipaji chake cha muziki na pia kujifunza zaidi lugha ya Kiswahili ambayo pamoja na kuwa miongoni mwa lugha maarufu ulimwenguni hivi sasa,bado haina matumizi makubwa nchini Uganda.Sababu za kihistoria kwa mfano vita ya Tanzania dhidi ya Uganda iliyokuwa chini ya utawala wa Iddi Amini,zinatajwa kuchangia katika kukifanya Kiswahili kutobamba zaidi nchini humo.
Pamoja na ndoto za kujifunza Kiswahili na kuendeleza kipaji chake cha muziki,Dan Flevor alikuwa na ndoto za kufanya kazi na wasanii kadhaa wa hapa nchini kama vile Lady Jaydee na Linex.Habari njema kwake ni kwamba jamaa wa Tetemesha Recordz iliyopo jijini Mwanza imeshafanikisha kipande cha ndoto zake kwani hapa chini utaweza kusikiliza ushirikiano wake na msanii Linex katika wimbo uitwao Kankutume(Kamwambie) .Producer wa wimbo huu ni Kid Bwoy.Ujazo Entertainment ndio wanaosimamia kazi za msanii huyo hapa nchini.Sikiliza then Kwamwambie.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
.

Msanii anaitwa WESU, na hii ndio kazi yake ya kwanza kutoka rasmi kwa ajili ya kumtambulisha. Wesu ni msanii kutokea Dar,jiji lenye kila aina ya raha na karaha..a city.
Huu wimbo unaitwa “NGOJA KUKUCHE”. Ni story ambayo inajieleza yenyewe kama ukiisikiliza kwa makini, hivyo tunaamini itaeleweka na itawagusa watu wengi kwa sababu imewakilisha maisha ya kawaida.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
CREDITS:
Tittle: NGOJA KUKUCHE
Artist : WESU
Written by: YAKI & WESU
Arranged by: AMBA
Produced by: AMBA
Mixed by: AMBA
Studio: AMBA RECORDS
SEPTEMBER 2011

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Artist: Nasreal
Song Title: Nalia
Producer/Studio: GQ-Tuff Records(Morogoro)

Nilishawahi kusema kwamba miongoni mwa mambo ninayoyapenda hapa BC ni pamoja na fursa ya kuwatambulisha wasanii chipukizi,producers,actors,actresses,comedians, nk.Kwa miaka kadhaa ambayo BC imekuwa hewani,jambo hilo bila shaka tumelifanya kwa upana wa aina yake.
Leo naomba kumtambulisha kwenu Fredrick Bundala au kwa jina la kisanii Skywalker. Huyu yawezekana asiwe mgeni sana kwa baadhi ya watu hususani wasikilizaji wa radio kwani yeye ni mtangazaji wa kituo cha Radio Free Africa kitu ambacho kwa njia moja ama nyingine tayari kinamuweka karibu na masikio ya wengi.
Mbali na utangazaji,Skywalker ni msanii na pia ni producer.Na kwa wimbo ambao utausikiliza hivi punde,naweza kumuingiza katika kundi la “uanaharakati”.Katika wimbo huu ambao ameupa jina la Esta, Skywalker anazungumzia kisa cha mtoto wa mtaani.Ni kisa cha kutunga lakini kinachoakisi maisha ya ukweli.
Nini huwa kinatokea mpaka mtoto anaishia mitaani na kubatizwa jina la “mtoto wa mtaani”?Ok…kuna wale wanaoondokewa na wazazi wote na kutokuwa na ndugu yeyote wa kujitolea kuwalea.Mambo yanapokuwa hivyo,wengine huamua kuishia mitaani.
Lakini unajua kwamba kuna watoto wengi tu ambao hukimbia nyumbani na kuishia mitaani kwa sababu mtaani kuna “nafuu” kuliko nyumbani?Jamii ina nafasi gani katika hilo?Usikilize wimbo wa Esta hapo chini.Producer wa wimbo huu ni mwenyewe Skywalker na hapa amemshirikisha msanii Salimo.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

At BC,we love introducing new artists and even new joints. Today we have a brand new song from a brand new studio. The song’s title is Falling In Love and it’s from Amba Records located at Tabata Kimanga in the suburbs of Dar-es-salaam. As I mentioned, this is the first track produced at Amba Records.
Now, Amba Records may be new. But the owner and the producer isn’t that fresh in the game. He is the man behind Hussein Machozi’s tracks such as Full Shangwe, Kwa Ajili Yako, Utaipenda and Za Mwizi.He also made it happen for Nakupenda Sana Hip Hop by Roho Saba, Tonight from Yaki and Saraha from Rama Dee. His name is Ambangile Mbwanji aka Amba.
The track Falling in Love is from a new artist who goes by the name K-Massive, a student at St Augustine University-Iringa Campus. Amba is featured in the chorus.
On a personal level,I kinda like the message in the song but felt like the song stands on “auto-tune” a bit too much. What happened to ala za muziki like guitars,drums,percussion,etc? I believe,that is still the better way to make music that will last long in the ears and hearts of listeners and music lovers.My opinion. Listen to Falling in Love and be the judge!
You can reach Amba Records by using these numbers: O753- 240 285 and 0713- 362 023
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Miongoni mwa mambo ambayo nayapenda hapa BC ni pamoja na kupata nafasi ya kuwatambulisha wasanii wapya au wanaochipukia.Naamini katika kuwapa vijana nafasi ya kusikika.Naamini katika kuwezeshana kwa njia yeyote ile halali na inayowezekana.
Hivi karibuni nilipata nafasi ya kukutana na vijana wanaokwenda kwa jina la Sababisha Empire. Makazi ya vijana hao ni Tegeta mitaa ya Chanika/Namanga jijini Dar-es-salaam.Pichani ni vijana hao;BQ (mwenye rasta), Kimo (mwenye lowcut), na Zungu (aliyesuka).
“Bro,tuna nyimbo yetu ambayo tungependa uisikilize na kama vipi warushie wasomaji wako” Waliniambia vijana hao kwa kujiamini kwamba kazi yao si lelemama.
“Sisi tuna uwezo wa kufanya miziki ya R&B(Zungu), ku rap (Kimo), na kuimba reggae na dancehall (BQ). Na kama kikundi, wote pamoja tuna uwezo wa kuimba nyimbo za asili” alieleza Kimo akijifuta jasho kwenye paji la uso lililotokana na kijua kikali kilichokuwa kinawaka.
Well,niliwaahidi kwamba nitauweka wimbo wao hapa ili wasomaji na mashabiki wa muziki wapate kuusikia.Wimbo unaitwa Bongo Fleva Time(Friday Nite). Umetengenezwa na Producer Tudd Thomas kutoka pale Ngoma Records.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Mojawapo ya mambo ambayo huwa nayapenda katika uendeshaji mzima wa BC ni pamoja na kumtambulisha msanii mpya,nyimbo mpya,makundi ya wasanii nk.Binafsi naamini sana katika sanaa kama njia mojawapo muafaka kabisa katika kufikisha ujumbe kwa jamii na hivyo kuwa chachu katika kuleta maendeleo ya kijamii,kisiasa na hata kiuchumi.
Tizama kwa mfano elimu inayotolewa kwa njia ya maigizo,nyimbo au enzi zile kupitia ngonjera(nasikia siku hizi ngonjera hakuna tena mashuleni,ni ushamba eti!).Mpaka leo nikikumbuka kisa cha sungura kukatazwa kutumia maji ya kisimani,nakumbuka kuhusu wajibu wa kuwajibika na kushirikiana!Si unakumbuka enzi za kina Mahoka?Naam hiyo ndio kazi ya sanaa.
Lakini pamoja na kuwa kioo cha jamii,sio mara nyingi ukakuta msanii akifanya kazi zake kutokana na matukio ya kweli katika maisha yake na akawa wazi kwamba anachokifanya kinatokana na uzoefu binafsi wa maisha yake.Wengi tumeumbwa ili kuwanyooshea tu vidole wenzetu.Yule kafanya vile,huyu kasema vile na mambo kama hayo.
Msanii mpya kutoka jijini Mwanza anayekwenda kwa jina la Sajna(pichani)yeye ni miongoni mwa wachache.Anakuja kwa kishindo na kisa cha kweli. Sajna ambaye ana umri wa miaka 18 tu huku bado akiwa shuleni(form II),amekuja na wimbo unaoitwa NADHIFA. Wimbo huu ni true story ambayo imemtokea yeye mwenyewe. Kila alichokiimba katika wimbo huu ni cha kweli na kinamhusu yeye na familia yake. Kwa ufupi amemuimba dada yake wa damu ambaye alitoweka nyumbani kwao bila taarifa miaka kadhaa iliyopita.Wimbo umetengenezwa na producer Sam Timber.Msikilize na mkaribishe Sajna.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Kama unafuatilia Bongo Fleva kwa makini bila shaka hivi sasa umeshalisikia jina la Sarah Kaisi au Shaa (pichani) kama ambavyo anajulikana kwa mashabiki na wapenzi wa B Fleva.
Shaa ameingia kwenye game kwa kishindo.Uwezo wake wa kumiliki jukwaa,kuimba na kwa ujumla kukidhi haja ya mashabiki wa muziki huo wa kizazi kipya,ndivyo vitu ambavyo vinamfanya azidi kupanda chati na hivyo kuungana na wasanii wengine wa kike ambao wanafanya vizuri.
Hivi sasa anatamba na nyimbo zake Zamu Yangu na Pambazuko huku akiwa anapika kitu kingine studio ambacho mwenyewe anasema ni zawadi aliyopewa na Judith Wambura aka Lady Jaydee.Tunasubiri.
Leo tunao wimbo wake Pambazuko. Katika wimbo huu amemshirikisha msanii maarufu wa B Fleva,Ambwene Yessayah au AY. Usikilize. Kama kawaida maoni yanakaribishwa(ila jitahidi kutoa maoni yanayojenga badala ya kubomoa au kuonyesha chuki na dharau).Umeupenda wimbo? Unasemaje.Shaa atazidi kushika chati?Karibu.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Shaa on stage!

Jina lake kamili ni Babu Sinare. Hivi sasa makazi yake makuu ni pale Columbus,Ohio nchini Marekani. Ni msanii mpya wa muziki wa kizazi kipya.Jina lake la kisanii ni Albino Fulani.
Hivi karibuni alifanya mahojiano marefu na jarida la Bang na kueleza kwa undani visa mbalimbali alivyopitia katika maisha yake na jinsi alivyodhamiria kuendesha kampeni ya kuelimisha jamii ili kuondoa mauaji ya albino ambayo yameigubika Tanzania kwa kipindi kirefu sasa. Ukitaka kusoma zaidi kuhusu mahojiano hayo,litafute jarida la Bang.
Miongoni mwa nyimbo zake,ni huu ambao ameutoa hivi majuzi ukiwa ni barua kwenda kwa mama yake ambaye alishaiaga dunia.Usikilize hapo chini.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.


sending...
