Mradi wa Zinduka.Nia ni kutokomeza malaria.Kila mtu analiunga mkono akiwemo Mheshimiwa Rais.Kumbe chini yake kuna mvutano.Mwanamuziki Sugu(Mr.II) ana kampuni yake.Inaitwa Deiwaka.Kwa upande mwingine kuna mfanyabiashara maarufu.Anaitwa Ruge Mutahaba.Anasaidia kuinua vipaji vya wasanii kupitia Tanzania House Of Talent(THT).Mpaka sasa wasanii kibao wameshainua vipaji vyao kupitia kwake. Kuna shirika la Malaria No More kutoka nchini Marekani.Mradi wa Zinduka ni wa nani?
Kama umechanganyikiwa na jinsi nilivyoandika hapo juu,pengine ni kwa sababu kitu chenyewe kinanichanganya hata mimi pia.Labda wasikilize wenyewe wahusika;
Sugu akiongea na waandishi wa habari.
Ruge Mutahaba akijibu mashambulizi ya Sugu
Miongoni mwa kesi na hukumu ambazo zimekuwa na mawazo au maoni yanayopishana sana katika historia ya hivi karibuni ya nchini Tanzania,ni pamoja na ile ya Nguza Viking, maarufu kama Babu Seya na wanawe watatu ambao ni Papii Kocha Nguza,Nguza Mbangu na Francis Nguza. Lipo kundi kubwa tu la raia ambao wanasema Babu Seya na wanawe walionewa(set-up) na pia lipo kundi lingine linalosema kwamba walipo(jela) ndipo wanapostahili kuwepo kwani wana hatia.Katika siku za karibuni,wanaosema kwamba Babu Seya na wanawe hawana makosa, wameongezeka zaidi.
Wakati maoni na mtizamo wa raia ukizidi kujiweka sawa,kesho ni kesho kwa Babu Seya na wanawe kwani mahakama ya Rufaa nchini Tanzania,kesho inatarajiwa kutoa hukumu dhidi ya rufaa dhidi ya hukumu ya awali ya wanamuziki hao ambao wanatetewa na mawakili wa kujitegemea Mabere Marando wa jijini Dar-es-salaam na Hamidu Mbwezeleni kutoka Zanzibar.
Je Babu Seya na wanawe wataachiwa huru hapo kesho?
Kwa undani zaidi wa kesi hii,hukumu za awali na mengineyo,bonyeza hapa

Miezi saba baadaye,aliyekuwa daktari wa Mfalme wa Muziki wa Pop ulimwenguni,Michael Jackson, Dr.Conrad Murray ameshtakiwa rasmi kwa kifo cha mwanamuziki huyo maarufu ambaye katika maisha yake,aligusa wengi.Michael Jackson alifariki dunia tarehe 25 June mwaka jana akiwa na umri wa miaka 50.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, Dr.Murray ambaye alifikishwa mahakamani mchana huu huko Los Angeles,amekana shtaka lake na ameachiwa kwa dhamana ya dola 75,000. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena tarehe 5 April.
Ndugu wa Michael Jackson,kaka zake Jermaine,Tito,Jackie na Randy ,dada yake LaToya na wazazi wake Joe na Katherine walikuwepo mahakamani kusikiliza kesi hiyo.
Hapo kabla Dr.Conrad Murray ambaye ni mzaliwa wa nchini Grenada,alikiri kwa polisi kwamba alimchoma Michael Jackson sindano ya dawa aina ya Anaesthetic Propofol kwa dhumuni la kumsaidia bingwa huyo wa Pop kulala.Alisema aliporudi tena chumbani alimkuta Michael akiwa hapumui.
Mchunguzi wa vifo wa Los Angeles alithibitisha baadaye kwamba dawa hizo ndizo zilizosababisha kifo cha Michael Jackson. Dr.Murray alikuwa ameajiriwa maalum kwa ajili ya kumuandaa Michael Jackson katika tour iliyokuwa ijulikane kama This Is It ambayo ilikuwa ianzie nchini Uingereza.

Nchini Marekani leo ni People’s Choice Awards. Sasa kwa wale wadau wa masuala ya fashion,urembo,vivazi nk, naambiwa kinachowavutia zaidi ni Red Carpet. Pale ndipo utaona nani kavaa nini,imetengenezwa na nani nk.Kumbuka tu kwamba wavaaji wale ambao ni celebrities,huwa wamepewa nguo,hereni,viatu vile nk kwa minajili ya kuzinadi.
Bonyeza hapa ili kuangalia mambo yalivyokwenda kwenye Red Carpet.
Nilichokipenda zaidi katika awards za mwaka huu ni kwamba kwa mara ya kwanza People’s Choice Awards zinachangia mradi wa Maji Safi kwa ajili ya watoto.Kwa kiingereza mradi huo unaitwa Children Safe Drinking Water. Celebrities wanapanda Mlima Kilimanjaro(nakumbusha Mlima upo Tanzania!) kwa ajili ya kuchangisha fedha. Tizama zaidi kuhusu mradi huu kutoka kwenye tovuti maalumu ya mradi huo.
Pichani juu ni Queen Latifah ambaye ndiye alikuwa Host kwa mwaka huu. As usual,I think she did a good job!

Rais wa Afrika Kusini,Jacob Zuma(66),anatarajiwa kuoa kwa mara ya tano hapo kesho huko kijijini kwake katika jimbo la KwaZulu- Natal nchini Afrika Kusini.Anatarajiwa kumuoa Tobeka Madiba mwenye umri wa miaka 37 ambaye tayari ameshazaa naye watoto wawili.
Kwa mujibu wa gazeti la Sunday Times,maandalizi ya harusi hiyo ambayo itafanyika kimila,tayari yamekamilika na kinachosubiriwa ni wageni waalikwa kuanza kuwasili tayari kwa shughuli hiyo.
Ndoa za zaidi ya mke mmoja zinaruhusiwa kisheria nchini Afrika Kusini.
Makao Makuu ya Kanisa Katoliki duniani yaliyopo Vatican hivi karibuni yametoa orodha ya nyimbo 12 katika ukurasa wao ndani ya MySpace.
Katika kile ambacho kimewashangaza wengi,miongoni mwa nyimbo hizo 12,umo wimbo uitwao “Changes” wa marehemu Tupac Shakur,mwanamuziki kutoka nchini Marekani ambaye anatambulika ulimwenguni kote kama miongoni mwa “mabalozi” wa kudumu wa muziki wa rap.
Wimbo wa “Changes” ulitolewa mwaka 1998 katika album ya Shakur’s Greatest Hits ambayo ilitolewa mwaka huo huo wa 1998.
Orodha nzima ya nyimbo zilizochaguliwa iliandaliwa na Father Giulio Neroni ambaye ni Artistic Director wa St.Paul’s Multimedia ambao ni wachapishaji wa kanisa.
Tupac ameorodheshwa sambamba na wasanii wengine kama vile Mozart,Dame Shirley Bassey,Fleet Foxes na Papa Benedict XVI mwenyewe.
Marehemu Tupac Omar Shakur alizaliwa tarehe 16 June mwaka 1971 huko East Harlem,Manhattan-New York na alifariki dunia mwaka tarehe 13 September mwaka 1996 huko Las Vegas ,Nevada. Mpaka hivi leo kuna watu ambao wanaamini kwamba Tupac Shakur hajafariki bali yuko sehemu kajichimbia. Kuna theories nyingi sana ambazo zimekuwa zikitolewa kuhusiana na dai hili la kifo au “uhai” wake mahali pengine.
Orodha kamili ya nyimbo hizo hii hapa chini; (more…)
Wanaowania tuzo maarufu za muziki za Grammy kwa mwaka 2010 wametangazwa usiku huu jijini Los Angeles ambapo mwanamuziki/mwanadada Beyonce Knowles ndiye ameongoza kwa kupata teuzi nyingi zaidi. Beyonce, kwa ujumla ameteuliwa kuwania tuzo hizo katika vipengele kumi vikiwemo albamu ya mwaka kupitia album yake ya “I am…Sasha Fierce, nyimbo ya mwaka kupitia wimbo wake “Single Ladies(Put a Ring On It) na rekodi ya mwaka kupitia wimbo wake wa “Halo”
Beyonce anafuatiwa kwa karibu na mwanamuziki ambaye ameibuka muda sio mrefu sana na kupanda chati kwa kasi ya aina yake,Taylor Swift. Taylor ameteuliwa kuwania tuzo hizo katika vipengele nane akishindana na Beyonce katika kipengele cha albamu ya mwaka kupitia albamu yake “Fearless” nyimbo na rekodi ya mwaka kupitia wimbo wake “You Belong With Me”.
Lady Gaga naye hakuachwa nyuma sana. Ameteuliwa katika vipengele vitano vikiwemo album bora ya mwaka kupitia album yake ya “The Fame” huku wimbo wake wa “Poker Face” ukichaguliwa kuwania kuwa rekodi ya mwaka na wimbo wa mwaka.
Wanamuziki wengine maarufu walioteuliwa kuwania tuzo hizo ni pamoja na The Black Eyed Peas, Maxwell na Kanye West ambao wamepata uteuzi mara sita huku Jay-Z na DJ David Guetta wamepata uteuzi mara tano au katika vipengele vitano.Black Eyed Peas wanawania rekodi ya mwaka kwa wimbo wao maarufu “I Gotta A Feeling”.
Tuzo za Grammy za mwaka huu zina jumla ya vipengele 109 na zinatarajiwa kufanyika tarehe 31 mwezi January mwaka 2010.Kwa orodha ya vipengele vya juu katika kuwania tuzo hizo,tizama orodha iliyopo hapo chini au bonyeza hapa kwa orodha kamili
Record of the Year: “Halo,” Beyonce; “I Gotta Feeling,” The Black Eyed Peas; “Use Somebody,” Kings Of Leon; “Poker Face,” Lady Gaga; “You Belong With Me,” Taylor Swift.
Album of the Year: “I Am Sasha Fierce,” Beyonce; “The E.N.D.,” The Black Eyed Peas; “The Fame,” Lady Gaga; “Big Whiskey And The Groogrux King,” Dave Matthews Band; “Fearless,” Taylor Swift.
Song of the Year: “Poker Face,” Lady Gaga and RedOne, songwriters (Lady Gaga); “Pretty Wings,” Hod David and Musze, songwriters (Maxwell); “Single Ladies (Put a Ring On It),” Thaddis Harrell, Beyonce Knowles, Terius Nash & Christopher Stewart, songwriters (Beyonce); “Use Somebody,” Caleb Followill, Jared Followill, Matthew Followill and Nathan Followill, songwriters (Kings Of Leon); “You Belong With Me,” Liz Rose and Taylor Swift, songwriters (Taylor Swift). (more…)
Rais wa zamani wa Marekani,Bill Clinton na mke wake,Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani hivi sasa,Hillary Clinton, wapo njiani kupata “mkwe” hivi karibuni kwani mtoto wao pekee,Chelsea,amechumbiwa.
Chelsea amechumbiwa na rafiki yake,Marc Mezvinsky. Habari zinapasha kwamba kitendo hicho cha kuchumbiwa kilifanyika hivi karibuni wakati wa kusheherekea sikukuu ya Thanksgiving. Chelsea na Marc walikutana Washington,DC na baadaye kuendeleza urafiki wao walipokuwa wanasoma katika Chuo Kikuu cha Stanford. Marc ambaye hivi sasa ni Investment Banker ni mtoto wa aliyewahi kuwa Mwakilishi kupitia chama cha Democrat kutoka Iowa,Edward Mezvinsky na mkewe Margolies-Mezvinsky ambaye pia aliwahi kuwa Mwakilishi kupitia tiketi ya chama cha Democrat kutoka Pennyslvania.Wote wanaishi New York hivi sasa. Wanatarajiwa kufunga ndoa katika majira ya summer hapo mwakani.
Bila shaka yule jamaa kutoka Kenya aliyewahi kutangaza kwamba angependa kumuoa Chelsea atakuwa amehuzunika kupita kiasi.Usijali best,ndio maisha.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, jana ilishindwa kuanza kusikiliza maelezo ya awali ya kesi ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221 inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumshi wa Benki Kuu ya Tanzania, Amatus Liyumba, kufuatia mshitakiwa huyo kutokuwepo mahakamani kwa sababu anaumwa. Kwa undani zaidi wa habari hii bonyeza hapa.
Takribani mwezi mmoja sasa umetimia tangu Mfalme wa Pop,Michael Jackson, afariki dunia na kuwaacha mashabiki waliokuwa wakimsubiri awape burudani katika concerts zilizokuwa zimepewa jina la This is It. Mfululizo wa concerts hizo ulikuwa uanzie huko nchini Uingereza.
Mpaka ninavyoandika habari hii,Michael Jackson hajazikwa bado. Kulikuwa na taarifa kwamba angezikwa kesho( angekuwa hai angetimiza miaka 51) lakini mpango huo ukaahirishwa kutokana na kile ambacho kimeelezewa kuwa “kutoelewana au kukubaliana rasmi” miongoni mwa wanafamilia kuhusu wapi azikwe na kwanini azikwe siku fulani. Mpango uliopo hivi sasa ni kumzika tarehe 3 September huko Forest Lawn Memorial Park, Glendale, California.
Wakati hayo yote yakiendelea,jana imetolewa taarifa ya kushtusha. Inasemekana Michael alipewa dozi kubwa ya dawa za maumivu za Propofol(dawa hatari hizi).
Kwa maana hiyo polisi wa California wamekiita kifo chake kuwa homicide kwa maana ya kwamba alifariki dunia kufuatia kitendo cha mtu mwingine kilichosababisha mauti imfike. Anayelaumiwa au kunyooshewa kidole zaidi ni Daktari wake, Conrad Murray, ambaye ndie inasemekana alimpa hizo dawa na pia alikuwa naye mpaka dakika za mwisho.Uchunguzi bado unaendelea na polisi hawajasema rasmi ni nani wanaelekea kumfungulia mashtaka ya kuua bila kukusudia.
Je Michael Jackson aliuawa na Dr.Murray? Je hakujiua mwenyewe huyu kwa kutumia madawa ambayo bila shaka alikuwa anajua madhara yake?Nani alaumiwe?

