Mojawapo ya mambo ambayo viongozi mbalimbali wa dunia hupenda kufanya wanapokutana ni kupiga picha.Katika nchi za magharibi kitu hicho huitwa Photo Opps au photo opportunity.Picha moja ni sawa na maneno elfu moja.Viongozi hulitambua hilo.Huwa ni nafasi ya kuwaonyesha wananchi mambo mbalimbali kwa kutumia picha.Wanaposalimiana na kujitega kwa picha huku wakiwa wanatabasamu,mwananchi wa kawaida atatafsiri kitu hicho kama amani,upendo na urafiki miongoni mwa viongozi hao na hivyo inamaanisha kwamba nchi zao zipo katika urafiki fulani ambao una manufaa kwa nchi husika.Yaweza kuwa kweli na pia yaweza kuwa sio kweli.
Photo Opps ni masuala ya kihistoria.Yamekuwepo tangu enzi na enzi.Ni masuala ya kidiplomasia.Viongozi kushikana mikono(kwa ishara ya kusalimiana),kutabasamu huku wakiwa wameelekeza nyuso zao upande walipo wapiga picha,ni mambo yaliyozoeleka.
Tangu Rais wa Marekani,Barack Obama aweke historia ya kuwa Rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya Afrika au mweusi na kutokana na jinsi yeye na mkewe Michelle Obama walivyoiteka dunia,hakuna kiongozi ambaye hutaka kubakia nyuma linapokuja suala la kupiga picha nao.Bila shaka utakumbuka jinsi viongozi wa G20 walivyokuwa wanahangaika kupiga picha na Obama kule nchini Ujerumani mapema mwaka huu.
Majuzi jijini New York na kule Pittsburgh hali ilikuwa ni hiyo hiyo.Viongozi wetu wa Afrika nao hawako nyuma katika suala la picha na kina Obama.Kina Obama nao bila shaka ni wapenzi wa masuala ya picha na kwa sababu wao ndio walikuwa wenyeji kidiplomasia iliwabidi.Hizi hapa ni baadhi ya picha wakiwa na viongozi mbalimbali wa Afrika akiwemo Rais wetu,Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais Kikwete (katikati) akiwa na Rais Obama(kulia) na US First Lady,Michelle Obama.Bila shaka picha hii ingependeza zaidi kama Mama Salma Kikwete angekuwepo.Mtizamo binafsi.

Kutoka kulia kwenda kushoto,Rais Barack Obama,Waziri Mkuu wa Kenya,Raila Odinga,US First Lady,Michelle Obama na mke wa PM Odinga,Mama Ida Raila Odinga.

Kutoka kulia kwenda kushoto,Rais Obama,Rais wa Uganda,Yoweri Kaguta Museveni,US First Lady,Michelle Obama na Ugandan First Lady,Janet Museveni

Kutoka kulia kwenda kushoto,Rais Obama,Rais Paul Biya wa Cameroon,US First Lady,Michelle Obama na First wa Cameroon,Mrs.Chantal Biya.Tayari kumeshazuka maneno katika blogs mbalimbali hususani nchini Marekani kuhusu wig alilovaa Mrs.Chantal Biya.Soma hapa.
Kwa picha zaidi bonyeza hapa

Tizama picha kwa makini. Unaweza kuwatambua wangapi kati ya hao waliopo pichani? Kwa ufupi ni kwamba wote ni wasanii. Kama sio sanaa ya muziki basi ni sanaa nyingine.

Ni wazi kwamba yapo mambo mengi sana(tena sana) ambayo wanaume wanaweza kujifunza kutoka kwa Rais wa Marekani,Barack H.Obama.Ni mengi kiasi kwamba tukianza kuyaorodhesha hapa sidhani kama patatosha.
Lakini kama wasemavyo wenzetu wa magharibi,Behind Every Successful Man, There is A Woman. Kwa upande wa Obama yupo Michelle.Hilo sidhani kama lina ubishi.Swali ambalo limejikita kichwani ni je,Michelle Obama anatoa mafunzo gani muhimu kwa wanandoa na zaidi wanawake?
Picha ya Michelle unayoiona hapo juu ndio picha yake rasmi (official potrait) kama ilivyotolewa na ikulu ya Marekani hapo majuzi.Picha kwa hisani ya White House/Joyce N.Boghosian.
It is every designers dream to be part of the London Fashion Week, and this year Ally Rehmtullah, a 22 year old Tanzanian designer was given this honour. On the 19th of September Ally Rehmtullah launched his new African Couture at the Museum of London during the London Fashion Week. Ally was also part of fashion diversity whereby as an established designer he was an inspiration to the young and upcoming designers in London. Ally Rehmtullah’s couture was modelled by MAHOGANY MODELS from London.Here are some images.

Kama wewe ni msomaji mzuri wa magazeti na majarida mbalimbali kutoka Tanzania,basi sina shaka kabisa kwamba jina Maggid Mjengwa (pichani) litakuwa sio geni kwako! Makala zake za kusisimua,kuchokoza hisia na kujenga hoja za nguvu ni miongoni mwa vivutio muhimu vya wasomaji wa magazeti ndani na nje ya Tanzania. Leo hii tunaweza kabisa kuthubutu kusema kwamba Maggid ni miongoni mwa wanahabari bora tulionao kwani hana uoga wowote pale anapokuwa anaandika au kuongelea jambo ambalo analiamini kwa dhati.
Lakini Maggid,kama ambavyo pengine unafahamu tayari, haishii magazetini tu bali pia ni blogger maarufu hivi sasa. Blog yake ya picha ambayo mwenyewe anaiita “kijiji” na hivyo wasomaji wake na watembeleaji wake “wanakijiji”, imejipatia umaarufu sana kwa kuonyesha au kwenda kule ambapo ndiko kunahesabika kuwa kwenye hali halisi ya maisha ya mtanzania. Ukiitembelea na kuisoma blog yake vizuri kwa kutizama picha lukuki zinazoipamba blog yake,utaweza kuwa jaji mzuri kama “bongo ni tambarare” au bado zile ahadi za uchaguzi uliopita ni mbwembwe za kisiasa tu.Mwenyewe anasema blog yake ni kimbilio na sauti kwa wale ambao kila mara huwa wanasahauliwa!
Maggid pia ni mjasiriamali.Yeye ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ijulikanayo kama Ikolo Investment Co ambao ndio wachapishaji wa Gozi Spoti; jarida la michezo, sanaa, maisha na burudani linalotoka kila Jumatano. Maggid pia ni mwanamichezo,mpenda michezo na shabiki mkubwa wa soka.
Hivi karibuni,baada ya kumsaka kwa muda mrefu kutokana na ratiba zake za kazi kumbana,tulifanikiwa kupata fursa ya kufanya naye mahojiano utakayoyasoma hivi punde.Kama ambavyo ungetegemea,Maggid anatoa “darasa” katika mahojiano haya.Mbali ya kukupa historia ya maisha yake kwa undani,Maggid anakumbusha vipengele fulani fulani vya historia ya nchi yetu ambavyo ni muhimu. Lakini kwa mapana, anaongelea kuhusu suala la uandishi na pia blog yake bila kusahau changamoto ambazo nchi yetu inakabiliwa nazo hivi leo katika nyanja mbalimbali. Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; (more…)

Kwa miaka nenda rudi,watu waishio katika miji ya pwani wamekuwa na jadi ya kutumia vyombo mbalimbali vya usafiri wa majini.Vyombo kama mitumbwi,ngalawa,ma-jahazi nk ndio vimekuwa mstari wa mbele katika kurahisisha shughuli za usafiri kwa watu waishio pwani na zaidi zaidi katika shughuli za uvuvi ambazo kwa wengi ndio chanzo chao kikuu cha mapato.
Lakini hivi karibuni vyombo hivyo vya usafiri vimeanza pia kuingia katika uwanja mpana wa burudani au michezo.Pameanzishwa vitu kama mashindano ya kukimbiza Ngalawa kama inavyoonekana pichani.Hapo ilikuwa ni huko Zanzibar hivi karibuni ambapo Issa Michuzi alishuhudia mbio za ngalawa(Canoe Race?).Hapo ngalawa na waendeshaji wake zilikuwa zinawekwa sawa tayari kwa shindano hilo ambalo lilishirikisha jumla ya ngalawa kumi na tisa(19)
Je unajua tofauti iliyopo kati ya Ngalawa,Mtumbwi na Jahazi?Tuelimishe.Hii ndio picha ya wiki.

Kwa miaka nenda rudi,maua yajulikanayo kama maua Rose(Rozi)yamekuwa yakitumika kuashiria mambo mbalimbali likiwemo suala zima la mapenzi au mahaba.Bustani zilizojaa maua Rose zimekuwa ni vivutio kwa wapendanao au wanaotaka kuanza kupendana.
Pamoja na hayo wapo baadhi yetu,akiwemo msomaji wetu mmoja aliyetuandikia na kutuomba tumsaidie kuwauliza wanaojua, hatujui chanzo,historia wala maana ya Maua Rose.
Je maua haya kwanini yamehusishwa zaidi na mapenzi?Jambo hili lilianzia wapi?Kwanini?Na leo hii maua rose bado yana maana gani?Nini tofauti kati ya mpenzi anayempa mwenzake ua rose na yule anayempa mwenzake zawadi ya kitu kama vile gari,mkufu,hereni nk?Je ni kweli kwamba kwa wengi wetu haya mambo ya maua rose ni katika kufuata tu mkumbo?Hii ndio picha yetu ya wiki.

Wikiendi inakwendaje au ilikuwaje? Hapo juu ni picha yetu ya wiki hii.Badala ya kutoa maelezo tumeona tumpe kila mtu fursa ya kutoa maelezo yake.Unadhani nini kinaendelea katika picha hii?Unaweza kutoa maelezo yapi kwa kuiangalia picha hii?
Hii ndio picha ya wiki na imepigwa na Ahmad Michuzi.Kama una picha ambayo ungependa tuiweke kama picha ya wiki,tafadhali tutumie,pamoja na maelezo yake kwa kutumia anuani pepe ya bongocelebrity at gmail dot com.

Picha rasmi ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete, imebadilika.Kama inavyoonekana pichani,picha ya Rais iliyoko kushoto ndio inakuwa picha rasmi mpya.Iliyopo kulia ndio iliyokuwa ikitumika mpaka hapo jana yalipotangazwa mabadiliko hayo.Haitotumika tena. Aliyezishikilia picha zote ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Kassim Mpenda. Hapo alikuwa akiwaonyesha picha hizo waandishi wa habari jijini Dar-es-salaam.Kwa hiyo kama ofisi yako inahitaji au ni mojawapo ya zile ambazo kiutaratibu ni lazima ziwe na picha ya Rais fanya hima uendane na mabadiliko haya.
Photo via Yahya Charahani

Picha na Father Kidevu.

