Mohamed Raza ni Msanii Maarufu wa kimataifa ambaye ni hazina Halisi ya Taifu letu la Tanzania, alianza kazi yake ya  sanaa za kuchora tokea enzi za Uhuru wa Tanganyika. Vizazi zaidi ya viwili vimenufanika na kuelimika kwa kusoma vitabu vyake tokea shule za msingi mpaka secondary hasa vya kiingereza kama familia ya Mr & Mrs Daudi na Mtakuja Primary School. Mbali na hapo Mzee Raza aliwahi kumchora Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere Miaka ya 1960 na kufanikiwa kupata kazi katika chama cha TANU. Pia aliwahi kufaya kazi katika ubalozi wa Marekani Hapa Tanzania miaka ya 70.Zaidi tizama video hii
You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Mheshimiwa Dr. Emmanuel Nchimbi(pichani), Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo atakutana na wasanii katika ukumbi wa BASATA kuanzia tarehe 31 Machi na tarehe 01 Aprili 2011.Waziri amepanga kuwaona wasanii kwa utaratibu ufuatao:-

31/03/2011 (Alhamisi) Saa 5:00 asubuhi

Wasanii wa Sanaa za Picha Jongevu na Sanaa za Maonyesho

Saa 7:00 Mchana

Wasanii wa Sanaa za Muziki na Sanaa za Ufundi

01/04/2011 (Ijumaa)Saa 3:00 asubuhi

Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya

Izingatiwe kwamba Waziri atawaona wasanii wa muziki kwa siku mbili tofauti. Tarehe 31/03/2011 ataongea na wasanii wa Muziki wote isipokuwa wale wa Kizazi Kipya. Wasanii hao ni pamoja na wale wa Muziki wa Bendi, Taarab, Disco, kwaya na Muziki wa Asili.

Tarehe 01/04/2011 ataongea na wasanii wa muziki wa kizazi kipya tu. Viongozi wa Mashirikisho ya Sanaa hakikisheni wasanii wamepata taarifa na kuhudhuria kwa wakati.

Lengo kuu ni kuongelea maendeleo ya fani za sanaa.

Ghonche Materego

KATIBU MTENDAJI


Nestory Fedeliko — wengi wetu tunamfahamu kwa jina “FeDë” — ni mchoraji katuni chipukizi kiumri. Lakini kwa upande wa kazi, utasamehewa ukidhani ni mtu ambaye labda mvi zimeanza kuota utosini!

Jamaa zetu wa Vijana FM walipata nafasi ya kumuhoji; kama ilivyo desturi yao, walimuuliza maswali matano tu. Walichopata ni majibu mazuri na ya kina — tafadhali, usiruhusu uvivu ukuingie kwasababu mahojiano yanaonekana ni marefu. Kuna hadithi na visa vya hapa na pale vitakavyokufanya utabasamu na ucheke. Majibu mengine yatakukumbusha mbali. Mengine yatakushangaza. Bila kusahau, FeDë ameamua kutoa nasaha kuhusu fani ya uchoraji wa katuni na maisha kwa ujumla.

BONYEZA HAPA KUSOMA MAHOJIANO HAYO:

Hivi karibuni kulikuwa na hekaheka mitandaoni kuhusu ujio wa filamu iliyokuwa inakwenda kwa jina “Shoga”.Mambo yalianzia mitaani.Maneno yakawa maneno.Jamii yetu ipo tayari kwa filamu kama hii?

Kabla haijatoka rasmi,panga la serikali likaipitia.Kupitia baraza la sanaa-filamu,ikaja “memo” kwamba isiingie mtaani.Inahitaji uhakiki kwanza.Baadaye inaelekea mambo yakawekwa sawa na filamu ikazinduliwa.

Lakini baada ya uzinduzi huo,suala lingine likajitokeza.Huyu Tino ni shoga?Wahakiki wa sanaa wakaanza kazi yao.Je,ule uigizaji ni umahiri wake tu katika fani au?

Kuweka mambo sawa,Hisani au maarufu kama Tino,amelonga na blog ya Mohamed Dewji na kuzungumzia suala hilo.BONYEZA HAPA KUSOMA MAHOJIANO HAYO

KUKUA kwa tasnia ya filamu Tanzania kunakwenda sambamba na kuibuka kwa vipaji vipya vya waigizaji mahiri na wenye mvuto kila kukikcha.

Mmoja kati ya Zena Mohamed Yussuf maarufu kama ‘Shilole’ ambaye tangu ajikite katika tasnia hiyo ameweza kuonyesha uwezo na kiwango cha hali ya juu licha ya kuwa amecheza filamu nne ambazo zimeshatoka mpaka sasa .

Kwa wanaofuatilia filamu hizo watakumbuka jinsi alivyofanya kweli katika ‘Fair Desecion’ akicheza na Ray, Johari na wengineo,ikifuatiwa ‘Crazy Of Love’ aliyocheza na Basupa, David Mjata na wengineo, ‘Pigo’ aliyocheza na Cloud na Aunty Ezekieli kabla ya kuibukia katika ‘Bed Rest’ akicheza na Ray, Thea, Johari na Mainda.

Hivi karibuni msani huyo ataonekana katika filamu mpya iliyosheheni nyota kibao katika nyanja mbalimbali nchini ‘Cut Off’ ambayo ipo katika matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya kuingia sokoni.

Filamu hiyo kali na ya kusisimua mbali na Shilole pia imeigizwa na wakali wengine wakiwemo Rose Ndauka, Cloud, Cheki Budi, Aunty, Darleen na wengine.

Akizungumzia tasnia nzima ya sanaa ya filamu nchini anasema kwamba imeonekana kuvamiwa kutokana na baadhi ya watu kuamua kujikita baada ya kuoana wamekosa kazi ya kufanya,huku pia wakiwa hawana vipaji hali ambayo inafanya sanaa hiyo idharaurike na kuonekana ya wababaishaji.

“Kiukweli sanaa yetu inapanda lakini kuibuka kwa watu kibao kila mmoja akijifanya msanii wakati hana kipaji kunatutilia doa na kufanya tuonekane waigizaji wote ni wababaishaji”, Anasema.

Shilole, likiwa na maana ya kioo alilopewa na bibi yake anasema kabla ya kufikia hapo alipo alipitia milima na mabonde katika kazi yake kitu anachokiona kuwa ni changamoto katika maisha yake ambavyo pia anaamini vinasaidia katika kuboresha na kukuza kipaji alichonacho.

Pamoja na hilo anasema hakukata tamaa kwani amedhamiria kuhakikisha anakuwa msanii mwenye jina kubwa zaidi alilonalo nje ya Tanzania na mipango yake zaidi kucheza hadi Hollywood.

“Ninataka kuwa first lady wa bongo movie siku moja, hilo linawezekana kwani ni moja ya dhamira yangu katika medani hii”, Anasema Shilole ambaye kabla ya kufikia hapo aliwahi kupitia katika kikundi kilichokuwa chini ya mpiga gitaa wa kundi la Jahazi Modern Taarab, Thabit Abdul ‘Mtoto wa Ilala’.

Akizungumzia hali ya sanaa hiyo kwa sasa anasema imekuwa ikikuwa kwa kasi kwa pamoja na kuibuka kwa waigizaji wengi, hata kipato wanacholipwa kimepanda akitolea mfano yeye alianza kucheza kwa ujira mdogo wa sh.20,000 lakini kwa sasa analipwa mpaka sh. 300,000 na kuendelea kwa ajili ya kazi hiyo.

Anaongeza kuwa kuibuka huko kwa wasanii kumeleta ushindani huku akimtaja Aunty Ezekiel kama ni mwanadada mkali zaidi katika movie za kibongo, huku kwa upande wa kiume akimtaja Vincent Kigosi ‘Ray’.

Msanii huyo anatoa ushauri wa bure kwa kuwataka wasanii waliokimbilia kuigiza kwa mapenzi yao tu bila ya kuwa na vipaji kuacha mara moja na kufanya vitu walivyo na vipaji nanvyo akimtolea mfano msanii wa bongo Fleva, Hemed Suleiman na kusema kwenye bongo fleva ndio nyumbani kwake.

Wasanii wengi wa kike wamekuwa wakidaiwa kutowakataa ‘mapedeshee’ pindi wanapowatokea analizungumziaje?

read more

Kama unafuatilia sanaa ya filamu nchini Tanzania, sina wasiwasi kwamba sura unayoiona hapo juu unaitambua. Unachoweza kuwa hukijui ni jina lake kwa sababu pamoja na kwamba yeye ni miongoni mwa wasanii katika tasnia ya filamu ambao tunaweza kuwaweka katika lile kundi la “wasanii makini”,bado yeye hupenda kubakia low profile.

Bila shaka utakubaliana nami nikisema uigizaji wake ni  ule ambao hauna papara.Pengine hii inatokana na nafasi(roles) anazopatiwa na kuzikubali lakini binafsi naamini ni kipaji cha uigizaji alichonacho.

Jina lake ni Hashim Kambi na kwa mujibu wa mtandao wa Filamu Central, Kambi alizaliwa tarehe 21/10/1961(muda mfupi kabla ya Uhuru) huko mkoani Morogoro.

Alianza uigizaji mwaka 1999 baada kuchaguliwa na msanii Single Mtambalike ” Ritchie” kushiriki katika igizo lililoitwa Uhondo wa Ngoma uliorushwa na kituo cha Televisheni cha TVT kwa sasa TBC1. Huo ndio ukawa mwanzo wake katika fani ya uigizaji. Mpaka hivi leo, Hashim Kambi ameshiriki katika filamu chungu mbovu zikiwemo;SIMU YA KIFO, KIPUSA, THE LOST TWINS, KIPURI, ZUADISWA, HONEY MOON, SURPRISE, RIPPLE OF TEARS, MISS CALL, ROMANCE, 20%FURAHA IKO WAPI, THE PASSION, DAMU YA MJOMBA, BWAGAMOYO, BINTI NUSA, SANDA NYEUSI, BABU SEYA, NGUVU YA MAPENZI, PENZI LA BABA, OLOPONG, SILENT KILLER, HUBA, MY FIANCEE BORN AGAIN,PRETTY GIRL, DANGEROUS DEAL.
Kambi ambaye ameoa na kubarikiwa kupata watoto ana urefu wa 5:9ft.

Photo Credit:Film Central

Ndani ya kipindi cha takribani miaka 5 iliyopita, kumekuwa kukianzishwa Reality TV Shows mbalimbali nchini kwetu. Miongoni mwa shows hizo ni pamoja na ile ya Maisha Plus ambayo kwa kipindi kifupi tu tayari ilikuwa imejizolea mashabiki lukuki.Bila shaka mafanikio hayo yalitokana na ubunifu na uhalisia uliombatana na kipindi hicho.

Hata hivyo Maisha Plus ni kama vile imepotea ghafla.Kulikoni?Baada ya kupata maswali kadhaa toka kwa wasomaji mbalimbali na hususani mashabiki wa Maisha Plus,BC ilimtafuta Masoud Kipanya ambaye ndiye mwanzilishi na mratibu mkuu wa Maisha Plus ili kupata ufafanuzi kuhusu hatma ya kipindi hicho.Haya hapa mahojiano mafupi na Masoud Kipanya(KP)

BC: Kwa muda sasa tumekuwa tukipokea maswali kadhaa kuhusu Maisha Plus.Wengi wanataka kujua kulikoni mbona hawasikii chochote na muda wa audition ndio huu?Je mwaka huu kutakuwa na Maisha Plus au ndio basi tena?

KP: Asante kaka kwa kunitafuta ili kujua kinachoendelea. Hii inamaanisha kwamba unatujali na unapenda maendeleo yetu.Ni kweli watu wengi wamekuwa wakiulizia kulikoni. Kuna sababu kadhaa ambazo zimesababisha hali iliyopo ya kuchelewesha mambo kiasi kwamba watu wengine kuona kama vile Maisha Plus imekufa. Ukweli ni kwamba Maisha Plus haijafa.Bado ipo. Kuna mambo kadhaa ambayo yalijitokeza na ndio yanachangia ucheleweshwaji huu. Miongoni mwa mambo hayo kubwa zaidi ni namna season 2 ilivyokwenda.Nitafafanua;

Kwanza kabisa naweza kusema wenzetu wa TBC kwa kiasi fulani walituangusha ingawa nashindwa kuwalaumu moja kwa moja kwa sababu mpaka leo hawajapata nafasi ya kukaa nasi meza moja kujua what happened. Tunafahamu walikuwa bize na uchaguzi na hivi karibuni pamekuwa na mtikisiko wa kuondoka kwa DG wao.

Season 2 ilirushwa vibaya sana in terms of timings. Kuna siku kipindi kilikuwa kinarushwa saa 9 mchana, siku nyingine saa 12 jioni, saa 4 usiku na hata saa 6 usiku.Yaani hakukuwa na ‘consistence’. Na kwa kawaida kipindi cha redio au tv lazima watazamaji wajue time moja, kama itatokea dharura basi mabadiliko ya muda huweza kuvumiliwa mfano nyakati za bunge au kama kuna hotuba ya Rais nk.Hii ilichangia kwa kiasi kikubwa season 2 isitazamwe na watazamaji wengi.

Bahati mbaya kwetu hakukuwa na sababu za msingi zilizowekwa wazi. Najua wasomaji wako watajiuliza kuhusu mkataba wetu na TBC, kwa kuwa tulianza kwa kutumia fedha zetu za mifukoni kutokana na kutokuwa na sponsors, tulikubaliana kwa pamoja, sisi kama waandaaji dmb Co.Ltd na TBC kukibeba kipindi kama wanavyofanya wengine mpaka kitakapochanganya na kuanza kuvuta mashabiki ambao ndio husababisha wadhamini kuingia.

Jukumu lao kwa mujibu wa mkataba wetu lilikuwa kurusha kipindi kwa wakati na sisi tulibeba jukumu la kutengeneza kipindi na gharama zake.

read more

For more cartoons,music etc visit them at www.artsfede.blogspot.com

Na Anastazia Anyimike wa Gazeti la Habari Leo

TECLA Mjata ni mwanamama mwenye kipaji cha hali ya juu katika uigizaji, ni mtu ambaye anaubeba uhusika wake ipasavyo huku akionesha kazi yake ya sanaa ya maigizo kwa kukupa uhalisia wa tukio lenyewe.

Pamoja na umahiri katika kuigiza kwenye filamu na michezo ya redio, Mjata ambaye anapenda kujitambulisha kama mama Mjata amepitia katika milima na mabonde ya maisha halisi hususani ya uigizaji.

Anasema, alianza fani ya uigizaji kati ya miaka ya 1955 na 1960 akiwa mwanafunzi ambapo alikuwa akishiriki katika michezo ya kuigiza wakati wa Siku ya Wazazi iliyokuwa ikifanyika kila mwaka shuleni kwao na hiyo ilitokana na fani ya uigizaji kuwa kwenye damu.

Baada ya kumaliza elimu ya msingi na baadaye chuo cha uwalimu mwaka 1963, alipangiwa kazi ya kufundisha Shule ya Msingi Kwamagome.

Mjata alifundisha shule mbalimbali baadhi yake zikiwa ni Kwamsangazi, Magunga Mombo na baadaye alihamishiwa Dar es Salaam ambapo alipangiwa kufundisha Shule ya Msingi Kisutu na kufuatia na Olimpio.

” Nikiwa ni mwalimu niliendelea na sanaa ya uigizaji kwa kuwafundisha wanafunzi michezo mbalimbali au hadithi, lakini mapenzi yangu zaidi yalikuwa ni mimi mwenyewe kuigiza na si vinginevyo.”

“Sababu hasa ya kuingia kwenye sanaa hii ilikuwa michezo ya kuigiza iliyokuwa ikifanyika Radio Tanzania (kwa sasa TBC1 Taifa), ambapo wasanii kama Ibrahimu Raha (Mzee Jongo), Hamisi Tajili, Tunu Mrisho (Mama Hambiliki), Ali Keto (Pwaguzi au Matuga) na Nyakomba walinivutia na mimi nikasema nikipata nafasi nitafanya vizuri zaidi.”

” Nilianza kuigiza michezo ya redio katika kipindi cha Mahoka na Pwagu na Pwaguzi ambapo tulikuwa tunaigiza vituko vilivyotokea mitaani. Kama utakumbuka yule mtoto aliyeng’olewa meno na koleo za baiskeli basi nilikuwa ni mimi. read more

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page