Mwaka jana mwezi wa nane(August),tuliuliza swali katika post hii hapa.Kichwa cha habari kilikuwa katika lugha ya Kiingereza kwamba Dr.Asha-Rose Migiro:The Next President? Swali lile tuliliuliza kufuatia kilichokuwa kikiendelea katika duru za kisiasa wakati ule. Kulikuwa na tetesi kwamba Dr.Migiro,huenda akajitupa ulingoni kuwania Urais mwaka 2015.Wadau mbalimbali wakawa wakiongelea uwezekano wa Tanzania kupata Rais wa Kwanza Mwanamke na mambo kama hayo.

Kwa bahati nzuri au mbaya,wakati ule Dr.Asha-Rose Migiro bado alikuwa akishikilia cheo chake cha U-naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(United Nations)  na hivyo kufanya tetesi zile ziishie hewani kama vile mvuke wa maji ya moto tu. Mambo yamebadilika kidogo hivi majuzi  ilipojulikana kwamba Dr.Migiro atakiachia cheo cha U-Naibu Katibu Mkuu wa UN kwa sababu muda wake umemalizika.Haijawekwa wazi kwamba kwanini yeye aondoke wakati Katibu Mkuu wake,Ban-Ki Moon bado yupo na kama walikuwa na ajenda basi ni yao wote kuitekeleza.Anyway,hayo ni mambo mengine,tuyaache kwa sasa.

Sasa kwa sababu Dr.Migiro anaondoka UN na hivyo kumaanisha kwamba atakuwa na nafasi zaidi ya kuwania Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, tayari fukuto la maoni ya wananchi limeanza kutanda. Je,agombee mwaka 2015? Je anafaa?Je,Tanzania ipo tayari kwa Rais Mwanamke? Hayo ni baadhi ya maswali yasiyo na majibu ya moja kwa moja ambayo yamekuwa yakisikika iwe ni mtaani,mitandaoni,katika vyombo mbalimbali vya habari hususani Radios nk.Nini maoni yako wewe msomaji wa BC?

Zaidi ya mwaka mmoja umeshapita sasa tangu Rais Jakaya Mrisho Kikwete aingie madarakani katika muhula wake wa pili wa kuliongoza taifa hili. Ingawa mwaka mmoja sio muda wa kutosha kwa kiongozi kukamilisha malengo na ahadi zote,ni muda wa kutosha kutoa picha ya mfumo na mtindo wa ki-uongozi.

Je,mwaka mmoja baadae,uchaguzi ungefanyika unadhani kura yako ungempa nani katika ya Rais Jakaya Kikwete na aliyekuwa mpinzani wake mkuu katika uchaguzi uliopita,Dr.Wilbrod Slaa?Kwanini?

Ninapoandika post hii, Dr.Wilbroad Slaa,kupitia tamko la CHADEMA wametoa msimamo wao kuhusu uongozi wa Rais Kikwete mwaka mmoja baadae.Gazeti la Mwananchi limeandika kwa kirefu kuhusu hilo na unaweza kulisoma kupitia hapa.

NB: Unaweza kutumia fursa hii kutoa maoni ya kujenga kwa maana ya kwamba kutoa maoni yenye tija na sio lawama na matusi.

TAREHE 31 DESEMBA, 2011

Ndugu Wananchi;

Leo tunauaga mwaka 2011 na kuukaribisha mwaka 2012. Naungana nanyi Watanzania wenzangu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na bahati ya kuiona siku ya leo. Wapo ndugu, jamaa na marafiki zetu wengi ambao hawakujaaliwa kuwa nasi kwa kuwa wametutangulia mbele ya haki. Tuzidi kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awape mapumziko mema na sisi tuendelee kumuomba Mola wetu atujaalie rehema na neema tele katika mwaka ujao.

Mapitio ya Mwaka 2011 na Matarajio kwa Mwaka 2012

Miaka 50 ya Uhuru

Ndugu wananchi;

Mwaka 2011 ulikuwa mwaka wa aina yake na wa kihistoria kwa nchi yetu na wenye mchanganyiko wa mambo. Kulikuwa na matukio ya furaha na majonzi na ulikuwa mwaka tuliopata mafanikio mengi na changamoto mbalimbali. Tumeweza kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa heshima stahiki kama nilivyoelekeza katika hotuba yangu ya kuuaga mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka 2011. Tumezitumia vizuri sherehe hizo kufanya tathmini ya maendeleo tuliyoyapata tangu Uhuru mpaka hapa tulipo sasa pamoja na kutambua changamoto zilizo mbele yetu.

Hakika tumepata mafanikio makubwa sana katika miaka 50 hii ya Uhuru wetu kuliko yale yaliyopatikana katika miaka 77 ya ukoloni wa Wajerumani (miaka 34) na Waingereza (miaka 43). Pamoja na mafanikio hayo tuliyoyapata bado nchi yetu ni miongoni mwa nchi maskini sana duniani hivyo bado tunayo kazi kubwa sana ya kufanya mbele yetu. Katika tathmini iliyofanywa na kila Wizara na Idara za Serikali, mambo yanayostahili kufanyika miaka ijayo pamoja na mikakati ya kufikia malengo hayo, yameainishwa vizuri.

Mpango wa Maendeleo

Ndugu Wananchi;

Bahati nzuri, mambo yote yaliyoainishwa kufanywa yanakuwa sehemu ya mambo ya kutekelezwa katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2011/2012 mpaka 2015/2016. Kama mtakavyokumbuka miongoni mwa matukio muhimu katika mwaka 2011 ni kukamilika kwa kazi ya kufanya tathmini ya kuhuisha Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025 na kutengenezwa kwa Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa kutekeleza Dira hiyo. Tumejipanga vizuri kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano katika Bajeti ijayo. Pia nimeunda Kikundi Kazi kinachoongozwa na Prof. Benno Ndulu cha kushauri juu ya vipaumbele na kufuatilia utekelezaji wa Mpango huo.

Ndugu Wananchi;

read more

Leo watanzania wote na wote wanaotupenda na kututakia kheri tunaungana katika kumkumbuka Baba wa Taifa letu,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alifariki tarehe kama ya leo,14th October 1999 kule nchini Uingereza.

Rais mstaafu,Benjamin Mkapa,ambaye ndiye alikuwa madarakani wakati wa msiba wa Mwalimu Nyerere,ameamua kuiweka upya risala aliyoisoma wakati wa mazishi ya kitaifa ya Mwalimu Nyerere.Tunaiweka hapa chini kwa ajili yako msomaji wetu.Isome na iwe chachu ya kutafakari.Je,tunamuenzi vipi Mwalimu Nyerere?Tunatenda au tunaishia katika maneno ya kwenye majukwaa ya siasa katika japo kujaribu kusimamia au kutekeleza yale aliyoyasimamia?Hii tuliyonayo hivi leo,ndio Tanzania aliyoiota Hayati Mwalimu Nyerere?Bila shaka,jibu ni hapana.Tumeteleza na kuanguka.Basi tunapotaka kuamka,kujipangusa na kuendelea na safari yetu,tufanye nini?Ni misingi ipi ambayo hatuna budi kuirudia?Je ni katika tamaduni zetu,katika siasa zetu,elimu,utawala au nini?Tusiishie kulalama na kujiona watu tulioshindwa.Tuna uwezo wa kumuenzi kwa vitendo.Tusione aibu ya kukiri makosa yetu.Ulimwengu umetuchanganya.Tuamke sasa.Miaka mingine ya Uhuru isije pita tukizidi kuporomoka kama taifa.Twendeni tukaifanye kazi.

Hii hapa chini ni kutoka kwa Rais mstaafu Benjamin William Mkapa;

Tribute to Nyerere

By Benjamin William Mkapa,

As Managing Editor of then ruling Party and Government Newspapers, I used to post a column regularly, entitled: What they say about US. In this I reproduce features or news analysis, both favourable and critical of Tanzania, written by journalists from all sort of local and International newspapers.

This year we celebrate fifty years of the independence of mainland Tanzania. And to-day we commemorate the passing on of its Founding Father, Mwalimu Julius K. Nyerere. Having worked with him I have been reflecting on what I could say about him. I have decided that the best tribute I can pay to his life and work is to recall the Eulogy I made on the occasion of the State Funeral at the National Stadium in Dar Es Salaam on 21st October 1999. Here it is.

State Funeral for Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

One of the legacies of President Mkapa is his handling of the illness, death and subsequent funeral of the Founding President of Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. On Mwalimu’s State Funeral on Thursday, 21st October 1999 at the National Stadium in Dar es Salaam, President Mkapa delivered the following eulogy.

This is the saddest day in the history of our country. It marks a life ceased and a service ended.

But, let me first thank the doctors, nurses and staff that day and night struggled to save the life of our beloved Founding Father of the United Republic of Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

I thank everyone who stood by us, and helped us, and all those that sent messages of support and encouragement during Mwalimu’s illness, and condolences on his demise.

I thank British Prime Minister Tony Blair and Her Majesty’s Government for being so helpful and supportive throughout the illness and death of Mwalimu Nyerere.

I thank most sincerely all of you, the leaders and other distinguished people from Africa and beyond that are here to support and comfort us. We really appreciate your coming.

I ask everyone who helped us and the bereaved family to accept the gratitude of the family, the gratitude of my Government, and the gratitude of the entire people of Tanzania to whom Mwalimu has always been, and will always be, much more than a Founding Father.

To you, the people of the United Republic of Tanzania, I am also very grateful. On 26th September, I addressed the Nation, explaining the illness of Mwalimu Nyerere and asking everyone to pray for his recovery. Across the country, across all religious faiths, prayers were said, day and night.

Now that he is no more, we have all joined hands across the country, regardless of tribe, faith, gender or race, to mourn his passing away in unity, solidarity, peace and tranquillity just like Mwalimu taught us. We have learnt well, and this is clearly a good beginning for life after Mwalimu.

Since he passed away I have received hundreds of messages of condolences from all corners of the continent and the world sent by Kings and Queens, Presidents and Prime Ministers, leaders of international and regional organisations, political and civil society leaders, and yes, from ordinary citizens of the world. They are unanimous in their description of Mwalimu as a person, as a national leader, as an African statesman and as an international personality.

I cannot read all of the messages to you. But on behalf of our continent I will read part of the message sent by the OAU Chairman, President Abdelaziz Bouteflika of Algeria. He refers to Mwalimu as:

“(T)he peerless leader who devoted his life to the service of his country and the continent, the tireless defender of just causes and worthy architect of the conquest by African peoples of their rightful place among nations of the world.”

On behalf of the international community I will quote the United Nations Secretary General Kofi Annan. Of Mwalimu he says:

“He set an example in Africa by voluntarily renouncing power and handing over to his successor through an orderly constitutional process.”

Mwalimu is one of the leaders of developing countries who challenged and critiqued the economic prescriptions of financial institutions such as the World Bank and the International Monetary Fund in the early 1980′s when he was still President, and afterwards as Chairman of the South Commission. I believe Mwalimu had an influence in changing the perspectives of these institutions and making them more responsive to our points of view. For that reason, on behalf of international financial institutions, I will read the full message of the President of the World Bank, Mr. James D. Wolfensohn. He said:

“For the men and women who have served the great cause of development in the world, one of the lights of our lives went out today. Mr. Julius Nyerere was one of the founding fathers of modern Africa. He was also one of the few world leaders whose high ideals, moral integrity, and personal modesty inspired people right around the globe.

While world economists were debating the importance of capital output ratios, President Nyerere was saying that nothing was more important for people than being able to read and write and have access to clean water.

He gave his compatriots a sense of hope and achievement early in their life as a country. And he gave them a sense of nation with few parallels in Africa and the world – bound by a common language (Kiswahili) and a history almost entirely free of internal divisions and conflict. His political ideals, his deep religious convictions, his equally deep religious tolerance, and his belief that people of all ethnic and regional origins should have equal access to knowledge and material opportunities have marked his country – and Africa – forever.

He was a leader in the liberation of Southern Africa. He looked after hundreds of thousands of refugees forced to live in western Tanzania by political turmoil in central Africa. And he left office peacefully at an age when he could certainly have continued. He was known as “Mwalimu” (or “Teacher”) – which was his first profession. Many of us still regard ourselves as his students, and we feel very honoured to have known and worked with him in his life.

To the people of Tanzania – and to his wider family across Africa and around the world – I want to say how much we share your sadness at his passing. However, the example he set and the ideals he represented will remain a source of inspiration and comfort for all of us. That is a legacy which even President Nyerere – modest as he was – would have been proud of.”

There are very many people in this country who, like me, consider ourselves lucky that our lives were touched by Mwalimu. I for one have no hesitation to say, with pride, that I learnt politics at the hand of a true master; a man who proved that politics does not have to be, as conventionally portrayed, a dirty game; an upright man, a man who would stand for what is right and just though the heavens fell.

Here was a man who friends, comrades and his fellow citizens loved deeply, and whose political foes respected highly. A man of outstanding integrity, imbued with an intense love for his fellow human beings across the lines of geography, race, colour, and gender.

read more

Naamini kwamba unatambua kwamba nchi ya Libya hivi sasa ina kiongozi mpya katika serikali ya mpito.Anaitwa Mustafa Abdel-Jalil.Kiongozi huyo ambaye ameshika usukani wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika baada ya kumng’oa madarakati Kanali Muamar Gaddafi,naye yupo nchini Marekani kuhudhuria mkutano wa UN na ametumia muda huo kukutana na viongozi mbalimbali akiwemo Rais wetu,Jakaya Mrisho Kikwete.Hizi hapa baadhi ya picha wakati viongozi hao walipokutana.

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Kiongozi wa Serikali ya Mpito ya Libya Bw.Mustafa Abdel Jalil

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo mafupi na kiongozi wa serikali ya mpito ya Libya,Bw.Mustafa Abdel-Jalil jijini New York nchini Marekani.Viongozi hao wanahudhuria Mkutano Mkuu wa 66 wa  Umoja wa Mataifa jijini New York

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Balozi wa Tanzania wa kudumu katika Umoja wa Mataifa,H.E Ombeni Sefue kwa Kiongozi wa Serikali ya Mpito ya Libya,Bw.Mustafa Abdel-Jalil.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,Mizengo Pinda, akimsikiliza kwa makini Mama Maria Nyerere alipomtembelea kijijini kwake Mwitongo Butiama.Waziri Mkuu Pinda yupo katika ziara mkoani Mara.

Unaweza kuhisi Mama Maria alikuwa akimwambia nini Waziri Mkuu Pinda?Can you caption this?

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo Jumatatu Agosti 22, 2011 amekutana na Balozi wa Misri nchini Tanzania Wael Adel Nasr ambaye amefika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam kumuaga kufuatia kupangiwa kazi nyingine, ikiwa ni baada ya kukaa nchini kwa miaka minne.

Balozi Nasr ambaye sasa anahamia kitengo cha nchi za Afrika Mashariki na Kati kama mwakilishi wa Misri alimwambia Makamu wa Rais Dkt. Bilal kuwa kuwepo kwake Tanzania kumemfunza mengi na kubwa ni kuwa Tanzania ni nchi ya amani na upendo hali iliyomfanya kuishi bila kujiona mgeni katika kipindi chote alichokuwepo nchini.

Balozi huyo aliongeza kuwa, hali inayoshabihiana katika utamaduni na maisha sambamba na mahusiano ya kihistoria baina ya nchi hizi mbili ni miongoni mwa sifa nyingine ambazo zimeyafanya maisha yake nchini Tanzania kuwa mazuri, hali inayomlazimu kutamka kuwa anaondoka Tanzania kimwili lakini moyo wake upo hapa Tanzania.

Akizungumzia mapinduzi yaliyofanyika nchini mwake, Balozi Nasr amefafanua kuwa, mapinduzi hayo yatabadili kwa kiasi kikubwa sera ya Mambo ya nchi za Nje ya Misri ambapo sasa nchi hiyo itarejesha sera inayotazama mahusiano ya karibu katika kuleta ukombozi na utanuzi wa demokrasia katika Afrika, kama ilivyokuwa wakati wa harakati za kupigania uhuru wa nchi za Afrika.

“Kama unakumbuka ndege ya kwanza kutua Tanganyika ilitoka Misri tena ilitua saa mbili baada ya Tanganyika kutangazwa huru. Hii inaonyesha kuwa ndege ile ilianza safari ya kuja Dar es Salaam saa kama nne kabla ya kutangazwa uhuru wa Tanganyika na hili ni moja ya mambo tunayoyakumbuka sana katika mahusiano yetu na Tanzania,” alisema Balozi Nasr.

Kwa upande wake Makamu wa Rais Dkt. Bilal alimwambia Balozi Nasr kuwa anashukuru kwa maelezo mazuri aliyoyatoa juu ya Tanzania na kwamba anatambua mchango wa Misri katika maendeleo ya Afrika na akasisitiza kuwa ni wakati sasa Afrika kujitegemea kwa kuongeza mashirikiano katika kukuza uchumi wa wananchi wa bara hili.

read more

Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA FEDHA

2011/2012

UTANGULIZI:

1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kujadili na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/2012. Pamoja na hotuba hii, vipo vitabu vinne vinavyoelezea kwa kina takwimu mbalimbali za Bajeti. Kitabu cha Kwanza kinahusu makisio ya mapato. Kitabu cha Pili kinaelezea makisio ya matumizi ya kawaida kwa Wizara na Idara zinazojitegemea ambapo cha Tatu kinahusu makisio ya matumizi ya kawaida kwa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na cha Nne kinaelezea makadirio ya matumizi ya maendeleo kwa Wizara, Idara zinazojitegemea, Mikoa pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, upo Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2011 ambao ni sehemu ya Bajeti hii.

2.   Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuchaguliwa tena kuongoza kwa muhula wa pili wa Serikali ya Awamu ya Nne. Aidha, ninamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa imani kubwa aliyonayo kwangu kwa kunichagua kwa mara nyingine tena kuongoza Wizara kubwa na nyeti, ninamuahidi kuwa sitamuangusha. Pia ninampongeza Dkt. Mohammed Gharib Billal kwa kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  Vile vile,

ninampongeza Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb.) kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge na kuteuliwa tena na hatimaye kupitishwa na Waheshimiwa Wabunge kuwa Waziri Mkuu kwa muhula wa pili wa Serikali ya Awamu ya Nne.

3.     Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewe binafsi Mhe. Spika Anne Makinda (Mb.) kwa kuchaguliwa kuwa Spika na hivyo kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza Bunge katika Afrika Mashariki. Kuchaguliwa kwako kunatokana na imani kubwa waliyonayo Waheshimiwa Wabunge kwa kuzingatia busara zako, uwezo na uzoefu wako ndani ya Bunge hili. Napenda pia kumpongeza Mhe. Job Ndugai (Mb.) kwa kuchaguliwa kuwa Naibu Spika. Nawapongeza pia mawaziri wenzangu wote pamoja na Naibu mawaziri wote, kwa kuteuliwa kwao na Mhe. Rais kushika nyadhifa hizo. Aidha, napenda niwapongeze wabunge wote kwa kuchaguliwa na kuteuliwa kuingia katika Bunge hili.

4.    Mheshimiwa Spika, naomba pia nichukue fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine kufanikisha matayarisho ya Bajeti hii. Maandalizi ya Bajeti ya Serikali yanahusisha wadau na vyombo mbalimbali. Kipekee ninaishukuru Kamati ya Fedha na Uchumi chini ya uenyekiti wa Mhe. Dkt. Abdallah Omari Kigoda, Mbunge wa Handeni, pamoja na kamati nyingine za kisekta kwa ushauri mzuri waliotoa wakati wakichambua mapendekezo ya Bajeti hii.

5.    Mheshimiwa Spika, naomba niishukuru kwa namna ya pekee Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kutayarisha kwa wakati Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2011 na nyaraka mbalimbali za sheria ambazo ni sehemu ya bajeti hii. Kwa upande wa Wizara ya Fedha, nawashukuru Naibu Mawaziri, Mhe. Gregory Teu (Mb) na Mhe. Pereira Ame Silima (Mb). Namshukuru Katibu Mkuu Ndugu Ramadhani M. Khijjah na Naibu Makatibu Wakuu, Ndugu Laston T. Msongole, Dkt. Servacius B. Likwelile na Ndugu Elizabeth Nyambibo. Napenda kuwashukuru Prof. Benno Ndulu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Ndugu Harry Kitilya, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na Dkt. Albina Chuwa, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa. Aidha, napenda kuwashukuru Wakuu wa Idara na wafanyakazi wote wa Wizara ya Fedha. Vile vile, namshukuru Mpigachapa Mkuu wa Serikali kwa kuchapisha Hotuba hii kwa wakati. Mwisho, nawashukuru wataalamu na wale wote waliotoa mapendekezo kuhusu sera, mikakati na masuala mbalimbali ya kodi ambayo yamezingatiwa katika kuandaa Bajeti hii.

6.      Mheshimiwa Spika, huu ni mkutano wa kwanza wa Bajeti kwa Bunge hili baada ya uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge uliofanyika mwezi Oktoba mwaka 2010 na kukirejesha Chama Cha Mapinduzi pamoja na Serikali yake katika kipindi cha pili cha Awamu ya Nne. Wananchi wana matumaini makubwa kwa Bunge hili kwamba litasaidia kuongeza kasi ya kuwapatia maendeleo na kuondokana na umasikini wa kipato unaowakabili wananchi walio wengi. Hili linajidhihirisha kwa uwepo wa Waheshimiwa Wabunge wenye umri, jinsia, elimu, na uzoefu mbalimbali. Ni matumaini ya Serikali kuwa uwepo huo wa Waheshimiwa Wabunge utakuwa ni chachu katika kuwaletea maendeleo wananchi kwa ari zaidi, kasi zaidi na nguvu zaidi.

7. Mheshimiwa Spika, Bajeti ya mwaka wa fedha unaoishia 2010/2011, imeendelea kutumika kama chombo muhimu katika kutekeleza Sera na Malengo ya Uchumi na Maendeleo ya Jamii. Katika kipindi hiki, yamekuwepo mafanikio ya kuridhisha katika kutoa huduma bora kwa wananchi na kuimarisha miundombinu ili kuwezesha kukua kwa uchumi na kupunguza umaskini.

8.    Mheshimiwa Spika, Bajeti ya mwaka 2011/12 itazingatia vipaumbele vifuatavyo:

i)        Umeme;

ii)      Maji;

iii)     Miundombinu ya usafiri na usafirishaji (reli, bandari, barabara, viwanja vya ndege, Mkongo wa Taifa);

iv)     Kilimo na umwagiliaji; na

v)      Kupanua ajira kwa sekta binafsi na ya umma.

Bajeti itahakikisha pia kuwa mafanikio yaliyopatikana katika sekta za elimu na afya yanalindwa pamoja na kuimarisha ubora wa huduma zinazotolewa.

Mikakati ya Kupunguza Makali ya Maisha kwa Mwananchi

9.    Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua changamoto zinazowakabili wananchi katika kupambana na makali ya maisha. Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011/12, pamoja na mambo mengine, inalenga katika kuchukua hatua za kurekebisha hali hiyo. Kumekuwepo na changamoto mbalimbali ambazo zinahitaji hatua za makusudi kuchukuliwa na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali, sekta binafsi na mwananchi mmoja mmoja ili kupunguza makali ya maisha kwa mwananchi. Hatua zitachukuliwa maeneo yafuatazo:-:

i)      Kasi ya kupanda kwa bei za bidhaa na huduma: Kasi ya ongezeko la bei za bidhaa na huduma nchini pamoja na mambo mengine inasababishwa na: kuongezeka kwa bei za mafuta katika soko la dunia; kutopatikana kwa umeme wa uhakika na hivyo kuathiri uzalishaji; na upungufu wa chakula nchini na nchi jirani. Serikali itachukua hatua mbalimbali kukabiliana na hali hiyo kama ifuatavyo:

a)    Ongezeko la bei za mafuta ya petroli: Ongezeko la bei za mafuta ya petroli linatokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa bei katika soko la dunia. Kwa mfano baada ya msukosuko wa uchumi duniani bei ya mafuta ilishuka hadi Dola za Kimarekani 40 kwa pipa. Kwa sasa bei ya mafuta katika soko la dunia imefikia takribani Dola 120 kwa pipa ambayo ni mara tatu ya bei iliyokuwepo awali. Aidha, ongezeko la bei linachangiwa pia na kuongezeka kwa gharama za bima ya mizigo kwa meli zinazoleta mizigo nchini kutokana na tishio la maharamia baharini, uagizaji wa mafuta wa kampuni moja moja na migogoro ya kisiasa katika nchi za Mashariki ya Kati na kaskazini mwa bara la Afrika. Pamoja na sababu zilizotajwa, bidhaa ya mafuta ya petroli inapoingia hapa nchini hutozwa ushuru wa bidhaa (excise duty) na ushuru wa mafuta (fuel levy). Zipo pia tozo mbalimbali zinazotozwa na Mamlaka zinazotoa huduma katika mfumo wa uagizaji na upokeaji wa mafuta. Taasisi zinazotoza tozo hizo ni pamoja na EWURA, SUMATRA, Shirika la Viwango la Taifa (TBS), Kiwanda cha TIPER, Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mamlaka ya Bandari na makampuni yanayoagiza mafuta. Pamoja na hatua zilizochukuliwa na Serikali za kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani na kuweka viwango maalum vya ushuru wa bidhaa kwenye mafuta, bado bei ya mafuta imeendelea kuwa kubwa na kuongeza gharama za maisha.

read more

Macho,masikio,fikra na mawazo ya wengi yanaelekea mjini Dodoma ambapo hapo kesho,serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete kupitia kwa Waziri wa Fedha,Mh.Mustafa Mkullo(pichani) itawakilisha bajeti yake kwa mwaka 2011/12. Kimsingi,kama unataka kujua mipango ya serikali na jinsi gani ahadi zilizotolewa na wabunge na hata Rais mwenyewe wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita,bajeti ndio msema kweli. Kwa maana hiyo kuna umuhimu wa kila mtu kufuatilia japo kwa kiasi fulani tu,ili kupata fununu ya jinsi gani kesho itakavyokuwa.

Bajeti hiyo kwa ufupi huanisha jinsi gani serikali imejiandaa kukusanya mapato yake(zaidi kutoka katika kodi na misaada kutoka kwa wafadhili-sijui mpaka lini) na jinsi gani itayatumia mapato hayo kutekeleza majukumu yake ya msingi kama vile ulinzi na usalama,upatikanaji wa huduma za afya, uendelezwaji na ukarabati wa miundo mbinu,utoaji wa elimu nk.

Je,kuna mapya gani kutoka katika bajeti ya mwaka jana kuja bajeti ya mwaka huu?Hali ya uchumi wa nchi hii(kama nchi na sio watu binafsi) ikoje?Je,itakuwa ni bajeti iliyolenga katika kumkomboa mwananchi au imelengwa katika kumwongezea aliyenacho? Majibu kwa maswali hayo na mengineyo mengi,yatategemea sana kitakachojiri au kitakachotamkwa kutoka katika mkoba utakaobeba “bajeti” hiyo hapo kesho.

Nchi za Kenya na Uganda nazo zinatarajiwa kuwa na sessions za uwasilishwaji wa bajeti hiyo kesho hiyo hiyo.

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page