MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Miongoni mwa wanawake wanaofahamika na kuheshimika katika fani ya sheria nchini Tanzania ni Jaji Eusebia Nicholas Munuo(pichani).Hivi leo yeye ndio Makamu wa Rais Mteule wa Chama Cha Majaji Wanawake Duniani(IAWT).Mbali ya cheo hicho,Jaji Munuo pia ndio Mwenyekiti wa Chama Cha Majaji Wanawake nchini Tanzania(TAWJA).Yeye ndio Hakimu wa kwanza mwanamke nchini Tanzania na pia Jaji wa kwanza mwanamke katika Mahakama ya Rufaa nchini Tanzania.

Miezi kadhaa iliyopita Jaji Munuo alifanya mahojiano maalumu na mwandishi Happy Katabazi kuhusiana na mambo mbalimbali ya kijamii,kisheria na pia kumhusu yeye binafsi.Je ni kweli kwamba Jaji huyu aliwahi kuamuru kwamba mumewe atiwe ndani kutokana na kuidharau mahakama?Ili kupata jibu la swali hilo na mengine mengi kumhusu Jaji Eusebia Munuo,bonyeza hapa uitembelee blog ya Happy Katabazi.

Photo/Happy Katabazi

 

Rais Jakaya Kikwete(kulia) akimuapisha Waziri Mkuu mpya,Mizengo Kayanza Peter Pinda hii leo katika Ikulu ndogo ya Chamwino mjini Dodoma.

Picha na MediaWorks News Agency.

Jina la Dr.Willibrod Peter Slaa (pichani),Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Karatu, hivi sasa linaweza kuwa jina ambalo linatajwa zaidi kushinda lingine lolote katika anga za kisiasa nchini Tanzania.Wananchi wengi wanamuongelea kama kiongozi shujaa,aliye tayari kudiriki kufanya au kusema chochote katika kutetea maslahi ya wananchi hususani wale wanaoitwa “wa kawaida” na wenye hali duni za kimaisha.Angekuwa anaishi katika nchi za magharibi,Dr.Slaa angeitwa “whistleblower” nambari wani jina ambalo hupewa mtu anayeamua kuwa mkakamavu na kukemea mienendo mibaya na isiyofaa ya watu walioko kwenye madaraka fulani nk, potelea mbali kinachoweza kumtokea kutokana na ujasiri huo.

Kwanini jina la Dr.Wilbrod Slaa liwe vinywani mwa watanzania wengi hivi sasa?Jibu ni rahisi;ni kutokana na mchango wake katika kufichua “ufisadi” uliokuwa unafanyika katika Benki Kuu ya Tanzania(BOT) na mambo mengi mengineyo ambayo anahisi yanakwenda visivyo.

Ingawa umaarufu wa Dr.Slaa haujaanzia na suala la BOT,ni wazi kwamba sakata hili ndilo limefanya jina lake liwe miongoni mwa majina maarufu sio tu kutoka kambi ya upinzani bali katika anga za wanasiasa kote nchini Tanzania.

Lakini Dr.Slaa ni nani?Anatokea wapi?Wangapi wanafahamu alikuwa akifanya nini kabla hajaingia kwenye siasa? Tangu ameingia kwenye siasa amepata mafanikio gani? Anasemaje kuhusu sakata zima la BOT?Ameridhika na maamuzi yaliyochukuliwa na Rais Kikwete?Ana ujumbe gani kwa wananchi?Ili kupata majibu ya maswali hayo na mengineyo, hivi karibuni tulipata fursa ya kufanya naye mahojiano rasmi.Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; (more…)

 

Nchi bila utawala wa sheria inakuwa ni kama sio nchi vile,haiongozeki wala kubebeka. Pichani ni Jaji Mkuu wa Tanzania,Augustino Ramadhani.Yeye ndio mwenye jukumu la kuhakikisha kwamba mhimili wa tatu wa dola(Mahakama) unafanya kazi inazotakiwa kufanya na si vinginevyo.

 

Habari mbili kubwa ziligusa hisia za wengi nchini Tanzania na pia sehemu mbalimbali duniani. Ya kwanza ni habari ambazo mpaka hivi leo bado hazijapoa za sakata zima la BOT. Ya pili,ambayo sio tu ilikuwa ni ya kuhuzunisha bali iliyostahili kukemewa kwa nguvu zote, ni habari ya kuvamiwa na kisha kumwagiwa tindikali Mhariri na mmiliki wa kampuni inayochapisha gazeti la MwanaHalisi, Bw. Saed Kubenea(pichani) huku mwandishi mwingine mkongwe na mbunge wa zamani wa NCCR-Mageuzi,Ndimara Tegambwange naye pia akijeruhiwa katika tukio hilo hilo.

Kama ambavyo wengi wenu mnafahamu,Saed Kubenea alipelekwa India kwa matibabu na alikwisharejea nyumbani nchini Tanzania. Habari za kutia moyo zaidi ni kwamba hapo jana,watu watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kujibu tuhuma za kuvamia ofisi za gazeti la MwanaHalisi na kummwagia kemilikali inayodhaniwa kuwa tindikali Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo Saed Kubenea na pia kumjeruhi kwa sime Mhariri wake wa habari, Ndimara Tegambwage. Unadhani watuhumiwa hawa walijituma wenyewe au kuna mtu aliwatuma kufanya waliyoyafanya?

Tizama picha za watuhumiwa na majina yao kama zilivyoripotiwa na Yahya Charahani kwa kubonyeza hapa.

Picha kwa hisani ya Mpoki Bukuku

Raisi Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Prof.Benno T.Ndulu (pichani) kuwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BOT). Uamuzi huo umefuatana pia na maamuzi mengine mazito kama ambavyo yameanishwa katika taarifa rasmi ya Ikulu iliyotolewa hivi leo jijini Dar-es-salaam. Yote haya yanafuatia utata na sakata zima lililokuwa limeigubika Benki Kuu ya Tanzania.

Wakati huo huo Raisi Kikwete amemteua Dr. Enos S.Bukuku kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu. Taarifa rasmi ya Ikulu unaweza kuisoma hapa. (more…)

 

Rushwa ni adui wa haki, ni adui wa maendeleo.Natumaini sote tunakubaliana na hilo.Rushwa ni mojawapo ya matatizo sugu sana yanayozikabili nchi zinazoendelea ulimwenguni ikiwemo yetu ya Tanzania.

Ndio maana nchini Tanzania kuna Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inayoongozwa na Dr.Edward Gamanya Hosea(pichani).Lakini swali au maswali magumu yanabakia.Nini chanzo cha rushwa?Nani wa kulaumiwa kuhusiana na tatizo hili?Je,wewe umeshawahi kutoa au kupokea rushwa?Ilikuwaje? Unashauri nini kifanyike?

Picha kwa hisani ya Issa Michuzi

 

Tunapoelekea kuimaliza wiki hii, pengine hakuna habari iliyokuwa ya kusisimua nchini Tanzania kuliko ya HARUNA Pembe Mgombela (54) pichani juu, ambaye ni mfungwa katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam ambaye hivi majuzi alihitimu rasmi shahada ya kwanza ya Sheria kutoka kutoka Chuo Kikuu Huria Tanzania aliyosoma akiwa gerezani humo. Haruna anaingia kwenye vitabu vya historia nchini Tanzania kwa kuwa mtanzania wa kwanza kufanya hivyo.Kweli Impossible Is Nothing kama wasemavyo Adidas.

↑ Go Back to Top of Page