Her name is Cynthia Masasi. She was born in Mwanza, Tanzania. Without a doubt, her name is among the most recognized name among Tanzanians especially abroad and even at home.
Although she has been in a limelight for a while through her career as a model, it is her appearances in a lot of rap/hip hop videos that made her popular. Those appearances, famously known as video vixen, have also been a point of attack and debates from her supporters and fans versus those who belong to the school of thought that claims; video vixen is something that degrade women and nobody’s daughter, mother or sister should be part of it.
She is now an aspiring actor, entrepreneur and continues being a model. In fact, she has already appeared in a couple of movies and has some serious upcoming projects this summer. We recently caught up with her to talk about her current career, her experiences as a video vixen and her entrepreneurship dreams and goals. How did she move from modelling to video vixen and now into much more serious acting? What is her motivation? What advice does she have for young models and artists? This is how it all went down;
BC: Cynthia, welcome to BongoCelebrity. It feels good to have you here. How are you doing?
CM: Thank you. I am doing great. How about yourself?
BC: I am doing great too Cynthia. Thanks for asking. Now I wish I could skip this question but because this is your first time on BC, there are tons of fans who’d like to know a bit about your life history. Can you briefly tell us where were you born, which schools did you go etc?
CM: I was born and raised in Mwanza. I come from a family of 6 children and I am the first born. I have one brother and four sisters. I started my academic journey at Progressive School which is in the city of Kampala in Uganda. Later on, I transferred to Nyanza Primary school in Mwanza. For secondary school, I went to Mwanza Secondary School in Mwanza. After that my mother suggested that I join Jitegemee Secondary School in Dar-es-salaam for A-Level studies. I therefore joined Jitegemee High School for the A-level. To this day I still have great memories of Jitegemee High School. Loved it! (more…)

Anaitwa Yusuf Mlela.Aliwahi kutajwa kuwa Ijumaa Sexiest Bachelor.Ni miongoni mwa movie stars wanaokuja juu kwa kasi nchini Tanzania.Una ushauri wowote kwake kuhusiana na uigizaji wake kama umeshatizama japo moja miongoni mwa filamu alizocheza?
Photo:GP
Unapoongelea sinema,hakuna ubishi kwamba majadiliano yako inabidi yaanzie Hollywood.Na unapokuwa Hollywood na kuamua kuanzisha mjadala wa Tuzo(awards) basi yakupasa uanzie kwenye tuzo maarufu za Academy au Oscars.
Muda mchache uliopita majina ya sinema,waigizaji,waongoza sinema na vipengele vingine walioteuliwa kuwania tuzo hizo kwa mwaka huu yametangazwa. Kama ambavyo ilitarajiwa, sinema ya Avatar iliyoongozwa na James Cameron pamoja na sinema ya The Hurt Locker ambayo imeongozwa na Kathryn Bigelow(mke wa zamani wa James Cameron) ndio zimepata teuzi nyingi zaidi katika kuwania tuzo hizo maarufu ambazo zinafanyika kwa mara ya 82 (miaka 82). Movie hizo zimeteuliwa mara 9 au katika vipengele 9.
Shughuli za mwaka huu za tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika tarehe 7 Mwezi Machi(takribani siku 33 zijazo).Zitaonyeshwa moja kwa moja(live) kupitia kituo cha televisheni cha ABC cha nchini Marekani.
Kwa orodha kamili ya Oscar Nominations kwa mwaka huu,bonyeza hapa. Je kuna movie,actor au actress ambaye ulitarajia angeteuliwa kuwania tuzo za mwaka huu ambaye hajatokea katika orodha?
Movie inaitwa Legion. Mungu amekosa imani na wanadamu.Anatuma malaika kuja kuiangamiza dunia. Starring Paul Bettany, Dennis Quaid,Lucas Black,Tyrese Gibson etc.Imeongozwa na Scott Stewart
Movie inaitwa Extraordinary Measures: Ni kisa cha kweli kinachowahusu wazazi John na Ailleen Crowley ambao wanajitolea kudhamini utatutwaji wa tiba kwa ugonjwa wa nadra ambao unawateketeza watoto wao wawili.Movie nzuri sana hii kwa wazazi.Starring Harrison Ford,Brendan Fraser, Courtney B.Vance nk.Imeongozwa na Tom Vaughan
Movie inaitwa The Book of Eli. Starring Denzel Washington, Gary Oldman,Mila Kunis na wengineo.
Movie inaitwa The Spy Next Door.Starring Jackie Chan, Amber Valleta,Billy Ray Cyrus(baba yake Miley Cyrus),George Lopez na wengineo. Director ni Brian Levant.

Kama ulidhani ya mwaka 2008 ndio yashaisha basi ulikosea.Mambo yangali yakiendelea.Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha na Mipango,Bw.Gray Mgonja leo ametinga kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Henzron Mwankenja, akikabiliwa na mashtaka mbalimbali.Mojawapo ya mashtaka anayokabiliwa nayo ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka kama ilivyokuwa kwa mawaziri wa zamani wa wizara hiyo nyeti, Daniel Yona na Basil Mramba waliofikishwa kizimbani wiki mbili zilizopita.
Habari hii inaendelea…stay tuned.

Muite Steven Kanumba.Hapa ilikuwa wiki iliyopita wakati wa utoaji wa tuzo za Vinara wa filamu Tanzania. Waandaaji wa tuzo hizo walimpa Kanumba Tuzo ya Heshima kutokana na mchango wake katika maendeleo ya filamu nchini Tanzania.Kuna watu wanakubaliana na uamuzi huo wa waandaaji wa tuzo hizo na kuna ambao hawakubaliani wakisema kwamba ni mapema mno kwa Kanumba kupewa “tuzo ya heshima”.Wewe unasemaje?
Mwingine aliyepewa tuzo ya heshima ni Ngumbagwe Misayo au maarufu kama Thea.Ukitaka kusoma mahojiano tuliyowahi kufanya na Steven Kanumba siku za nyuma,bonyeza hapa.
Photo/A.Mrisho

Moja kwa moja kutoka mjini Dar-Es-Salaam, tunafurahi kutangaza siku ya uzinduzi maalumu wa sinema ya Bongoland II. Tarehe ya uzinduzi ni mwezi April 5, 2008 hapa mjini Minnepolis, Minnesota katika ukumbi wa sinema wa Oakstreet Cinema.
Sinema hii ilitengenezwa mwaka jana July pale mjini Dar. Vitongoji maarufu vya mji huo kama Manzese na Magomeni vilitumika katika utengenezaji wa sinema hii. Kusema kweli, hii itakuwa ni hadhi kubwa ya wasanii wa ki-Tanzania maana sinema hii itaonyeshwa katika tamasha mbali mbali za sinema za kimataifa.
Sinema hii ni inamhusu Juma Pondamali ambaye baada ya maisha na malengo yake kutofanikiwa nchini Marekani, aliamua kurudi nyumbani. Lakini visakato alivyovikuta nyumbani vilimshangaza sana na hakuna kitu chochote hapa ulimwenguni ambacho kingemtayarisha kupambana na visakato hivyo.
Jitayarishe kuwaona wacheza sinema wakongwe wa Tanzania kama Mzee Kipara, Bi Chuma Selemani Mzee na Bi Thecla Mjatta. Vile vile pia kuwaona wachezaji chipukizi kutoka mjini Dar-es-salaam.
Msanii mhusika mkuu ni Peter Omari ambaye anacheza kama Juma. Peter, ambaye kwa sasa anishi Mwanza, aliwahi kucheza katika sinema yetu iliyopita iliyoitwa TUSAMEHE.
Habari hii ni kutoka kwa Kibira Films International

Pichani ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Dr.Rose Asha Migiro(kulia),akiwa na George Clooney(46),mwigiza filamu na mwanaharakati maarufu kutoka Marekani.
George Clooney aliteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki-Moon hivi karibuni kuwa mjumbe au balozi mpya wa tisa wa amani wa Umoja wa Mataifa (U.N. Messenger of Peace ). Dr.Migiro alimkabidhi George Clooney Cheti Cha Mjumbe wa Amani.
Mwaka huu Clooney amechaguliwa kuwania tuzo maarufu ya Oscar kwa uigizaji wake katika filamu iitwayo Michael Clayton.

MWANAMUZIKI nyota wa muziki wa kizazi kipya, Banana Ally Zorro(pichani), baada ya kutesa vilivyo katika anga la muziki hivi karibuni anatarajiwa kuibuka kivingine katika filamu mpya ya ‘Kibongo’ inayokwenda kwa jina la ‘Mr. Handsome’, imefahamika. Habari zaidi bonyeza hapa.


