MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Sijui kama nitakuwa nimekosea nikisema kwamba pengine AY na MwanaFA mpaka hivi sasa wanaweza kuwa wanashikilia rekodi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao wameshirikiana zaidi katika kazi zao.Kumbuka hawa wametoka mbali tangu enzi zao wakiwa East Coast Team iliyokuwa ikiongozwa na King Crazy GK ambaye sina uhakika yuko wapi siku hizi na anafanya shughuli gani.

Kuthibitisha kuzidi kukomaa kwa ushirikiano wao,AY na MwanaFA wakimshirikisha Hard Mad,wameachia single inayokwenda kwa jina Dakika Moja. Hii ni production kutoka B’Hitz Production iliyo chini ya Hermy B.

Sikiliza hapo chini;Ujumbe ni kwamba anaomba dakika moja tu aseme yaliyopo moyoni.Mmh,inawezekana kweli ndani ya dakika moja kikaeleweka?Sijui.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

“Kama maisha tumejaliwa,kama vipaji tumeshapewa,kwanini leo tuogope?Wanafiki tuwashangae,Wanachekesha”

Si maneno yangu bali maneno kutoka kwa vijana wa TMK Majita.Yamo katika wimbo wao walioutoa hivi karibuni unaokwenda kwa jina la Wanachekesha.Hii ni production kutoka Sound Crafters Studio chini ya Producer Enrico na Muba Touch.Burudika.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Miongoni mwa mambo ambayo nayapenda hapa BC ni pamoja na kupata nafasi ya kuwatambulisha wasanii wapya au wanaochipukia.Naamini katika kuwapa vijana nafasi ya kusikika.Naamini katika kuwezeshana kwa njia yeyote ile halali na inayowezekana.

Hivi karibuni nilipata nafasi ya kukutana na vijana wanaokwenda kwa jina la Sababisha Empire. Makazi ya vijana hao ni Tegeta mitaa ya Chanika/Namanga jijini Dar-es-salaam.Pichani ni vijana hao;BQ (mwenye rasta), Kimo (mwenye lowcut), na Zungu (aliyesuka).

“Bro,tuna nyimbo yetu ambayo tungependa uisikilize na kama vipi warushie wasomaji wako” Waliniambia vijana hao kwa kujiamini kwamba kazi yao si lelemama.

“Sisi tuna uwezo wa kufanya miziki ya R&B(Zungu), ku rap (Kimo), na kuimba reggae na dancehall (BQ). Na kama kikundi, wote pamoja tuna uwezo wa kuimba nyimbo za asili” alieleza Kimo akijifuta jasho kwenye paji la uso lililotokana na kijua kikali kilichokuwa kinawaka.

Well,niliwaahidi kwamba nitauweka wimbo wao hapa ili wasomaji na mashabiki wa muziki wapate kuusikia.Wimbo unaitwa Bongo Fleva Time(Friday Nite). Umetengenezwa na Producer Tudd Thomas kutoka pale Ngoma Records.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.



Sensational and sexy is all that human being can say when listening to the vocals of Ray-C. Begging and asking for the forbidden love of a taken man in this song; Ray C can be quite tempting and convincing.

She has been away for sometime but god given talent is not something that goes away like that and here she proves again she can do it.

Ray C approached Amani for a new song after hearing the song Amani Composed for K- Lynn (Not a Flirt). The song was composed, written and recorded within 10 hours, from 9pm-7am over energy drinks but it came out beautifully.

Ray C loved this song so much she decided to use the same title to her upcoming album, and this comes as an official second release from that album.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

CREDITS:

Song:  Japo Suna

Artist: Ray C

Composed and Arranged by: Amani

Written By: Amani

Produced & Recorded By: Pancho Latino At B’Hits  Studio 2,Dar Es Salaam.

Additional instruments: Pancho Latino

Mixed and Mastered By: Pancho Latino At B’Hits Studio 3, Namanga, Dar Es Salaam.

Pancho Latino and Amani appears courtesy of B’Hits Music Group Located In Dar es Salaam Tanzania.

You can read past BC’s interview with Ray C by clicking here.

Bila shaka mimi na wewe tunakubaliana kwamba miongoni mwa miradi ambayo imefanyika katika kuinua vipaji vya vijana nchini Tanzania katika miaka ya karibuni,miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na ile ya kuanzisha Tanzania House of Talent(THT).

Kama umewahi kuhudhuria shughuli fulani na vijana kutoka THT wakawa miongoni mwa watoa burudani,bila shaka utakubaliana nami katika kumpa pongezi Mkurugenzi wa THT,Bw.Ruge Muhataba ambaye pia ni Mkurugenzi wa PrimeTime Promotions na Clouds FM.

Lina(pichani) ni miongoni mwa vipaji vinavyokuzwa au kuendelezwa na THT.Hivi karibuni amekuja na kibao kinachoitwa Bora Nikimbie. Anasema amechoshwa na manyanyaso na vipigo na hivyo anaona bora atoke mkuku.Msikilize;

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

NB: Kiburudisho cha ziada: Pamoja na kuwa na kipaji cha usanii wa muziki,Lina ni shabiki wa soka.Lakini hivi majuzi alitoa kali ya mwaka alipoulizwa kitu kuhusu mashindano ya Kombe la Dunia yanayoendelea huko Afrika Kusini.Unajua aliulizwa nini na akajibu nini?Bonyeza hapa.

Mara ya mwisho msanii Juma Nature alipotoa wimbo mpya,baadhi ya wapenzi wa muziki wake hawakusita kuelezea hisia zao kwamba Nature amebadilika. Kivipi? Walisema haimbi na hana tena yale mashairi yaliyomfanya akakubalika sana hapo mwanzoni. Wakamsihi arudi kule kule alipoanzia.Kule kule kwenye nyimbo kama vile Hili Gemu,Kighetogheto,Sitaki Demu,Mzee wa Busara na nyinginezo.

Huenda ombi la washika dau hao wa muziki likawa limesikilizwa.Wimbo mpya wa Nature unaitwa Msichana Mtundu.Kwa upande wangu kilichonivutia zaidi katika wimbo huu ni ujumbe uliomo. Shule,maisha,baba-sukari,mapenzi,jamii.Usikilize hapa.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Anajulikana kwa jina la Pipi.Ni msanii wa kizazi kipya ambaye ni matunda ya Tanzania House of Talent(THT).Wimbo wake mpya unaitwa First Time.Usikilize hapa

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Rafiki yangu mmoja aliwahi kuniuliza “Eti kaka,unavyoona wewe,tofauti ya elimu itolewayo nchi za nje na inayotolewa hapa nyumbani zina tofauti gani”? Kawaida huwa sipendi kukurupikia kujibu maswali ya “mitego” namna hiyo.Lakini kwa hili sikukawia sana kumjibu.

Kimsingi elimu hazitofautiani sana kwani kama alivyowahi kusema Mwalimu Nyerere, elimu ni kile kinachobakia kichwani baada ya kumaliza shule.Unaweza kusoma nje ya nchi na kisibaki kitu kichwani wakati unaweza kusomea Bongo na vingi vikabaki kichwani.Nani kaelimika zaidi? Kama nimefundishwa vitu 30 na baada ya kumaliza shule ninavyovikumbuka au kuvifanyia kazi ni vitu viwili au kimoja,basi hapo kuna mushkeli.

Lakini tofauti ambayo ni rahisi kuiona ni katika ufundishaji na uwajibikaji wa Mwalimu pindi mwanafunzi anaposhindwa mtihani. Mwanafunzi anaposhindwa mtihani, nani wa kulaumiwa? Nchini kwetu,Mwalimu ambaye mitihani yake ni migumuuu kiasi kwamba wa kwanza anatoka na C,huyo hupewa sifa…Mwalimu mkali(mkali kwa maana ya kwamba ni mzuri,kiboko cha wanafunzi nk) sana yule!Hakuna anayemtupia lawama Mwalimu. Lawana ni kwa wanafunzi.Ni vilaza hawa,mbumbumbu mzungu wa reli.

Kwa upande mwingine, Mwalimu ambaye wanafunzi wake wote wanafaulu mitihani yake kiasi kwamba wa mwisho anakuwa na B,huwa anaonekana kilaza fulani hivi.Iweje wanafunzi wafaulu hivyo? Anatunga mitihani rahisi sana.

Katika nchi nyingi za nje hali ni tofauti kabisa. Wanafunzi wakifeli,mwalimu anaulizwa kwanini.Lawama zinakwenda kwa Mwalimu.Kwanini mwanafunzi huyu amefeli au kwanini wanafunzi hawa alama zao haziridhishi?

Mambo kama hayo ndio wanayoyaongelea Mandojo na Domokaya katika wimbo wao Elimu ya Juu. Wananikumbusha enzi za viboko,mikononi na makalioni. Enzi za “kujaladia” ili njiti zisiingie sana.Mwalimu akikushtukia unaambiwa nenda chooni kavue nguo ulizogandamiza ndani.Unarudi unakula njiti kisawasawa.

Usikilize wimbo wao kwa kubonyeza player hapo chini.Niliwahi kuwahoji Mandojo na Domokaya. Bonyeza hapa kusoma mahojiano hayo.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Kwa takribani miongo isiyopungua mitatu sasa,dunia imegubikwa na hofu,majonzi na wasiwasi kutokana na maradhi yatokanayo na Upungufu wa Kinga Mwilini(UKIMWI). Barani Afrika hivi leo,karibuni kila mtu ameshampoteza rafiki,ndugu au jamaa kutokana na maradhi haya.

Ukweli ni kwamba Ukimwi upo,unaua na ni hatari.Ni wajibu wa kila mtu kuchukua tahadhari zote ili kupunguza maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.Lakini ni wangapi leo hii wanakufa kwa wasiwasi tu? Wasiwasi kwamba kwa sababu amepata malaria kila mwezi,homa za mara kwa mara hazimwishi na anakumbuka mara ya mwisho alipojamiiana,ile mipira ya kiume aliiacha pembeni ya kitanda ikiwa kama ilivyotoka dukani,basi tayari anao!

Kuna umuhimu wa kupima ili kuwa na uhakika wa afya zetu na kupata ushauri wa kitaalamu wa jinsi ya kuishi na matumaini. Wimbo Hali Yangu Mbaya kutoka kwa wasanii Tunda,Chege na Madee umelenga katika kukumbushana kuhusu janga hili la ukimwi.Usikilize ujumbe uliomo katika wimbo huo kwa kubonyeza “player” hapo chini;

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Kama mwandishi, sitakiwi kuishiwa maneno. Natakiwa kuwa na uwezo wa kusikiliza kwa makini,kuufanyia kazi ujumbe,kisha kuupeleka ujumbe huo kwa jamii baada ya kuufanyia tathmini ya mwisho bila kusahau maoni yangu binafsi.

Lakini zipo siku huwa naishiwa maneno.Nasikiliza ujumbe kwa makini kisha nashindwa kuuelewa vizuri au nashindwa niseme nini. Mambo huwa yananiwia magumu zaidi pale ninayemsikiliza anakuwa ni msanii kwani kwa kawaida,msanii ni (au anatakiwa kuwa kioo cha jamii). Useme nini zaidi wakati msanii kishasema? Umbeya?

Hali ninayoiongelea hapo juu ndio iliyonitokea baada ya kusikiliza wimbo mpya mpya kutoka kwa Mike T(naam yule yule ‘mnyalu” aliyewahi kujiuliza what if angekuwa star,je angebadilika?) Wimbo wake unaitwa Tujiibe Tukiweza. Anachosema Mike ni kwamba, mapenzi sio lazima yawe ya wazi.Ukiweza iba au ibeni. Kwanini unadhani sijaelewa au kupata cha kusema haraka haraka? Sababu ni kwamba naiangalia jamii yetu. Je wizi huu ukiendelea na majanga tuliyonayo tutafika?

Kwa upande mwingine najiuliza,anachokiongelea Mike T si ndicho kilichotawala jamii zetu hivi leo? Kibustani,king’asti, ku-Zuma,nyumba ndogo nk? Unadhani Mike yupo nje ya mipaka au hii ni kazi nyingine nzuri ya sanaa? Msikilize kwa makini hapo chini; Warning: Explicit Contents

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

SINGLE: MIKE TEE – TUJIIBE TUKIWEZA (TANZANIA)

PRODUCED BY: PANCHO

COMPOSED BY: MIKE TEE / MWANA FA

STUDIO: B-HITZ / MYKEY RECORDS

SOUND ENGINEER BY: PANCHO

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page