
Ukanda wa Afrika Mashariki unaendelea kuwa ukanda uliojaa simanzi kwani wakati Tanzania tukiendelea kuomboleza msiba mzito wa watu waliofariki katika ajali ya kupinduka kwa meli ya MV Spice Islander huko Zanzibar,jirani zetu Kenya nao wapo katika msiba mzito kufuatia watu wengi kupoteza maisha kufuatia mlipuko wa bomba la mafuta katika eneo la viwanda la Lunga Lunga jijini Nairobi.

Rais wa zamani wa Cuba,Fidel Castro,mwishoni mwa wiki hii ametimiza miaka 85 tangu azaliwe mnamo August 13 mwaka 1926 huko Biran nchini Cuba.Akiwa na miaka 32,Fidel Castro aliongoza mapinduzi yaliyomn’goa madarakani Fulgencio Batista aliyetambulika kwa wengi kama dikteta.Katika mapinduzi hayo,Fidel Castro alishirikiana kwa karibu na mdogo wake Rais wa sasa wa Cuba,Raul Castro na rafiki yake mwanamapinduzi maarufu mzaliwa wa Argentina,Che Guevara.
Cuba ni miongoni mwa nchi ambazo zina uhusiano wa karibu na Tanzania.Mpaka hivi leo tunao wasomi mbalimbali hususani madaktari waliopata na wanaoendelea kupata mafunzo yao nchini Cuba.Happy Birthday Fidel.

The Revolutionaries,Che Guevara and Fidel Castro
Kama mnavyojua wenzetu wa Gongo la Mboto na maeneo mengine ya jiji la Dar-es-salaam walipatwa na janga la mabomu yaliyolipuka kutoka katika ghala nambari 5 la Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ)
Ni tukio la kusikitisha ambalo bado linatatiza wengi.Katika kuonyesha mshikamano na wote walioathirika,CEO wa Tongwe Records “Jay Murder” alijiwa na wazo la kuwaunganisha wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya ili kutengeneza wimbo ambao sio tu ni kama rambirambi kwa wote waliopoteza maisha au kuondokewa na ndugu,jamaa na marafiki bali pia kuelezea mambo kadhaa waliyonayo kama wasanii(kioo cha jamii).
Matokeo ya mkusanyiko huo wa wasanii ni wimbo uliopewa jina Toa Ndugu.Usikilize hapa.The Song was Produced By J-Ryder From Tongwe Records. To Know More About This Song, Contact Fid Q (Main Speaker of The Song)
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Mpangilio wa wasanii walioshiriki katika wimbo huu ni kama ifuatavyo;
Verse 1
Banana Zorro, G – Nako, Adam Mchomvu, Barnaba, Dj Fetty.
Chorus (Nurueli)
Verse 2
Cyrill, R.O.M.A, Domokaya, Jos Mtambo, Lord Eyez, Chege.
Chorus (Nurueli)
Verse 3
C Pwa, Ncha Kali, Bwana Misosi, Papaya, Darasa.
Chorus (Nurueli)
Verse 4
Anna, Soprano, Amini, Ditto.
Chorus (Nurueli)
Outro (Fid Q)
God Bless Tanzania, Bless Gongo La Mboto, and Bless Tongwe Records.

Baada ya tukio la jana la milipuko ya mabomu huko Gongo la Mboto,suala ambalo limebakia kuumiza vichwa vya watu wengi ni suala la uwajibikaji. Nini kimesababisha tukio hili la kusikitisha ambalo wengi tunashindwa kuliita “ajali” kutokana na ukweli kwamba miaka miwili tu iliyopita(April 2009),tukio linalofanana na hili lilitokea kule Mbagala na maisha ya watu wengi kupotea? Nani awajibike?
Katika kutafuta majibu kwa swali hilo na mengineyo,Shirika la Sauti ya Amerika(Voice of America) kupitia idhaa yake ya Kiswahili na kupitia mtangazaji wake Sunday Shomari,lilimuuliza Waziri wa Ulinzi wa Tanzania,Dr.Hussein Mwinyi swali hilo na mengineyo. Sikiliza mahojiano hayo hapa;
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Kwa habari zingine kuhusu tukio hili,tembelea tovuti ya VOA Swahili kwa kubonyeza hapa.
Ni siku nyingine ya majonzi makubwa nchini Tanzania kufuatia milipuko iliyotikisa jiji la Dar-es-salaam jana jioni.Milipuko hiyo ilitokea katika ghala la kuhifadhi silaha za kijeshi huko Gongo la Mboto.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Uingereza(BBC) kupitia idhaa yake ya Kiswahili,watu 20 wameuawa na mamia ya watu kujeruhiwa. Taarifa hiyo imemnukuu mnadhimu mkuu wa majeshi,Lt.Gen Shimbo
Mashirika mbalimbali ya habari ulimwenguni likiwemo la CNN,yameripoti kuhusu tukio hili.Hii ni mara ya pili kwa milipuko kama hiyo kutoka jijini Dar es Saalam katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.Mwaka 2009 zaidi ya watu 20 waliuawa na wengine 300 kujeruhiwa kufuatia milipuko iliyotokea katika ghala lingine la kijeshi katika maeneo ya Mbagala jijini Dar-es-salaam.
Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu wote mahali pema peponi na awaponye majeruhi wote.

Kila lenye mwanzo,lina mwisho.Usemi huu umethibitika leo huko nchini Misri baada ya utawala wa miaka 30 wa Hosni Mubarak kufikia kikomo.Muda mfupi uliopita,Makamu wa Rais wa Misri, Omar Suleiman, ametangaza kwamba Hosni Mubarak ameondoka madarakani na kuikabidhi nchi mikononi mwa vikosi vya kijeshi (Supreme Council of the Armed Forces).Tangazo hilo linamfanya Waziri wa Ulinzi,Mohammed Hussein Tantawi, kuwa ndio kinara mkuu wa nchi kwa hivi sasa.
Kwa bahati mbaya kwake na nzuri kwa wananchi,Mubarak hajaondoka madarakani kwa matakwa yake. Ameondolewa na nguvu ya umma.Nguvu ya wananchi.Wengi wao,wameiita siku ya leo “Siku ya Uhuru”. Egypt is now Free. Wamesikika wakisema huku wakipeperusha bendera za nchi yao zenye rangi nyeusi,nyekundu na nyeupe.

Kila mashindano Kombe la Dunia la Soka(FIFA) huwa na vituko au vitu fulani ambavyo huwekwa katika kumbukumbu ya kudumu vichwani mwa wapenzi wa soka na hata wale ambao sio wapenzi.
Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu zitakumbukwa kwa mambo mawili makubwa.Kwanza ni zile tarumbeta za Vuvuzela na Pili ni Paulo,yule Pweza wa nchini Ujerumani aliyetabiri matokeo ya mechi mbalimbali na kuwa sahihi kwa asilimia 100%.
Bahati mbaya ni kwamba wakati Vuvuzela bado zinadunda na kuzidi kusambaa ulimwenguni kote, Paulo Pweza amefariki. Paulo Pweza amefariki akiwa nyumbani huko Oberhausen, nchini Ujerumani akiwa na miaka miwili.

Mke wa Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe,kwa mara nyingine tena amejaza kurasa za mbele za magazeti na vyombo vya habari huko kusini na kati mwa Afrika baada ya kuenea kwa uvumi kwamba amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye ni miongoni wa marafiki wa karibu wa mumewe.
Kwa mujibu wa Gazeti la Times Live la nchini Afrika Kusini,Mugabe aliambiwa siri hiyo nzito na dada yake,Sabina, alipokuwa mahtuti kitandani kabla hajafariki baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Grace Mugabe,ambaye ni kiumri ni mdogo kwa Rais Mugabe kwa miaka 41,mara kwa mara amekuwa akihusishwa na kashfa za kimapenzi nje ya ndoa.Miaka kadhaa iliyopita alisemekana kuwa na uhusiano na jamaa aliyeitwa Peter Pamire kabla jamaa huyo hajafariki katika ajali ya gari ambayo ilitokea katika mazingira ya kutatanisha. Jamaa mwingine anayeitwa James Makamba,ilibidi akimbie nchi baada ya kuenea kwa tuhuma hizo.
Mtu ambaye anahusishwa katika uvumi ulioenea hivi sasa ni Gideon Gono,ni Gavana wa Benki Kuu ya nchi hiyo,mshauri wa karibu wa Mugabe na pia mfuasi mzuri wa chama anachokiongoza Mugabe cha ZANU-PF.
Hii inaweza kuwa hadithi ya what comes around,goes around,kwani uhusiano wa Mugabe na mkewe Grace pia ulianza katika wigo wa mapenzi ya nje ya ndoa.Wawili hao walianza mapenzi yao wakati Grace alipokuwa Katibu Muhtasi(Secretary) wa “Jongwe”.Watatu miongoni mwa watoto wao,walipatikana katika kipindi hicho huku Mugabe akiwa ndani ya ndoa halali na mkewe Sally ambaye alikuwa akiugua kabla ya kufariki dunia mwaka 1992

Mwanamuziki maarufu wa mtindo wa Reggae ulimwenguni, mzaliwa wa Jamaica, Gregory Isaacs, amefariki dunia hivi leo nyumbani kwake jijini London nchini Uingereza. Gregory Isaacs alizaliwa jijini Kingston nchini Jamaica mwaka 1951.Amefariki akiwa na umri wa miaka 59.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na meneja wake, Copeland Forbes,Gregory Isaacs amefariki kutokana na ugonjwa wa kansa ya mapafu(Lung Cancer) ambayo aligunduliwa kuwa nayo mwaka mmoja uliopita ingawa aliendelea kuwa jukwaani mpaka wiki chache zilizopita.
Gregory ambaye wapenzi wa muziki walimpa jina la “Cool Ruler” kutokana na aina yake ya muziki wa reggae iliyokuwa imejaa nyimbo zenye dhana za mapenzi au mahaba,alianza kazi za muziki tangu akiwa kijana mdogo kabisa.
Baadhi ya nyimbo zake zilizowahi kutamba ni kama vile “Love is Overdue”, “All I Have is Love”,”Soon Forward” and What Feeling bila kusahau kibao chake kilichompatia umaarufu ulimwenguni kote cha “Night Nurse” kilichomo katika albamu yake ya mwaka 1982 iliyobeba jina hilo.
Maisha yake katika muziki yaliingia dosari,pale alipojiingiza katika utumiaji wa madawa ya kulevya kitu ambacho kilipelekea kuswekwa lupango mara kadhaa. Mwaka 2007 aliwahi kusema kwamba yeye amepitia “Cocaine High School”, shule bora kupita zote lakini pia ya bei mbaya kupindukia!
Utumiaji wa madawa ya kulevya ulisababisha kupotea kiasi kwa sauti yake iliyokuwa imezoeleka ingawa hali hiyo haikuathiri sana mauzo ya albamu yake ya mwisho aliyoitoa mwaka 2008 na kwenda kwa jina “Brand New Me”


sending...