Pichani ni viongozi mbalimbali wa nchi za barani Afrika.Picha hii ya Ikulu,ilipigwa huko Addis Ababa hivi majuzi wakati viongozi hao walipokuwa wakihudhuria mkutano wa nchi za Umoja wa Afrika.Je,unaweza kuwatambua wangapi kwa majina na nchi wanazoziongoza?
Zawadi ya Tshirt ya BongoCelebrity.com itatolewa kwa yeyote atakayeweza kuwataja viongozi zaidi ya 10.

Unaowaona pichani,wote ni wanasiasa.Wote ni vijana.Nape Nnauye(kushoto katika picha) ni Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM )anayesimamia Itikadi na Uenezi.Kulia ni Mh.John Mnyika(MB) ambaye ni Mkuu wa Habari na Uenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA). Kazi zao zinafanana.Wanaongea na sisi tunawasikiliza.Wanaeneza itikadi na kunadi sera za vyama vyao.
Lakini suala la siasa ni imani.Unaamini kwamba anachokisema yule ni cha kweli na anayo dhamira nzuri kuhusu maendeleo yangu. Sasa wanaposimama hawa wawili kuongea,unamwamini yupi zaidi? Ni kitu gani kinachokufanya umwamini zaidi huyo unayemwamini? Tungependa kupata maoni yako.
NB: Vipima joto hivi vya BC,ni sehemu ya kuhakikisha kwamba viongozi na wananchi wanajua wapi wanaposimama au wanapobidi kusimama kila wakati na sio wakati wa uchaguzi tu.
Pichani ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika, ambaye duru za kisiasa kupitia wadau wanaofutilia masuala ya siasa zinamtaja kuwa miongoni mwa wabunge wa uhakika na wanaofanya kazi nzuri ya uwakilishi wa wananchi ndani na nje ya Bunge.
Lakini siasa sio sababu ya kuweka picha hii hapa.Ni kukuuliza wewe msomaji kama unaona tofauti zipi au ngapi katika picha hizi. Quiz Time!

![John-Mnyika[1]](http://www.bongocelebrity.com/wp-content/uploads/2011/11/John-Mnyika1.jpg)

Hawa jamaa…ni kina nani?Wanapelekaje mkono kinywani?

Diamond

Bob Junior
Hivi ni kitu gani kinamfanya mwanamuziki mmoja kuwa zaidi kuliko mwingine? Ni sauti,ni muonekano,ni tungo nzuri au ni bahati tu ya kupendwa?Au ni “swagger” kama wanavyosema vijana wa kileo?
Swali au maswali kama hayo nilikuwa nikijiuliza hivi leo wakati nikisikiliza mpambano katika kipindi cha Nani Zaidi kinachorushwa na Radio One Stereo(89.5fm) kutokea Mikocheni jijini Dar-es-salaam.Ni kipindi ambacho kimekuwepo katika kituo hicho toka enzi zile za kina Charles Hillary(Mzee wa Macharanga)
Katika kipindi hicho wasanii Diamond Platinumz na Bob Junior ndio waliokuwa wanashindanishwa katika kipindi hicho ambapo wasikilizaji huwa ndio waamuzi kwa njia ya simu wanazopiga na kuweka bayana ni nani aliye kipenzi chao au wanayedhani ni zaidi ya mwingine.
Pamoja na maswali yangu au yetu,katika kipindi cha Nani Zaidi kilichorushwa leo hii tarehe 9 Oct.2011,Msanii Diamond Platinumz ndiye aliyeibuka mshindi kwa jumla ya kura 26 dhidi ya kura 10 zilizokwenda kwa Bob Junior.
Je,endapo ungelikuwa na nafasi ya kusema chochote juu ya mpambano katika ya Diamond na Bob Junior ungesemaje ?Nani zaidi kwa mtizamo wako ?Kwa kutumia vigezo gani ?

Kawaida habari kama hii huwa naziweka katika ukurasa wa GLOBAL CELEBRITIES NEWS & ENTERTAINMENT unaopatikana kwa kubonyeza link hapo juu.Naiweka hapa ili kukukumbusha kutembelea ukurasa huo na pia kukutakia wikiendi njema.
Je,unaweza kuwatambua waliopo pichani?

Kuna wakati napenda kuwaza(sio mara zote,naomba nikiri).Ninapowaza na kushindwa kupata majibu,sina budi kushirikisha wenzangu.Mara nyingi kimbilio langu huwa ni wewe msomaji.Nathamini mchango wako na naheshimu thamani ya ubongo wako.Nakukubali.Leo nimewaza na kushindwa kupata majibu.Hivi nini chanzo cha majina haya ya mitaa na sehemu mbalimbali za jiji la Dar-es-salaam?Unajua?Unamjua anayejua?Kwanini leo tusitumie muda wetu kujuzana?Eti nini chanzo cha majina haya?Asili yake nini?Mfano;
- Kariakoo
- Magomeni
- Msasani
- Upanga
- Kunduchi
- Buguruni
- Vingunguti
- Tabata
- Mikocheni
- Mbezi
- Kimara
- Tegeta
- Boko
- Kigamboni
- Masaki
- Oysterbay
- Na mengineyo mengi….

Ingawa historia ya filamu za kitanzania au Kiswahili ina historia ndefu(tangu enzi za kina Yombayomba,Chale Mwembamba na Mnene,Maangamizi nk),hakuna ubishi kwamba unapoongelea masuala ya sanaa hiyo hivi sasa,ni vigumu kuwaweka kapuni vijana wawili;Steven Kanumba na Ray Kigosi(kama wanavyoonekana hapo juu pichani).Kwa sababu mbalimbali,zikiwemo wingi wa filamu walizocheza na kuongoza(hili bado halinipi amani ya kweli),ndizo zinazowaweka mbele ya wenzao.
Mbaya au zuri ni kwamba Kanumba na Kigosi ni marafiki.Wenyewe wanapenda kutumia neno “swahiba” wanapotajana iwe ni hadharani au katika blog zao(Ya Kanumba hii hapa na ya Kigosi hii hapa).Pamoja na urafiki walionao,ninavyojua mimi Ray na Kanumba ni washindani. Wamewahi wenyewe kuongelea suala na “kufunikana” kama filamu.Kwamba mimi ni zaidi ya wewe na mambo kama hayo.
Hilo ndilo linalonifanya leo nikuletee wewe msomaji (natumaini u-mpenzi wa filamu za kitanzania[bongo films/movies]) nafasi ya kuwa jaji.Kwa mtizamo wako na kwa jinsi ambavyo umekuwa ukifuatilia filamu au uigizaji wa Steven Kanumba na Ray Kigosi nani unadhani ni zaidi ya mwenzake? Na je unaweza kusema ni kwanini unadhani huyo unayesema ni zaidi ni zaidi ya mwenzake?Una ushauri gani kwake au kwao?

Tip: She recently became a Mom and worked on a radio before and we interviewed her.

Anaitwa Elizabeth Michael.Jina maarufu ni Lulu.Ni msanii mdogo lakini anafanya vizuri katika medani ya filamu nchini Tanzania.Pamoja na kufanya kwake vizuri,mara kwa mara amekuwa akiibukiwa na “skendo” za hapa na pale.Lipo suala la maadili na lipo suala la “usasa” au ukipenda kwenda na wakati au fashion.Ashike lipi aache lipi?Jamii isimame wapi?Njia panda?Mwaka jana alikuwemo katika orodha ya Global Publishers ya mastaa wenye skendo “live“. Ushauri?


sending...
