MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Bila shaka unatambua kwamba miongoni mwa mitandao maarufu zaidi ulimwenguni ni mtandao wa Facebook. Historia ya Facebook ni nzuri sana.Ukipata muda isome hapa.

BC ipo pia katika Facebook.Kule watu hukutana,kujadiliana mambo kadhaa na pia kupashana habari mbalimbali. Kama bado hujajiunga nasi katika Facebook Group yetu(shukrani kwa wale ambao mmeshajiunga) unaweza kufanya hivyo kwa kubonyeza hapa na kisha kuingia(login) kupitia akaunti yako ya Facebook

Familia ya Mzee Gembe wa Upanga Dar-es-salaam na Tabora,kwa moyo mkunjufu, tunapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru ndugu,jamaa,majirani na marafiki wote waliofanikisha shughuli zote za msiba wa Marehemu mtoto wetu,mdogo wetu,dada yetu, Evaline Gembe ambaye alifariki huko Toronto nchini Canada katika hospitali ya Mtakatifu Michael tarehe 30/March/2010 na hatimaye kuzikwa tarehe 13/Aprili/2010 kijijini Inyonga Mkoa wa Tabora.

Shukrani za pekee tunaomba ziwafikie Jumuiya yote ya watanzania wanaoishi nchini Canada hususani katika Jiji la Toronto na vitongoji vyake. Asanteni sana kwa michango yenu ya hali na mali ambayo ilisaidia katika mipango na mikakati yote ya kuuhifadhi mwili hadi kuusafirisha kwa gharama kubwa kutoka Toronto hadi Dar-es-salaam mnamo tarehe 8/April/2010.Asanteni kwa sala,maombi na kujitokeza kwenu katika kutufariji na kututia nguvu.Shukrani za pekee ziwaendee kamati nzima iliyoratibu na kufanikisha shughuli nzima ya kuusafirisha mwili wa Marehemu Evaline kuja Tanzania.

Tunapenda pia kutoa shukrani nyingi kwa majirani,ndugu,jamaa na marafiki kwa misaada yenu ya hali na mali na pia kushiriki katika shughuli zote za mazishi. Shukrani kwa wote mliofika nyumbani Dar-es-salaam na Tabora katika kutufariji,mliotupigia simu au kutuma ujumbe kwa njia zingine kwa nia ya kutufariji na kututia nguvu.Asanteni sana.

Shukrani pia ziuendee Ubalozi wa Tanzania nchini Canada na Jumuiya mbalimbali za ki-Tanzania nchini Marekani na wanablogu wote waliolitoa tangazo la kifo kwenye Blogu zao.

Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru kila mtu kipekee,tunaomba shukrani hizi mzipokee wote mliohusika kwa njia moja ama nyingine katika kufanikisha shughuli nzima ya msiba huu wa ndugu yetu Evaline.Hatuna cha kuwalipa bali tunamwomba Mwenyezi Mungu awajalie na kuwazidishia katika shughuli zenu za kila siku.

Sisi tulimpenda sana Evaline lakini

Mwenyezi Mungu amempenda zaidi,

Jina la Bwana lihimidiwe.

Amen


Familia ya Bwana na Bibi Gembe wa Upanga-Dar-es-salaam na Tabora, wanasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao mpendwa Evaline Gembe(pichani) kilichotokea hapo juzi tarehe 30.3.2010 huko Toronto,Canada.Evelyne amefikwa na mauti katika hospitali ya St.Michael’s ya Toronto alipokuwa amelazwa.

Taratibu na mipango ya  kusafirisha mwili wa marehemu kwenda nyumbani Tanzania kwa mazishi zinafanyika nyumbani kwa dada yake, Julie huko huko Toronto,Canada.

Ukiwa kama mtanzania,ndugu,jamaa au rafiki, unaombwa kuchangia fedha,hali na mali kwa ajili ya kuwezesha kuusafirisha mwili wa marehemu kurudi nyumbani kwa mazishi mapema kadri iwezekanavyo kwani kama wengi wenu mnavyofahamu, mwili unavyozidi kukaa Funeral-Home,gharama ndivyo zinavyozidi kuongezeka. Mwili utasafirishwa punde tu zitakapopatikana fedha za kutosha kwa ajili ya kulipia gharama husika.

Unaweza kutuma mchango wako kwenye Account maalumu ya wafiwa kama ifuatavyo:

BANK : CIBC (Canadian Imperial Bank of Commerce)

ACCOUNT NUMBER: 5681839

TRANSIT NUMBER: 00902

INSTITUTE NUMBER: 010

SWIFT CODE: CIBCCATT

Vilevile unaweza kutumia E-mail Money Transfer kwa Sania Esmail.Anuani yake ni saniae@yahoo. ca au kuwakilisha msaada wako kwa kutumia anuani hii:

1025 SCARLETT ROAD, APT 606, BUZZ # 178

TORONTO ON, M9P 3V3.

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana na wafuatao:

Julie +1 416-247-8318

Esmail Manambi- +1 647- 299-2572

Victor Wambura- +1 647-428-4118

Prosper Luteganya- +1 905 626 3764

Tafadhali chukua muda kuwafariji na kuwaombea ndugu,jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huu. Tunatanguliza shukrani kwa misaada yote iliyotolewa na itakayotolewa. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amen.

Kwa wale ambao hawaupati mtandao wa www.globalpublisherstz.com; Wanashauriwa kubadilisha Browser na kutumia Mozilla Firefox.

Imeonekana kwa sasa website(tovuti) hiyo haifunguki kwa kutumia Browser ya Internet Explorer(IE).

Ni rahisi kubadilisha kutoka Internet Explorer kwenda Mozilla Firefox.Unachoweza kufanya ni ku-download Mozilla Firefox kwa kufungua link ifuatayo;

http://www.mozilla.com/en-US/products/download.html

Samahani kwa usumbufu wowote unaojitokeza kwa sasa.Tatizo linashughulikiwa.

GLOBAL PUBLISHERS


summit-logo

Je wewe ni mwanablogu (Blogger) au mdau wa habari na mawasiliano kwa umma kwa kutumia mtandao? Kama jibu ni ndio, tafadhali unaombwa kujiorodhesha kwa ajili ya maandalizi ya Kongamano Maalumu la Kitaifa kwa ajili Wanablogu (Bloggers) na wadau wa habari na mawasiliano wa Tanzania (Tanzanians Bloggers Summit) linalotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu jijini Dar-es-salaam,Tanzania.

Dhumuni la kongamano hili ni Kuelimishana, Kufahamiana, Kuamsha Utambuzi Rasmi Kuhusu Tekinolojia ya Blogu na Mawasiliano ya Umma kwa Kutumia Mitandao, Kusaidia Utambuzi Rasmi juu ya mchango wa blogu nchini Tanzania kama chombo muhimu cha habari na mawasiliano, Kuelimishana jinsi gani blogu zinaweza kutumika katika kuleta maendeleo katika nyanja za kijamii, kisiasa na kiuchumi, kuburudisha, kukuza utamaduni nk.

Wataalamu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wataalikwa kutoa mada na mafunzo mbalimbali kuhusiana na tekinolojia ya kublogu, zana nyinginezo za mawasiliano mtandaoni kama vile mitandao jamii(social networking), online forums nk.Kutakuwa na vipindi vya maswali na majibu.

Ili kufanikisha maandalizi ya Kongamano hili la kihistoria, kujiorodhesha kwako ni muhimu sana. Muda wa kujiodhoresha ni kuanzia tarehe 12/8/2009 (Jumatano) mpaka 12/9/2009 (Jumamosi) tu.

Kinachohitajika ili kujiandikisha ni :

Jina Lako, Anuani yako ya barua pepe (E-mail), Mahali Ulipo au unapoishi (Nchi,mji nk),Namba ya Simu (sio lazima) na Anuani au URL(Universal Resource Locator) ya blogu yako (mfano www.kongamano.blogspot.com/wordpress.com/.com/typepad nk). Vyeti vya Ushiriki vitatolewa kulingana na habari utakazoziorodhesha hapa.

Unaweza kujiorodhesha kwa kutuma ombi lako kwa barua pepe kwenda; summit@bongocelebrity.com.

Zingatia tarehe za kujiandikisha.

Ni mwezi mmoja tu! Asante kwa ushirikiano. UMOJA NI NGUVU!

vinara-voting3-copybc

TUZO ZA
VINARA WA FILAMU 2009 KUWASHIRIKISHA WANANCHI

Mchakato wa kutafuta vinara wa filamu Tanzania kwa mwaka huu utawahusisha wananchi kupitia upigaji kura.

Wapenzi wa tasnia ya filamu nchini watapendekeza filamu ambazo wanaona zinastahili kuingia tuzo za vinara wa filamu. Mbali an wananchi pia kuna taasisi mbali mbali kama vile kampuni ya uhasibu inayotambulika kimataifa litasimamia zoezi la mapendekezo ya filamu. Filamu zenye kura nyingi ndizo zitakazoingia katika tuzo hizi. Pia filamu zitakubaliwa kutokana na mapendekezo ya waandaaji na majaji.

Kuteua filamu ni kwa njia ya ujumbe mfupi ambapo mpenzi atatakiwa kuandika neon vinara kasha jina la filamu anayoipenda na kutuma kwenda 15551 kwa gharama ya Tshs 300.

Vipengele vitakavyowaniwa mwaka huu katika tuzo za vinara ni Mwigizaji bora wa kiume na wa kike wa mwaka, Mwigizaji chipukizi wa kiume na wa kike, Filamu bora ya mwaka, Muongozaji bora wa Mwaka, Mwandishi bora wa filamu, Adui bora, Msanii bora msaidizi wa kiume na wa kike, Mhariri bora wa mwaka, Mtunza Sauti bora, Mtunza Mwanga bora, Mpiga picha bora wa mwaka, Mtayarishaji bora wa filamu, Mtunzi bora wa filamu, Mapambo na maleba bora, msanii maarufu wa kiume na kike na Tuzo ya heshima.

Vipengele vilivyoongezwa ni mtunza taa bora, mtayarishaji bora wa filamu (producer) na wasanii maarufu wa kike na wakiume (People’s choice Award).

Mwaka huu kampuni mbali mbali zimejitokeza kudhamini mashindano haya lakini yatatajwa baada ya upigaji kura

Filamu zinazostahili kupendekezwa ni zile zilizotengenezwa kuanzia januari 2009. Filamu zitakazo ingia moja kwa moja ni zile ambazo bado hazijaingia sokoni lakini yatawasilishwa na watengeza filamu wenyewe.

Zoezi la kupendekeza filamu litafanyika hadi septemba 30 kabla ya kupatikana wahusika kwenye kila kipengele kabla ya wananchi kupiga kura kuwapata washindi.

Khadija Khalili

Mratibu


zara-tours-logoLeo tunapenda kuwashukuru wadhamini wetu kampuni ya Zara Tours ambao wanaongoza kwa huduma zote zinazohusiana na utalii nchini Tanzania.Zara Tours ndio inayoongoza pia kwa kuandaa safari za kupanda Mlima Kilimanjaro.Shukrani nyingi kwa udhamini wenu.

Kwa habari zaidi kuhusu huduma za utalii zitolewazo na Zara Tours,bonyeza hapa ili kutembelea tovuti yao.

NB: Kama na wewe una biashara au kampuni na ungependa kuwa mmoja wa wadhamini wa BC,usisite kuwasiliana nasi kupitia bongocelebrity at gmail dot com au kupitia kwenye fomu inayopatikana katika ukurasa wa “Kuhusu BongoCelebrity” hapo juu.

party

Kazi kwenu wakazi wa Washington DC,maeneo ya jirani na wote wanaojua maana ya kujumuika na kustarehe!

Piga picha hii.Unanunua gazeti,unapata habari mbalimbali,unaburudika,kuelimika na kufahamu mengi yanayoendelea nchini Tanzania na hata sehemu zinginezo za ulimwengu.Kwa wengi hilo ni jambo muhimu na linalojitosheleza kabisa.Lakini je ungepewa pia nafasi ya kujishindia zawadi kama gari aina ya Mercedez Benz kwa ununuzi na usomaji wako huo huo wa gazeti/magazeti ungechangamkia tenda?

Basi hilo linawezekana kupitia promosheni kabambe inayoendeshwa na kampuni ya uchapishaji magazeti ya Global Publishers.GP ndio wachapishaji wa magazeti ya Uwazi,Championi,Ijumaa,Risasi,Amani,Ijumaa,Wikienda,Bongo Sun na Jarida la School & College.Kwa habari zaidi na jinsi ya kushiriki kwenye promosheni hii,bonyeza hapa.Kazi kwenu,Benz sio kwa ajili ya kina nani hii tu kumbe!

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page