
This is to inform the general public that the Muhimbili National Hospital Board of Trustees has appointed Dr. Marina Aloyce Njelekela as the Executive Director of the Hospital with immediate effect. Before her appointment, Dr. Njelekela was a Senior Lecturer and Head of the Department of Physiology at the Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS).
Dr. Njelekela has worked with MUHAS since 2001 and prior to that, she had worked at Kisarawe District Hospital as a Medical Officer and at the Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI) as a Registrar until 1998 when she went for further studies in Japan.
Dr. Marina Njelekela holds a Doctor of Medicine Degree from the Univeristy of Dar es Salaam, and a PhD in Human and Environmental Studies from Kyoto University, Japan. Her area of specialization was Pathogenesis of Lifestyle Related Diseases in Developing countries.
As a team player, Dr. Marina Njelekela led the Medical Women Association of Tanzania (MEWATA) for six years. During her two terms as a MEWATA leader, she was in the forefront of health awareness among women and the general public, especially on Breast Cancer Awareness and Screening Campaigns that were conducted in Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Mtwara, Lindi, Dodoma, and Manyara.
She is also well known for her role in advocacy campaigns and has brought to light the real extent of the problem of breast and cervical cancers in Tanzania that led to significant improvement on the prevention and management of Cancers in the country.
Dr. Njelekela sits on various Boards, including the Aerial Glaser Paediatric AIDS Healthcare Initiatives (AGPAH) and Management Development for Health (MDH). She is a recipient of various awards in academia and social services, including the prestigious Martin Luther King Drum Major Award for Justice that was bestowed on her by the US Embassy in January 2010 for her efforts to improve women’s access to health care services.


Takribani siku 4 zilizopita,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,alihutubia taifa katika utaratibu aliojiwekea wa kila mwisho wa mwezi hususani panapokuwa na mambo ya msingi ambayo ni muhimu yeye kuyazungumzia kama Mkuu wa Nchi.Hii hapa chini ni hotuba kamili kwa wale ambao hamkuweza kupata nafasi ya kumsikiliza hapo majuzi.
Ndugu Watanzania Wenzangu;
Kwa mara nyingine tena naomba tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na uzima, na kunipa fursa ya kuzungumza nanyi kwa kupitia utaratibu wetu huu mzuri wa kila mwisho wa mwezi. Mwezi huu tunaoumaliza leo ulijawa na mchanganyiko wa mambo, yalikuwepo mambo ya furaha na ya majonzi.
Tuliuanza mwezi kwa sherehe za Eid El-Fitr, kuadhimisha kumalizika kwa swaumu ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Nafurahi kwamba sherehe hizo zilifana na kuisha salama.
Lakini, usiku wa tarehe 10 Septemba, 2011 katika mkondo wa bahari wa Nungwi, Zanzibar kulitokea ajali ya kuzama kwa meli ya MV Spice Islander iliyokuwa na watu wengi na shehena kubwa ya mizigo. Mara baada ya taarifa ya ajali kutufikia hatua zilichukuliwa za kuokoa watu, meli na mali iliyokuwamo. Bahati nzuri ndugu zetu 619 waliweza kuokolewa wakiwa hai na sasa wanaendelea na shughuli zao za ujenzi wa taifa na kujiletea maendeleo yao. Maiti 203 waliweza kupatikana na kuzikwa kwa heshima. Maiti 197 walipatikana eneo la tukio, tano walipatikana Kenya na mmoja Tanga. Maiti waliopatikana eneo la tukio walizikwa Unguja na wale waliopatikana Kenya na Tanga walizikwa huko huko. Meli iliyozama haikuweza kuopolewa. Wataalamu wa uzamiaji wanasema ipo kwenye kina kirefu cha mita 300 ambacho hawakuweza kuifikia. Wao walifikia mita 58 tu. Wametushauri kuwa haitakuwa rahisi kuifikia meli hiyo, hivyo tukubali kuwa ndiyo makazi yake ya kudumu na vyote vilivyokuwamo ndani yake. Kwa kweli hatujui kwa uhakika kama wapo watu waliozama pamoja na meli hiyo au hapana. Bahati mbaya idadi kamili ya watu waliokuwamo katika meli hiyo haijulikani kwa uhakika. Orodha rasmi ya wenye meli inaonesha idadi ya watu waliokuwemo kwenye meli wakati inaondoka bandari ya Malindi, Zanzibar kuwapungufu kuliko idadi ya watu waliookolewa na maiti waliopatikana. Kwa sababu hiyo, huenda wapo watu waliozama na meli na kushindwa kutoka.
Ndugu Wananchi;
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amekwishaunda Tume ya Uchunguzi ambayo baada ya kumaliza kazi yake ndipo undani kuhusu ajali hiyo utapoweza kujulikana. Tume hiyo imekwishaanza kazi na kama kila kitu kitaenda kama ilivyopangwa, baada ya mwezi mmoja wataimaliza kazi hiyo. Napenda kutumia fursa hii kuwaomba watu mwenye taarifa zinazoweza kufanikisha kazi ya Tume hiyo wafanye hivyo.
Kwa mara nyingine tena narudia kutoa mkono wa pole na rambirambi kwa ndugu zetu waliopoteza ndugu na jamaa zao katika ajali ile. Nawaomba waendelee kuwa na moyo wa subira na sisi wengine tujumuike nao kuwaombea marehemu wapate mapumziko mema. Kwa walionusurika tunaendelea kuwapa pole na
kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwaponya.
Ndugu Wananchi;
Narudia kutoa pongezi maalum kwa vyombo vyetu vya usalama na wale wote walioshiriki kuokoa maisha ya ndugu zetu waliozama na kuwaopoa maiti. Natoa pongezi za pekee kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, na Makamu wake wawili kwa uongozi wao thabiti. Aidha, nawapongeza sana viongozi na watendaji wa ngazi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na wananchi wa Zanzibar kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya tangu kutokea kwa ajali, jitihada za uokoaji, maiti kuzikwa, majeruhi kutibiwa na kurejea makwao na kuwafariji wafiwa na walionusurika.
Mwisho, lakini siyo mwisho kwa umuhimu, nawapongeza sana wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa jumla kwa moyo wao wa upendo, ustahamilivu na mshikamano waliouonesha katika maafa haya ya kitaifa.
Safari ya Marekani
Ndugu Wananchi;
Kati ya tarehe 16 na 23 Septemba, 2011 nilifanya ziara ya kikazi nchini Marekani. Nilikwenda kuhudhuria Kikao cha 66 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na shughuli zake. Pamoja na hayo nimehudhuria mikutano mingine kama vile Mkutano wa Open Government, ulioitishwa na Rais Barrack Obama wa
Marekani,Mkutano wa Umoja wa Marais wa Afrika wa kupambana na malaria ,Mkutano wa Tatu wa Watanzania Waishio Marekani (DICOTA 3) na mkutano kuhusu Wanawake na Lishe ulioandaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mama Hilary Clinton. Aidha, mimi na Waziri Mkuu, Stephem Harper wa Canada tulipata nafasi ya kuwasilisha taarifa ya Tume ya Afya ya Mama na Mtoto aliyoiunda Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambayo tulikuwa Wenyeviti wenza. Nafurahi kwamba taarifa yetu imepokelewa vizuri na kuelezwa kuwa itakuwa msingi mzuri wa kutatua matatizo ya vifo vya kina mama na watoto duniani.
Katika hotuba yangu kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, nilieleza jinsi nchi yetu ilivyoshiriki katika shughuli za Umoja wa Mataifa katika miaka 50 ya Uanachama wetu ambayo pia ndiyo miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara na miaka 47 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Nchi yetu inayo historia iliyotukuka kwamba, pamoja na udogo na umaskini wetu, tumetoa mchango muhimu katika shughuli za Umoja wa Mataifa za kudumisha amani na usalama wa dunia na kuleta maendeleo. Tunayo fahari kwa mchango tuliotoa mpaka sasa. Niliwaahidi kuwa Tanzania itaendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa Umoja wa Mataifa na
kuendelea kutoa mchango wake ipasavyo.

Macho,masikio,fikra na mawazo ya wengi yanaelekea mjini Dodoma ambapo hapo kesho,serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete kupitia kwa Waziri wa Fedha,Mh.Mustafa Mkullo(pichani) itawakilisha bajeti yake kwa mwaka 2011/12. Kimsingi,kama unataka kujua mipango ya serikali na jinsi gani ahadi zilizotolewa na wabunge na hata Rais mwenyewe wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita,bajeti ndio msema kweli. Kwa maana hiyo kuna umuhimu wa kila mtu kufuatilia japo kwa kiasi fulani tu,ili kupata fununu ya jinsi gani kesho itakavyokuwa.
Bajeti hiyo kwa ufupi huanisha jinsi gani serikali imejiandaa kukusanya mapato yake(zaidi kutoka katika kodi na misaada kutoka kwa wafadhili-sijui mpaka lini) na jinsi gani itayatumia mapato hayo kutekeleza majukumu yake ya msingi kama vile ulinzi na usalama,upatikanaji wa huduma za afya, uendelezwaji na ukarabati wa miundo mbinu,utoaji wa elimu nk.
Je,kuna mapya gani kutoka katika bajeti ya mwaka jana kuja bajeti ya mwaka huu?Hali ya uchumi wa nchi hii(kama nchi na sio watu binafsi) ikoje?Je,itakuwa ni bajeti iliyolenga katika kumkomboa mwananchi au imelengwa katika kumwongezea aliyenacho? Majibu kwa maswali hayo na mengineyo mengi,yatategemea sana kitakachojiri au kitakachotamkwa kutoka katika mkoba utakaobeba “bajeti” hiyo hapo kesho.
Nchi za Kenya na Uganda nazo zinatarajiwa kuwa na sessions za uwasilishwaji wa bajeti hiyo kesho hiyo hiyo.

Mwaka juzi niliandika kidogo kuhusu umuhimu wa kuandika na kutunza historia zetu hususani mitandaoni katika zama hizi za maendeleo makubwa na ya kasi ya sayansi na tekinolojia.
Nakumbuka niliandika na kuomba wajuzi wa historia ya nchi yetu,kushiriki katika kuandika na kuitunza historia ya Mwanasiasa Mkongwe,Hayati Bibi Titi Mohammed kupitia mradi wa Wikipedia ambao leo hii unasifika na kuaminika kuwa chanzo cha maarifa mbalimbali.Kwa bahati mbaya,mpaka hivi leo ukurasa wa Bibi Titi Mohammed katika Wikipedia bado una mapungufu.Unahitaji kuendelezwa.Ni kweli kwamba hakuna anayejua kwamba Bibi Titi alizaliwa wapi na kwamba hata tarehe yake ya kuzaliwa haijulikani zaidi ya kwamba alizaliwa mwaka 1926?
Pamoja na utata ambao umekuwa ukijitokeza mara kadhaa kuhusu usahihi wa kinachoandikwa katika Wikipedia,hivi leo inasemekana kwamba wanafunzi wengi,hupata maarifa yao kupitia Wikipedia.
Utata unaojitokeza kuhusu usahihi au kinyume chake katika Wikipedia, unatokana na ukweli kwamba Wikipedia inaandikwa na kila mtu.Wewe na mimi.Kila mtu ana uhuru wa kujiunga na Wikipedia na kuchangia.
Hatari ya uhuru huo ni kwamba kuna uwezekano mkubwa wa mtu au watu kuandika historia katika jinsi ambayo itakidhi mahitaji yao na hivyo kuandika habari potofu au za uongo.Hilo linaweza kufanyika kwa bahati mbaya au makusudi.
Kama hunipendi mimi Jeff Msangi,basi unaweza ukaingia katika Wikipedia na kuandika unachokitaka wewe mpaka hapo mwingine anayeijua historia yangu kwa jicho lingine,atakapoingia na kusahihisha.Kama mimi mwenyewe nipo hai pia naweza kuwaandikia Wikipedia na kutoa malalamiko yangu na wao watarekebisha.Kwa kawaida,mtu binafsi haruhusiwi kujiunga na Wikipedia na kuandika habari zake binafsi kwa minajili ya kujitangaza na mambo kama hayo.Historia yako inaandikwa na watu wengine.
Sikumbuki nilikuwa nawaza nini leo nilipoamua kujaribu kutafuta habari zinazomhusu Mwanasiasa mkongwe,Marehemu Oscar Kambona(13th August 1928-July 1997). Historia yake,kwa mujibu wa Wikipedia, imeandikwa vizuri na kwa umakini.Nasema kwa umakini kwa sababu imeandikwa kwa nia ya makusudi ya kuelezea maisha ya mwanasiasa huyo katika miale ya kumtaka msomaji kuelewa vizuri historia yake na kile kilichojiri mpaka akaja kutoelewana na serikali ya awamu ya kwanza na bila shaka Hayati Baba wa Taifa,Julius Kambarage Nyerere mwenyewe. Lakini kila kitu kilichoandikwa pale ni sahihi? Mtiririko ule wa matukio ndivyo ulivyokuwa? Ni kweli kwamba Kambona na Nyerere walishindwa kuelewana katika suala zima la siasa za Ujamaa na Azimio la Arusha peke yake? (Nyerere aliamini katika Ujamaa wakati Kambona aliamini katika Ubepari)

Baraza la Kwanza la Mawaziri baada ya Muungano.Oscar Kambona ni wa tatu kutoka kushoto mstari wa mbele.
Hapo ndipo linapokuja tena suala la sisi sote,hususani wale wasomi wa historia,kuwa mstari wa mbele katika kuchangia katika miradi kama Wikipedia.Nia ni kuhakikisha kwamba historia ya nchi yetu,ya watu wetu,inaandikwa kwa usahihi wa kutosha na unaokubalika. Tusipofanya hivyo,tunahatarisha kuzidi kuupoteza ukweli kuhusu historia.Muda ni jambo la ajabu.Hutufanya kusahau.Vizazi vya baadae vitasoma nini na kujifunza kutoka kwa nani juu ya historia yetu?
Shime.Wewe msomi.Jiunge sasa na Wikipedia.Sahihisha.Andika.Historia yetu,za kwetu,za watu wetu ni muhimu zikaandikwa na watu miongoni mwetu.

Kutoka kushoto; Jaji Mkuu,Othman Chande, Spika wa Bunge,Anna Makinda,Rais wa Jamhuri ya Muungano,Jakaya Kikwete. Wana madaraka sawa?Katiba inasemaje?
Kama kungekuwepo na software ya kutambua neno au maneno ambayo kwa muda sasa yametawala vinywa na mijadala mbalimbali inayoendelea nchini Tanzania na hata nje ya nchi miongoni mwa watanzania, bila shaka maneno yafuatayo yangeshika nafasi za juu sana; Katiba ya Tanzania, Dowans,Tanesco,Mgao,Migomo, Bodi ya Mikopo,CHADEMA,CCM…
Kwa ujumla mijadala yote ni muhimu.Kadri tunavyojadiliana ndivyo tunavyopanua mawazo na kutafuta mbinu za kutatua masuala husika. Tatizo linakuja pale tunapojadiliana kwa jazba na kisha kuishia kulaumiana tu bila kuwa na mapendekezo halisi au huku wengine wakiona mijadala hiyo kama vitisho na hivyo kuamua kunyamazisha mijadala hiyo kwa kutumia mbinu mbalimbali.
Miongoni mwa mijadala ambayo ni muhimu sana kuwa nayo au kuiendeleza ni pamoja na huu wa Katiba ya Tanzania.Kama tunavyoelewa,Katiba ya nchi ni mama na baba wa sheria zote.Katiba ndio nchi.Muongozo. Yapo maoni mbalimbali yanayoendelea; Je kuna haja ya kuibadili katiba iliyopo,kuiandika upya au kuiwekea tu viraka hii tuliyonayo ya mwaka 1977? Tuliyonayo inasema nini,ina kasoro gani?Mijadala kama hiyo.

Wasomi mbalimbali,wataalamu wa masuala ya katiba,wameshaanza kuchangia vizuri sana kuhusu mchakato huo.Mfano mzuri ni lile Kongamano la Katiba lililoandaliwa hivi karibuni pale University of Dar-es-salaam na kushirikisha wasomi,wakufunzi na wataalamu mbalimbali wa masuala ya katiba. Kama hukuwahi kuona japo video clips mbalimbali kutoka katika kongamano lile,nakushauri U-Google “Kongamano la Katiba” ujionee na kujifunza .
Lakini tunaposubiri kutangazwa rasmi kwa tume ya katiba(nilitumaini ingeshaanza kazi) kama alivyoahidi Rais Kikwete wakati wa salamu zake za mwaka mpya, ni wazi kwamba kazi kubwa ipo mikononi mwetu;wananchi. Kama Tume itakusanya maoni,itaweka vikao mbalimbali na wananchi na kujadili au kusikiliza mapendekezo kuhusu Katiba, kuna ulazima wa wananchi hao kujua kilichomo kwenye katiba ya sasa ambayo wengi tunataka ibadilishwe kwa sababu haiendani na wakati uliopo!
Hapo ndipo umuhimu wa kuisoma Katiba unapokuja.Kwa bahati mbaya,Katiba haifundishwi mashuleni. Wanaopata nafasi ya kujifunza katiba wakiwa darasani ni wale wanaosomea Constitutional Law katika ngazi ya vyuo. Huku chini ambapo ndipo walipo au walipoishia watanzania wengi, katiba haipo katika mitaala(curriculum).
Sitoshangaa wala kukulaumu msomaji wa post hii ukiniambia kwamba hujawahi kusoma hata kifungu kimoja kutoka ndani ya Katiba. Hukupewa nafasi.Maktaba ya shule uliyosomea haikuwahi kuwa hata na copy moja ya Katiba.Ufanyeje?
Bahati nzuri ni kwamba hivi sasa tunaishi katika zama za sayansi na tekinolojia. Leo hii katiba inaweza kusomeka kutoka katika simu ya kiganjani(mobile phone). Inasomeka katika computer na pia kuna machapisho mengi zaidi ya katiba. Ukienda kwenye duka la vitabu hivi leo,bila shaka utapata copy.
Tunachotakiwa ni kuisoma Katiba(kama hujawahi kuisoma),kuwasomea wenzetu ambao kwa sababu moja ama nyingine hawajapata muda au nafasi ya kuisoma.Na unapoisoma usiisome kama vile unavyosoma kitabu cha hadithi.Hiki ni kitabu cha marejeo(reference book).Unaweza kurejea katika vifungu fulani fulani kila mara kadri inavyohitajika.
Ushauri wangu ni kwamba ukishasoma ufafanuzi wa mwanzo kuhusu katiba,inavyoundwa nk, unaweza kurukia katika vifungu fulani fulani ambavyo unahisi vinakugusa zaidi. Kama wewe ni mtu unayependa kushiriki mijadala mbalimbali kwa kutoa maoni yako, tafuta kifungu kwa mfano kinachoongelea haki yako ya kutoa maoni. Kama suala la madaraka ya Rais(inasemekana katiba ya sasa inampa madaraka makubwa sana) dhidi ya madaraka ya Bunge na Mahakama soma vifungu vinavyohusiana na madaraka ya mihimili hiyo mitatu. Ukifanya hivyo,siku Tume ikifika kwako utakuwa na cha kuchangia. La sivyo…
Unaweza kuisoma Katiba ya Tanzania kwa kubonyeza hapa. Isome,anzisha mijadala.

Katika pitapita zangu mitandaoni,nimekuta mjadala fulani ndani ya ukumbi wa Facebook ambao kila kukicha unazidi kuwa sehemu pana zaidi ya watu kubadilishana mawazo,kuchanganua sera nk.
Muungwana mmoja ameuliza; hivi kuna ulazima wa wakuu karibuni wote wa nchi(kama vile Makamu wa Rais, Waziri Mkuu,Mkuu wa Majeshi, Inspekta General wa Polisi,Mkuu wa Mkoa nk) kwenda kumpokea Rais kila anapokuwa anarejea kutoka safari za nje ya nchi?
Nimeona niulete huu mjadala hapa kwa sababu naamini kuna wataalamu wa Protocol ambao huingia humu au kupekua kurasa hizi ambao wanaweza kutusaidia kupata majibu. Wakiamua kubania majibu,itakuwa ni kuendeleza tu zile sera zetu za “Don’t Ask,Don’t Question,Just Do It”.It’s nothing personal bali kuelimishana tu.
Pichani ni Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Makamu wa Rais, Dr.Gharib Bilal huku Waziri Mkuu, Mh.Mizengo Pinda akiwa pembeni. Hii ilikuwa wakati walipokwenda kumlaki Rais Kikwete alipokuwa akirejea kutoka nchini Ethiopia (alifanya ziara katika nchi zingine pia) alipohudhuria kikao cha Umoja wa Afrika(AU).Picha na Father Kidevu

Pichani ni Jenerali Davis A.Mwamunyange-Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania. Amekuwa Mkuu wa Majeshi tangu tarehe 13 Septemba mwaka 2007 na bado anashikilia cheo hicho mpaka hivi sasa.
Ukitaka kujifunza mengi kuhusiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) au kwa Kiingereza Tanzanian’s People Defense Forces(TPDF) ikiwemo historia yake,muundo wake,shughuli zake,jinsi ya kujiunga na jeshi na mengineyo mengi,Tembelea Tovuti ya JWTZ kwa kubonyeza hapa.

President Jakaya Mrisho Kikwete

Nimemaliza kusikiliza hotuba ya salamu za mwaka mpya toka kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Rais amegusia mambo mbalimbali.Lakini kubwa zaidi ambalo nadhani watu wengi watakuwa wametoka nalo ni lile la kuafiki kwake kwamba wakati umefika kwa Tanzania kuwa na Katiba Mpya.
Rais amesema anaunda Constitutional Review Commission(Tume ya Kurekebisha Katiba) ambayo itawashirikisha watu wote katika upatikanaji wa mapendekezo na kisha katiba mpya.
Ninapouanza mwaka mpya,hili ndilo ninalosonga nalo mbele.Katiba itakayokidhi mahitaji ya nchi katika karne hii.Hongera Mheshimiwa Rais.Itazame hotuba nzima ya Rais hapo chini;

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania,Mheshimiwa Anna Makinda amesema hatogombea tena nafasi ya Ubunge pindi atakapomaliza muda wake mwaka 2015.
Akiongea katika mahojiano maalumu na blog ya Mohamed Dewji,Mheshimiwa Makinda ambaye ni Mbunge wa Njombe Kusini na mwanamke wa kwanza kushikilia nafasi ya Spika wa Bunge nchini Tanzania, pia amesema kwa sasa hana mpango wa kugombea nafasi ya Urais ifikapo mwaka 2015.
Unaweza kusoma mahojiano kamili ya Mheshimiwa Spika na Mo Blog kwa kubonyeza hapa.
Photo Credit:Mo Blog


sending...
